Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI |
Utakatifu wa Mungu (III)
Mwenyezi Mungu alisema, Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.)Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Anatumia maarifa, sayansi, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii kutupotosha.) Sahihi, hii ndiyo ilikuwa mada kuu tuliyojadili wakati uliopita. Shetani hutumia maarifa, sayansi, ushirikina, desturi ya kitamaduni, na mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu; hizi ndizo njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Hizi ni njia ngapi kwa jumla? (Tano.) Ni njia zipi tano? (Sayansi, maarifa, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii.) Mnafikiri Shetani anatumia nini zaidi kumpotosha mwanadamu, kitu ambacho kinampotosha kwa kina zaidi? (Desturi ya kitamaduni.) Kaka na dada wengine wanadhani kwamba ni desturi ya kitamaduni. Kuna nyingine? (Maarifa.) Inaonekana kwamba mna kiwango cha juu cha maarifa. Kuna mengine zaidi? (Maarifa.) Mnashiriki mtazamo sawa. Kaka na dada waliosema desturi ya kitamaduni, mnaweza kutueleza mbona mnafikiri hivi? Je, mna uelewa wowote wa jambo hili? Je, hamtaki kueleza uelewa wenu? (Filosofia za Shetani na mafundisho ya Confucius na Mencius zimetopea sana katika akili zetu, kwa hivyo tunahisi kwamba haya yanatupotosha sana.) Wale wanaofikiria kwamba ni maarifa, mnaweza kueleza mbona? Semeni sababu zenu. (Maarifa hayawezi kuturuhusu kumwabudu Mungu. Yanapinga kuwepo kwa Mungu, na yanapinga kanuni ya Mungu. Yaani, maarifa yanatuambia tusome kuanzia umri mdogo, na kwamba ni kupitia tu kusoma na kupata maarifa ndipo siku zetu za baadaye na kudura zetu zinahakikishwa. Kwa njia hii yanatupotosha.) Kwa hivyo Shetani anatumia maarifa kudhibiti siku zako za baadaye na kudura yako, kisha anakuongoza kuendelea kupitia pua lako; hivi ndivyo unavyofikiria Shetani anampotosha mwanadamu kwa kina zaidi. Kwa hivyo wengi wenu wanafikiri Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu kwa kina. Kuna mengine zaidi? Je, sayansi na mienendo ya kjamii, kwa mfano? Kuna yeyote anayekubaliana na haya? (Ndiyo.) Leo Nitashiriki tena kuhusu njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu, na, baada ya Mimi kumaliza, Nitawauliza baadhi ya maswali ili kuona ni katika kipengele kipi hasa Shetani anampotosha mwanadamu kwa kina zaidi. Mnaelewa mada hii, siyo?
Upotovu wa Shetani wa mwanadamu unadhihirika kimsingi katika vipengele vitano; hivi vipengele vitano ni njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Ya kwanza kati ya njia hizi tano tulizotaja ni maarifa, kwa hivyo wacha kwanza tuchukue maarifa kama mada ya kushiriki. Shetani hutumia maarifa kama chambo. Sikiza kwa makini: Ni aina tu ya chambo. Watu wanavutiwa “kusoma kwa bidii na kuboreka kila siku,” kujihami kwa maarifa, kama silaha, kisha kutumia maarifa kufungua njia ya sayansi; kwa maneno mengine, kadri unapopata maarifa zaidi, ndivyo utavyoelewa zaidi. Shetani huwaambia watu haya yote. Shetani huwaambia watu kuwa na fikira za juu pia, kwa wakati sawa wanaposoma maarifa, akiwaambia kuwa na matarajio na maadili. Bila kujua kwa watu, Shetani anasambaza ujumbe mwingi kama huu, na kuwafanya watu kuhisi bila kujua kwamba vitu hivi ni sahihi, ama ni vya manufaa. Bila kujua, watu wanatembea njia ya aina hii, bila kujua wanaongozwa mbele na matarajio na maadili yao. Hatua kwa hatua, watu bila kujua wanajifunza kutoka kwa maarifa waliyopewa na Shetani kufikiria kwa watu wakubwa ama maarufu, na kukubali fikira hizi. Wanajifunza pia jambo moja baada ya lingine kutoka kwa matendo ya wengine ambao watu wanachukulia kuwa “mashujaa.” Mnaweza kujua baadhi ya yale ambayo Shetani anatetea kwa mwanadamu katika matendo ya hawa “mashujaa,” ama kile anachotaka kuingiza kwa mwanadamu. Ni kipi ambacho Shetani anaingiza kwa mwanadamu? Mwanadamu lazima awe mzalendo, awe na uadilifu wa kitaifa, na awe shujaa. Ni yapi ambayo mwanadamu anajifunza kutoka kwa baadhi ya hadithi za kihistoria ama kutoka kwa wasifu wa mashujaa? Kuwa na hisia ya uaminifu wa kibinafsi, ama kufanya lolote kwa ajili ya rafiki ya mtu ama kwa rafiki. Miongoni mwa maarifa haya ya Shetani, mwanadamu bila kujua anajifunza mambo mengi, na anajifunza mambo mengi hasi. Katikati ya kutojua huku, mbegu zilizotayarishwa kwa ajili yao na Shetani zinapandwa katika akili zao zisizokomaa. Mbegu hizi zinawafanya kuhisi kwamba wanapaswa kuwa watu wakubwa, wanapaswa kuwa maarufu, wanapaswa kuwa mashujaa, kuwa wazalendo, kuwa watu wanaopenda familia zao, ama kuwa watu wanaoweza kufanya chochote kwa ajili ya rafiki na kuwa na hisia za uaminifu wa kibinafsi. Baada ya kushawishiwa na Shetani, bila kujua wanatembea njia ambayo amewatayarishia. Wanapotembea njia hii, wanalazimika kukubali kanuni za Shetani za kuishi. Bila kujua na bila wao kuwa na uelewa kabisa, wanakuwa na kanuni zao za kuishi, wakati hizi si chochote ila kanuni za Shetani ambazo zimeingizwa kwao kwa nguvu. Wakati wa mchakato wa kujifunza, Shetani anawasababisha kukuza malengo yao wenyewe, kuamua malengo yao ya maisha wenyewe, kanuni za kuishi, na mwelekeo wa maisha, wakati huo wote anawaingizia mambo ya Shetani, kwa kutumia hadithi, kwa kutumia wasifu, kwa kutumia mbinu zote zinazowezekana kuwapata watu, kuchukua chambo polepole. Kwa njia hii, watu wanakuwa na mambo yao ya kupitisha muda na shughuli katika mkondo wa kujifunza kwao: Wengine wanakuja kupenda fasihi, wengine uchumi, wengine unajimu ama jiografia. Kisha kuna wengine wanaokuja kupenda siasa, wengine wanaopenda fizikia, wengine kemia, na hata wengine wanaopenda theolojia. Haya yote ni sehemu ya maarifa na nyote mmepatana nayo. Katika mioyo yenu, kila mmoja wenu anajua yalivyo na mambo haya, kila mmoja amepatana nayo awali. Kuhusiana na maarifa ya aina hii, yeyote anaweza kuzungumza bila kikomo kuhusu moja yao fulani. Na hivyo ni wazi jinsi maarifa haya yameingia kwa kina katika akili ya mwanadamu, inaonyesha nafasi iliyochukuliwa na maarifa haya katika akili ya mwanadamu na jinsi yalivyo na athari ya kina kwa mwanadamu. Punde tu mtu anapenda sehemu ya maarifa, wakati katika moyo wake mtu amependa kwa dhati mojawapo, basi bila kujua anaendeleza maadili: Watu wengine wanataka kuwa watunzi, wengine wanataka kuwa waandishi, wengine wanataka kuwa na kazi kutokana na siasa, na wengine wanataka kushiriki katika uchumi na kuwa wanabiashara. Kisha kuna kundi la watu ambao wanataka kuwa mashujaa, kuwa wakubwa ama maarufu. Bila kujali mtu anataka kuwa mtu wa aina gani, lengo lake ni kuchukua mbinu hii ya kujifunza maarifa na kuitumia kwa ajili yake, kufikia matamanio yake, maadili yake mwenyewe. Haijalishi inasikika kuwa nzuri namna gani—anataka kufikia ndoto yake, asiishi katika maisha haya bure, ama anataka kushiriki katika kazi—anakuza haya maadili na matarajio ya juu lakini, kimsingi, yote ni ya nini? Je, mmeyafikiria haya awali? Mbona Shetani anataka kufanya hivi? Madhumuni ya Shetani ni yapi, kuyaweka mambo haya kwa mwanadamu? Mioyo yenu lazima ielewe vizuri swali hili.
Sasa wacha tuzungumze kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kutokana na yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, mmeanza kutambua malengo husuda ya Shetani? (Kidogo.) Mbona Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu? Anataka kufanya nini kwa mwanadamu kutumia maarifa? Kumwongoza mwanadamu kufuata njia ya aina ipi? (Kumpinga Mungu.) Bila shaka ni kumpinga Mungu. Hii ni athari unayoweza kuona kwa watu wanaojifunza maarifa, na matokeo unayoyaona baada ya kujifunza kwa maarifa—kumpinga Mungu. Hivyo ni nini malengo husuda ya Shetani? Hujayaelewa, sio? Katika mchakato wa mwanadamu kujifunza maarifa, Shetani atatumia mbinu zozote ili watu waridhishe tamaa yao wenyewe na kutambua maadili yao. Je, uko wazi kuhusu njia hasa anayotaka Shetani kukuongoza? Bila kutia chumvi, watu wanafikiri kwamba hakuna chochote kibaya na kujifunza maarifa, kwamba ni mkondo wa kiasili. Wanafikiri kwamba kukuzaa maadili ya juu ama kuwa na matarajio kunaitwa tu kuwa na hamu ya kupata, na kwamba hii inapaswa kuwa njia sawa ya watu kufuata katika maisha. Iwapo watu wanaweza kupata maadili yao wenyewe, ama kuwa na kazi maishani—je, si ni adhimu zaidi kuishi namna hii? Sio tu kuheshimu babu za mtu kwa njia hiyo bali pia kuacha alama yako katika historia—hili si jambo zuri? Hili ni jambo zuri na linalofaa katika macho ya watu wa kidunia. Je, Shetani, hata hivyo, na malengo yake husuda, anawapeleka watu kwa njia ya aina hii na kisha kuamua amemaliza? Bila shaka la. Kwa kweli, haijalishi jinsi yalivyo juu maadili ya mwanadamu, haijalishi matamanio ya mwanadamu ni ya uhalisi jinsi gani ama jinsi yote yanaweza kuwa ya kufaa, yote ambayo mwanadamu anataka kufikia, yote ambayo mwanadamu anatafuta yameunganishwa bila kuchangulika na maneno mawili. Haya maneno mawili ni muhimu sana kwa maisha ya kila mtu, na haya ni mambo ambayo Shetani ananuia kuingiza ndani ya mwanadamu. Maneno haya mawili ni yapi? Moja ni “umaarufu” na nyingine ni “faida”: Ni umaarufu na faida. Shetani anatumia njia ya hila sana, njia ambayo iko pamoja sana na dhana za watu; si aina ya njia kali. Katikati ya kutoelewa, watu wanakuja kukubali njia ya Shetani ya kuishi, kanuni zake za kuishi, kuanzisha malengo ya maisha na mwelekeo wao katika maisha, na kwa kufanya hivyo wanakuja pia bila kujua kuwa na maadili katika maisha. Haijalishi maadili haya yanaonekana kusikika kuwa ya juu kiasi gani katika maisha, ni kisingizio tu ambacho kinahusiana kwa kutochangulika kwa umaarufu na faida. Mtu yeyote aliye mkubwa ama maarufu, watu wote kwa hakika, chochote wanachofuata maishani kinahusiana tu na haya maneno mawili: “umaarufu” na “faida.” Sivyo? (Ndiyo.) Watu hufikiri kwamba punde tu wanapata umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao kufurahia hadhi ya juu na utajiri mwingi, na kufurahia maisha. Baada ya wao kuwa na umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao katika kutafuta kwao raha na kufurahia kwao kwa fidhuli mwili. Watu kwa hiari, lakini bila kujua, wanachukua miili na akili zao na vyote walivyonavyo, siku zao za baadaye, na kudura zao na kuzikabidhi zote kwa Shetani ili kupata umaarufu na faida wanayotaka. Watu hufanya hivi kamwe bila kusita kwa muda, kamwe bila kujua haja ya kupata tena yote. Je, watu bado wanaweza kujidhibiti baada ya wao kwenda upande wa Shetani kwa njia hii na kuwa mwaminifu kwake? Bila shaka, la. Wanadhibitiwa na Shetani kikamilifu na kabisa. Hawawezi kikamilifu na kabisa kujinusuru kutoka kwa bwawa ambamo wamezama ndani. Baada ya mtu kukwama katika umaarufu na faida, hatafuti tena kile kilichong’aa, kile chenye haki ama yale mambo ambayo ni mazuri na mema. Hii ni kwa sababu nguvu za ushawishi ambazo umaarufu na faida yanayo juu ya watu ni kubwa mno, na vinakuwa vitu vya watu kutafuta katika maisha yao yote na pia milele bila kikomo. Hili silo ukweli? Watu wengine watasema kwamba kujifunza maarifa si chochote zaidi ya kusoma vitabu ama kujifunza mambo kadhaa ambayo hawajui tayari, wakisema kwamba wanafanya hivi ili wasiwe nyuma ya nyakati ama wasiwachwe nyuma na dunia. Watasema kwamba maarifa yanafunzwa tu ili waweke chakula mezani, kwa sababu ya siku zao za baadaye ama kwa sababu ya mahitaji ya kimsingi. Sasa unaweza kuniambia iwapo kuna mtu yeyote ambaye atastahimili mwongo wa kusoma kwa bidii kwa mahitaji ya kimsingi tu, ili kutatua swala la chakula tu? (La, hakuna.) Hakuna watu kama hawa! Kwa hivyo ni nini anatesekea matatizo haya na kutesekea miaka hii yote? Ni kwa sababu ya umaarufu na faida: Umaarufu na faida yanamgoja mbele, yanamwita, na anaamini tu kwa kupitia bidii yake mwenyewe, matatizo na mapambano ndiyo anaweza kufuata ile njia na hivyo kupata umaarufu na faida. Lazima ateseke matatizo haya kwa sababu ya njia yake ya siku za baadaye, kwa sababu ya raha yake ya siku za baadaye na kwa sababu ya maisha bora. Mnaweza kuniambia haya yanayoitwa maarifa kwa hakika ni nini? Si kanuni za kuishi na njia ya kupitia maisha iliyoingizwa kwa watu na Shetani, iliyofundishwa kwao na Shetani katika kujifunza kwao maarifa? Je, si maadili ya juu ya maisha yaliyoingizwa kwa mwanadamu na Shetani? Chukua, kwa mfano, mawazo ya watu wakubwa, uadilifu wa watu maarufu ama roho jasiri ya watu mashujaa, ama chukua uungwana na wema wa nguli na wenye panga katika riwaya za kareti; mawazo haya yanashawishi kizazi kimoja baada ya kingine, na watu wa kila kizazi wanaletwa kuyakubali mawazo haya, kuishi kwa sababu ya mawazo haya na kuyafuata bila kikomo. Hii ndiyo njia, mbinu, ambayo Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kwa hivyo baada ya Shetani kuwaongoza watu kwa njia ya umaarufu na faida, inawezekana wao kumwamini Mungu bado, kumwabudu Yeye? (La, haiwezekani.) Je, maarifa na kanuni za kuishi zilizoingizwa kwa mwanadamu na Shetani zina fikira yoyote ya kumwabudu Mungu? Zina fikira yoyote ya ukweli? (La, hazina.) Je, zina uhalisi wowote wa kumcha Mungu na kuepuka uovu. (La, hazina.) Mnaonekana kuongea kwa uhakika kidogo, lakini haijalishi. Tafuteni ukweli kwa mambo yote na mtapata majibu sahihi; ni kwa majibu sahihi tu mnaweza basi kutembea njia sahihi.
Wacha turejelee tena kwa ufupi: Shetani hutumia nini kuendelea kumfungia mwanadamu na kumdhibiti? (Umaarufu na faida.) Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kudumisha na kupata umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa katika miili ya watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo watu kamwe wanatembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa, wakibeba pingu hizi bila kujua. Kwa ajili ya umaarufu na faida, binadamu hutenganishwa na Mungu na anamsaliti. Kwa kupita kwa kila kizazi, binadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mweusi wa moyo zaidi na zaidi, na hivyo kwa njia hii kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, ni nini hasa nia zake husuda? Ni wazi sasa, sivyo? Shetani si wa kuchukiza? (Ndiyo!) Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu; hapo tu ndipo utaweza kutembea njia sahihi ya uhai katika ufuataji wa ukweli.
Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, kwa kutumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu [a] kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadmu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi. Inaonekana kwamba mmedhuriwa sana na hili, na pia mmeathirika sana na yeye. Mbali na kutumia sayansi kumdanganya mwanadamu, kutumia matokeo yote ya utafiti na mahitimisho mbalimbali ya sayansi kumdanganya mwanadamu, Shetani pia hutumia sayansi kama mbinu ya kutekeleza uangamizi na unyonyaji tele wa mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu. Anafanya hivi chini ya kisingizio kwamba iwapo mwanadamu anatekeleza utafiti wa kisayansi, basi mazingira ya kuishi ya mwanadamu yatakuwa bora na bora zaidi na viwango vya kuishi vya mwanadamu daima vitaboreka, na zaidi ya hayo kwamba maendeleo ya kisayansi yanafanywa ili kuhudumia mahitaji ya mwili ya mwanadamu yanayozidi kila siku na haja ya daima ya kuinua ubora wao wa maisha. Kama sio kwa sababu ya sababu hizi, basi huuliza kile unachofanya hata kuendeleza sayansi. Huu ni msingi wa kidhahania wa maendeleo ya Shetani ya sayansi. Sayansi, hata hivyo, ina matokeo yapi kwa binadamu? Mazingira yetu ya karibu kabisa yana nini? Si hewa ambayo binadamu hupumua imechafuliwa? Maji tunayoyanywa kweli bado ni safi? (La.) Basi, je, chakula tunachokula, kingi chake ni cha kiasili? (La.) Basi ni nini tena? Kinakuzwa kwa kutumia mbolea na kupaliliwa kwa kutumia vinasaba, na pia kuna mabadiliko yanayozalishwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za sayansi, ili kwamba hata mboga na matunda tunayoyala sio ya kiasili tena. Si rahisi sasa kwa watu kupata mazao ya vyakula ambavyo havijabadilishwa kula. Hata mayai hayaonji yalivyokuwa yakionja awali, baada ya kusindikwa na inayoitwa sayansi na Shetani. Kwa kuangalia taswira kubwa, anga nzima imeharibika na kuchafuliwa; milima, maziwa, misitu, mito, bahari, na kila kitu juu na chini ya ardhi vyote vimeharibiwa na inayoitwa mafanikio ya kisayansi. Kwa maneno mengine, ikolojia nzima, mazingira yote ya kuishi yaliyopewa mwanadamu na Mungu yamechafuliwa na kuharibiwa na iitwayo sayansi. Ingawa kuna watu wengi waliopata walichotarajia katika suala la ubora wa maisha wanaotafuta, kuridhisha tamaa na miili yao, mazingira ambayo mwanadamu anaishi kimsingi yameharibiwa na kuangamizwa na “mafanikio” mbalimbali yaliyoletwa na sayansi. Hata nje ama katika nyumba zetu hatuna tena haki ya kupumua pumzi moja ya hewa safi. Wewe niambie, hii ni huzuni ya mwanadamu? Bado kuna furaha yoyote ya kuzungumzia kwa mwanadamu kuishi katika nafasi hii ya kuishi? Mwanadamu anaishi katika nafasi hii ya kuishi na, kutoka mwanzoni, haya mazingira ya kuishi yaliumbwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Maji ambayo watu hunywa, hewa ambayo watu hupumua, chakula ambacho watu hula, mimea, miti, na bahari—haya mazingira ya kuishi yote yalipewa mwanadamu na Mungu; ni asili, na hutekeleza kulingana na amri asili iliyotolewa na Mungu. Kama hakungekuwa na sayansi, na watu wangefurahia alichopewa mwanadamu kulingana na njia ya Mungu, wangekuwa na furaha na wangefurahia kila kitu kikiwa cha asili kabisa. Sasa, hata hivyo, haya yote yameangamizwa na kuharibiwa na Shetani; nafasi ya kimsingi ya kuishi ya mwanadamu haipo tena katika hali yake asili zaidi. Lakini hakuna anayeweza kutambua kilichosababisha matokeo ya aina hii ama jinsi haya yalikuja kuwa, na zaidi ya hapo hata watu zaidi wanaelewa na kukaribia sayansi kwa kutumia mawazo waliyoingiziwa na Shetani, na kwa kutazama sayansi kwa macho ya dunia. Je, hii si ya kuchukiza sana na ya kusikitisha? Kwa kuwa Shetani sasa amechukua nafasi ambamo wanadamu wapo na mazingira yao ya kuishi na kuwapotosha kuwa katika hali hii, na kwa kuwa wanadamu wanaendelea kwa njia hii, kuna haja yoyote ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu hawa duniani ambao wamepotoshwa sana na ambao wamekuwa maadui Wake? Kuna haja ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu? (La.) Iwapo wanadamu watazidi kuendelea kwa njia hii, watachukua mwelekeo upi? (Uharibifu.) Wanadamu wataharibiwa vipi? Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza, mapigo, na ukungu uliosambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? (Uharibifu.) Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati! Inaonekana sasa kama sayansi ni aina ya ushombwe ama sumu inayofanya kazi polepole ambayo Shetani amemwandalia mwanadamu, ili wakati mnapojaribu kupambanua mambo mnafanya hivyo katika hali ya ukungu; haijalishi mnaangalia kwa ugumu aje, hamwezi kuona mambo kwa wazi, na haijalishi mnajaribu sana vipi, hamwezi kuyatambua. Shetani, hata hivyo, bado anatumia jina la sayansi kuzidisha hamu yako na kukuongoza kwa pua, mguu mmoja mbele ya mwingine, kuelekea shimo na kuelekea kifo. Sivyo? (Ndiyo.) Hii ndiyo njia ya pili.
Suala la jinsi Shetani hutumia desturi ya kitamaduni kumpotosha mwanadamu pia linahitaji maelezo. Kuna usawa mwingi kati ya desturi ya kitamaduni na ushirikina, ni tu kuwa desturi ya kitamaduni ina hadithi fulani, vidokezo, na vyanzo fulani. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo watu wengine hawajui maelezo yote, bado wanajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Haya ni mambo ambayo Shetani alimwekea mwanadamu kitambo sana, baada ya kusambaza katika nyakati tofauti mawazo yake na filosofia zake mbalimbali za maisha. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya fingo moja baada ya jingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali mambo haya yanayotoka kwa desturi ya kitamaduni, hadithi ama ushirikina, baada ya mambo haya kuwekwa kwa akili yako, baada ya hayo kukwama katika moyo wako, ni kama tu apizo—unakamatwa na kushawishika na hizi tamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hii bila shaka ni apizo! Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakata chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Sivyo? (Ndiyo.) Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu bila kujua kuwekwa chini ya aina hii ya apizo, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali zaidi na kuichukulia kwa njia sawa ambayo wangemchukulia Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi, kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Katika kutojua, unapokea haya mawazo bila kufahamu na kuwepo kwa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—hii bila shaka ni apizo. Je, mnahisi sawa? (Ndiyo.) Kuna yeyote miongoni mwenu ambao wamechoma ubani na kuabudu Budhaa? (Ndiyo.) Kwa hivyo madhumuni ya kuchoma ubani na kumwabudu Budhaa yalikuwa yapi? (Kuombea amani.) Je ni ujinga kuombea amani kutoka kwa Shetani? Shetani analeta amani? (La.) Kuifikiria sasa, mlikuwa wajinga hapo nyuma? (Ndiyo.) Namna ya aina hiyo ni ya upuuzi, jinga na nyofu, siyo? Shetani hawezi kukupa amani. Mbona? Shetani anafikiria tu jinsi ya kukupotosha na hawezi kukupa amani; anaweza tu kukupa nafasi ya kupumua ya muda mfupi. Lakini lazima uchukue kiapo na ukivunja ahadi yako ama ukivunja kiapo ulichofanya, basi utaona jinsi anavyokuadhibu. Kwa kukufanya uchukue kiapo, kwa kweli anataka kukudhibiti, sivyo? Wakati mlipoombea amani, mlipata amani? (La.) Hamkupata amani, lakini kinyume na hayo alileta bahati mbaya, majanga yasiyoisha na majanga mengi—kweli bahari isiyo na mipaka ya uchungu. Amani haiko miongoni mwa miliki ya Shetani, na hili ni ukweli. Haya ndiyo matokeo kwa wanadamu ya ushirikina wa kikabila na desturi ya kitamaduni.
Suala la Shetani kutumia kwa manufaa yake mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu pia linahitaji maelezo maalum. Hii mienendo ya kijamii ina mambo mengi. Watu wengine husema: “Je, ni kuhusu nguo tunazovaa? Je, ni kuhusu mtindo wa karibuni, vipodozi, kutengeneza nywele na chakula cha kidomo? Je, ni kuhusu mambo haya? Hii ni sehemu ya mienendo, lakini hatutaki kuzungumzia haya hapa. Tunataka tu kuzungumza kuhusu mawazo ambayo mienendo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inasababisha watu kutenda duniani, malengo ya maisha na mtazamo ambao inaleta kwa watu. Hii ni muhimu sana: inaweza kudhibiti na kushawishi hali ya akili ya mwanadamu. Moja baada ya nyingine, hii mienendo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote. Hivyo mienendo hii ni ipi? Huwezi kuona mienendo hii kwa macho. Wakati upepo wa mwenendo unavuma, pengine ni idadi ndogo ya watu tu watakuwa waanzisha mitindo. Wanaanza kwa kufanya jambo la aina hii, kukubali wazo la aina hii ama mtazamo wa aina hii. Wengi wa watu, hata hivyo, katikati ya kutojua kwao, bado watazidi kuambukizwa, kufanywa wenyeji na kuvutia aina hii ya mwenendo, hadi wote bila kujua na bila kujitolea wanamkubali, na wote wanazama na kudhibitiwa na yeye. Kwa mwanadamu ambaye si wa mwili na akili timamu, ambaye kamwe hajui ukweli, ambaye hawezi kusema tofauti kati ya vitu vyema na hasi, mienendo ya aina hii moja baada ya nyingine inawafanya wote wawe radhi kukubali mienendo hii, mtazamo wa maisha, filosofia za maisha na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani juu ya jinsi ya kukaribia maisha na jinsi ya kuishi ambayo Shetani amewapa. Hawana nguvu, wala hawana uwezo, wala ufahamu wa kupinga. Kwa hivyo hii mienendo hasa ni nini? Nimechukua mfano rahisi ambao mnaweza kuja kuelewa. Kwa mfano, watu wa kale waliendesha biashara zao kwa njia ambayo haikudanganya wazee wala vijana, na ambayo iliuza bidhaa kwa bei sawa bila kujali aliyekuwa akinunua. Je, dokezo la dhamiri na ubinadamu haliwasilishwi hapa? Wakati watu walitumia aina hii ya imani walipokuwa wakifanya biashara zao, tunaweza kusema kwamba bado walikuwa na baadhi ya dhamiri, baadhi ya ubinadamu wakati huo? (Ndiyo.) Lakini na mahitaji ya mwanadamu ya kiasi kinachopanda daima cha pesa, watu bila kujua walikuja kupenda pesa, hupenda faida na hupenda raha zaidi na zaidi. Kwa hivyo watu walikuja kuona pesa kuwa muhimu zaidi? Wakati watu wanaona pesa kuwa muhimu zaidi, bila kujua wanapuuza sifa, umashuhuri wao, ufahari, na uadilifu wao; wanapuuza mambo haya yote, sivyo? Unapojihusisha katika biashara, unaona mtu mwengine akichukua mbinu tofauti na kutumia njia mbalimbali kuibia watu na kuwa tajiri. Ingawa pesa iliyopatwa ni faida iliyopatwa vibaya, wanakuwa tajiri zaidi na zaidi. Familia yao yote inajihusisha na biashara sawa na wewe, lakini wanafurahia maisha kukuliko, na unahisi vibaya, ukisema: “Mbona siwezi kufanya hivyo? Mbona siwezi kupata kama wapatavyo? Ni lazima nifikirie njia ya kupata pesa zaidi, kufanya biashara yangu kufanikiwa.” Kisha unafikiria hili. Kulingana na mbinu ya kawaida ya kutengeneza pesa, kutodanganya wazee wala vijana na kuuza vitu kwa bei sawa kwa wote, pesa unayotengeneza ni kwa dhamiri nzuri, lakini haiwezi kukufanya kuwa tajiri haraka. Hata hivyo, chini ya tamaa ya kutengeneza faida, kufikiria kwako kunapitia mabadiliko taratibu. Katika mabadiliko haya, kanuni zako za tabia pia zinaanza kubadilika. Wakati unamdanganya mtu kwa mara ya kwanza, unapomlaghai mtu kwa mara ya kwanza, una mashaka, ukisema “Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena. Siwezi kudanganya watu. Kudanganya watu kutapata tu adhabu na kutaleta majanga kwangu! Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena.” Unapomdanganya mtu kwa mara ya kwanza, moyo wako una aibu kiasi; hii ndiyo kazi ya dhamiri ya mwanadamu—kuwa na aibu na kukushutumu, ili ihisi kuwa siyo asili wakati unamdanganya mtu. Lakini baada ya wewe kufanikiwa kumdanganya mtu unaona kwamba sasa una pesa zaidi kuliko awali, na unafikiria mbinu hii inaweza kuwa ya manufaa sana kwako. Licha ya maumivu madogo ndani ya moyo wako, bado unahisi kujipongeza kwa “mafanikio” yako, na unahisi kuridhishwa kidogo na wewe mwenyewe. Kwa mara ya kwanza, unakubali tabia yako mwenyewe na unakubali uwongo wako mwenyewe. Baadaye, wakati mwanadamu amechafuliwa na kudanganya huku, ni sawa na mtu ambaye anahusika na kamari na kisha anakuwa mchezaji kamari. Katika kutoelewa, anapenda tabia yake ya kudanganya na anaikubali. Katika kutoelewa, anachukua kudanganya kuwa tabia halali ya kibiashara, na anachukua kudanganya kuwa mbinu ya manufaa zaidi ya kusalimika kwake na maisha yake; anafikiria kwamba kwa kufanya hivi anaweza kuwa tajiri haraka. Mwanzoni mwa mchakato huu watu hawawezi kukubali tabia ya aina hii, wanadharau tabia hii na njia hii ya kufanya mambo, hadi wanapoijaribu na kuijaribu kwa njia yao wenyewe, kibinafsi na moja kwa moja, na kisha mioyo yao inaanza kubadilika polepole. Kwa hivyo mabadiliko haya ni yapi? Ni kukubali na kukiri mwenendo huu, kukiri na kukubali wazo la aina hii lililoingizwa kwako na mwenendo wa jamii. Katika kutoelewa, unahisi kwamba usipodanganya katika biashara basi utapata hasara, kwamba usipodanganya basi utakuwa umepoteza kitu. Bila kujua, kudanganya huku kunakuwa nafsi yako, tegemeo kuu lako, na pia kunakuwa aina ya tabia ambayo ni kanuni isiyoweza kutupiliwa mbali katika maisha yako. Baada ya mwanadamu kukubali tabia hii na kufikiria huku, je, moyo wa mwanadamu unapitia mabadiliko? Moyo wako umebadilika, basi uadilifu wako umebadilika? Ubinadamu wako umebadilika? (Ndiyo.) Basi dhamiri yako imebadilika? (Ndiyo.) Uwepo wote wa mwanadamu unapitia mabadiliko bora, kutoka kwa mioyo yao hadi kwa mawazo yao, hadi kwa kiwango ambapo wanabadilika kutoka ndani hadi nje. Mabadiliko haya yanakuweka mbali na mbali zaidi kutoka kwa Mungu, na unakuwa na uafikiano zaidi na zaidi na Shetani, unakuwa sawa zaidi na zaidi na yeye.
Sasa mienendo hii ya kijamii ni rahisi kwako kuelewa. Nilichagua tu mfano rahisi, mfano unaoonekana kawaida ambao watu watakuwa wanajua. Hii mienendo ya kijamii ina ushawishi mkubwa kwa watu? (Ndiyo!) Kwa hivyo hii mienendo ya kijamii ina athari inayodhuru kwa kina kwa watu? (Ndiyo!) Athari ya kudhuru kwa kina kwa watu. Shetani hutumia moja ya mienendo hii ya kijamii baada ya nyingine kupotosha nini ya mwanadamu? (Dhamiri, akili, ubinadamu, maadili.) Nini tena? (Mtazamo wa mwanadamu wa maisha.) Je, inasababisha kuzorota polepole ndani ya watu? (Ndiyo.) Shetani hutumia hii mienendo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mienendo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu, ni nini basi mwanadamu anakuwa? Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Hii ni kwa sababu ya mwelekeo kisaikolojia upi katika moyo wa mwanadamu? Ni kipi ambacho mwanadamu anatetea? Mwanadamu huanza kupenda uwovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka. Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mienendo ya aina hii, maarifa ambayo wamefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Je, desturi ya kitamaduni na ushirikina wanayojua yanaweza kuwasaidia kutupilia mbali hii hatari ya kutisha? Je, maadili ya desturi na sherehe za desturi ambazo mwanadamu huelewa zinaweza kumsaidia kujizuia? Chukua Fasihi Bora ya Herufi Tatu, kwa mfano. Inaweza kusaidia watu kutoa miguu yao katika mchanga unaomeza wa mienendo hii?[b] (La, haiwezi.) Kwa njia hii, mwanadamu anakuwa nini zaidi na zaidi? Zaidi na zaidi mwovu, mwenye kiburi, mwenye kushusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote kati ya jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa udanganyifu, yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia njia za udanganyifu na mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanadanganya, wanalaghai, na kuwa wakatili ili kukamata riziki zao; wanashinda vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha? (Ndiyo.) Baada ya kunisikia Nikiongea kuhusu vitu hivi sasa, hamfikiri kwamba inatisha kuishi miongoni mwa aina hii ya umati, katika dunia hii na katika mazingira haya ambayo Shetani amepotosha? (Ndiyo.) Kwa hivyo mmewahi kujihisi kuwa wenye kusikitisha? Lazima mnaihisi kiasi sasa. (Ndiyo.) Kwa kusikiza sauti zenu, inaonekana kana kwamba mnafikiria “Shetani hutumia njia nyingi mbalimbali kumpotosha mwanadamu. Anakamata kila fursa na yupo kila mahali tunageukia. Mwanadamu bado anaweza kuokolewa? Bado kuna matumaini kwa wanadamu? Wanadamu wanaweza kujiokoa? (La.) Je, Mfalme Mkuu wa Jade anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Confucius anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Guanyin Bodhisattva anaweza kumwokoa mwanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nani anayeweza kumwokoa mwanadamu? (Mungu.) Watu wengine, hata hivyo, wataibua katika mioyo yao maswali kama: “Shetani anatudhuru kwa kiasi kikubwa sana, kwa hasira sana basi hatuna matumaini ya kuishi, wala imani katika kuishi. Sote tunaishi miongoni mwa upotovu na kila mtu anampinga Mungu hata hivyo, ili mioyo yetu sasa yote imekuwa baridi kabisa. Kwa hivyo wakati Shetani anatupotosha, Mungu yuko wapi? Mungu anafanya nini? Chochote Mungu anatufanyia kamwe hatukihisi!” Watu wengine wanapata hasara bila kuepukika, na bila kuepukika wanahisi kuvunjika moyo kiasi. Kwenu, kichocheo hiki, hisia hii ni ya kina sana kwa sababu vyote ambavyo Nimekuwa nikisema vimekuwa kuwafanya watu kuja kuelewa polepole, kuhisi zaidi na zaidi kwamba hawana matumaini, kuhisi zaidi na zaidi kwamba wameachwa na Mungu. Lakini usijali. Mada yetu ya kushiriki leo, “uovu wa Shetani,” siyo dhamira yetu ya kweli. Kuongea kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, hata hivyo, lazima kwanza tuongee kuhusu jinsi Shetani anampotosha mwanadamu na uovu wa Shetani ili kuifanya kuwa wazi zaidi kwa watu, mwanadamu sasa yuko katika hali ya aina gani na ni kwa kiwango kipi hasa mwanadamu amepotoshwa. Lengo moja la kuongea juu ya hili ni kuruhusu watu kujua uovu wa Shetani, ilhali jingine ni kuwaruhusu watu kuelewa kwa kina zaidi utakatifu ni nini. Mnaelewa sasa, sivyo?
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni