Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma
Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...),
mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...),
ukiangaza njia yote kwenda magharibi.
Mwana wa Adamu ameshuka duniani.
Mwana wa Adamu ameonekana. (Siyo?)
Mungu amekuja. (Eh!)
Mbingu mpya, dunia mpya, enzi mpya,
binadamu wapya, njia mpya, maisha mapya.
Yerusalemu mpya umeshuka duniani.
Tumerudi kwa familia ya Mungu na tunaishi maisha ya kanisa,
Wewe kuja na uimbe! (Sawa!)
Nitacheza ngoma! (Ngoma!)
Maisha yetu ni ya furaha kweli (furaha kweli).
Tuko katika uwepo wa Mungu. (Tunaufurahia kweli.)
Tuna baraka za Mungu. (Tuna furaha sana.)
Ufalme wa Kristo ni nyumba kunjufu.
Kila mstari Anenao ni ukweli, utunyinyiziao.
Anatufundisha jinsi ya kutenda, jinsi ya kuwa waaminifu.
Tukiishi kati ya baraka za Mungu, tunampenda Mungu kwa moyo wetu wote.
Hukumu ya neno la Mungu inaishinda mioyo ya watu wote.
Wakiwa wametakaswa, watu wa Mungu humtolea ushuhuda.
Hebu tuwe wenye akili moja (tukitimiza wajibu wetu),
tukilipiza upendo wa Mungu (kuwa na ushuhuda kwa Mungu),
tukieneza injili ya Ufalme wa Mungu (injili ya Ufalme wa Mungu).
Neno la Mungu linaenea duniani kote.
Jina takatifu la Mungu linasifiwa na wote.
Ufalme wa Kristo unafanyika duniani.
Hebu tuwe wenye akili moja (tukitimiza wajibu wetu),
tukieneza injili ya Ufalme wa Mungu (injili ya Ufalme wa Mungu).
Neno la Mungu linaenea duniani kote.
Jina takatifu la Mungu linasifiwa na wote.
Ufalme wa Kristo unafanyika duniani.
Ufalme wa Kristo unafanyika duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni