Mwenyezi Mungu alivyosema, "Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu hasa wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili.
Ukiweza kuliona hili wazi, utaweza kuhusisha sehemu zote za Mungu, na utaacha kuthamini sana kazi Yake ya uungu, na kuwa mwenye kupuuza sana kazi Yake katika ubinadamu, na hautazidi mipaka wala kupita njia za michepuo. Kwa jumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika."
Sikiliza zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni