Kuuonja Upendo wa Mungu Katikati ya Dhiki
Chen Lu Wilaya ya Tonglu, Mkoa wa Zhejiang
Nilizaliwa miaka ya 1980 katika kijiji—tulikuwa tumekuwa familia ya wakulima kwa vizazi vingi. Nilijiingiza katika masomo yangu ili niweze kuhitimu kuingia katika chuo na kuepuka maisha ya kijijini ya umasikini na hali ya kuwa nyuma. Nilipoanza shule ya upili, nilikutana na Historia ya Sanaa ya Magharibi, na wakati nilipoona picha nyingi za kupendeza kama vile "Mwanzo," "Bustani ya Edeni," na "Mlo wa Mwisho," ni hapo tu nilipojua kwamba kulikuwa na Mungu katika ulimwengu aliyeumba vitu vyote.