Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)
Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita?(Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu. Ni kupitia tu kwa mawasiliano ya Mungu ya kipengele hiki cha ukweli ndipo ninaona sasa kwamba uhai wa vitu vyote unapewa na Mungu, kwamba Mungu anatengeneza sheria hizi, na kwamba Anavilea vitu vyote. Kutokana na uumbaji Wake wa vitu vote ninaona upendo wa Mungu na kuhisi kwamba Mungu ni chanzo cha vitu vyote.) Mm, wakati uliopita, kimsingi tuliwasiliana kuhusu uumbaji wa Mungu wa vitu vyote na jinsi Aliunda sheria na kanuni kwa ajili ya vitu hivyo. Chini ya sheria hizi na chini ya kanuni hizi, vitu vyote huishi na kufa na wanadamu na kuishi pamoja kwa amani na wanadamu chini ya utawala wa Mungu na machoni pa Mungu. Tulizungumzia nini kwanza? Mungu aliumba vitu vyote na akatumia mbinu Zake kutunga sheria za ukuaji wa vitu vyote, na vilevile njia na mpangilio wa ukuaji wa vitu hivyo, na pia alitunga njia za kuwepo kwa vitu vyote duniani, ili viweze kuishi kwa kuendelea na kutegemeana. Kwa mbinu na sheria hizi, vitu vyote vinaweza kuwepo na kukua katika nchi hii kwa ufanisi na kwa amani. Ni kwa kuwa tu na mazingira kama haya ndipo wanadamu wanaweza kuwa na makao na mazingira ya kuishi yaliyo thabiti, na chini ya uongozi wa Mungu, waendelee kukua na kusonga mbele, kukua na kusonga mbele.
Wakati uliopita tulijadili kuhusu wazo la msingi la Mungu kupeana vitu vyote. Mungu kwanza huvipa vitu vyote kwa njia hii ili vitu vyote viwepo na kuishi kwa ajili ya wanadamu. Mazingira kama haya yapo kwa ajili ya sheria zilizotungwa na Mungu. Ni tu kwa Mungu kudumisha na kusimamia sheria kama hizi ndio wanadamu wana mazingira ya kuishi waliyonayo sasa. Tulichozungumzia wakati uliopita ni hatua kubwa kutoka kwa ufahamu wa Mungu tuliozungumzia awali. Kwa nini hatua kama hiyo ipo? Kwa sababu tulipozungumzia hapo awali kuhusu kuanza kumjua Mungu, tulikuwa tunajadili katika eneo la Mungu kuwaokoa na kuwasimamia wanadamu—yaani, uokoaji na usimamizi wa watu waliochaguliwa na Mungu—kuhusu kumjua Mungu, matendo ya Mungu, tabia Yake, kile Anacho na Alicho, makusudi Yake, na vile Anampa mwanadamu ukweli na uhai. Lakini mada tuliyozungumza kuihusu wakati uliopita haikujikita tu katika mipaka ya Biblia na katika eneo la Mungu kuwaokoa watu Wake waliochaguliwa. Badala yake, ilitoka nje ya eneo hili, nje ya Biblia, na nje ya mipaka ya hatua tatu za kazi ambayo Mungu anafanya kwa watu Wake waliochaguliwa na kujadili Mungu Mwenyewe. Hivyo basi ukisikia sehemu hii ya mawasiliano Yangu, lazima usiwekee mipaka ufahamu wako wa Mungu kwa Biblia na hatua tatu za kazi ya Mungu. Badala yake, unahitaji kuuweke wazi mtazamo wako na uone matendo ya Mungu na kile Anacho na alicho miongoni mwa vitu vyote, na vile Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote. Kupitia kwa mbinu hii na juu ya msingi huu, unaweza kuona vile Mungu anapeana vitu vyote. Hii inawawezesha wanadamu kuelewa kwamba Mungu ni chanzo halisi cha uhai kwa vitu vyote na kwamba huu ni utambulisho halisi wa Mungu Mwenyewe. Hiyo ni kusema, utambulisho wa Mungu, hadhi na mamlaka na kila kitu Chake havilengwi tu kwa wale wanaomfuata Yeye wakati huu—kumaanisha havilengwi tu kwa ninyi watu—bali kwa vitu vyote. Basi ni nini eneo la vitu vyote? Eneo la vitu vyote ni pana sana. Ninatumia “vitu vyote” kueleza eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote kwa sababu Ninataka kuwaambia kwamba vitu vinavyotawaliwa na Mungu si vile mnavyoweza tu kuona kwa macho yenu, bali vinahusisha ulimwengu yakinifu ambao watu wote wanaweza kuuona, na vilevile ulimwengu mwingine usioweza kuonekana kwa macho ya binadamu nje ya ulimwengu yakinifu, na zaidi unahusisha anga na sayari nje ya mahali ambapo wanadamu wapo sasa. Hilo ni eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, na wazo hili kwamba Mungu anatawala kila kitu. Eneo la utawala wa Mungu juu ya vitu vyote ni pana zaidi. Kwenu ninyi, mnachopaswa kuelewa, mnachopaswa kuona, na kutoka kwa vitu mnavyopaswa kupata maarifa—hivi ndivyo kila mmoja wenu anayeketi hapa anahitaji na ni lazima aelewe, aone, na awe na hakika navyo. Ingawa eneo la hivi “vitu vyote” ni pana, Sitawaambia kuhusu eneo msiloweza kuona kabisa au msiloweza kukutana nalo. Nitawaambia tu kuhusu eneo ambalo binadamu wanaweza kukutano nalo, wanaweza kuelewa, na wanaweza kufahamu, ili kila mmoja aweze kuhisi maana halisi ya kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Hivyo, chochote Ninachowasilisha kwenu hakitakuwa maneno matupu. Wakati uliopita, Nilitumia mbinu ya kuhadithia ili kutoa maelezo rahisi ya jumla ya mada hii “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” ili muwe na ufahamu wa msingi wa jinsi Mungu huvipa vitu vyote. Ni nini kusudi la kuwafundisha kidogokidogo wazo hili la msingi? Ni kuwafanya mjue kwamba, nje ya Biblia na hatua tatu za kazi Yake, Mungu pia anafanya hata kazi nyingi zaidi ambayo wanadamu hawawezi kuiona au kukutana nayo. Kazi kama hiyo inatendwa binafsi na Mungu. Kama Mungu angekuwa anaongoza tu watu Wake waliochaguliwa kwenda mbele, bila hii kazi iliyo nje ya kazi Yake ya usimamizi, basi ingekuwa vigumu sana kwa ubinadamu huu, pamoja na ninyi nyote, kuendelea kusonga mbele, na ubinadamu huu na ulimwengu huu haungeweza kuendelea kukua. Huo ndio umuhimu wa kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” Ninachowasilisha kwenu siku hii.
1. Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu
Tumejadili mada nyingi na maudhui yanayohusiana na kirai hiki “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” lakini mnajua ndani ya mioyo yenu ni vitu vipi Mungu anatoa kwa wanadamu mbali na kuwapa ninyi neno Lake na kutenda kazi Yake ya kuadibu na hukumu kwenu? Watu wengine huenda wakasema, “Mungu hunipa neema na baraka, na kunipa nidhamu, faraja, na utunzaji na ulinzi kwa kila njia iwezekanayo.” Wengine watasema, “Mungu hunipa chakula cha kila siku na kinywaji,” ilhali wengine hata watasema, “Mungu hunipa kila kitu.” Kuhusu vitu hivi ambavyo watu wanaweza kukutana navyo katika maisha yao ya kila siku, nyote mnaweza kuwa na majibu yanayohusiana na matukio mnayopitia katika maisha yenu ya kimwili. Mungu humpa kila mtu vitu vingi, ingawa tunachojadili leo hakijajikita tu katika mipaka ya eneo la mahitaji ya watu ya kila siku, lakini kinamruhusu kila mmoja wenu kutazama mbali zaidi. Kutokana na mtazamo mkubwa, kwa vile Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, Anadumisha vipi uhai wa vitu vyote? Ili vitu vyote viweze kuendelea kuwepo, ni nini ambacho Mungu huleta kwa vitu vyote ili kudumisha kuwepo kwa vitu hivyo na kudumisha sheria za kuwepo kwa vitu hivyo? Hilo ndilo wazo kuu la kile tunachojadili leo. Je, mnaelewa Nilichosema? Je, mnaweza kuendelea sawa na vile Ninavyozungumza haraka? (Ndiyo.) Kwa vile sasa nina hakika mnasikiliza, Nitaendelea. Mada hii huenda ikawa msiyofahamu sana, lakini Sitazungumza kuhusu mafundisho ya dini yoyote ambayo ni ya kina sana. Nitajitahidi kuwafanya nyote muelewe baada ya kusikiliza. Hamhitaji kuhisi mzigo wowote—mnachotakiwa kufanya tu ni kusikiliza kwa makini. Kwa hali yoyote, bado Ninahitaji kuisisitiza zaidi kidogo: Ninazungumza juu ya mada gani? Niambieni. (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Basi ni vipi ambavyo Mungu huvipa vitu vyote? Ni nini ambacho Mungu huvipa vitu vyote? Kwa nini inaweza kusemwa kwamba “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote”? Je, mna dhana na mawazo yoyote kuhusu hili? Inaonekana kwamba mada hii Ninayozungumzia kimsingi haileti kinachotumainiwa ndani ya mioyo yenu na ndani ya akili zenu. Lakini Natumai mtaweza kuunganisha mada hii pamoja na vitu Ninavyoenda kuzungumzia kwa matendo ya Mungu, na sio kuviunganisha kwa ufahamu wowote au kuvihusisha na desturi zozote za binadamu au uchunguzi. Ninazungumza tu kuhusu Mungu na kuhusu Mungu Mwenyewe. Hilo ni pendekezo Langu kwenu. Je, mnaelewa? (Ndio.)
Mungu ametoa vitu vingi kwa wanadamu. Nitaanza kwa kuzungumza kuhusu kile ambacho watu wanaweza kuona, yaani, wanachoweza kuhisi. Hivi ni vitu ambavyo watu wanaweza kuvielewa na wanaweza kukubali. Hivyo basi kwanza tuanze na ulimwengu yakinifu kujadili kile ambacho Mungu amewapa wanadamu.
(1) Hewa
Kwanza, Mungu aliumba hewa ili mwanadamu aweze kupumua. Je, ‘hewa’ hii si hewa ya maisha ya kila siku ambayo wanadamu hukutana nayo kila mara? Je, hewa hii si kitu ambacho wanadamu hutegemea kila wakati, hata wanapolala? Hewa ambayo Mungu aliumba ina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu: ni kijenzi muhimu cha kila pumzi yao na cha uhai wenyewe. Kiini hiki, kinachoweza tu kuhisiwa lakini hakionekani, kilikuwa zawadi ya Mungu ya kwanza kwa vitu vyote. Baada ya kuumba hewa, je, Mungu aliacha kufanya kazi? Kuna vipengele vya haya visivyoweza kufikiriwa na watu. Baada ya kuumba hewa, uzito sahihi na kiasi cha hewa vilitakiwa kuandaliwa kwa hali maalum kwa wanadamu kwa wao kuendelea kuishi. Kuhusu uzito, kwanza kuna jambo la kadiri ya oksijeni. Hili ni swali la fizikia. Mungu alikuwa anafikiria nini alipoumba hewa? Kwa nini Mungu aliumba hewa, na fikira Yake ilikuwa gani? Wanadamu wanahitaji hewa, na wanahitaji kupumua. Kwanza kabisa, uzito wa hewa unapaswa kukubaliana na pafu la mwanadamu. Kuna yeyote anayejua uzito wa hewa? Hili si jambo ambalo watu wanahitaji kujua; hakuna haja ya kujua hili. Kuwa na wazo la jumla ni vizuri—hatuhitaji namba kamili kuhusiana na uzito wa hewa. Kwanza, Mungu aliumba hewa yenye uzito ambao ungefaa zaidi mapafu ya mwanadamu kupumua—imerekebishiwa upumuaji wa mwanadamu. Yaani, pumzi inapovutwa, hewa ina uzito usiodhuru mwili. Hili ndilo wazo kuhusu uzito wa hewa. Kimsingi, yaliyomo ndani ya hewa si sumu kwa wanadamu na hivyo hayatadhuru mapafu na mwili. Mungu alihitaji kuzingatia haya yote. Mungu alihitaji kuzingatia kwamba hewa ambayo wanadamu wanapumua inapaswa kuingia na kutoka taratibu, na kwamba, baada ya kuvuta hewa, kadiri na kiasi cha hewa vinapaswa kuhakikisha damu pamoja na hewa chafu ndani ya mapafu na mwili vingejenga na kuvunjavunja kemikali mwilini vizuri, na pia kwamba hewa hiyo haipaswi kuwa na vijenzi vyovote vya sumu. Kuhusu viwango hivi viwili, Sitaki kuwalisha mafungu ya maarifa, lakini badala yake nataka tu mjue kwamba Mungu alikuwa na mchakato maalum wa mawazo akilini mwake Alipoumba kila kitu—bora zaidi. Kuhusu kiasi cha vumbi katika hewa, kiasi cha vumbi, mchanga na uchafu duniani, na vilevile vumbi inayoelekea chini kutoka angani, Mungu alikuwa na mpango wa vitu hivi pia—njia ya kuondoa au kutatua vitu hivi. Huku kukiwa na vumbi kiasi, Mungu aliiumba ili vumbi isidhuru mwili na upumuaji wa mwanadamu, na kwamba vipande vya vumbi viwe na ukubwa usiokuwa na madhara kwa mwili. Je, uumbaji wa Mungu wa hewa haukuwa wa ajabu? (Ndiyo.) Je, ulikuwa rahisi kama kupuliza pumzi ya hewa kutoka kinywani Mwake? (La.) Hata katika uumbaji wake wa vitu rahisi sana, maajabu ya Mungu, akili Zake, mawazo Yake, na hekima Yake vyote ni dhahiri. Je, Mungu ni mwenye uhalisi? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema, hata katika kuumba kitu rahisi, Mungu alikuwa akifikiria kuhusu mwanadamu. Kwanza kabisa, hewa ambayo wanadamu hupumua ni safi, yaliyomo si ya sumu na yanafaa kwa upumuaji wa mwanadamu na hayasababishi madhara kwa wanadamu, na uzito huo umekadiriwa kwa upumuaji wa wanadamu. Hewa hii ambayo wanadamu huvuta pumzi na kutoa ni muhimu kwa mwili wao na, umbo lao. Ili wanadamu waweze kupumua kwa uhuru, bila kizuizi au wasiwasi. Waweze kupumua kwa kawaida. Hewa ni kile ambacho Mungu aliumba mwanzo na ambacho ni cha lazima kwa upumuaji wa wanadamu.
(2) Halijoto
Kitu cha pili ni halijoto. Kila mtu anajua halijoto ni nini. Halijoto ni kitu ambacho mazingira yanayofaa kuishi kwa wanadamu ni lazima yawe nacho. Ikiwa halijoto iko juu sana, tuseme ikiwa halijoto iko juu zaidi ya nyuzi 40 Selisiasi, basi itakuwa yenye taabu kwa wanadamu kuishi. Je, haitakuwa ya kumaliza sana? Je, na halijoto ikiwa chini sana, na kufikia nyuzi hasi 40 Selisiasi? Wanadamu hawataweza pia kuistahimili. Kwa hiyo, Mungu alikuwa mwangalifu sana katika kuviweka vipimo hivi vya halijoto. Vipimo vya halijoto ambavyo mwili wa mwanadamu unaweza kufanya mabadiliko kimsingi ni nyuzi hasi 30 Selisiasi hadi nyuzi 40 Selisiasi. Hiki ndicho kipimo cha halijoto cha msingi kutoka kaskazini mpaka kusini. Katika maeneo ya baridi, halijoto inaweza kufika nyuzi hasi 50 Selisiasi. Eneo kama hilo si mahali ambapo Mungu anamruhusu mwanadamu kuishi. Mbona kuna maeneo ya baridi hivyo? Katika hayo kuna hekima na makusudi ya Mungu. Hakuruhusu kusonga karibu na sehemu hizo. Mungu hulinda sehemu zilizo na joto sana na baridi sana, kumaanisha Hayuko tayari kumruhusu mwanadamu kuishi huko. Si kwa wanadamu. Kwa nini akaruhusu sehemu kama hizo kuwepo duniani? Ikiwa Mungu hangemruhusu mwanadamu kuishi au kuwepo huko, basi kwa nini akaziumba? Hekima ya Mungu imo humo. Yaani, halijoto ya msingi ya mazingira ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu pia imerekebishwa na Mungu vya kutosha. Kuna sheria hapa pia. Mungu aliumba vitu vingine kusaidia kudumisha halijoto kama hiyo, kudhibiti halijoto hiyo. Ni vitu gani vinatumiwa kudumisha halijoto hii? Kwanza kabisa, jua linaweza kuwaletea watu uvuguvugu, lakini watu hawataweza kustahimili iwapo ni vuguvugu sana. Je, kuna kifaa chochote duniani kinachoweza kusonga karibu na jua? (La.) Mbona? Ni joto sana. Kitayeyuka. Kwa hiyo, Mungu pia ametengeneza kipimo maalum cha umbali wa jua kutoka kwa wanadamu. Mungu ana kiwango cha umbali huu. Vilevile kuna Ncha ya kusini na Ncha ya Kaskazini za dunia. Kuna nini katika Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini? Kote kuna mito ya barafu. Wanadamu wanaweza kuishi juu ya mito ya barafu? Inafaa kuishi kwa wanadamu? (La.) La, hivyo hutaenda huko. Kwa vile huendi katika Ncha za Kusini na Kaskazini, mito ya barafu itahifadhiwa, na itaweza kufanya wajibu wake, ambao ni kudhibiti halijoto. Unaelewa? Ikiwa hakuna Ncha za Kusini na Kaskazini na jua linawaka juu ya dunia kila wakati, basi watu wote juu ya dunia watakufa kutokana na joto. Je, Mungu hutumia tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto? La, Hatumii tu vitu hivi viwili kudhibiti halijoto inayofaa kuishi kwa wanadamu. Pia kuna kila aina za viumbe vyenye uhai, kama vile nyasi juu ya mbuga za malisho, aina mbalimbali za miti na kila aina ya mimea iliyo ndani ya misitu. Vinafyonza joto la jua na kusanisi nishati ya joto ya jua kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Pia kuna vyanzo vya maji, kama vile mito na maziwa. Sehemu ya juu ya mito na maziwa si kitu kinachoweza kuamuliwa na yeyote. Je, kuna yeyote anayeweza kudhibiti kiasi cha maji yaliyo juu ya dunia, wapi maji hayo yanatiririka, mwelekeo wa kutiririka huko, wingi wa maji hayo, au spidi ya mtiririko huo? Hakuna anayeweza kuidhibiti. Mungu pekee ndiye ajuaye. Vyanzo hivi mbalimbali vya maji, yakiwemo maji ya chini ya ardhi na mito na maziwa yaliyo juu ya ardhi ambayo watu wanaweza kuona, yanaweza pia kurekebisha halijoto ambayo wanadamu wanaishi ndani. Mbali na hayo, kuna kila aina ya uumbaji wa kijiografia, kama vile milima, tambarare, korongo kuu na ardhi ya majimaji. Sehemu ya juu na ukubwa wa uumbaji huu mbalimbali wa kijiografia vinaweza vyote kudhibiti halijoto. Kwa mfano, ikiwa mlima huu una nusu kipenyo cha kilomita 100, kilomita hizi 100 zitakuwa na athari ya kilomita 100. Lakini kuhusu safu za milima na korongo kuu ngapi kama hizo ambazo Mungu ameumba juu ya dunia, hili ni jambo ambalo Mungu amelifikiria kabisa. Kwa maneno mengine, nyuma ya kuwepo kwa kila kitu kilichoumbwa na Mungu kuna hadithi, na pia ina hekima na mipango ya Mungu. Tuseme, kwa mfano, misitu na kila aina ya mimea—sehemu ya juu na ukubwa wa sehemu ambamo vinakua haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote, wala mwanadamu yeyote hana usemi wa mwisho kuhusu vitu hivi. Kiasi cha maji ambayo vinafyonza, kiasi cha nishati ya joto ambayo vinafyonza kutoka kwa jua pia haviwezi kudhibitiwa na mwanadamu yeyote. Vitu hivi vyote viko katika eneo la kile kilichopangwa na Mungu alipoumba vitu vyote.
Ni kwa sababu tu ya upangaji wa makini, fikira, na utaratibu wa Mungu katika vipengele vyote ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Kwa hiyo, kila kitu ambacho mwanadamu anakiona kwa macho yake, kama vile jua, au Ncha za Kusini na Kaskazini ambazo watu mara nyingi husikia kuzihusu, vilevile viumbe mbalimbali vilivyo hai juu na chini ya ardhi na ndani ya maji, na sehemu za juu zenye misitu na aina zengine za mimea, na vyanzo vya maji, mikusanyiko mbalimbali ya maji, kuna kiasi gani cha maji chumvi na maji baridi, kuongezea mazingira mbalimbali ya kijiografia—Mungu hutumia vitu hivi kudumisha halijoto ya kawaida kwa kuishi kwa mwanadamu. Hii ni thabiti. Ni kwa sababu tu Mungu ana fikira kama hizi ndio mwanadamu anaweza kuishi katika mazingira yaliyo na halijoto ya kufaa hivyo. Haiwezi kuwa baridi zaidi wala joto zaidi: sehemu zenye joto zaidi na ambapo halijoto inazidi kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kubadilikia bila shaka hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili yako. Sehemu zenye baridi zaidi na ambapo halijoto ni ya chini zaidi; sehemu ambazo, punde tu wanadamu wanapowasili, zitawafanya wagande sana baada ya dakika chache mpaka wasiweze kuzungumza, ubongo wao utaganda, wasiweze kufikiri, na hatimaye watakosa hewa—sehemu kama hizo pia hazijatayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Haijalishi ni aina gani ya uchunguzi wanadamu wanataka kufanya, au kama wanataka kuvumbua au wanataka kutengua mipaka hiyo—haijalishi watu wanafikiria nini, hawataweza kamwe kuzidi mipaka ya kile ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kubadilikia. Hawataweza kuondoa mipaka hiyo ambayo Mungu alimuumbia mwanadamu. Kwa vile Mungu aliwaumba wanadamu, Mungu anajua bora zaidi ni halijoto gani mwili wa mwanadamu unaweza kubadilikia. Je, wanadamu wenyewe wanajua? (La.) Mbona unasema wanadamu hawajui? Ni mambo gani ya upumbavi ambayo wanadamu wamefanya? Je, hakujakuwa na watu wachache ambao kila mara wanataka kushindana na Ncha za Kaskazini na Kusini? Kila mara wanataka kwenda huko kumiliki ardhi hiyo, ili waweze kukita mizizi na kuiendeleza. Je, hiki si kitendo cha kujiangamiza? (Ndiyo.) Tuseme umechunguza kikamilifu Ncha za Kusini na Kaskazini. Lakini hata kama unaweza kubadilikia halijoto hiyo, je, kubadilisha mazingira ya kuishi na mazingira ya kuendelea kuishi ya Ncha za Kusini na Kaskazini kungemfaidi mwanadamu kwa njia yoyote? Je, utafurahi ikiwa barafu ya Ncha za Kusini na Kaskazini itayeyuka? Hili ni la kushangaza. Ni kitendo cha upuuzi. Wanadamu wana mazingira wanayoweza kuendelea kuishi ndani, lakini hawawezi tu kukaa hapa kimya na kwa uangalifu, na wanapaswa kwenda wasikoweza kuendelea. Kwa nini ni hivyo? Wamechoshwa na kuishi katika halijoto hii ya kufaa. Wamefurahia baraka nyingi sana. Mbali na hayo, haya mazingira ya kuishi ya kawaida yameharibiwa kiasi sana na wanadamu, hivyo wanaweza basi kwenda kwa Ncha ya Kusini na Ncha ya Kaskazini ili wafanye madhara mengi zaidi au kujihusisha katika “kusudi,” fulani ili waweze kuwa “watangulizi” wa aina fulani. Si huu ni upumbavu? Chini ya uongozi wa babu yao Shetani, wanadamu hawa wanaendelea kufanya kitu kimoja cha upuuzi baada ya kingine, wakiharibu bila hadhari na kwa utukutu makao mazuri ambayo Mungu aliwaumbia wanadamu. Hili ndilo Shetani alifanya. Zaidi ya hayo, kwa kuona kwamba kuendelea kuishi kwa wanadamu duniani kuko katika hatari kidogo, watu wengi sana wanataka kutafuta njia za kwenda kuishi juu ya mwezi, kutafuta njia ya kuondoka kwa kuona ikiwa wanaweza kuishi huko. Hatimaye, ni nini kinakosekana huko? (Oksijeni.) Je, wanadamu wanaweza kuendelea kuishi bila oksijeni? (La.) Kwa vile mwezi hauna oksijeni, si mahali ambapo mwanadamu anaweza kuishi huko, ilhali mwanadamu anaendelea kutaka kwenda huko. Hii ni nini? (Ni kujiangamiza na kutafuta taabu.) Ni kujiangamiza, sivyo? Ni mahali pasipo na hewa, na halijoto haifai kwa kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hivyo hapajatayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu.
Halijoto ambayo tumezungumzia ni kitu ambacho watu wanaweza kukutana nacho katika maisha yao ya kila siku. “Hali ya hewa ni nzuri sana leo, nyuzi 23 Selisiasi. Hali ya hewa ni angavu, anga haina mawingu, na hewa inaburudisha. Vuta pumzi ya hewa safi. Jua linawaka. Jinyoshe chini ya mwanga wa jua. Ninajisikia vizuri!” Au “Leo hali ya hewa ni baridi sana. Ukinyosha nje mikono yako itaganda mara moja. Kuna baridi kali, hivyo usikae nje muda mrefu. Harakisha na urudi, usije ukaganda!” Halijoto ni kitu ambacho miili yote ya wanadamu inaweza kuhisi, lakini hakuna anayefikiria vile halijoto hii iliumbwa, au ni nani anasimamia na kudhibiti halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu. Hiki ndicho tunaanza kujua sasa. Je, kuna hekima ya Mungu katika hili? Je, kuna kitendo cha Mungu katika hili? (Ndiyo.) Ukifikiria kwamba Mungu aliumba mazingira yenye halijoto ya kufaa kuishi kwa wanadamu, je, hii ni njia moja ambayo Mungu huvipa vitu vote? Ndiyo kweli. Hii inaonyesha kwamba upaji na usimamiaji wa vitu vyote na Mungu kweli ni wa utendaji!
(3) Sauti
Kitu cha tatu ni sauti. Hiki pia ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Sauti iliumbika Mungu alipoumba vitu vote. Mungu aliishughulikia vizuri sana wakati huo. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Kama Mungu hangeshughulikia suala la sauti vizuri, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Pia inaweza kusemwa kwamba viumbe vyote vyenye uhai haviwezi kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Hivyo hiki ni kitu gani? Ni sauti. Mungu aliumba kila kitu, na kila kitu kinaishi mikononi mwa Mungu. Machoni pa Mungu, vitu vyote vinasonga na vinaishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kuwepo kwa kila mojawapo kuna thamani na maana. Yaani, vyote vina umuhimu katika kuwepo kwao. Kwa hali yoyote, miongoni mwa vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, kila kitu kina uhai; kwa kuwa vyote viko hai na vinasonga, vitatoa sauti kwa kawaida. Kwa mfano, dunia daima inazunguka, jua daima linazunguka, na mwezi daima unazunguka pia. Sauti daima zinatolewa katika maisha na miendo ya vitu vyote. Vitu juu ya dunia pia daima vinazaa na kukua na kusonga. Kwa mfano, misingi ya milima inasonga na kubadilisha nafasi, huku vitu vyote vyenye uhai katika kina cha bahari vinasonga na kuogelea. Vitu hivi vyenye uhai, vitu vyote machoni pa Mungu, vyote daima, kwa kawaida, na mara kwa mara viko katika mwendo. Hivyo ni nini kinaletwa na uzalishaji wa siri na maendeleo na miendo ya vitu hivyo? Sauti za nguvu. Mbali na dunia, kila aina ya sayari daima ziko katika mwendo, na viumbe vyenye uhai na viumbe hai juu ya sayari hizo pia daima vinazaa, vinakua na viko katika mwendo. Yaani, vitu vyote vilivyo na uhai na visivyo na uhai daima vinasonga mbele machoni pa Mungu, na wakati kila aina ya vitu vyenye uhai viko katika mwendo pia vinatoa sauti wakati huo huo. Mungu pia ameshughulikia sauti hizi. Kwa nini? Mnapaswa kujua hili, sivyo? Unaposonga karibu na ndege, sauti ya kunguruma ya ndege itakufanyia nini? (Masikio yatazibwa.) Je, itadhuru kusikia kwa watu? Mioyo yao itaweza kuistahimili? (La.) Wengine wenye mioyo hafifu hawataweza kuistahimili. Bila shaka, hata wale wenye mioyo yenye nguvu hawataweza kuistahimili ikiendelea kwa muda mrefu. Hiyo ni kusema, athari ya sauti kwa mwili wa mwanadamu, kama ni kwa masikio au moyo, ni yenye maana kabisa kwa kila mtu, na sauti ambazo ni za juu sana zitaleta madhara kwa watu. Kwa hiyo, Mungu alipoumba vitu vyote na baada ya hivyo kuanza kufanya kazi kwa kawaida, Mungu pia aliweka sauti hizi—sauti za vitu vyote vilivyo katika mwendo—kupitia kwa utendeaji wa kufaa. Hii pia ni mojawapo ya fikira muhimu alizokuwa nazo Mungu alipoumbia wanadamu mazingira.
Kwanza kabisa, kimo cha angahewa kutoka kwa uso wa dunia kitaondosha na kuzuia sauti. Pia, ukubwa wa nafasi katikati ya ardhi, yaani, ukubwa wa utupu ndani ya mchanga, pia utaendesha na kuathiri sauti. Kisha kuna mahali mito miwili inapoungana pa mazingira mbalimbali ya kijiografia, ambapo pia pataathiri sauti. Hiyo ni kusema, Mungu hutumia mbinu fulani kuondoa sauti zengine, ili wanadamu waweze kuendelea kuishi katika mazingira ambayo masikio na mioyo yao vinaweza kustahimili. La sivyo sauti zitaleta kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu, na italeta matatizo makubwa kwa maisha yao. Hili ni tatizo kubwa. Hiyo ni kusema, Mungu alikuwa mwenye kujali sana katika uumbaji Wake wa nchi, angahewa, na aina mbalimbali za mazingira ya kijiografia. Hekima ya Mungu iko ndani ya haya yote. Ufahamu wa wanadamu kuhusu haya hauhitaji kuwa kinaganaga sana. Kila wanachohitaji kujua ni kwmaba kitendo cha Mungu kimo humo. Uumbaji wa Mungu wa vitu vyote ulikuwa kweli kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Sasa Niambieni, Je, kazi ya Mungu ya uendeshaji wa sauti ilikuwa muhimu? Je, hamwezi kuhisi umuhimu wa Mungu kufanya hili? Kazi ambayo Mungu alifanya ilikuwa kuongoza uendeshaji wa taratibu sana wa sauti. Alifanya kazi hii ili kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu na maisha yao ya kawaida. Je, kazi hii ilikuwa muhimu? (Ndiyo.) Ikiwa kazi hii ilikuwa muhimu, basi kutokana na mtazamo huu, je, inaweza kusemwa kwamba Mungu alitumia mbinu kama hii kupeana vitu vyote? Mungu aliwapa wanadamu na kuumba mazingira haya tulivu, ili kwamba mwili wa mwanadamu uweze kuishi kwa kawaida kabisa katika mazingira haya, na ili kwamba mwanadamu hataweza kupata kuingiliwa kati kokote na ataweza kuwepo na kuishi kwa kawaida. Je, hii si njia mojawapo ambayo kwayo Mungu huwapa wanadamu? (Ndiyo.) Je, jambo hili alilofanya Mungu lilikuwa muhimu sana? (Ndiyo.) Lilikuwa muhimu sana. Je, ni vipi ambavyo mnashukuru hili? Hata kama hamwezi kuhisi kwamba hiki kilikuwa kitendo cha Mungu, wala hamjui vile Mungu alikifanya wakati huo, je, bado mnaweza kuhisi umuhimu wa Mungu kufanya hilo? Je, mnaweza kuhisi hekima ya Mungu au umakini na wazo Aliyoweka katika jambo hili? (Ndiyo.) Kuweza tu kuhisi hili ni sawa. Yatosha. Kuna vitu vingi ambavyo Mungu amefanya miongoni mwa vitu vyote ambavyo watu hawawezi kuhisi na ni vigumu kwa wao kuona. Lengo la Mimi kukitaja hapa ni kuwapa tu habari kiasi kuhusu matendo ya Mungu ili muweze kuanza kumjua Mungu. Vidokezo hivi vinaweza kuwafanya mjue na kuelewa matendo ya Mungu vizuri zaidi.
(4) Nuru
Kitu cha nne kinahusiana na macho ya watu—nacho ni, nuru. Hiki ni muhimu sana. Unapoona nuru inayong’aa, na mwangaza wa nuru hiyo ukafikia kiasi fulani, macho yako yatapofushwa. Hata hivyo, macho ya wanadamu ni macho ya mwili. Hayana kinga dhidi ya madhara. Je, kuna yeyote anayethubutu kulitazama jua moja kwa moja? (La.) Yeyote amewahi kujaribu? Watu wengine wamejaribu. Unaweza kutazama ukiwa umevaa miwani ya jua, sivyo? Hilo linahitaji usaidizi wa vifaa. Bila vifaa, macho makavu ya mwanadamu hayathubutu kutazama jua moja kwa moja. Binadamu hawana uwezo huu. Mungu aliumba jua ili awape wanadamu nuru, lakini pia aliendesha nuru hii. Mungu hakuliacha tu jua na kulipuuza baada ya kuliumba. “Nani anajali iwapo macho ya mwanadamu yanaweza kulistahimili!” Mungu hafanyi vitu hivyo. Yeye hufanya vitu kwa uangalifu sana na huzingatia vipengele vyote. Mungu aliwapa wanadamu macho ili waweze kuona, lakini Mungu ametayarisha pia umbali wa mwangaza ambao wanaweza kutazama chini yake. Haitawezekana iwapo hakuna nuru ya kutosha. Iwapo kuna giza sana mpaka watu hawawezi kuona mkono wao ulio mbele yao, kisha macho yao yatapoteza kazi yake na hayatakuwa na faida yoyote. Macho ya watu hayataweza kustahimili sehemu zilizo na mwangaza mwingi, na pia hawataweza kuona chochote. Hivyo katika mazingira wanayoishi ndani wanadamu, Mungu amewapa kiasi cha nuru kinachofaa macho ya wanadamu. Nuru hii haitaumiza wala kudhuru macho ya watu. Zaidi ya hayo, haitayafanya macho ya watu yapoteze matumizi yake, na pia inaweza kuhakikisha kwamba macho ya watu yataweza kuona kwa dhahiri kila kitu ambacho yanapaswa kukiona. Hii ndiyo sababu ambayo Mungu aliongeza kiasi kinachofaa cha mawingu yanayozunguka jua na dunia, na uzito wa hewa unaweza pia kuchuja kwa kawaida nuru inayoweza kuumiza macho ya watu au ngozi. Haya yanahusiana. Kuongezea, rangi ya dunia iliyoumbwa na Mungu huakisi pia nuru ya jua na kuondoa ile sehemu ya mwangaza katika nuru inayofanya macho ya wanadamu kutokuwa na raha. Kwa njia hiyo, watu hawahitaji kila mara kuvaa miwani myeusi sana ya jua ili waweze kutembea huko nje na kufanya shughuli za maisha yao. Katika hali za kawaida, macho ya wanadamu yanaweza kuona vitu vilivyo katika eneo la kuona kwao na hayataingiliwa kati na nuru. Yaani, nuru hii haiwezi kuwa ya kuchoma sana wala ya kufifiliza, ikiwa ya kufifiliza sana, macho ya watu yatadhuriwa na hawataweza kuyatumia kwa muda mrefu sana kabla ya macho yao kuacha kutumika; ikiwa ina mwangaza sana, macho ya watu hayataweza kuistahimili, na macho yao hayataweza kutumika katika miaka ya 30 hadi 40 au miaka 40 hadi 50. Hiyo ni kusema, nuru hii inafaa kwa macho ya wanadamu kuona, na madhara yanayoletwa kwa macho ya wanadamu na nuru yamepunguzwa na Mungu kupitia kwa mbinu mbalimbali. Haijalishi ikiwa nuru huleta faida au kikwazo kwa macho ya wanadamu, inatosha kuyawezesha macho ya watu kuendelea kuishi mpaka mwisho wa maisha yao. Sivyo? (Ndiyo.) Je, Mungu hajalifikiria hilo kikamilifu sana? Lakini wakati Shetani, ibilisi, anafanya mambo, hafikirii mambo haya. Hajali kabisa ikiwa kitu fulani kitaleta madhara kwa watu. Amefanya mambo mengi sana kudhuru mazingira ya ikolojia, na watu sasa wameona baadhi yake. Nuru hiyo ama ina mwangaza sana au inafifiliza sana—hajali kamwe hisia za wanadamu.
Mungu alifanya vitu hivi katika vipengele vyote vya mwili wa mwanadamu—kuona, kusikia, kuonja, kupumua, hisia … kuongeza hadi upeo uwezo wa kubadilisha wa kuendelea kuishi kwa wanadamu ili waweze kuishi—kuishi kwa kawaida na kuendelea kuishi. Mazingira ya kuishi kama hayo yaliyopo yaliyoumbwa na Mungu ni mazingira ya kuishi yanayofaa zaidi na yenye faida kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wengine wanaweza kufikiri kwamba hii haitoshi na kwamba yote ni ya kawaida sana. Sauti, nuru, na hewa ni vitu ambavyo watu hufikiria kwamba walizaliwa navyo, vitu wanavyoweza kufurahia tangu wakati wa kuzaliwa. Lakini kile alichofanya Mungu kinachosababisha kufurahia kwako kwa vitu hivi ni kitu unachohitaji kujua na kuelewa. Haijalishi ikiwa unahisi kuna haja ya kuelewa au kujua vitu hivi, kwa ufupi, Mungu alipoumba vitu hivi, alikuwa ametumia fikira, Alikuwa na mpango, Alikuwa na mawazo fulani. Hakuwaweka wanadamu katika mazingira ya kuishi kama haya kwa kawaida, kwa bahati, au bila kufikiria. Huenda mkadhani kwamba kila kitu ambacho Nimezungumzia si muhimu, lakini kwa mtazamo Wangu, kila kitu ambacho Mungu aliwapa wanadamu ni muhimu kwa kuendelea kuishi kwa ubinadamu. Kuna tendo la Mungu katika hili.
(5) Bubujiko la Hewa
Kitu cha tano ni kipi? Kitu hiki kinahusiana sana na maisha ya kila mwanadamu, na pia ni kitu ambacho mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila katika ulimwengu huu yakinifu. Kitu hiki ni bubujiko la hewa. “Bubujiko la hewa” ni neno ambalo watu wote labda wanaelewa. Hivyo bubujiko la hewa ni nini? Jaribuni kueleza katika maneno yenu wenyewe. (Bubujiko la hewa ni kububujika kwa hewa.) Mngesema hilo. Kububujika kwa hewa kunaitwa “bubujiko la hewa.” Je, kuna maelezo mengine? Je, maneno haya “bubujiko la hewa” yanamaanisha nini? Bubujiko la hewa ni upepo ambao jicho la mwanadamu haliwezi kuona. Pia ni njia ambayo gesi husonga. Hiyo ni sahihi pia. Lakini ni bubujiko la hewa gani tunalozungumzia hapa? Mtaelewa punde Nitakaposema. Dunia hubeba milima, bahari, na vitu vyote inapogeuka, na inapogeuka kuna spidi. Hata ikiwa huwezi kuhisi kuzunguka kokote, mzunguko wake upo kweli. Mzunguko wake huleta nini? Ni nini hufanyika mtu anapokimbia? Huwa kuna upepo kando ya masikio yako unapokimbia? (Ndiyo.) Ndilo hilo. Ikiwa upepo unaweza kuzalishwa unapokimbia, basi inawezekanaje kutokuwepo kwa nguvu za upepo dunia inapozunguka? Dunia inapozunguka, vitu vyote viko katika mwendo. Iko katika mwendo na kuzunguka katika spidi fulani, wakati vitu vyote duniani daima vinazaa na kukua. Kwa hiyo, kusonga kwa spidi fulani kwa kawaida kutaleta bubujiko la hewa. Hilo ndilo bubujiko la hewa. Bubujiko la hewa hilo litaathiri mwili wa mwanadamu kwa kiasi fulani? (Ndiyo.) Litafanya hivyo. Ikiwa dunia nzima ingejaa tambarare, basi wakati dunia na vitu vyote vinapozunguka kwa spidi fulani, mwili mdogo wa mwanadamu haungeweza kustahimili nguvu za upepo. Taiwan na Hong Kong zote zina tufani. Tufani hizo hazina nguvu sana, lakini zinapotokea, watu hawawezi kusimama kwa utulivu na huona vigumu kutembea katika upepo huo. Ni vigumu hata kutembea hatua moja. Hii ni mojawapo ya njia ambazo bubujiko la hewa linaweza kuathiri wanadamu. Ikiwa dunia nzima imejaa tambarare, bubujiko la hewa linalozalishwa dunia inapozunguka si kitu ambacho mwili wa mwanadamu unaweza kustahimili. Ingekuwa vigumu zaidi kustahimili. Ingekuwa hivyo, hili bubujiko la hewa halingeleta tu madhara kwa wanadamu, bali uharibifu. Hakuna ambaye angeweza kuendelea kuishi katika mazingira hayo. Ndio maana Mungu hutumia mazingira ya kijiografia mbalimbali kutatua aina hiyo ya bubujiko za hewa, kudhoofisha bubujiko za hewa kama hizo kwa kubadilisha mwelekeo, spidi na nguvu zake kupitia kwa mazingira mbalimbali. Ndio maana watu wanaweza kuona mazingira ya jiografia mbalimbali, kama vile milima, safu za milima, tambarare, vilima, vidimbwi, mabonde, uwanda wa juu, na mito. Mungu hutumia haya mazingira mbalimbali ya jiografia kubadilisha spidi, mwelekeo na nguvu za bubujiko la hewa, akitumia mbinu kama hiyo kupunguza au kuiendesha kuwa spidi ya upepo, mwelekeo wa upepo, na nguvu za upepo zinazofaa, ili wanadamu waweze kuwa na mazingira ya kuishi ya kawaida. Kufanya jambo kama hilo kunaonekana kuwa vigumu kwa wanadamu, lakini ni rahisi kwa Mungu kwa sababu Anaangalia kwa makini vitu vyote. Kwa Yeye kuumba mazingira yenye bubujiko la hewa linalofaa wanadamu ni kitu sahili sana, rahisi sana. Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo yaliyoumbwa na Mungu, kila kitu na vitu vyote miongoni mwa vitu vyote ni vya lazima. Kuna thamani na umuhimu katika kila kuwepo kwa vitu hivyo. Hata hivyo, Shetani na wanadamu wapotovu hawana aina hiyo ya falsafa. Wanaendelea kuharibu na kukuza, wakiota bure juu ya kugeuza milima kuwa ardhi tambarare, kujaza korongo kuu, na kujenga magorofa juu ya ardhi tambarare kuunda misitu ya saruji. Ni matumaini ya Mungu kwamba wanadamu wataishi kwa furaha, kukua kwa furaha, na kutumia kila siku kwa furaha katika mazingira ya kufaa zaidi Aliyowatayarishia. Ndiyo maana Mungu hajawahi kuwa mzembe inapohusu kushughulikia mazingira ya kuishi ya wanadamu. Kutoka kwa halijoto mpaka kwa hewa, kutoka kwa sauti mpaka kwa nuru, Mungu amefanya mipango na utaratibu tatanishi, ili mazingira ya kuishi ya wanadamu na miili yao visiweze kupatwa na kuharibiwa kokote kutoka kwa hali za asili, na badala yake wanadamu waweze kuishi na kuongezeka kawaida na kuishi na vitu vyote kawaida kwa kuishi pamoja kwa amani yenye kuridhisha. Hii yote inapeanwa na Mungu kwa vitu vyote na wanadamu.
Je, unaweza kuona, kutokana na jinsi Alishughulikia hali hizi tano za msingi za kuendelea kuishi kwa wanadamu, upeanaji wa Mungu kwa wanadamu? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema kwamba Mungu aliumba hali tano zote za msingi kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wakati huo huo, Mungu pia anasimamia na kudhibiti vitu hivi vyote, na hata sasa, baada ya wanadamu kuwepo kwa maelfu ya miaka, Mungu bado daima anabadilisha mazingira yao ya kuishi, kupeana mazingira ya kuishi yaliyo bora zaidi na ya kufaa zaidi kwa wanadamu ili maisha yao yaweze kudumishwa kwa kawaida. Haya yatadumishwa mpaka lini? Kwa maneno mengine, Mungu ataendelea kupeana mazingira kama haya kwa muda gani? Mpaka Mungu akamilishe kabisa kazi Yake ya usimamizi. Kisha, Mungu atabadilisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Huenda ikawa kupitia kwa mbinu zile zile, au huenda ikawa kupitia kwa mbinu tofauti, lakini kile ambacho watu wanahitaji kujua sasa ni kwamba Mungu daima anapeana mahitaji ya wanadama, anasimamia mazingira ya kuishi ya wanadamu, na kutunza, kuhifadhi na kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Ni kwa sababu ya mazingira kama hayo ndiyo watu waliochaguliwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kawaida hivyo na kukubali wokovu wa Mungu na kuadibu na hukumu. Vitu vyote vinaendelea kuwepo kwa sababu ya kanuni ya Mungu, wakati wanadamu wote wanaendelea kusonga mbele kwa sababu ya upeanaji wa Mungu kwa jinsi hii.
Je, sehemu hii ambayo Nimewasilisha sasa hivi imewaletea mawazo yoyote mapya? Je, sasa mnahisi tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu? Nani hasa ndiye bwana wa vitu vyote? Ni mwanadamu? (La.) Basi mnajua ni nini tofauti kati ya vile Mungu na wanadamu hushughulikia vitu vyote? (Mungu hutawala na kupanga vitu vyote, ilhali mwanadamu hufurahia vitu hivyo vyote.) Je, mnakubaliana na maneno hayo? (Ndiyo.) Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Sivyo? Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. Je, wanadamu wanaweza kuona vitu vyote? (La.) Kile ambacho wanadamu huona kimewekewa mipaka. Huwezi kuita hicho “vitu vyote” —ni tu kile wanachoona mbele ya macho yao. Ukiukwea mlima huu, unachoona ni mlima huu. Huwezi kuona kilicho upande mwingine wa mlima huo. Ukienda pwani, unaweza kuona upande huu wa bahari, lakini hujui upande ule mwingine wa bahari ulivyo. Ukiwasili katika msitu huu, unaweza kuona mimea iliyo mbele ya macho yako na inayokuzunguka, lakini huwezi kuona iliyo mbele zaidi. Wanadamu hawawezi kuona sehemu zilizo juu sana, mbali sana na kina sana. Kile wanachoweza kuona ni kilicho mbele ya macho yao na katika mpaka wa upeo wao wa kuona. Hata kama wanadamu wanajua mpangilio wa misimu minne katika mwaka na mpangilio wa ukuaji wa vitu vyote, hawawezi kusimamia au kutawala vitu vyote. Kwa upande mwingine, vile Mungu aonavyo vitu vyote ni kama vile Mungu angeona mashine Aliyotengeneza binafsi. Angejua kila kijenzi vizuri kabisa. Kanuni zake ni zipi, mipangilio yake ni ipi, na kusudi lake ni lipi—Mungu anajua vitu hivi vyote wazi na dhahiri. Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli. Ndiyo maana ukitumia ufahamu na kile ulichojifunza kumsoma Mungu, hutaweza kamwe kujua au kuelewa Mungu. Lakini ukitumia njia ya ukweli na kumtafuta Mungu, na kumtazama Mungu kutokana na mtazamo wa kuanza kumjua Mungu, basi siku moja utakubali kwamba matendo na hekima ya Mungu viko kila mahali, na utajua pia hasa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote na chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kadiri unavyokuwa na maarifa kama hayo, ndivyo utakavyoelewa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote. Vitu vyote na kila kitu, pamoja na wewe, daima vinapokea mtiririko thabiti wa upeanaji wa Mungu. Utaweza pia kuhisi dhahiri kwamba katika ulimwengu huu, na miongoni mwa wanadamu hawa, hakuna yeyote isipokuwa Mungu anayeweza kuwa na nguvu kama hizo na kiini kama hicho kutawala, kusimamia, na kudumisha kuwepo kwa vitu vyote. Ukitimiza ufahamu kama huo, utakubali kwa kweli kwamba Mungu ni Mungu wako. Ukifikia kiwango hiki, umemkubali Mungu kwa kweli na kumruhusu awe Mungu wako na Bwana wako. Ukiwa na ufahamu kama huo na maisha yako yakifikia kiwango kama hicho, Mungu hatakujaribu na kukuhumu tena, wala Hatakushurutisha ufanye mambo, kwa sababu unamfahamu Mungu, unajua moyo Wake, na umemkubali Mungu kwa kweli ndani ya moyo wako. Hii ni sababu muhimu ya kuwasilisha mada hizi kuhusu utawala na usimamizi wa Mungu juu ya vitu vyote. Ni kuwapa watu maarifa na ufahamu zaidi; sio tu kukufanya ukubali, lakini kukupa maarifa zaidi na ufahamu wa utendaji wa matendo ya Mungu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni