![]() |
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX |
Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)
Mwenyezi Mungu alisema, Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu. Matendo haya yanayofanywa na Mungu hayakomei tu kwenye maandalizi Yake ya mazingira kwa ajili ya watu kuendelea kuishi na riziki zao za kila siku–yana mawanda mapana zaidi kuliko hayo. Licha ya aina mbili hizi za kazi, pia Anaandaa mazingira mengi na hali kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni lazima kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Hii ni mada nyingine ambayo tutaijadili leo, ambayo pia inahusiana na matendo ya Mungu. Vinginevyo, kuizungumzia hapa isingekuwa na maana. Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu lakini wana maana ya moja kwa moja na ya kimafundisho ya "Mungu," ya neno hilo, au ya vipengele vyote vya kile Mungu anacho na alicho, huo sio uelewa wa kweli. Sasa, njia kwa ajili ya maarifa ya Mungu ni ipi? Ni kumjua Yeye, kujua kila kipengele Chake kupitia matendo Yake. Kwa hiyo, kinachofuata tunapaswa kushiriki kuhusu matendo ya Mungu pale alipoumba vitu vyote.
Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida. Chini ya uangalizi Wake, chini ya kanuni Yake, vitu vyote vimekuwa vikiendelea kwa kawaida sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu. Hakuna kitu hata kimoja kinaweza kubadilisha sheria hizi, na hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kuziharibu sheria hizi. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu ndipo viumbe vyote vinaweza kuongezeka, na kwa sababu ya kanuni na usimamizi Wake ndipo vitu vyote vinaweza kuendelea kuishi. Hii ni kusema kwamba chini ya kanuni ya Mungu, viumbe vyote vinakuwepo, vinastawi, vinatoweka, na kuzaliwa upya kwa namna ya mpangilio. Msimu wa machipuo unapowadia, mvua ya manyunyu huleta hisia hiyo ya machipuo na kuipatia nchi unyevunyevu. Ardhi huanza kuyeyuka, majani huota na kujipenyeza juu ya udongo na miti taratibu hubadilika kuwa ya kijani. Viumbe hai hivi vyote vinaleta uzima mpya katika dunia. Hii ndiyo picha ya viumbe vyote kuwepo na kustawi. Wanyama wa kila aina pia hutoka matunduni mwao ili kupata uvuguvugu wa msimu wa machipuo na kuanza mwaka mpya. Viumbe vyote vinaota jua kwenye joto wakati wa kiangazi na kufurahia uvuguvugu unaoletwa na msimu huu. Vinakua haraka; miti, nyasi, na aina zote za mimea inakua haraka sana, kisha inachanua na kuzaa matunda. Viumbe vyote vinakuwa vimetingwa sana wakati wa kiangazi, binadamu wakiwemo. Katika msimu wa majani kupukutika, mvua inaleta utulivu wa msimu wa majani kupukutika, na aina zote za viumbe hai vinaanza kupitia uzoefu wa msimu wa kiangazi. Viumbe vyote vinazaa matunda, na binadamu pia wanaanza kuvuna aina zote za vitu kwa sababu ya msimu wa majani kupukutika kuzalisha viumbe vyote hivi, ili kuandaa chakula kwa ajili ya msimu wa baridi. Katika msimu wa baridi viumbe vyote taratibu vinaanza kupumzika katika ubaridi, kuwa kimya, na watu pia wanachukua pumziko wakati wa msimu huu. Mabadiliko haya kutoka masimu wa machipuo kwenda msimu wa kiangazi kwenda msimu wa mapukutiko na kwenda msimu wa baridi--mabadiliko haya yote yanatokea kulingana na sheria zilizoanzishwa na Mungu. Anawaongoza viumbe na binadamu kwa kutumia sheria hizi na Ameanzisha maisha yenye utajiri na ya kupendeza kwa ajili ya mwanadamu, Akiandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo yana halijoto tofautitofauti na misimu tofautitofauti. Chini ya mazingira haya yaliyopangiliwa kwa ajili ya kuendelea kuishi, binadamu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka kwa namna ya mpangilio. Binadamu hawawezi kuzibadilisha sheria hizi, na hakuna mtu hata mmoja au kiumbe ambacho kinaweza kuzivunja. Haijalishi ni mabadiliko makubwa kiasi gani yanatokea duniani, sheria hizi zinaendelea kuwepo na zipo kwa sababu Mungu yupo. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Kwa aina hii ya mpangilio, mazingira makubwa, maisha ya watu yanaendelea ndani ya sheria na kanuni hizi. Sheria hizi ziliendeleza kizazi baada ya kizazi cha watu na kizazi baada ya kizazi cha watu wameendelea kuishi ndani ya sheria hizi. Watu wamefurahia viumbe na mazingira haya ya mpangilio kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kizazi baada ya kizazi cha binadamu. Ingawa watu wanahisi kwamba aina hii ya sheria ni za kiasili, ingawa wanazipuuza kabisa sheria hizo, na ingawa hawawezi kuhisi kuwa Mungu ndiye anaweka utaratibu wa sheria hizi, kwamba Mungu anatawala sheria hizi, haijalishi, Mungu siku zote anajihusisha katika kazi hii isiyobadilika. Kusudi lake katika kazi hii isiyobadilika ni kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na ili binadamu waweze kuendelea.
1. Mungu Anaweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote
Leo nitazungumza juu ya mada ya jinsi aina ya kanuni hizi ambazo Mungu anazileta kwa binadamu na viumbe vyote humlea binadamu. Kwa hiyo mada hii ni nini? Ni jinsi ambavyo aina hii ya sheria ambazo Mungu amezileta kwa viumbe vyote humlea binadamu. Hii ni mada kubwa, kwa hiyo tunaweza kuigawanya katika sehemu kadhaa na kuzijadili moja baada ya nyingine ili ziweze kufafanuliwa vizuri kwenu. Kwa njia hii itakuwa rahisi kwenu kupata maana na taratibu mnaweza kuielewa.
Kwanza, Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji–haya yote ni nini? Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, je, hiyo inamaanisha nini? Ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha mlima ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha tambarare ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Alipokuwa anaumba viumbe vyote pia Aliamua mawanda ya jangwa, vilevile mawanda ya vilima na uwiano wao, na vile vilivyopakana navyo–pia Aliamua yote haya. Aliamua mawanda ya mito na maziwa Alipokuwa anaviumba–vyote vina mipaka yao. Kwa hiyo ina maana gani tunaposema "mipaka"? Tulizungumza tu kuhusu ambavyo utawala wa Mungu kwa vitu vyote unavyoanzisha sheria kwa viumbe vyote. Kwa mfano, mawanda na mipaka ya milima havitaongezeka au kupungua kwa sababu ya mzunguko wa dunia au muda kupita. Hii haibadiliki: Hii "isiyobadilika" ni kanuni ya Mungu. Kwamaeneo ya tambarare, mawanda yao, kile kilichopakana nayo, hii imewekwa na Mungu. Yana mipaka, na tuta haliwezi kutokea tu bila mpangilio, katikati ya tambarare. Tambarare haiwezi tu kubadilika na kuwa mlima–hii haitatokea. Sheria na mipaka tuliyoizungumzia inarejelea hili. Kwa jangwa, hatutataja wajibu wa jangwa au mandhari nyingineyo au eneo la kijiogarafia hapa, ni mipaka yake tu. Chini ya kanuni ya Mungu mawanda ya jangwa nayo pia hayatapanuka. Hii ni kwa sababu Mungu amelipatia sheria yake, mawanda yake. Eneo lake ni kubwa kiasi gani na wajibu wake ni upi, kile kilichopakana nalo, na lipo mahali gani–hii imeshawekwa na Mungu tayari. Halitazidisha mawanda yake, kuhamisha sehemu yake, na halitaongeza eneo lake kiholela tu. Ingawa mtiririko wa maji kama vile mito na maziwa yote yapo katika mpangilio na mwendelezo, hayajawahi kwenda nje ya mawanda yao au kwenda zaidi ya mipaka yao. Yote yanafuata mwelekeo mmoja kwa namna ya mpangilio, yakitiririka kuelekea mwelekeo yanaopaswa kwenda. Kwa hiyo chini ya sheria ya kanuni ya Mungu, hakuna mto au ziwa ambalo litakauka kiholela tu, au kubadilisha mwelekeo au kiwango cha kutiririka kwake kiholela tu kwa sababu ya mzunguko wa dunia au kupita kwa muda. Hii yote ipo ndani ya maarifa ya Mungu, ndani ya kanuni Yake. Hiyo ni sawa na kusema, viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu katikati ya binadamu vina sehemu zao, maeneo yao, na mawanda yao yasiyobadilika. Yaani, Mungu alipoviumba viumbe vyote, mipaka yao ilianzishwa na hii haiwezi kugeuzwa kiholela tu, kufanywa upya au kubadilishwa. "Kiholela" inamaanisha nini? Ina maana kwamba havitahama, kupanuka, au kubadilisha umbo lao asilia bila mpangilio kwa sababu ya hali ya hewa, halijoto, au kasi ya mzunguko wa dunia. Kwa mfano, mlima una kimo fulani, kitako chake ni cha eneo fulani, una mwinuko fulani, na una kiasi fulani cha uoto. Hii yote imepangwa na kukokotolewa na Mungu na kimo au eneo lake halitabadilika kiholela. Kwa tambarare, idadi kubwa ya binadamu wanaishi katika tambarare, na hakuna mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri maeneo yao au thamani ya uwepo wao. Sio hata kile ambacho kimejumuishwa katika mandhari haya na mazingira ya kijiografia ambayo yaliumbwa na Mungu yatabadilika kiholela. Kwa mfano, vipengele vya jangwa ni vipi, ni aina gani ya madini yaliyopo chini ya ardhi, yanajumuisha mchanga kiasi gani na rangi ya mchanga, upana wake–haya hayatabadilika kiholela. Kwa nini hayatabadilika kiholela? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiogorafia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya–yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu–yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio. Sasa kwa nini Mungu anasimamia mandhari yote haya yaliyopo duniani kwa njia hii? Kusudi ni ili viumbe hai vinavyoendelea kuishi katika mazingira mbalimbali ya kijiografia yote yatakuwa na mazingira imara, na kwamba wataweza kuendelea kuishi na kuongezeka katika mazingira hayo imara. Viumbe vyote hivi–vile vinavyotembea na vile ambavyo havitembei, vile ambavyo vinapumua kupitia pua zao na vile ambavyo havipumui—vinaunda mazingira ya tofauti kabisa kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ni aina hii tu ya mazingira ndiyo inaweza kulea kizazi baada ya kizazi cha binadamu, na ni aina hii tu ya mazingira inaweza kuruhusu binadamu kuendelea kuishi kwa amani, kizazi baada ya kizazi.
Mmeona nini kutokana na kile ambacho nimekizungumzia? Ni kwamba sheria za Mungu katika utawala wake wa vitu vyote ni muhimu sana–muhimu sana! Je, masharti ya awali ni yapi kwa viumbe vyote kukua ndani ya sheria hizi? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu. Ni kwa sababu ya kanuni Yake ndipo viumbe vyote vinafanya kazi zao ndani ya kanuni Yake. Kwa mfano, milima inalea misitu, halafu misitu inalea na kuwalinda ndege mbalimbali na wanyama wanaoishi ndani yake. Tambarare ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya binadamu kupanda mazao vilevile kwa ajili ya ndege na wanyama mbalimbali. Zinaruhusu idadi kubwa ya binadamu kuishi katika ardhi tambarare na kutoa hali isiyo na taabu katika maisha ya binadamu. Na tambarare pia zinajumuisha ukanda wa mbuga—malundo ya ukanda wa mbuga. Ukanda wa mbuga ni uoto wa nchi. Unalinda ardhi na kuwalea ng'ombe, kondoo na farasi wanaoishi katika ukanda wa mbuga. Jangwa pia linafanya kazi yake. Sio sehemu kwa ajili ya binadamu kuishi; jukumu lake ni kufanya hali ya hewa ya unyevunyevu kuwa kavu. Kutiririka kwa mito na maziwa kunaleta hali isiyo ya usumbufu kwa ajili ya watu kunywa maji na kwa mahitaji ya viumbe vyote. Vyovyote vile yanavyotiririka, watu watakuwa na maji kwa ajili ya kunywa. Hii ni mipaka iliyochorwa na Mungu kwa ajili ya mandhari mbalimbali. Kwa sababu ya mipaka hii ambayo Mungu ameichora, mandhari mbalimbali yamezalisha mazingira tofautitofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na mazingira haya kwa ajili ya kuendelea kuishi yamekuwa na hali isiyokuwa na usumbufu kwa ajili ya aina tofautitofauti ya ndege na wanyama na vilevile kuleta nafasi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kutokana na hili, mipaka kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa viumbe hai mbalimbali imeendelezwa. Hiki ndicho tutakachokwenda kuzungumzia baadaye.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni