Jumamosi, 23 Desemba 2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

2. Chakula cha Kila Siku na Kinywaji Ambavyo Mungu Anawatayarishia Wanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Tulikuwa tumezungumza sasa hivi kuhusu sehemu ya mazingira ya jumla, yaani, hali zilizo muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu ambazo Mungu aliwatayarishia wanadamu tangu Alipoumba ulimwengu. Tumezungumza sasa hivi kuhusu vitu vitano, na vitu hivi vitano ndivyo mazingira ya jumla.Tunachoenda kuzungumzia baada ya hapo kinahusiana kwa karibu na kila maisha ya wanadamu katika mwili. Ni hali muhimu inayolingana zaidi na inayokubaliana zaidi na maisha ya mtu katika mwili. Kitu hiki ni chakula.Mungu alimuumba mwanadamu na akamweka ndani ya mazingira ya kuishi yanayofaa. Baadaye, mwanadamu alihitaji chakula na maji. Mwanadamu alikuwa na hitaji hilo, hivyo Mungu alimtengenezea mwanadamu matayarisho hayo. Kwa hiyo, unaweza kuona kwamba kila hatua ya kazi ya Mungu na kila kitu Anachofanya sio maneno matupu tu, lakini vinafanyika kwa kweli. Je, chakula ni kitu ambacho watu hawawezi kukosa kuwa nacho katika maisha yao? (Ndiyo.) Chakula ni muhimu zaidi kuliko hewa? (Vyote ni muhimu kwa njia sawa) Vyote ni muhimu kwa njia sawa. Vyote ni hali na vitu muhimu kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu na kuhifadhi mwendelezo wa maisha ya binadamu. Hewa ni muhimu zaidi au maji ni muhimu zaidi? Halijoto ni muhimu zaidi au chakula ni muhimu zaidi? Vyote ni muhimu. Watu hawawezi kuchagua kwa sababu hawawezi kuishi bila chochote kati ya hivyo vyote. Hili ni tatizo halisi, si kitu unachoweza kuchagua. Hujui, lakini Mungu anajua. Unapoviona vitu hivi, utahisi, “Siwezi kuishi bila chakula!” Lakini ungewekwa pale baada tu ya wewe kuumbwa, je, ungejua kwamba unahitaji chakula? Hungejua, lakini Mungu anajua. Ni wakati tu unapokuwa na njaa na kuona kuna matunda juu ya miti na nafaka juu ya ardhi ili uweze kula ndipo unatambua, “Ah, nahitaji chakula.” Ni wakati tu unapokuwa na kiu na unataka kunywa maji ndipo utatambua, “Ninahitaji maji. Ninaweza kupata maji wapi?” Unaona chemchemi ya maji mbele yako, kisha unakunywa kutoka hapo. Unasema, “Kinywaji hiki kina ladha nzuri sana. Ni nini?” Ni maji, na Mungu alimtayarishia mwanadamu. Kuhusu chakula, haijalishi ikiwa wewe hula milo mitatu kwa siku, milo miwili kwa siku, au hata zaidi ya hiyo; kwa ufupi, chakula ni kitu ambacho wanadamu hawawezi kukosa kuwa nacho katika maisha yao ya kila siku. Ni mojawapo ya vitu muhimu vya kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa binadamu. Hivyo chakula hasa hutoka wapi? Kwanza, kinatoka ndani ya udongo. Udongo kwanza ulitayarishwa na Mungu kwa ajili ya wanadamu. Udongo unafaa kwa kuendelea kuishi kwa mimea mbalimbali, sio tu kwa ajili ya miti au nyasi. Mungu aliwatayarishia wanadamu mbegu za kila aina ya nafaka na vyakula mbalimbali, na vilevile udongo na ardhi vinavyofaa kwa watu kupanda, na hivyo kuwapa chakula. Kuna aina gani za chakula? Mnapaswa kulijua hili vizuri. Kwanza, kuna aina mbalimbali za nafaka. Ni nini kinahusishwa katika nafaka. Ngano, mtama wa mkia wa mbweha, mtama wa proso, mchele…, inayokuwa na maganda. Mazao ya nafaka pia yametenganishwa katika aina nyingi mbalimbali. Kuna aina nyingi za mazao ya nafaka kutoka kusini mpaka kaskazini, kama vile shayiri, ngano, oti, na nafaka inayofanana na ngano. Aina mbalimbali zinafaa kukuzwa katika maeneo mbalimbali. Pia kuna aina mbalimbali za mchele. Kusini ina aina zake za mchele, iliyo ndefu zaidi na inawafaa watu kutoka kusini kwa sababu si ya kunata sana. Kwa vile hali ya nchi ni joto zaidi kusini, wanahitajika kula aina mbalimbali kama vile mchele wa indica. Hautakiwi kunata sana la sivyo hawataweza kula na watapoteza hamu yao ya kula. Mchele unaoliwa na watu wa kaskazini ni wa kunata zaidi. Kwa vile kaskazini huwa na baridi zaidi kila mara, wanahitajika kula mchele wa kunata zaidi. Kuongezea, kuna aina mbalimbali za maharagwe. Haya yanakuzwa juu ya ardhi. Pia kuna vile vinavyokuzwa chini ya ardhi, kama viazi, viazi vitamu, jimbi, na vinginevyo. Hizi ni aina mbalimbali za nafaka, muhimu kwa chakula cha watu cha kila siku. Watu hutumia nafaka mbalimbali kutengeneza nudo, mkate mdogo wa mviringo uliopikwa kwa mvuke, mchele, na nudo za mchele. Watu pia hula viazi na kutumia viazi na viazi vitamu kutayarisha chakula kikuu. Jimbi, ambalo huliwa mara nyingi na watu wa kusini, linaweza pia kuwa chakula kikuu. Mungu ametoa aina hizi mbalimbali za nafaka kwa wanadamu kwa wingi. Kwa nini kuna aina nyingi sana? Makusudi ya Mungu yanaweza kupatikana humo: Kwa upande mmoja, ni kwa ajili ya kufaa aina mbalimbali za udongo na hali ya nchi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi; kwa upande mwingine, vijenzi na kadiri mbalimbali vya nafaka hizi vinakubaliana na vijenzi na kadiri mbalimbali vya mwili wa mwanadamu. Watu wanaweza tu kudumisha virutubishi na vijenzi mbalimbali vinavyohitajika kwa miili yao kwa kula nafaka hizi. Ingawa chakula cha kaskazini na chakula cha kusini ni tofauti, vina mifanano mingi kuliko tofauti. Vyakula hivi vyote vinaweza kuridhisha mahitaji ya kawaida ya mwili wa mwanadamu na vinaweza kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa mwanaamu. Hivyo, sababu ya aina zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali kuwa nyingi mno ni kwamba mwili wa mwanadamu unahitaji kinachotolewa na vyakula hivyo. Wanahitaji kinachotolewa na vyakula mbalimbali vinavyokuzwa kutoka kwa udongo ili kudumisha kuendelea kuishi kwa kawaida kwa mwili wa mwanadamu na kutimiza maisha ya kawaida ya mwanadamu. Umeelewa? (Ndiyo.) Viazi huota kaskazini. Sifa ya viazi vya kaskazini ni nzuri sana. Watu wakikosa nafaka za kula, viazi vinaweza kuwa chakula kikuu cha mlo wao ili waweze kudumisha milo mitatu kwa siku. Viazi pia vinaweza kuwa ugavi wa chakula. Viazi vitamu si vizuri kama viazi kulingana na sifa, lakini bado vinaweza kutumiwa na watu kama chakula cha kudumisha milo yao mitatu kwa siku. Ikiwa nafaka hazipatikani, watu wanaweza kutumia viazi vitamu kujaza matumbo yao. Jimbi pia inaweza kutumiwa kwa njia hiyo. Kwa ufupi, Mungu aliwafikiria sana wanadamu. Vyakula mbalimbali ambavyo Mungu aliwapa watu si vya kuchosha—ni vyenye maarifa mengi mno. Ikiwa watu wanataka kula nafaka wanaweza kula nafaka. Wengine huenda wakasema, “Sipendi kula nudo, ninataka kula mchele,” na wanaweza kula mchele. Kuna aina nyingi za mchele—mchele mrefu, mchele mfupi, na yote inaweza kuridhisha ladha walizonazo watu, sivyo? Kwa hiyo, watu wakila nafaka hizi—bora tu si wa kuchaguachagua au kulalamika kuhusu vyakula vyao—hawatakosa lishe na wanahakikishiwa kuishi kwa afya nzuri mpaka umri wa uzeeni. Hilo lilikuwa wazo la asili ambalo Mungu alikuwa nalo akilini Alipowapa wanadamu chakula. Mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila vitu hivi—je, hiyo si kweli? (Ndiyo.) Wanadamu hawawezi kutatua matatizo haya halisi, lakini Mungu alikuwa tayari ametayarisha na kulifikiria kabisa. Mungu alikuwa amewatayarishia wanadamu vitu zamani sana, na alivitayarisha kwa wingi. Huo ni ukweli.
Mungu amempa mwanadamu zaidi ya vitu hivi tu—pia kuna mboga. Unapokula mchele, ikiwa mchele ndio kila kitu unachokula, huenda ukakosa lishe. Ikiwa kisha utakaranga kwa mafuta kidogo vyakula kadhaa kiasi kidogokidogo au uchanganye kachumbari ya kula na mlo huo, basi vitamini katika mboga hizo na kiasi kidogo cha vitu vya msingi au lishe zengine vitaweza kupeana mahitaji ya mwili wa mwanadamu kwa njia ya kawaida sana. Wakati watu hawali vyakula vikuu wanaweza pia kula matunda, sivyo? Wakati mwingine, watu wanapohitaji uowevu au lishe zengine au ladha tofauti, pia kuna mboga na matunda ya kuwapa vitu hivyo. Kwa vile udongo na hali ya nchi ya kaskazini, kusini, mashariki na magharibi ni tofauti, pia kuna aina mbalimbali za mboga na matunda. Kwa vile hali ya nchi ya kusini ni joto sana, matunda mengi na mboga ni vya aina ya baridi vinavyoweza kusawazisha baridi na joto ndani ya miili ya watu wanapokula vitu hivyo. Kwa upande mwingine, kuna aina chache ya mboga na matunda kaskazini, lakini hata hivyo vinatosha kwa watu wa kaskazini kufurahia. Je, hilo si sahihi? (Ndiyo.) Kwa hali yoyote, kwa sababu ya ustawi wa kijami katika miaka ya hivi karibuni, kwa sababu ya kile kinachoitwa maendeleo ya kijamii, na vilevile maendeleo katika usafiri na mawasiliano vinavyounganisha kaskazini na kusini na mashariki na magharibi, watu walio kaskazini wanaweza pia kula matunda mengine, vitu vya sifa maalum vya mahali maalum au mboga kutoka kusini, hata katika mwaka mzima. Kwa njia hiyo, hata kama watu wanaweza kuridhisha hamu yao ya chakula na matamanio ya vitu vya mwili, miili yao bila kujua inapatwa na viwango mbalimbali vya madhara. Hii ni kwa sababu miongoni mwa vyakula ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu, kuna vyakula na matunda na mboga vinavyofaa watu walio kusini, na vilevile vyakula na matunda na mboga vinavyofaa watu walio kaskazini. Yaani, ikiwa ulizaliwa kusini, kula vitu kutoka kusini kunakufaa wewe sana. Mungu alitayarisha vyakula hivi na matunda na mboga kwa sababu kusini ina hali ya nchi mahsusi. Kaskazini ina vyakula vinavyohitajika kwa miili ya watu walio kaskazini. Lakini kwa vile watu wana hamu ya chakula ya ulafi, wamefagiliwa bila kujua katika mkondo wa maendeleo ya kijamii, na kuwafanya kukiuka sheria hizi bila kujua. Ingawa watu wanahisi kwamba maisha yao sasa ni bora zaidi, maendeleo ya kijamii kama hayo huleta madhara ya kufichika kwa miili ya watu wengi zaidi. Hiki si kile ambacho Mungu anataka kuona na si kile ambacho Mungu alikusudia mwanzoni Alipoleta vitu vyote pamoja na vyakula hivi, matunda na mboga kwa wanadamu. Hii ilisababishwa kabisa na wanadamu kukiuka sheria za maumbile na kufanya maendeleo ya kisayansi, na haijasababishwa na Mungu kwa vyovyote vile.
Yale ambayo Mungu aliwapa wanadamu ni ya fahari na mengi, kila sehemu ikiwa na vitu maalum vya mahali maalum. Kwa mfano, sehemu nyingine zina utajiri wa tende nyekundu (zinazozujulikana kwa kawaida kama jujubes), ilhali zengine zina utajiri wa jozi, karanga, au aina nyingine mbalimbali za njugu. Vitu hivi yakinifu vyote vinatoa lishe inayohitajika na mwili wa mwanadamu. Lakini Mungu huwapa wanadamu vitu kulingana na misimu na wakati, na pia anawapa kiasi sahihi kwa wakati sahihi. Wanadamu hutamani kujifurahisha kwa kimwili na ni walafi, hiyo inafanya kuwa rahisi kukiuka na kuharibu sheria za kawaida za ukuaji wa mwanadamu tangu Alipowaumba wanadamu. Kama mfano, hebu tutazame matunda ya cheri, ambazo kila mtu anapaswa kuzijua, sivyo? Msimu wa cheri huwa wakati gani? (Juni.) Hizo huvunwa karibu Juni. Kwa kawaida, hizo huisha lini? (Agosti.) Watu huanza kuzila tangu zinapopatikana, tangu Juni mpaka Agosti, kipindi cha miezi miwili. Cheri huwa mbichi kwa miezi miwili pekee, lakini kupitia mbinu za kisayansi watu sasa wanaweza kurefusha muda huo mapaka miezi 12, hata mpaka msimu wa cheri wa mwaka unaofuata. Hiyo inamaanisha cheri zipo kwa mwaka mzima. Je, jambo hili ni la kawaida? (La.) Basi msimu bora zaidi wa kula cheri ni upi? Ni kipindi cha kuanzia Juni mpaka Agosti. Zaidi ya kikomo hiki, haijalishi utaziweka mbichi vipi, hazitakuwa na ladha sawa, wala sio kile ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji. Mara tu tarehe ya kuisha kutumika inapopita, haijalishi ni vitu vipi vya kemikali unatumia, hutaweza kuzifanya ziwe kama zinavyokuwa wakati zinakuzwa kwa kawaida. Zaidi, madhara ambayo kemikali huleta kwa wanadamu ni kitu ambacho hakuna anayeweza kufanya chochote kuyaondoa au kuyabadilisha. Unaelewa? Ni nini ambacho soko la uchumi la wakati huu linawaletea watu? Maisha ya watu yanaonekana kuwa mazuri zaidi, usafiri katika pande zote umekuwa wa kufikika kwa urahisi sana, na watu wanaweza kula aina zote za matunda katika msimu wowote kati ya misimu minne ya mwaka. Watu wa kaskazini mara kwa mara huweza kula ndizi na chakula chochote, vitu maalum vya mahali maalum au matunda kutoka kusini. Lakini haya si maisha ambayo Mungu anataka kuwapa wanadamu. Haya yaliletwa na maendeleo ya kisayansi ya wanadamu. Kile ambacho soko hili la uchumi limeleta kwa mwili wa mwanadamu ni ukiukaji wa sheria za kawaida za ukuaji wa asili. Kilicholetwa ni madhara na maafa, sio furaha. Unaelewa? (Ndiyo.)
Hebu tazama. Zabibu huuzwa sokoni katika misimu yote minne ya mwaka? (Ndiyo.) Zabibu kwa kweli huwa mbichi tu kwa muda wa kipindi kifupi sana baada ya kuchumwa. Ukiziweka mpaka Juni inayofuata, bado zinaweza kuitwa zabibu? Je, unaweza kuziita takataka? Hazitakosa tu vijenzi vya asili vya zabibu, lakini pia zina kemikali zaidi juu yake. Baada ya mwaka mmoja, hazijapoteza tu ubichi wake, lakini pia lishe zake zimepotea kitambo. Watu wanapokula zabibu, wanahisi: “Ninafurahi sana! Inafurahisha sana! Je, tungeweza kula zabibu wakati wa msimu huu miaka 30 iliyopita? Hungeweza kuzila hata kama ungetaka. Maisha ni mazuri jinsi gani wakati huu!” Je, hii ni furaha kweli? Ukipenda, unaweza kwenda kusoma juu ya zabibu zilizohifadhiwa kwa kemikali na uone hasa vijenzi vyake ni vipi na iwapo vijenzi hivi vinaweza kuleta manufaa yoyote kwa wanadamu. Kumbuka wakati wa Enzi ya Sheria. Waisraeli walipokuwa njiani baada ya kuondoka Misri, Mungu aliwapa kware na mana. Je, Mungu aliwaruhusu watu kuvihifadhi? (La.) Watu wengine walikuwa na fikira ndogo na waliogopa kwamba hakungekuwa na zaidi siku iliyofuata, hivyo walihifadhi nyingine. “Tuweke akiba iwapo tutahitaji baadaye!” Kisha nini kilifanyika? Kufikia siku iliyofuata ilikuwa imeoza. Mungu hakuwaruhusu kuweka nyingine kama akiba kwa sababu Mungu alikuwa amefanya matayarisho fulani, yaliyohakikisha hawangekufa kwa njaa. Lakini watu hawakuwa na hakika na kila mara walitaka kubakisha nyingine kwa sababu walifikiria: “Matendo ya Mungu si ya kutegemewa! Huwezi kuiona wala huwezi kuigusa. Lakini ni bora tu kuweka nyengine kando kwa ajili ya baadaye. Unahitaji kuwahi kufanya jambo kabla ya wengine kwa sababu hakuna atakayekutunza usipotafuta njia ya kufanya hivyo wewe mwenyewe!” Kama unavyoona, wanadamu hawana hakika hiyo, wala hawana imani ya kweli kwa Mungu. Kila mara wanaweka nyengine kando kwa ajili ya baadaye na hawawezi kamwe kuona utunzi wote na mawazo yaliyo ndani ya kile ambacho Mungu amewatayarishia wanadamu. Kila mara hawawezi kuhisi hasa, kila mara wanakosa kumwamni Mungu, kila mara wanafikiria: “Matendo ya Mungu si ya kutegemewa! Nani anajua iwapo Mungu atawapa wanadamu au ni lini Atawapa! Ikiwa nina njaa sana na Mungu hanipi, basi si nitakufa njaa? Si nitakosa lishe?” Ona jinsi hakika ya mwanadamu ni ndogo sana!
Nafaka, matunda na mboga, na kila aina ya njugu vyote ni vyakula vya wala mboga. Hata kama ni vyakula vya wala mboga, vina lishe za kutosha kuridhisha mahitaji ya mwili wa mwanadamu. Kwa hali yoyote, Mungu hakusema: “Kuwapa wanadamu hiki kunatosha. Wanadamu wanaweza tu kula vitu hivi.” Mungu hakuachia hapo na badala yake aliwatayarishia wanadamu vitu vyenye ladha nzuri zaidi. Vitu hivi ni gani? Ni aina mbalimbali ya nyama na samaki mnaopenda kuona juu ya meza zenu na kula kila siku. Kuna aina nyingi sana za nyama na samaki. Samaki wote huishi majini; umbile asili la nyama yao ni tofauti na la nyama inayokuzwa juu ya ardhi na wanaweza kuwapa wanadamu lishe mbalimbali. Sifa za samaki zinaweza kubadilisha baridi na joto ndani ya mwili wa mwanadamu, kwa hiyo ni za manufaa makubwa sana kwa wanadamu. Lakini kilicho na ladha nzuri hakitakiwi kuliwa zaidi. Bado msemo ni huo huo: Mungu huwapa wanadamu kiasi sahihi kwa wakati sahihi, ili watu waweze kufurahia kwa kawaida na vizuri vitu hivi kulingana na msimu na wakati. Ndege wa kufugwa wanahusisha nini? Kuku, kware, njiwa, n.k. Watu wengi hula pia bata na bata bukini. Ingawa Mungu alifanya matayarisho, kwa watu waliochaguliwa na Mungu, bado Mungu aliwawekea masharti na alikuwa ameweka eneo fulani katika Enzi ya Sheria. Sasa eneo hili linatokana na kupendelea kwa mtu binafsi na ufahamu wa mtu binafsi. Aina hizi mbalimbali za nyama hupatia mwili wa mwanadamu lishe mbalimbali, zinazoweza kusheheneza protini na madini ya chuma, kusitawisha damu, kuimarisha misuli na mifupa, na kupeana nguvu zaidi. Haijalishi ni mbinu gani watu hutumia kupika na kula vitu hivyo, kwa ufupi, vitu hivi vinaweza kwa upande mmoja kuwasaidia watu kuendeleza ladha na hamu ya chakula, na kwa upande mwingine kuridhisha matumbo yao. Kitu cha muhimu zaidi ni kwamba zinaweza kupatia mwili wa mwanadamu mahitaji yao ya lishe ya kila siku. Hizi ndizo fikira ambazo Mungu alikuwa nazo Alipowatayarishia wanadamu chakula. Kuna vyakula vya wala mboga na pia nyama—je, hiyo si ya faharina nyingi? (Ndiyo.) Lakini watu wanapaswa kuelewa kusudi la asili la Mungu lilikuwa gani Mungu alipowatayarishia wanadamu vyakula vyote. Je, ilikuwa ni kuwaacha wanadamu wafurahie kwa ulafi vyakula hivi vya kimwili? Na je, watu wakiendekezwa katika kuridhisha hamu zao za vitu vya kimwili? Je, hawatakuwa na lishe kupita kiasi? Je, lishe kupita kiasi haitaleta kila aina ya magonjwa kwa mwili wa mwanadamu? Bila shaka si vizuri kusaliti sheria za asili zilizoumbwa na Mungu, na ndiyo maana Mungu hutoa kiasi sahihi kwa wakati sahihi na kuwaacha watu wafurahie vyakula mbalimbali kulingana na vipindi vya wakati na misimu. Hiyo ndiyo njia bora zaidi. Kwa mfano, baada ya kuishi katika majira ya joto sana, watu watakusanya kiasi fulani cha joto, la kusababisha ukavu wa viini na unyevunyevu katika miili yao. Majira ya kupukutika kwa majani yakija, matunda mengi sana yataiva, na watu wakila baadhi ya matunda unyevunyevu wao utaondolewa. Wakati huo huo, ng’ombe na kondoo watakuwa wamekua na kupata nguvu, ili watu wale nyama kiasi kama lishe. Baada ya kula aina mbalimbali za nyama, miili ya watu itakuwa na nguvu na joto la kuisaidia kustahimili baridi ya majira ya baridi, na kutokana na hayo wataweza kupita katika majira ya baridi kwa amani. Wakati upi wa kutayarisha vitu vipi kwa ajili ya wanadamu, na wakati upi wa kuacha vitu vipi vikue, vizae matunda na kuiva—yote haya yanadhibitiwa na Mungu na yalitayarishwa na Mungu zamani sana, na kwa kupimwa kabisa. Ni vile tu wanadamu hawaelewi mapenzi ya Mungu. Hii ni mada kuhusu “jinsi Mungu alitayarisha chakula kilicho muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku.”
Mbali na aina zote za chakula, Mungu pia huwapa wanadamu vyanzo vya maji. Watu huhitaji kunywa maji kiasi baada ya kula. Je, kula matunda tu kunatosha? Watu hawataweza kustahimili kula matunda pekee, licha ya hayo, huwa hakuna matunda katika misimu mingine. Hivyo tatizo la wanadamu la maji litawezaje kutatuliwa? Kwa Mungu kutayarisha vyanzo vingi vya maji juu ya ardhi na chini ya ardhi, ikiwemo maziwa, mito, na chemchemi. Vyanzo hivi vya maji vinaweza kunywewa maji katika hali ambazo hakuna kuchafuliwa kokote, au maendeleo ya wanadamu au uharibifu. Kuhusu vyanzo vya chakula kwa maisha ya miili ya wanadamu, Mungu amefanya matayarisho sahihi sana, yasiyo na hitilafu yoyote na ya kufaa sana, ili maisha ya watu yawe ya fahari na yenye wingi na yasiyokosa chochote. Hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kuhisi na kuona. Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote, iwe ni wanyama, mimea, au kila aina ya nyasi, Mungu aliumba pia baadhi ya mimea ambayo ni muhimu kwa kutatua madhara au magonjwa kwa mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka? Je, unaweza kuosha kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Utafanya nini, kwa mfano, ukiungua kwa bahati na moto au na maji moto? Unaweza kumimina maji juu yake? Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote. Kuna mimea inayoendeleza mzunguko wa damu kuondoa ukwamaji, kutuliza maumivu, kukomesha kutokwa na damu, kutia ganzi, kuwasaidia watu kupata tena ngozi ya kawaida, kuondoa ukwamaji wa damu mwilini, na kuondoa sumu mwilini. Kwa ufupi, yote inaweza kutumiwa katika maisha ya kila siku. Ni ya kufaa watu na imetayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwili wa mwanadamu iwapo inahitajika. Baadhi ya hiyo iliruhusiwa na Mungu kugunduliwa bila uangalifu na mwanadamu, ilhali mingine iligunduliwa kutoka kwa vitu fulani maalum au na watu fulani waliotayarishwa na Mungu. Baada ya ugunduzi wao, wanadamu wangeipitisha kwa wengine, na halafu watu wengi wangejua kuihusu. Kwa njia hii, uumbaji wa Mungu wa mimea hii unakuwa na thamani na maana. Kwa ufupi, vitu hivi vyote vinatoka kwa Mungu na vilitayarishwa na kupandwa Alipowaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Vitu hivi vyote ni muhimu sana. Je, hii haionyeshi kwamba Mungu alipoumba mbingu na dunia na vitu vyote, fikira Zake zilifikiriwa vizuri sana kuliko za wanadamu? Unapoona yote ambayo Mungu amefanya, unaweza kuhisi upande wa Mungu wa vitendo? Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, ili waweze kuishi kwa furaha, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo, lakini si wengi wanaweza kufahamu kwamba Mungu alikuwa amewaumbia wanadamu kila kitu. Badala yake, Shetani amedai kwamba viliumbwa na ulimwengu.
Niambie; Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai. Hivyo kuku alitangulia au yai lilitangulia? (Kuku.) Mnajibu “kuku” kwa uhakika. Kwa nini? (Biblia inasema Mungu aliumba ndege na wanyama wa mwitu.) Hiyo ina msingi katika Biblia. Ninataka mzungumze kuhusu maarifa yenu wenyewe kuona iwapo mna maarifa ya kweli ya matendo ya Mungu. Je, mna hakika kuhusu jibu lenu au la? (Kwa sababu vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu vinaimarishana na kuzuiana, na kutegemeana vyenyewe. Mungu aliumba kuku, anayeweza kutaga mayai, na kuku anahitaji kuatamiza mayai. Kuna haja hiyo na hali ya utendaji.) Baadhi ya ndugu na dada walicheka. Mbona msizungumze kuhusu jambo hilo? Mungu aliumba kuku, halafu akampa uwezo wa kuzaa uhai.) Uwezo gani? (Uwezo wa kuatamiza mayai, na uwezo wa kufanya maisha yaendelee.) Mm, maelezo haya yanakaribia ukweli. Je, ndugu au dada wengine wana maoni? Zungumza kwa huru na kuwasiliana. Hii ni nyumba ya Mungu. Ni kanisa. Ikiwa mna kitu cha kusema, semeni. (Hivi ndivyo ninavyofikiria: Mungu aliumba vitu vyote, na kila kitu alichoumba ni kizuri na kamili. Kuku ni kiumbe hai na ana kazi ya kuzaa na kuatamiza mayai. Hili ni kamili. Kwa hiyo, kuku alitangulia, na kisha yai. Hiyo ndiyo taratibu.) (Kwanza kuku, na kisha yai.) Hili ni hakika. Si fumbo la maana sana, lakini watu wa dunia huliona kuwa la maana sana na hutumia falsafa kwa utoaji hoja. Mwishowe, bado huwa hawana hitimisho. Jambo hili linahusiana na mwanadamu kutojua kwamba aliumbwa na Mungu. Wanadamu hawajui kanuni hii, na pia hawaelezi wazi iwapo yai au kuku anapaswa kutangulia. Hawajui ni nini kinapaswa kutangulia, hivyo kila mara wao hushindwa kupata jibu. Basi Niambie: Je, ni kuku angepaswa kutangulia au yai? Ni kawaida kabisa kwamba kuku alitangulia. Ikiwa yai lingetangulia kabla ya kuku, basi hiyo haingekuwa kawaida! Bila shaka kuku alitangulia. Hiki ni kitu rahisi sana. Hakiwahitaji nyinyi kuwa wenye maarifa mengi. Mungu aliumba hivi vyote. Kusudi lake la mwanzo lilikuwa ni mwanadamu kuvifurahia. Kuku akiwepo tu yai litakuja kwa kawaida. Je, hilo si dhahiri? Ikiwa yai lingeumbwa kwanza, je, halingehitaji kuku kuliatamiza? Kuumba kuku moja kwa moja ni rahisi kabisa. Hivyo Mungu aliumba kuku moja kwa moja, na kuku angeweza kutaga mayai na pia kuatamiza vifaranga wadogo, huku mwanadamu akiweza kula kuku pia. Je, hilo si la kufaa zaidi. Vile Mungu afanyavyo mambo ni kwa maneno machache ya wazi na sio kwa usumbufu. Yai pia lina babu, na huyo ni kuku. Alichoumba Mungu ni kiumbe chenye uhai! Mwanadamu aliyepotoshwa ni wa upuuzi na wa dhihaka, kila mara anajitatanisha katika mambo haya rahisi, na mwishowe hata anafikia kifungu kizima cha hoja za uwongo. Hayo ni ya kitoto! Uhusiano kati ya yai na kuku ni dhahiri: Kuku alitangulia. Hayo ndiyo maelezo sahihi kabisa, njia sahihi kabisa ya kulielewa, na jibu sahihi kabisa. Hii ni ya kweli.
Hapo mwanzo, tulizungumza kuhusu mazingira ya kuishi ya wanadamu na kile Mungu alifanya, alitayarisha, na kushughulikia kwa ajili ya mazingira haya, na vilevile mahusiano kati ya vitu vyote ambavyo Mungu aliwatayarishia wanadamu na jinsi Mungu alishughulikia mahusiano haya yote kuzuia vitu vyote kuleta madhara kwa wanadamu. Mungu pia alitatua vitu vya asili mbalimbali vinavyoletwa na vitu vyote na athari hasi iliyosababishwa navyo kwa mazingira ya wanadamu, Akaruhusu vitu vyote kuongeza hadi upeo shughuli za vitu hivyo, Akawaletea wanadamu mazingira ya kufaa, na Akafanya vitu vyote vya asili viwe vya manufaa, kuwawezesha wanadamu kuwa wepesi kubadilika kwa mazingira hayo na kuendelea na mfuatano wa kuzaa na wa maisha kwa kawaida. Kilichofuata kilikuwa chakula kilichohitajika na mwili wa mwanadamu—chakula cha kila siku na kinywaji. Hii pia ni hali muhimu ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu. Hiyo ni kusema, mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi tu kwa kupumua, kuwa na mwangaza wa jua au upepo pekee, au halijoto za kufaa tu. Wanahitaji pia kujaza matumbo yao. Vitu hivi vya kujaza matumbo yao vyote vimetayarishwa pia na Mungu kwa ajili ya wanadamu—hiki ni chanzo cha chakula cha wanadamu. Baada ya kuona mazao haya ya fahari na mengi—vyanzo vya chakula cha wanadamu na kinywaji—unaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha kupeana wanadamu na vitu vyote? Unaweza kusema hivyo bila shaka. Ikiwa Mungu angeumba tu miti na nyasi au hata viumbe mbalimbali vyenye uhai Alipoumba vitu vyote, na wanadamu hawangekula chochote kati ya hivyo, je, wanadamu wangeweze kuendelea kuishi hadi wakati huu? Na je, viumbe mbalimbali vyenye uhai na mimea miongoni mwa vitu vyote ambavyo Mungu aliumbe vingekuwa vya ng’ombe na kondoo kula, au vya pundamilia, paa na aina nyingine mbalimbali za wanyama—kwa mfano, simba wale chakula kama pundamilia na paa, chui wakubwa wenye milia wale chakula kama wanakondoo na nguruwe—lakini kusiwe na hata kitu kimoja cha kufaa wanadamu kula? Je, hilo lingefaulu? Halingefaulu. Ingekuwa hivyo basi wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi. Na je, wanadamu wangekula tu majani ya miti? Hilo lingefaulu? Matumbo ya wanadamu hayangeweza kustahimili. Huwezi kujua usipojaribu, lakini mara unapofanya hivyo utajua vizuri sana. Basi ungeweza kula nyasi ambayo ng’ombe na kondoo hutayarishiwa? Huenda ikawa sawa ukijaribu kidogo tu, lakini ukiendelea kula kwa muda mrefu, hutadumu kwa muda mrefu. Vitu vingine vinaweza kuliwa na wanyama, lakini wanadamu wakivila watapata sumu. Kuna vitu vingine vyenye sumu ambavyo wanyama wanaweza kuvila bila kuathiriwa, lakini wanadamu hawawezi kufanya vivyo hivyo. Mungu aliwaumba wanadamu, hivyo Mungu anajua vizuri sana kanuni na muundo wa mwili wa mwanadamu na wanachohitaji wanadamu. Mungu ana hakika kamili kuhusu sehemu na vijenzi vyake, na inachohitaji, vilevile jinsi sehemu za ndani ya mwili wa mwanadamu hufanya kazi, hufyonza, huondosha, na kuvunjavunja kemikali mwilini. Watu hawana hakika kuhusu hili na wakati mwingine hula na kujaliza bila kujua. Wao hujaliza kupita kiasi na mwisho husababisha kutolingana nguvu. Ukila vitu hivi alivyokutayarishia Mungu, na ule na kuvifurahia kwa kawaida, hutakuwa na shida yoyote. Hata kama wakati mwingine una hali mbaya ya moyo na una ukwamaji wa damu, haidhuru. Unahitaji tu kula aina fulani ya mmea na ukwamaji utatatuliwa. Mungu ametayarisha vitu hivi vyote. Machoni mwa Mungu, wanadamu wako juu zaidi ya kiumbe chengine chote chenye uhai. Mungu alitayarishia kila aina ya mimea mazingira ya kuishi na Akatayarishia kila aina ya wanyama chakula na mazingira ya kuishi, lakini mahitaji ya wanadamu pekee kwa mazingira yao ya kuishi ndiyo makali zaidi na yasiyostahamili kutotunzwa. La sivyo, wanadamu hawangeweza kuendelea kukua na kuzaa na kuishi kwa kawaida. Mungu anajua hili vizuri zaidi moyoni Mwake. Mungu alipofanya hili, alilipa umuhimu zaidi kuliko kitu chengine chochote. Labda huwezi kuhisi umuhimu wa kitu fulani kisicho na maana unachokiona na kufurahia au kitu unachohisi ulizaliwa nacho na unaweza kufurahia, lakini Mungu alikuwa tayari amekutayarishia zamani sana. Mungu ameondoa na kutatua kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo vipengele vyote hasi visivyofaa kwa wanadamu na vinavyoweza kudhuru mwili wa mwanadamu. Nini ambacho hiki kinaweka wazi? Je, kinahakikisha mtazamo wa Mungu kwa wanadamu Alipowaumba wakati huu? Mtazamo huo ulikuwa upi? Mtazamo wa Mungu ulikuwa wa msimamo na maana kubwa, na Hakustahimili kuingilia kati kwa vipengele au hali au nguvu zozote za adui isipokuwa Mungu. Kutokana na hili, unaweza kuona mtazamo wa Mungu alipoumba wanadamu na anaposimamia wanadamu wakati huu. Mtazamo wa Mungu ni upi? Kupitia kwa mazingira ya kuishi na kuendelea kuishi ambayo wanadamu wanafurahia pamoja na chakula chao cha kila siku na kinywaji na mahitaji ya kila siku, tunaweza kuona mtazamo wa Mungu katika kudumisha kuzaa na kuishi kwa wanadamu na wajibu Alionao kwao, na vilevile uamuzi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu wakati huu. Je, tunaweza kuona uhalisi wa Mungu kupitia kwa haya yote? Tunaweza kuona ustaajabishaji wa Mungu? Tunaweza kuona kutoweza kueleweka kwa Mungu? Tunaweza kuona kudura ya Mungu? Mungu anatumia tu njia Yake ya uweza na hekima kuwapa wanadamu wote, na vilevile kuvipa vitu vyote.
Licha ya hayo, baada ya Mimi kusema mengi sana, mnaweza kusema kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo.) Bila shaka! Hili ni hakika. Upeanaji wa Mungu wa vitu vyote ni wa kutosha kuonyesha kwamba Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote, kwa sababu Yeye ni chanzo cha upeanaji ambao umewezesha vitu vyote kuwepo, kuishi, kuzaa, na kuendelea. Mbali na Mungu hakuna mwingine. Anapeana mahitaji yote ya vitu vyote na mahitaji yote ya wanadamu, bila kujali iwapo ni hitaji la msingi kabisa, wanachohitaji watu kila siku, au upeanaji wa ukweli kwa roho za watu. Kutokana na mitazamo yote, inapofikia utambulisho wa Mungu na hadhi Yake kwa wanadamu, ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hii ni hakika bila shaka. Mungu ni Mtawala, Bwana, na Mpaji wa dunia hii yakinifu ambayo watu wanaweza kuona kwa macho yao na kuhisi. Kwa wanadamu, je, huu si utambulsho wa Mungu? Hii ni kweli kabisa. Hivyo unapoona ndege wakiruka angani, unapaswa kujua kwamba Mungu aliumba vitu vinavyoweza kuruka. Lakini kuna viumbe vyenye uhai vinavyoogelea majini, navyo pia huendelea kuishi kwa njia mbalimbali. Miti na mimea inayoishi ndani ya udongo huchipuka katika majira ya kuchipuka na huzaa matunda na kupoteza majani katika majira ya kupukutika kwa majani, na ifikapo wakati wa majira ya baridi majani yote huwa yameanguka na kupitia katika majira ya baridi. Hiyo ni njia yao ya kuendelea kuishi. Mungu aliumba vitu vyote, na kila kimojawapo huishi kupitia taratibu mbalimbali na njia mbalimbali na hutumia mbinu mbalimbali kuonyesha nguvu zake na taratibu ya maisha. Haijalishi ni mbinu gani, yote iko chini ya utawala wa Mungu. Ni nini kusudi la Mungu la kutawala taratibu zote mbalimbali za maisha na viumbe vyenye uhai? Je, ni kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu? (Ndiyo.) Anadhibiti sheria zote za maisha kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hii inaonyesha hasa vile kuendelea kuishi kwa wanadamu ni muhimu kwa Mungu. Unaweza kuona hilo sasa?
Wanadamu kuweza kuendelea kuishi na kuzaa kwa kawaida ni jambo la muhimu zaidi kwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu daima huwapa wanadamu na vitu vyote. Anapeana vitu vyote kwa njia mbalimbali, na chini ya hali za kudumisha kuendelea kuishi kwa vitu vyote, Anawawezesha wanadamu kuendelea kusonga mbele ili Aweze kudumisha kuwepo kwa kawaida kwa wanadamu. Hivi ndivyo vipengele viwili tunavyowasiliana leo. Vipengele hivi ni vipi? (Kutokana na mtazamo mkubwa, Mungu aliwaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Hicho ni kipengele cha kwanza. Pia, Mungu alitayarisha hivi vitu yakinifu ambavyo wanadamu wanahitaji na wanaweza kuona na kugusa.) Tumewasilisha mada yetu kuu kupitia vipengele hivi viwili. Mada yetu kuu ni gani? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Mnapaswa sasa kuwa na ufahamu fulani wa mbona Niliwasilisha maudhui haya chini ya mada hii. Je, kumekuwa na majadiliano yoyote yasiyohusiana na mada kuu? Hakuna, sivyo? Labda baada ya kusikia mambo haya, wengine wenu wanaweza kupata ufahamu fulani na kuhisi kwamba maneno haya ni muhimu sana, lakini wengine huenda wakapata tu ufahamu kidogo wa kawaida na kuhisi kwamba maneno haya hayana maana. Haijalishi vile nyinyi mlio hapa mtaelewa hili wakati huu, mnapoendelea kupitia matukio itafika siku ambayo ufahamu wenu utafikia kiwango fulani, yaani, wakati maarifa yenu ya matendo ya Mungu na Mungu Mwenyewe yatafikia kiwango fulani, mtatumia maneno yenu wenyewe ya kiutendaji kuwasilisha ushuhuda wa maana na wa kweli kuhusu matendo ya Mungu.
Ninafikiri ufahamu wenu sasa bado ni sahili na wa kawaida, lakini mnaweza angaa, baada ya kunisikiliza Nikiwasilisha vipengele hivi viwili, kutambua ni mbinu zipi Mungu hutumia kuwapa wanadamu au ni vitu vipi Mungu huwapa wanadamu? Je, mna wazo la msingi na vilevile ufahamu wa msingi? Lakini vipengele hivi viwili Nilivyowasilisha vinahusiana na Biblia? (La.) Vinahusiana na hukumu na kuadibu kwa Mungu katika Enzi ya Ufalme? (La.) Basi kwa nini Niliwasilisha vipengele hivi? Je, ni kwa sababu watu ni lazima wavielewe ili kumjua Mungu? (Ndiyo.) Ni muhimu sana kuvijua na pia ni muhimu sana kuvielewa.Usizuiwe tu kwa Biblia, na usizuiwe tu kwa Mungu kuhukumu na kuadibu wanadamu ili kuelewa kila kitu kuhusu Mungu. Ni nini kusudi la Mimi kuruka kutoka eneo la kuwasilisha Biblia na kuondoka katika maneno ya Mungu kutoka kwa Enzi ya Ufalme? Ni kuwafanya watu wajue kwamba Mungu si Mungu wa watu Wake waliochaguliwa pekee. Wewe sasa unamfuata Mungu, na Yeye ni Mungu wako, lakini kwa wale walio nje ya watu wanaomfuata Mungu, je, Mungu ni Mungu wao? Je, Mungu ni Mungu wa watu wote walio nje ya wale wanaomfuata Yeye? (Ndiyo.) Basi Mungu ni Mungu wa vitu vyote? (Ndiyo.) Basi Mungu hutenda kazi Yake na kutekeleza matendo Yake kwa wale tu wanaomfuata Yeye? (La.) Eneo lake ni ulimwengu mzima. Kutoka kwa mtazamo mdogo, eneo lake ni wanadamu wote na miongoni mwa vitu vyote. Kutokana na mtazamo mkubwa, ni ulimwengu mzima. Hivyo tunaweza kusema kwamba Mungu hufanya kazi Yake na kutekeleza matendo Yake miongoni mwa wanadamu wote. Hili ni la kutosha kuwafanya watu wajue yote kuhusu Mungu Mwenyewe. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Unamwona Mungu kama asiye na maana sana. Ni athari gani ungepata kutoka kwa matokeo kama hayo? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako wa Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kupeana vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na upeanaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote. Vitu vyote viko chini ya mamlaka ya sheria zao, ambazo ziko chini ya utawala wa Mungu, na vitu vyote vina sheria zao za kuendelea kuishi, ambazo pia ziko chini ya utawala wa Mungu, huku majaliwa ya wanadamu na wanachohitaji pia vikihusiana kwa karibu na utawala wa Mungu na upeanaji Wake. Ndiyo maana, chini ya utawala wa Mungu na uongozi, wanadamu na vitu vyote vinahusiana, vinategemeana, na vinafumana. Hili ni kusudi na thamani ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Unaelewa hili sasa? (Ndiyo.) Iwapo unaelewa basi acha tumalizie mawasiliano yetu hapa siku hii. Kwaheri!
Februari 2, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni