Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 29 Septemba 2019

New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu




New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu


Jina lake ni Wang Hua, na ni mhubiri wa kanisa la nyumbani Kusini mwa Uchina. Baada ya kuanza kumwamini Bwana, alipata kwenye Biblia kuwa Mungu aliitwa Yehova katika Agano la Kale, na aliitwa Yesu katika Agano Jipya. Ni kwa nini Mungu ana majina tofauti? Wang Hua alishangazwa sana na hili. Alijaribu kutafuta jibu katika Biblia, lakini akakosa kuelewa fumbo hilo...

Jumapili, 16 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: ‘Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.’ Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: ‘Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.’ Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. 

Jumatatu, 1 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 47

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu mwenye haki—Mwenyezi! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo binadamu hawajawahi kufichua, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndilo fumbo ambalo limefichuliwa, na Wewe ni Mungu aliye hai Mwenyewe, na kwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na kwa sisi kuona nafsi Yako ni kuona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho.