New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu
Jina lake ni Wang Hua, na ni mhubiri wa kanisa la nyumbani Kusini mwa Uchina. Baada ya kuanza kumwamini Bwana, alipata kwenye Biblia kuwa Mungu aliitwa Yehova katika Agano la Kale, na aliitwa Yesu katika Agano Jipya. Ni kwa nini Mungu ana majina tofauti? Wang Hua alishangazwa sana na hili. Alijaribu kutafuta jibu katika Biblia, lakini akakosa kuelewa fumbo hilo... Lakini alikuwa na imani thabiti kuwa hakuna jina lingine chini ya mbingu lililopewa wanadamu, hivyo Yesu pekee ndiye Mwokozi, na kuwa muradi tushikilie jina la Yesu, bila shaka tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Hata hivyo, siku moja Wang Hua alisikia habari za kushtusha: jina la Mungu limebadilika! Baada ya hapo, moyo wake haungetulia tena …
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni