Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kristo-ndiye-ukweli-njia-na-uzima. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kristo-ndiye-ukweli-njia-na-uzima. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 26 Mei 2018

Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu"

Swahili Gospel Praise Music "Kila Kitu Kinaishi Chini ya Sheria na Masharti Yaliyowekwa na Mungu"

Miaka elfu kadhaa imepita,
na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu,
angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe,
angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu,

Jumapili, 20 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

 "Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

Biblia inasema, "Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba" (Ufunuo 5:1). "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa; Kwa yule ashindaye nitampa mana iliyofichwa aile" (Ufunuo 2:17). Kulingana na Biblia, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho Atafungua kitabu, afungue mihuri saba na ampe mwanadamu mana iliyofichwa.

Alhamisi, 3 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (4) - Je, Kuamini katika Biblia ni Sawa na Kuamini katika Bwana?

"Imani katika Mungu" (4) - Je, Kuamini katika Biblia ni Sawa na Kuamini katika Bwana?

Watu wengi zaidi katika ulimwengu wa dini huamini kwamba Biblia ni kanuni ya Ukristo,kwamba mtu lazima ashikilie Biblia na kuweka msingi wa imani yake katika Bwana kwenye Biblia kabisa, na kwamba mtu hawezi kuitwa muumini akipotoka kutoka kwenye Biblia. Hivyo imani katika Bwana na imani katika Biblia ni sawa? Uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi hasa?

Jumatatu, 26 Machi 2018

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Mwenyezi Mungu alisema,  Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. 

Jumanne, 20 Machi 2018

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya



Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaisha, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? 

Jumatano, 14 Machi 2018

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo"Kuvunja Pingu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada


Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo"Kuvunja Pingu"

Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena
Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani. Baada ya miaka kadhaa ya kujitafakari, nilikuwa kwa kiwango fulani na maarifa ya asili yangu mwenyewe, lakini kuhusu kipengele cha ukweli ambacho ni kiini cha Mungu bado sikuwa na maarifa mengi. Baadaye, kanisa lilinipa nafasi nyingine, lakini nilipokuwa nikisimamia kazi ya injili, nilianza kuwa na shaka kumhusu Mungu: Mimi ni mpotovu sana na pia nilikuwa nimeichukiza tabia ya Mungu. Ni kwa nini Mungu angenitumia mimi? Je, Ananidanganya? Je, nitaondolewa baada ya kudanganywa? Aa! Kwa kuwa kanisa lilinipa nafasi nitaitunza, hata kama ni lazima niwe mtenda huduma. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilitimiza wajibu wangu nikiwa na akili kama hiyo, lakini bila kutafuta lengo la juu—kufanywa mkamilifu na Mungu.
Wakati fulani, nilipokuwa nikitenda ibada ya roho, niliona maneno haya ya Mungu: “Leo hii, huwezi tu kuridhika na jinsi wewe umeshindwa, lakini lazima pia uzingatie njia ambayo utatembelea siku zijazo. Lazima uwe na matarajio na ujasiri wa kufanywa mkamilifu, na hupaswi daima kufikiria kwamba huwezi. Je, ukweli una maonevu? Je, ukweli huwapinga watu kwa makusudi? Kama wewe utaufuata ukweli, je unaweza kukushinda? Kama wewe utasimama imara kwa ajili ya haki, je utakuangusha chini? Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli haukutambui, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha…. Kama huwezi kufuata, basi inaweza kusemwa kwamba wewe ni taka usiye na maana, na huna ujasiri katika maisha Yako, na huna roho ya kupinga nguvu za giza. Wewe ni mdhaifu mno! Huwezi kutoroka nguvu za Shetani ambazo zimekuzingira, na kuwa uko tayari tu kuishi haya maisha ya usalama na kufa katika ujinga. Kile unachopaswa kufanya ni kutekeleza azma Yako ya kuwa mshinde; huu ni wajibu wako uliokushikilia. Kama wewe umeridhika na kushindwa, basi unafukuza kuwepo kwa mwanga” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kula na kunywa kifungu hiki cha neno la Mungu, niliguswa sana ndani. Niliona kwamba nia ya Mungu ni kuwaruhusu watu wote kutafuta kufanywa wakamilifu na wanaofaa kutumiwa na Mungu. Kisha nilifanya uamuzi: Nitaweka mbali wasiwasi wangu mwenyewe na nisiwe tena hasi na baridi. Nitaamini katika maneno ya Mungu na nifanye bidii ili kukamilishwa na Mungu. Lakini pole pole, kwa sababu bado sikujua kiini cha uaminifu wa Mungu, nilianza kuacha kuamini katika maneno ya Mungu tena, kila mara nikiamini kuwa maneno haya yalilengwa kwa mtu mwingine, na kwa mtu kama mimi yangetoa tu faraja na kutia moyo kwa kiasi kidogo. Nilizidi kukumbuka jinsi wakati mmoja nilivyoikosea tabia ya Mungu, kwamba asili yangu ni potovu sana, kwamba wakati mwingine hata nilifichua tabia yangu potovu huku nikitimiza wajibu wangu, kwamba singeweza kukamilishwa haijalishi jinsi nilivyofuatilia, na kufikiri kwamba ninapaswa kuridhika tu na kuwa mtenda huduma. Kwa namna hiyo tu, bila kujua nilianza kuishi katika ubaridi tena. Yule wa juu kisha aliwasiliana mara nyingi juu ya kipengele cha ukweli kuhusu kujua kiini cha Mungu, lakini bado sikuwa nimepata nuru sana. Mpaka siku moja nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno yafuatayo ya Mungu: “Kiini cha Mungu ni uaminifu—Yeye hufanya Anachosema na chochote Afanyacho hutimizwa. Yeye ni mwaminifu …” (“Kipengele cha Pili cha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Wakati huu, ilionekana kana kwamba wazo lilieleweka ndani mwangu kwa ghafla, kana kwamba ukungu uliokuwa umetanda juu ya moyo wangu ulitawanyika mara moja. Miaka mingi ya kutoelewa na wasiwasi kwa ghafla iliisha. Kisha tena nikakumbuka kile kifungu cha neno la Mungu ambalo nilikuwa nikila na kunywa: “Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli haukutambui, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha …” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huu, nilihisi upitishaji wa haki ya ajabu na upendo usio na mipaka kutoka katikati ya mistari ya maneno ya Mungu, yakimfanya Aonekane mwema na mkuu, huku wakati uo huo yakinifanya nione upweke wangu mwenyewe, ufinyu, na uoza. Mungu ni mwaminifu. Hili ni bila shaka na lisiloweza kushukiwa. Mungu ana kiini cha uaminifu, Yeye ni wa kuaminika, na Anajaribu kumwokoa binadamu kwa kiasi kikuu iwezekanavyo. Mradi tu binadamu anafuatilia ukweli na mabadiliko katika tabia kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu atamfanya mwanadamu kamili, kwa sababu kile asemacho Mungu atafanya, Atakifanya na kile Afanyacho kitafanyika! Badala yake, nilishuku kuwa Mungu alikuwa kama binadamu na Angenitupilia mbali mara tu ningekoma kuwa mwenye maana. Sikulichukulia neno la Mungu kama ukweli hata kidogo, na zaidi ya hayo sikuamini katika Mungu kwa kweli na kwa uzuri. Badala yake, niliishi katika fikira na shaka katika mawazo yangu, nikikosa ujasiri mbele ya ukweli na kwa woga kukubali ushawishi wa giza, nisiweze kutetea haki. Ilikuwa ni hapo ndipo nilifahamu kwa kweli kuwa kufuatilia maarifa ya kiini cha Mungu ni muhimu sana. Kama ningekuwa tayari nimekuwa makini kufuatilia ufahamu wa tabia ya Mungu na kiini Chake kabla, nisingeliishi miaka mingi vile katika wasiwasi, nikichelewesha kuendelea kwa maisha yangu mwenyewe.
Asante, Mwenyezi Mungu! Ni Wewe uliyenitunza na kunipa nuru na kuniongoza kujitoa katika pingu ambazo zilikuwa zimenidhibiti kwa miaka mingi sana, kuniruhusu kutoka katika ukungu. Zamani, sikukujua Wewe na mara nyingi niliishi katika kutoelewa, nisiweze kuamini neno Lako na kulichukulia kama tu la kuliwaza na kuwatia watu moyo. Sikulichukulia neno Lako kama ukweli na uzima, na zaidi sikukuchukulia wewe kama Mungu. Lakini hukunitendea kulingana na dhambi zangu. Ulinivumilia, Ulikuwa mwenye subira kwangu, na kunipa fursa ya kutubu. Ulinipa nuru na kuangaza mwanga Wako kwangu, ili kwamba niwe na ufahamu kidogo wa kiini Chako cha haki na uaminifu. Hii hasa ni mfano kamili wa upendo Wako kwa mwanadamu. Ee Mungu! Kuanzia sasa kuendelea nitaweka juhudi kubwa katika ukweli kuhusu kukujua Wewe, kufuata kile unachotarajia kutoka kwangu, nifuatilie ufahamu wa kiini Chako, na kutafuta mabadiliko katika tabia hivi karibuni ili niweze kukamilishwa na Wewe!
Baada ya kujua mambo haya, aina ya nguvu nzuri mno ilivimba ndani ya moyo wangu. Mimi siko baridi tena nikikabiliwa na ugumu, na miaka yangu mingi ya kutoelewa, shaka, na wasiwasi yote imepotea. Sasa ninaishi kabisa katika hali ya kujishughulisha, nikitafuta kukamilishwa na Mungu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Alhamisi, 1 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Ufafanuzi wa Tamko la Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Ufafanuzi wa Tamko la Nane

Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa Roho, sauti Yake huelekezwa kwa wanadamu wote. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa mwanadamu, sauti Yake huelekezwa kwa wote wafuatao uongozi wa Roho Wake. Mungu anenapo neno Lake kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu (kile ambacho watu hutaja kama mtazamaji), Anaonyesha neno Lake moja kwa moja kwa watu ili watu wamwone kama mtoa maoni, na huonekana kwamba kutoka kinywani Mwake hutoka mambo yasiyo na kikomo ambayo mwanadamu hayajui, mambo ambayo mwanadamu hawezi kuelewa.

Jumatano, 24 Januari 2018

Sura ya 55. Usieleze Kile Mungu Alicho Nacho na Kile Alicho

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,hekima ya Mungu
hekima ya Mungu

Sura ya 55. Usieleze Kile Mungu Alicho Nacho na Kile Alicho

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi na matamshi ya Mungu ya miaka michache iliyopita yote yamerekodiwa kimsingi katika kitabu, Neno Laonekana katika Mwili. Baadhi ya maneno katika kitabu hiki ni ya kinabii na yanatabiri vile enzi za baadaye zitakavyokuwa.

Jumatatu, 8 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)
Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu?

Jumapili, 7 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

 Nne, Mungu alichora mipaka kati ya jamii za rangi tofautitofauti. Duniani kuna watu weupe, watu weusi, watu wa kahawia na watu wa njano. Hawa ni aina tofuati za watu. Mungu pia aliweka mawanda kwa ajili ya maisha ya aina hizi tofauti za watu, na bila kutambua, watu wanaishi ndani ya mazingira yao stahiki kwa kuendelea kuishi chini ya usimamizi wa Mungu.

Ijumaa, 5 Januari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu| Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,imani ya kidini
imani ya kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu| Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia

    Ni nini mnafahamu kuhusu mabadiliko katika tabia? Asili ya mabadiliko katika tabia na mabadiliko katika mwenendo ni tofauti, na mabadiliko katika matendo pia ni tofauti—yote ni tofauti kwa asili.