Jumapili, 28 Januari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Mwenyezi Mungu alisema, Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. Kwa hiyo hatuthubutu kuyataja au kuyatumia. Je, na kama yakikanushwa mara tu tunapoyatumia? Na je, tukikosolewa? "Sasa Nawaambieni kwamba mnaweza kuyatumia mambo haya kwa ujasiri. Lakini ni lazima mpitie ukaguzi wa ndugu zenu wa kiume na wa kike. Usiwe wa kujidai, na kusema: "Mungu amesema wakati huu tunaweza kutumia mambo haya kwa ujasiri, kwa hiyo tutatumia mambo haya kwa ujasiri." Kuwa na ujasiri sio kuenea pote au kuwa wenye dharau. Lazima kuwe na mipaka ya kuwa na ujasiri, ni lazima kukubaliane na kanuni, na ndugu wa kiume na wa kike wanapaswa kulifikiria kuwa linafaa. Mtu fulani akisema, "Hili halikubaliki," basi si unahitaji kulibadilisha? Je, watu wakaidi ni watu wema? (Hapana.) Haishauriwi kuwa hivyo. Ni lazima usikilize maoni ya wengine, na unapowasikia wakisema hivi, unasema, "Uko sawa. Ni lazima nilibadilishe." Baada ya kulibadilisha, watu wengine husema: "Uko karibu hapo, nahisi vyema kuhusu hili. Liko sawa, limefaulu." Safi sana! Kwa kufanya mambo kwa njia hii, kipengele kimoja ni kwamba mnaweza kuingia kwa kina katika kipengele cha weledi, na muwe wakomavu na wenye uzoefu; kipengele kingine ni kwamba nyinyi pia mna uwezo wa kujifunza mambo mengi; na bado kipengele kingine ni kwamba mmejifunza somo. Unapokabiliwa na masuala, hupaswi kujidai, ukifikiri, "Nina kauli ya mwisho. Hamna sifa ya kuzungumza. Ninaelewa kanuni, nyinyi mnaelewa nini? Hamuelewi, ninaelewa!" Huku ni kujidai. Kuwa wa kujidai ni tabia potovu ya kishetani; si kitu kilicho ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kwa hiyo, ni nini maana ya kutokuwa wa kujidai? (Kupata mapendekezo kutoka kwa kila mtu, na kila mtu kuyapima pamoja.) Wakati kila mtu anapoliidhinisha, na kila mtu anapokubaliana nalo, basi mmefanya kazi nzuri. Mradi baadhi ya watu au kikundi cha watu hudakiza kipingamizi, basi ni lazima muwe mahsusi zaidi kuhusu kipengele cha weledi. Ni lazima msijifanye kutotambua na kusema: "Nani? Aliyedakiza nini? Ni nini kinachoendelea? Je, wewe ndiye unayelielewa hili au ni mimi? Je, unaelewa hili vyema kuniliko? Unaelewa nini? Huelewi!" Hii ni tabia mbaya, sivyo? Ijapokuwa aliyedakiza kipingamizi huenda asielewe vizuri sana na anaweza kuwa mlei, na unaweza kuwa na haki na kile ulichokifanya kinaweza kuwa sahihi, tatizo hapa ni tabia yako. Kwa hiyo ni nini maonyesho na vitendo sahihi vinavyokubaliana na kanuni na kukubaliana na ukweli? Unasema: "Tatizo ni nini? Acha niangalie. Sio mimi tu, lakini kila mtu anaangalia. Wale ambao wana mapendekezo fulani kuhusu kipengele hiki au utambuzi fulani ndani yake, au ambao wana uzoefu fulani katika kipengele hiki, hebu sote tuangalie pamoja na tuweze kuzungumza juu yake. "Ikiwa kila mtu huamini kweli kuwa kufanya kitu kwa njia hii ni vibaya, kwamba kuna shida kidogo hapa, na unatazama mara moja na huwezi kuona tatizo, unatazama mara mbili na bado huwezi kuliona, kisha unaangalia mara tatu au mara nne na unavyozidi kuangalia ndivyo unavyozidi kuona kuna shida, basi hili kwa kweli ni tatizo. Na lazima ulisahihishe, lifanye liwe zuri na uombe mawazo ya kila mtu. Je, hili ni jambo jema au jambo baya? (Ni jambo jema.) Unaomba mawazo ya kila mtu, kila mtu analizungumzia, unashirikiana pamoja na Roho Mtakatifu anakupa nuru; unafuata hilo, na tatizo linarekebishwa ipasavyo. Kila mtu huangalia na kusema, "Hilo ni sawa, na ni bora zaidi kuliko hapo awali!" Je, si huu ni mwongozo wa Mungu? Hili ni jambo kubwa! Unapofanya mambo kwa njia hii, kama wewe hujidai, unapoacha mawazo yako mwenyewe na fikira zako mwenyewe, na unapotenda ukweli, unanyenyekea na kusikiliza mawazo ya wengine, kisha ni nini hutokea? Wewe hupata fursa ya Roho Mtakatifu kufanya kazi kwako na Roho Mtakatifu hukupatia nuru. Nini hutokea wakati Roho Mtakatifu anapokupatia nuru? Umejifunza kitu kingine cha weledi. Je, si hiki ni kitu chema?
Mara unapokuwa umepitia hili, wewe hufikiri, "Ninapokabiliwa na masuala, ni lazima nisijidai. Kila mtu hunichukia ninapojidai." Wakati kila mtu anapomchukia mtu fulani, Mungu humchukia? (Ndiyo, Yeye humchukia.) Unajifunza somo, kweli? Unapotenda kwa njia hii daima, kipengele kimoja ni kwamba utaona maendeleo katika hali ya weledi ya wajibu wako, na Mungu atakupa nuru na kukubariki; kipengele kingine ni kwamba utakuwa na njia ya kufuata katika kutenda ukweli, utajua jinsi ya kutenda ukweli, hatua kwa hatua utakuja kuelewa kanuni na kupata njia, utajua jinsi ya kufanya mambo kwa namna ambayo itasababisha kupata nuru ya Mungu na uongozi, ni njia zipi za kufanya mambo ambazo humsababisha Mungu kukupuuza au kukuchukia, na jinsi ya kufanya mambo kwa njia ambayo inaweza kubarikiwa na Mungu. Watu wanapopata baraka za Mungu na nuru, kuna furaha au huzuni ndani ya mioyo yao? Kuna furaha. Unapokuja kuwajibika kwa kile ambacho umekifanya mbele ya Mungu, utapata furaha na utafikiri, "Nilikifanya vizuri." Ndani yako utajisikia mwenye amani na furaha. Hisia hii ya amani na furaha hutolewa kwako na Mungu, na ni kuchochea ulikopewa na Roho Mtakatifu. Ikiwa hutendi hili lakini daima huhimili kwa njia zako mwenyewe, ukisema, "Sitamsikiliza mtu yeyote. Hata nikisikiliza, nitaonekana tu kusikiliza na sitabadilika. Nitafanya mambo kwa njia hii, ninahisi niko sawa na nahisi nimethibitishwa kabisa, "ni nini kitakachotokea? Huenda kuwa umethibitishwa na huenda kusiwe na kosa katika kile ufanyacho, huenda hujafanya makosa yoyote na huenda ukaelewa kipengele cha weledi vyema zaidi kuliko wengine, lakini mara unapofanya aina hizi za maonyesho na kutenda kwa njia hii, wengine wataona na watasema: "Tabia ya mtu huyu si nzuri. Unapokabiliwa na masuala, huwa hawakubali lakini hupinga kitu chochote mtu mwingine yeyote anachosema, kama kiko sahihi au la. Mtu huyu huwa hakubali ukweli." Watu wanaposema wewe hukubali ukweli, Mungu atafikiri nini? Je, Mungu anaweza kuona maonyesho haya yako? Bila shaka, Mungu anaweza kuyaona. Mungu hachunguzi tu chokomeani mwa moyo wa mwanadamu, Yeye pia huangalia kila kitu usemacho na kufanya wakati wote na mahali pote. Na Anapoona mambo haya, Yeye hufanya nini? Yeye husema: "Wewe umefanywa mgumu. Uko jinsi hii katika hali ambapo wewe uko sawa, na uko jinsi hii pia katika hali ambapo umekosea. Bila kujali uko katika hali gani, kila kitu unachofichua na kuonyesha ni kupingana na upinzani. Hukubali hata kidogo mawazo au mapendekezo ya mtu yeyote mwingine. Moyo wako unapingana kabisa, kukataa na kutokubali mawazo ya wengine. Wewe ni mgumu sana!" Ni kwa njia gani unakuwa mgumu? Kuwa kwako mgumu ni kwamba maonyesho yako sio njia mbaya ya kufanya mambo au tabia mbaya, lakini kwa usahihi zaidi ni ufichuzi wa tabia yako. Je, tabia yako imefichua nini? Unauchukia ukweli na una uhasama mintarafu ya ukweli. Na wakati umefafanuliwa kama mtu ambaye ana uhasama mintarafu ya ukweli, machoni mwa Mungu uko katika shida. Si zaidi ya haya, kila mtu atasema, "Mtu huyu ana tabia mbaya, yeye ni mkaidi na mwenye kiburi. Mtu huyu ni vigumu kukubaliana naye, hana matendo ya ukweli na hapendi ukweli. Hajawahi kuukubali ukweli." Si zaidi ya haya, kila mtu atakutathmini kwa njia hii; lakini tathmini hii inaweza kuamua jaala yako? Watu hufanya tathmini yako, lakini hili haliwezi kuamua jaala yako. Lakini kuna jambo moja ambalo hupaswi kulisahau: Mungu huuchunguza moyo wa mwanadamu, na wakati huo huo Yeye huangalia kila kitu ambacho mtu husema na kufanya. Mungu akimfafanua mtu kwa kusema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," Yeye hamfafanui tu kwa kusema, "Mtu huyu ana tabia potovu kidogo na kwa kiasi kidogo si mtiifu," bali kwa usahihi zaidi Yeye anasema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," hii ni hoja kubwa au hoja ndogo? (Ni hoja kubwa.) Na hili husababisha shida? (Ndiyo.) Je, hili huleta shida gani? Shida hii haiko katika jinsi watu wengine hukuona au jinsi wanavyokutathmini, lakini liko katika jinsi Mungu anavyoona tabia yako potovu ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli. Hivyo ni vipi basi Mungu huona tabia yako ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, unajua? Mungu husema, "Ana uhasama mintarafu ya ukweli na hapendi ukweli." Je, Mungu huliona kwa jinsi gani? Ukweli hutoka wapi? Ukweli humwakilisha nani? (Humwakilisha Mungu.) Hivyo fikiria hili: Mungu anapaswa kuonaje tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, Yeye atalionaje? (Mungu huliona kuwa na uhasama kwelekea Kwake na kama adui Yake.) Na hili ni jambo zito? Mtu aliye na uhasama mintarafu ya ukweli ana uhasama mintarafu ya Mungu. Kwa nini Ninasema kuwa ana uhasama mintarafu ya Mungu? Je, huwa anamtukana Mungu? La. Huwa anampinga Mungu bayana? La. Je, huwa anamshushia Yeye hadhi kisiri? La. Hivyo kufichua tabia ya jinsi hii huwaje uhasama mintarafu ya Mungu? Je, si huu wote ni msukosuko wa bure? Kuna kitu ndani yake, sivyo? Unajua ni kitu gani? Mtu fulani ana tabia hii na hufichua aina hii ya tabia wakati wote na katika maeneo yote na, zaidi ya hayo, yeye huitegemea ili kuishi na haachi kamwe njia hii ambayo kwayo yeye huishi na kufanya mambo, na haitupi kamwe. Wewe hutegemea mambo na tabia hii ili kuishi, na wakati hakuna kitu kinachotokea, ikiwa mtu atasema kuwa una uhasama mintarafu ya Mungu, unaweza kukubaliana naye? Huwezi kukubaliana naye. Hata hivyo, matatizo yanapochipuka, unapokuwa na aina hii ya tabia, wewe huifichua wakati wote na mahali pote? Kwa hiyo hii ni tabia gani? Ni tabia ambayo ni uhasama mintarafu ya Mungu na uhasama mintarafu ya ukweli. Unayasaili maneno ya Mungu, unayachangua, unayachambua na kuyatilia shaka. Inamaanisha nini unapofanya mambo haya? Inamaanisha kwamba unaposikia maneno ya Mungu, wewe hufikiria, "Je, haya ni maneno ya Mungu? Sifikiri huu ni ukweli na sifikiri yote ni lazima yawe ni sahihi." Tabia yako imefichuliwa, ni kweli? Je, una uwezo wa kutii wakati unapofikiria jinsi hii? Hakika huna uwezo. Na kama huna uwezo wa kutii, Mungu bado ni Mungu wako? Hapana, Yeye si Mungu wako. Je, wewe basi humuona Mungu kama nini? Kama chombo cha kujifunza na cha shaka, na hata kama tu mtu wa kawaida, kama mtu mwenye tabia potovu kama tu mtu. Je, si hili linaletwa na tabia potovu ya mtu?
Wakati mtu amekwenda mbali hivyo na wakati ana uhusiano wa aina hii na Mungu, ni uhusiano gani uliopo kati ya mtu huyu na Mungu? Ni wa uhasama na yeye amekuwa mpinzani wa Mungu, sivyo? Ikiwa unamwamini Mungu lakini huwezi kuupata ukweli au kuukubali ukweli, Mungu si Mungu wako. Mungu hakuoni kama adui lakini wewe unamwona Mungu kama mpinzani wako na huwezi kukubali kwamba Yeye ni ukweli wako na njia yako, basi tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa jinsi gani? Unapokabiliwa na maswala unapaswa kwanza kufikiria, "Hali ni ipi hapa? Siielewi vizuri sana, na haiko dhahiri kwangu. "Bila kujali suala ni nini, hufafanui suala hilo kwanza, badala yake kwanza ni lazima uone kile maneno ya Mungu yanachosema juu yake. Unaweza kushindwa kupata maneno husika ya Mungu, na huenda pia usijue ni ukweli gani suala hili linahusisha, lakini unang'amua kanuni—ni kutii, kwanza kabisa. Kwanza kabisa, endelea kutii, tuliza moyo wako na usubiri, usiwe na mawazo au fikira za binafsi, subiri kwa muda na uone jinsi Mungu anavyopanga kukabiliana nalo na kile ambacho Mungu atafanya. Hili ni katika hali ambapo huelewi kabisa. Na je, wakati ambapo huelewi? Kwa mfano, mtu anatoa maoni; unashughulikiaje suala hili? Je, unalishughulikiaje kwa njia inayopatana na ukweli? Kwanza unalikubali; unasikiliza na kusema, "Haya yote ni nini? Aa, kuna shida kwangu kulifanya kwa njia hii? Ikiwa kuna shida, basi hebu tuangalie." Usiichukulie hoja hiyo kwa wepesi; inahusisha mambo katika upeo wa wajibu wako, kwa hiyo unapaswa kulitazama kwa uangalifu. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuchukua na hali sahihi ya kuwemo. Unapokuwa katika hali sahihi, wewe hufichua tabia ambayo imechoshwa na ukweli? (Hapana.) Hufichui tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli, na unapotenda kwa njia hii tabia yako ya upotovu inabadilishwa; unatenda ukweli. Unapotenda ukweli kwa njia hii, ni matokeo gani yanayofanikishwa? (Roho Mtakatifu hutuongoza.) Mwongozo wa Roho Mtakatifu ni kipengele kimoja. Kwa Mungu, unatenda ukweli. Wakati mwingine una mwongozo wa Roho Mtakatifu na tatizo linarekebishwa; wakati mwingine baada ya kusikia juu ya suala hili, unalielewa kwa urahisi, na unaliona likiwa rahisi sana. Hicho ni kitu ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanikisha na unahitaji tu kukirekebisha. Hii ni hoja ndogo. Na hoja kubwa ni ipi? Unapotenda kwa njia hii, Mungu hukuona kama mtu anayetenda ukweli na kama mtu anayependa ukweli, na Yeye huona kwamba wewe si mtu anayeuchukia ukweli au ana uhasama mintarafu ya ukweli. Wakati huo huo Mungu anapoona moyo wako, Yeye pia huona tabia yako. Hii ni hoja kubwa. Yaani, unalolifanya mbele za Mungu, unaloishi kwa kudhihirisha mbele ya Mungu na unachokifichua mbele ya Mungu, na vilevile mtazamo unaouchukua, mawazo uliyo nayo na hali uliyomo katika kila kitu unachokifanya—maonyesho haya yote unayo mbele ya Mungu—haya ndiyo mambo muhimu zaidi.
Watu daima wanalalamika juu ya watu na masuala, na hili ni tatizo kubwa. Je, wao daima hufikiri nini? Wanafikiri kuwa ni watu wengine ambao ni wakatili kwao, au kwamba wengine huyafanya mambo kuwa magumu kwa makusudi, au huyapata makosa tu na watu wengine. Je, mtazamo huu ni sahihi? (Hapana, si sahihi.) Kwa nini unasema hapana? Ni kosa kabisa kulalamika daima juu ya masuala na watu. Hawafanyi jitihada na ukweli, na wao wanajaribu daima kuepuka aibu na kutafuta uthibitisho mbele ya wengine au miongoni mwa watu wengine, na wao daima hutaka kutumia njia za kibinadamu kuzitatua hoja hizi zote. Hiki ndicho kikwazo kikubwa mno kwa kuingia kwa maisha. Kwa kufanya kwa njia hii, kutenda kwa njia hii na kumwamini Mungu kwa njia hii, hutaweza kamwe kupata ukweli, kwa kuwa kamwe huji mbele ya Mungu. Huji kamwe mbele ya Mungu kukubali vitu vyote ambavyo Mungu hupanga kwa ajili yako, hutumii kamwe ukweli ili kutatua mambo haya yote, na daima wewe hutaka kutumia mbinu za kibinadamu kuyatatua. Hivyo machoni pa Mungu, umeenda mbali sana na Yeye na sio tu kwamba moyo wako umekwenda mbali sana na Mungu, lakini mawazo yako yote, nia zako zote na hali yako yote havijawahi kuwa mbele ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu huwaona wale ambao hulalamika juu ya masuala na watu. Kwa hiyo, watu wengine ambao wana kipaji cha kuzungumza na ni wepesi kung'amua, hufikiria, "Nina ufasaha, na wakati ninapokuwa na watu wengine, wote hunihusudu na kunipenda. Wao hunitukuza, na watu wengi sana huridhishwa nami. "Je, hili ni la manufaa yoyote? Sifa yako njema miongoni mwa watu wengine imeanzishwa, lakini mbele ya Mungu, Amekupuuza daima, na anasema kuwa wewe ni mtu asiyemwamini Mungu na kwamba una uhasama mintarafu ya ukweli. Miongoni mwa wengine wewe hutenda kwa njia ambayo ni laini na ya hila, unaweza kumshughulikia mtu yeyote, una uwezo mkubwa wa kushughulikia hoja, na unaweza kukubaliana na mtu yeyote. Lakini mwishowe, kwa tathmini moja kutoka kwa Mungu utakwisha, utafika mwisho mbaya, na jaala yako itapangwa. Mungu atasema: "Huyu ni mtu asiyeamini, akipeperusha bendera ya imani katika Mungu ili kupata baraka. Huyu mtu ana uhasama mintarafu ya ukweli, hajawahi kamwe kufanya jitihada na ukweli, na hajawahi kuukubali ukweli." Mnafikiria nini juu ya aina hii ya tathmini? Je, hii ndiyo tathmini mnayoitaka? (Hapana.) Bila shaka sicho kile mnachokitaka. Labda watu wengine hawajali, na wao husema, "Sijali. Hatuwezi kumwona Mungu kwa njia yoyote. Suala la kweli zaidi ambalo tunalo ni kuwa tunapaswa kukubaliana na watu walio nasi. Ikiwa hatuwezi kufanya mahusiano haya yafaulu basi tunawezaje kuishi miongoni mwa watu hawa? Maisha yetu yangekuwa magumu sana. Angalau sana tunapaswa kukubaliana na watu hawa na kushughulikia mahusiano vizuri. Chochote kingine kinaweza kusubiri." Ni watu wa aina gani hawa? Je, hawa bado ni watu ambao wanamwamini Mungu? (Hapana.) Mtu ni lazima aishi mbele ya Mungu nyakati zote na ni lazima aje mbele ya Mungu na kutafuta ukweli nyakati zote na kwa hoja zote, ili mwishowe Mungu atasema: "Wewe ni mtu anayeupenda ukweli na Mungu anafurahishwa nawe, Mungu anakukubali. Mungu huuona moyo wako na huiona tabia yako. "Unafikiria nini kuhusu tathmini hii? Hii ina maana kwamba wewe ni salama, sivyo?
Je, nyinyi kwa kawaida huzingatia hoja hizi? Hebu niwaambie, mnapomwamini Mungu, bila kujali kama unafanya wajibu wa nje, au unafanya wajibu unaohusiana na kazi yoyote au kipengele chochote cha kazi ya weledi ndani ya familia ya Mungu—bila kujali ni wajibu gani unaoufanya—ikiwa huwezi daima kuja mbele ya Mungu, ikiwa huwezi kuishi mbele ya Mungu, basi wewe si muumini na hakuna tofauti kati yako na mtu asiyeamini. Je, hili linasikika sahihi kwako? Je, mnaweza kufahamu jambo hili? Labda kuna baadhi ya watu sasa ambao hawawezi kufanya wajibu wao kwa sababu ya mazingira yasiyofaa, na wanaishi miongoni mwa wasioamini, lakini daima wanaweza kupata nuru na mwongozo wa Mungu—hivyo hali ni ipi hapa? Mnajua? (Ni kwa sababu daima wao huja mbele ya Mungu.) Ndiyo, hili huamua jinsi hali ya kiroho ya mtu ilivyo. Ikiwa, ndani yako mwenyewe, daima huwezi kumhisi Mungu, ikiwa daima u mdhaifu, daima u hasi, au wewe daima ni mwasherati, au daima hubebi mzigo katika wajibu wako na moyo wako siku zote unaboronga bila lengo lolote, basi hii ni hali nzuri au hali mbaya kuwemo? Je, ni hali ambapo unaishi mbele ya Mungu? Au ni hali ambapo huishi kamwe mbele ya Mungu? (Ni hali ambapo hatuishi mbele ya Mungu.) Basi fikirieni hili kwa makini—katika hali nyingi, huwa mnaishi mbele ya Mungu au hamuishi mbele ya Mungu? Je, mnafahamu vyema juu ya hili ndani ya mioyo yenu? Je, nyinyi huishi mbele ya Mungu wakati mwingi, au ni kwa nyakati chache tu? (Ni kwa nyakati chache tu.) Hili ni sumbufu kwenu. Kama mtu ni mchezaji, mwimbaji, mwandishi au mtengenezaji filamu, ikiwa moyo wake haujishughulishi kamwe na kufanya wajibu wowote unaofaa, ikiwa yeye ni mpotovu na hastahimiliki, ikiwa huwa daima anavurugika anapokabiliwa na masuala, hana wazo lolote ni hoja ipi inayohusisha kipengele kipi cha ukweli, wala hana wazo lolote kama kile anachokifanya kina athari yoyote, ikiwa hajui mambo gani anayoyafanya kila siku yanayomchukiza Mungu, ni mambo gani ambayo Mungu anaweza kuyakubali au ni mambo gani Mungu huyachukia, na wao huendelea tu siku baada ya siku katika kiwewe, basi ni hali aina gani hii ya kuwemo? Je, wale wanaoishi katika hali hii wana moyo wa kumuogopa Mungu ndani yao? Je, wana uwezo wa kutenda na kanuni? Je, wana uwezo wa kufanya chochote cha maana? (Hapana.) Wanapofanya wajibu wao, wanaweza kusema, "Ni lazima nivumilie vikwazo fulani, ni lazima nifanye kazi kwa bidii, kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote, na kuwa mwaminifu"? Je, ana uwezo wa kuwa na uaminifu wowote? (Hapana.) Basi mnafanya nini hapa kwa kweli mnapofanya wajibu wenu? (Mkitumia nguvu.) Mko sawa; Mnatumia nguvu. Nyinyi ni wenye uwezo wa kazi, sivyo? Chakula chenu na nyumba zenu zote zimeshughulikwa, na halafu nyinyi hufanya kazi hapa. Ingawa hamchumi fedha hapa, mnahisi ni sawa mnapopata chakula, kinywaji na mahali pa kuishi. Lakini nyinyi huchuma ukweli? (Hapana.) Basi nyinyi hupoteza sana. Nyinyi ni wapumbavu mno! Mmemwamini Mungu kwa miaka mingi sasa, hazijakuwa siku chache tu. Mmesikia ukweli mwingi sana na hamjui mnamwamini Mungu kwa minajili gani, mnachohitaji kufanya, mnachopaswa kupata, au ni kitu gani cha muhimu zaidi kupata. Mnajua kidogo sasa? (Ndiyo.) Mnajua nini? Niambieni. (Kwa kumwamini Mungu, kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi.) Kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi? Kweli au uongo? (Kweli.) Bila shaka ni kweli. Lakini labda huenda msiwe na maarifa halisi ndani ya mioyo yenu hivi sasa, na huenda hamjalitambua kwa kiwango hiki.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni