Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini
Je, mmekisoma Kitabu cha Ayubu? (Ndiyo.) Na mlipokisoma Kitabu cha Ayubu, mioyo yenu ilisisimka? (Ndiyo.) Hivyo mlipata fikira za shauku, na kutaka kuwa mtu kama Ayubu? (Ndiyo.) Ni kwa muda gani mliweza kuendeleza hali hiyo na hisia hiyo? Nusu siku, siku mbili, juma moja?
Au kwa mwezi mmoja au miwili, au mwaka mmoja au miwili? (Labda siku mbili hadi tatu.) Hisia hiyo iliondoka baada ya siku tatu? Wakati hisia hiyo inapoondoka, wewe huendelea kusoma, na unapoendelea kusoma unaweza kuiendeleza kwa siku zingine tatu. Lakini hivyo sivyo ilivyo, au ndivyo? Unaposoma kitabu hicho na unahisi msisimko, unapaswa kuomba, kindani fanya uamuzi wako kuwa unataka kuwa kama Ayubu, mtu ambaye anaweza kumjua Mungu, ambaye anaweza kupata ukweli, na anayeweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unasali kwa Mungu afanye vivyo hivyo kwako, na kwamba Mungu akuongoze na kukupangia mazingira, kukutolea nguvu, kukukinga katika mazingira yoyote ambayo unaweza kukabiliana nayo ili uweze kusimama imara, ili usimuasi Mungu, na unaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unahitaji daima kumsihi Mungu kwa lengo hili na kwa kile unachokitamani sana na unachotaka kukipata moyoni mwako, unahitaji kusihi na kuomba kwa ajili yalo, na wakati Mungu anapouona moyo wako wa kweli Yeye atalifanya. Huhitaji kuogopa Mungu akifanya jambo hili, kwa maana Mungu hawezi kuufanya mwili wako kufunikwa na vidonda kama wakati Alipomjaribu Ayubu na kukunyang'anya kila kitu ulicho nacho; Mungu hatakufanyia hivyo. Hatua kwa hatua Atafanya kazi Yake kwako kwa mujibu wa kimo chako. Ni lazima usihi kwa uaminifu; usilisome tu leo, ujihisi kusisimka na kumsihi Mungu, na kisha baada ya siku mbili usifanye chochote, na yawe yameisha mara unapogeuka. Watu husema, "Ayubu ni nani?" "Nani? Ayubu? Ayubu ni nani? Je, nawezaje kutojua? Huenda nimesikia kumhusu." Hili ni sumbufu! Usilisome kwa siku tatu na lote limesahaulika, limetoka moyoni mwako. Ukiwahusudu watu kama Ayubu na ungependa kuwa mtu kama huyo, moyoni mwako unapaswa kuwa na njia ya jinsi ya kuwa mtu kama huyo, lazima uweke moyo wako mbele ya Mungu, kisha ni lazima uombe kuihusu, omba kuihusu mara nyingi, chukua hoja hii kutoka moyoni mwako na kuitafakari mara nyingi, soma vitabu, soma makala kuhusu Ayubu na maneno ya Mungu yanayohusiana na Ayubu, itafakari daima na tena na tena, fanya ushirika pamoja na watu ambao wana aina hii ya maarifa, uzoefu au azimio , na lazima ufanye kazi kwa bidii mintarafu ya lengo hilo. Unapaswa vipi kufanya kazi kwa bidii? Kusoma tu kwa kweli sio kufanya kazi kwa bidii. Unahitaji kufanya jitihada na hoja hii, utoe maombi yako na kuiweka katika matendo, huku wakati huo huo ukiwa na azimio la kuvumilia mateso na kuwa na moyo wa shauku na hamu. Kisha unarairai, utoe maombi yako na kumwomba Mungu afanye hivi. Ikiwa Mungu haifanyi, itakuwa bure bila kujali ni jitihada kiasi gani unayoiweka, na jitihada zako ni za bure. Mungu huifanyaje? Yeye huanza kwa kuweka na kupanga mambo kwa ajili yako kulingana na kimo chako. Kwa mfano, unakaribia kuchukua mtihani wa kuingia chuo cha elimu, na unasema, "Ninataka alama ili kuingia katika Chuo Kikuu cha Tsinghua." Unaanza kuweka jitihada ili kufanikisha hili, unapitia upya masomo yako, unatafuta vifaa vya kujifunza juu ya chochote na kila kitu na unatafuta walimu kukufundisha. Kisha unawaambia wazazi wako na wanasema, "Mtoto wetu ana azimio zuri. Yeye huanza jambo kwa dhati, ana azimio na hajakosa ustadi." Kwa hiyo, wazazi wako watafanya nini? Wote wawili wataandaa ada yako ya masomo na kukupatia mwalimu. Watafanya mipango sahihi ya maisha yako, wakati unapopaswa kupumzika, na masomo yako, wakupeleke shuleni na kukuchukua baadaye, na watalifanya ili kwamba, wakati huu, usipate uchovu, au njaa, au kukosa chakula cha kutosha. Watakusaidia kwa kushughulikia na kusimamia mambo katika ulimwengu wa nje ili usichanganyikiwe. Watakufanyia mipango sahihi katika vipengele vyote. Kwa njia hii, utakuwa na wakati wa kutosha wa kupitia upya, kusoma na kufanikisha ndoto yako. Kuhusu kumwamini Mungu, chochote unacholenga au uamuzi wowote ulio nao, unapaswa kuzungumza na Mungu. Unahitaji kuomba juu ya hoja hii na kusihi sana juu yalo; itachukua muda mrefu! Itakuwa bure kuwa na moyo usio mwaminifu. Ikiwa unasali mara kadhaa tu mara kwa mara na kisha unapoona kwamba Mungu hajakufanyia chochote, unasema, "Lisahau. Sijali. Liwe liwalo, nitaacha tu mambo yatokee kama kawaida yake, na nitachukua mambo kama yanavyokuja," basi hili litakuwa bure, na moyo wako si mwaminifu. Je, Mungu atakufanyia chochote ikiwa una dakika kadhaa tu za shauku? Je, Mungu atapanga mazingira kwa ajili yako? Je, hilo linakubalika? Kwa kweli Mungu hafanyi kazi kwa njia hiyo. Mungu anataka kuona uaminifu wako na Anataka kuona ni kwa muda gani uaminifu wako na bidii ya moyo wako vinaweza kudumishwa, na kama moyo wako ni kweli au uongo. Mungu atangoja; Yeye husikiliza sala zako na kile unachorairai, na Yeye husikia maazimio yako na shauku zako, lakini Yeye bado hajaona maazimio yako ya kuvumilia mateso, kwa hivyo Yeye hatakufanyia chochote. Ikiwa wewe husema maneno machache na kisha kwenda, Mungu atakufanyia chochote? Hakika hapana. Lazima uendelee kurairai, endelea kuomba, jitahidi na kulitafakari, kisha uonje mazingira ambayo Mungu hukupangia—yatakujia kidogo kidogo, na Mungu ataanza kutenda. Bila moyo wa kweli, ni bure. Wewe husema, "kwa kweli mimi humhusudu Ayubu na kwa kweli mimi humhusudu Petro." Ni haja gani kuwahusudu? Huwezi kuwa wao bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, na bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, Mungu hatakufanyia kazi sawa na ile Aliwafanyia. Kwa nini hivyo? Kwa sababu wewe si aina moja ya mtu kama walivyokuwa. Humiliki azimio lao, au ubinadamu wao, na humiliki moyo wao wa shauku uliotafuta ukweli. Wakati utakapokuja utakapomiliki vitu hivi, ni hapo tu ndipo Mungu atakapokufanyia zaidi. Unaelewa?
Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli, kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe? (Ndiyo.) Azimio lako ni kubwa kiasi gani? Je, unaweza kufanya liendelee kwa muda gani? Unajua? (Nina azimio hili wakati niko katika hali nzuri. Wakati mambo yanapotokea ambayo hayakubaliani na mwili wangu au kupatana na dhana zangu, na ninapopatwa na usafishaji au matatizo ndani yangu, basi imani yangu hupotea, mimi hukwama kwa namna ya hali hasi, na azimio nililokuwa nalo mwanzo hupungua hatua kwa hatua.) Hili halitaweza. Huku ni kuwa dhaifu sana. Lazima ufikie hatua ambapo azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili; huku tu ndiko kuwa mwaminifu, na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu. Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo au shida inapotokea, au kuwa hasi, kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo. Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema, "Bila kujali kinachotokea, hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili." Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia, na Mungu atakufanyia jambo hili. Aidha, lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, "Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Ni lazima nisisalimu amri. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu. "Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Suala lolote dogo unalokabiliana nalo ni pumziko dogo katika mfanyiko tendani wa kufanya maendeleo katika maisha, na ni sharti usiruhusu lizuie kwendelea kwako au kuzuia mwelekeo wako wa mbele. Ni vyema kwako kuchukua pumziko dogo au upumzike kwa muda, lakini mwelekeo wako haupaswi kubadilika, na ni lazima usikome kabisa kwa hali yoyote; hii ndiyo aina ya azimio na uamuzi unayopaswa kuwa nayo. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika. Mungu asema, "Sikutaki tena," nawe unasema, "Mungu hanitaki tena, kwa hivyo nitasahau tu kulihusu." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Au Mungu asema, "Wewe umepotoka sana, na Ninakuchukia," nawe unasema, "Mungu ananichukia, nitaishi kwa sababu gani tena? Nitatafuta kamba ili kujinyonga." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Hutafanikisha lengo lako jinsi hii. Kwa mintarafu ya hadhi yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye ameweza kujaribiwa na Mungu bado, na kusema, "Mungu, tafadhali nijaribu." Huna hadhi hii. Je, mna uwezo wa kufanya nini tu? Ni lazima muombe: "Ee Mungu, tafadhali niongoze, nipe nuru, nipe bidii ya kuendelea na unipe bidii ili niweze kuitembea njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa mujibu wa shauku zangu. Bila kujali namna gani ya mateso ninayoyapitia, Wewe hunipa nguvu na Wewe hunilinda. Ingawa ninaweza kuwa dhaifu na ingawa kimo changu ni kichanga, ninakuomba Unipe nguvu, kunilinda na kunionyesha wema. Sitasalimu amri." Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba, na ni lazima daima mje mbele ya Mungu kuomba. Wakati wengine wanacheka na kufanya mzaha na kujiendekeza, ombea hili; wakati wengine wanapojifurahisha, ombea hili; wakati wengine ni hasi, ombea hili; wakati wengine wanalala fofofo, au kuchelewa kuamka, wewe tayari unaliombea hili; wakati wengine wanatembea njia ya ulimwengu na kwa ulafi kufurahia anasa za kimwili, au kufuata mienendo ya kidunia, ombea hili. Wakati unapoweza kuishi mbele ya Mungu katika mambo yote na unaweza kujiweka katika mipaka fulani, wakati unapoweza kujiweka ukiishi mbele ya Mungu na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi Mungu anaweza kuliona hili. Wakati Mungu anapouona moyo wa mtu, Yeye hayatumii tu macho Yake; Yeye hupanga mazingira kwa ajili yako na Yeye hugusa moyo wako kwa mikono Yake. Kwa nini Nasema hili? Wakati Mungu anapokupangia mazingira, Yeye hutazama kuona kama moyo wako unachafuliwa nayo, unayachukia, unayapenda au ni mtiifu, au kama husubiri kwa utulivu, au hutafuta ukweli—Yeye huona jinsi moyo wako unavyobadilika na ni katika mwelekeo gani huenda. Mabadiliko katika moyo wako, kila badiliko la fikira na mawazo ndani ya moyo wako kuhusu watu, hoja, na mambo ambayo Mungu hupanga kwa ajili yenu, na kila badiliko ya hali ya moyo uliyo nayo—Mungu anaweza kuyahisi yote. Ingawa huenda hujamwambia yeyote na huenda hujaomba, badala yake kufikiria tu mawazo haya kwa moyo wako mwenyewe au katika ulimwengu wako mwenyewe, lakini kwa Mungu ni wazi kabisa na Yeye huliona wazi kwa tazamo moja. Watu hutumia macho yao kukuona, na Mungu hutumia moyo Wake kuugusa moyo wako—Yeye yu karibu hivi nawe. Na kama unaweza kuuhisi uchunguzi wa Mungu, basi unaishi mbele ya Mungu. Kama huwezi kuuhisi kabisa na unaishi ndani ya ulimwengu wako, basi uko katika shida. Wewe huishi mbele ya Mungu, wewe uko mbali na Mungu na mbali sana kutoka Kwake, huendi karibu Yake kwa moyo wako au moyo wako uukaribie moyo Wake, na hukubali uchunguzi wa Mungu. Na Mungu anajua hili! Mungu anaweza kabisa kuhisi yote haya. Kwa hivyo, wakati una azimio na lengo la kukamilishwa na Mungu, kuwa mtu anayetekeleza mapenzi ya Mungu, mtu anayemcha Mungu na aepukanaye na maovu, unapoweza kuomba mara nyingi juu ya hoja hii na kusihi kwa ajili yalo, unapoweza kuishi mbele ya Mungu, kutokwenda mbali na Mungu au kumwacha Mungu, basi wewe unalielewa hili, na Mungu anajua kuhusu hilo pia. Watu wengine wanasema: "Mimi ni dhahiri kulihusu, lakini sijui kama Mungu anajua kulihusu." Hili si jambo la busara. Kwa hiyo hali ni gani hapa? Kama wewe mwenyewe u dhahiri kulihusu, na hujui kama Mungu anajua kulihusu, basi huna uhusiano na Mungu. Umeelewa? Kwa nini Nasema wewe huna uhusiano na Mungu? Wewe huishi mbele ya Mungu, kwa hivyo unashindwa kuhisi kama Mungu yu pamoja nawe, kama Mungu anakuongoza au kukulinda, na kama Mungu anakushutumu wakati unapofanya jambo baya. Huwezi kuhisi jambo lolote kati ya haya, kwa hiyo hili linamaanisha kwamba huishi mbele ya Mungu. Wewe hufikiria tu mwenyewe na kuleweshwa na mawazo yako mwenyewe; huko ni kuishi katika ulimwengu wako mwenyewe na sio kuishi mbele ya Mungu, na hakuna uhusiano kati yako na Mungu.
Mtu anawezaje kuudumisha uhusiano wake na Mungu? Ni kwa njia gani anaweza kuudumisha? Kwa njia ya kusihi, kuomba na kuwa na ushirikiano na Mungu katika moyo wake. Aina hii ya uhusiano itakuwezesha kuishi daima mbele ya Mungu, na kwa hiyo utakuwa mtu mwenye amani sana. Watu wengine daima hufanya mambo ya nje na hujihusisha na mashauri ya nje. Baada ya siku moja au mbili bila kushiriki katika maisha ya kiroho, moyo wao hauna utambuzi, na baada ya siku tatu, au siku tano, bado hauna utambuzi, au bado hauna utambuzi baada ya mwezi mmoja au miwili. Hili lina maana kwamba hawaombi au kurairai chochote, na hawajishughulishi na ushirikiano wa kiroho. Kusihi ni wakati unapokabiliwa na masuala, unamwomba Mungu akusaidie, akuongoze, akukimu, akupe nuru, akuruhusu ujue mapenzi ya Mungu na kujua ukweli ni nini. Kuomba kuna mawanda mapana kiasi. Wakati mwingine ni kusema maneno ndani ya moyo wako, kuzungumza na Mungu wakati unapokabiliwa na shida na kusema maneno yaliyo moyoni mwako kwa Mungu wakati unapokuwa hasi na dhaifu. Unaweza pia kumwomba Mungu unapokuwa mwasi, au unasema na Mungu juu ya masuala yanayokukabili kila siku, yote kuhusu yale ambayo unaweza kuyabaini na yale ambayo huwezi kuyabaini. Huku ni kuomba. Mawanda ya kuomba kimsingi ni kuwa na mazungumzo na Mungu, wakati mwingine kwa nyakati zilizopangwa na wakati mwingine kwa nyakati zisizoratibiwa, na yanaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Ushirikiano wa kiroho kwa kweli haushikilii muundo fulani. Labda kuna suala, labda hakuna; wakati mwingine kutakuwa na kitu cha kusema, na wakati mwingine hakutakuwa. Huu ni ushirikiano wa kiroho. Wakati kuna suala maalum la kuzungumzia na Mungu, basi unaweza kuomba. Wakati hakuna suala lolote, unafikiri tu juu ya Mungu, "Mungu humpendaje mwanadamu? Mungu anamtunzaje mwanadamu? Mungu humshutumuje mwanadamu?" "Ee Mungu, ninahisi nimefanya jambo hili vibaya. Kama kwa kweli nimefanya jambo hili vibaya, basi nishutumu na unifanye nifahamu." Huu ni ushirika wa kiroho, na unaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Wakati mwingine uko barabarani na unafikiria kuhusu kitu ambacho huufanya moyo wako uhisi huzuni kweli. Huna haja ya kupiga magoti au kuyafunga macho yako, lakini badala yake unasema mara moja kwa Mungu moyoni mwako: "Ee Mungu, naomba Uniongoze na suala hili. Mimi ni dhaifu na siwezi kulishinda. "Moyo wako umesisimuliwa, na kwa maneno haya machache rahisi Mungu anajua yote kulihusu. Wakati mwingine unafikiria kuhusu familia yako, na unaweza kusema: "Ee Mungu, kwa kweli nimeikosa familia yangu …." Humkosi mtu yeyote hasa, unahisi tu vibaya, hivyo unaongea na Mungu. Usizungumze na watu wengine kulihusu, kwa kuwa hilo halina maana. Unapozungumza na mtu mwingine kulihusu, huenda ikawa kwamba anaikosa familia yake hata zaidi ya wewe, basi hili linakuathiri na unaishia kuikosa yako hata zaidi, na hili halikuletei faida yoyote kamwe. Unapozungumza na Mungu kulihusu, basi Mungu atakufariji, Akufurahishe tena na kukupisha katika wakati huu mgumu na kupita hali hii ndogo. Hali hii, jiwe hili dogo njiani mwako halitakukwaa, halitakuzuia au kuathiri utekelezaji wa wajibu wako. Wakati mwingine, unapozungumza au kufanya ushirika na wengine, moyo wako unaweza ghafla kuwa na hisia ya kuvunjika kidogo au kujisikia mwenye wasiwasi sana, hivyo unafanya haraka kumwomba Mungu, na unaweza kufanya hivi wakati wowote na katika mahali popote. Kunaweza kuwa hakuna chochote unachokisihi, au chochote unachotaka Mungu akufanyie au akunurishie, unaongea tu na Mungu na kuzungumza Naye wakati wowote na katika mahali popote. Ni hisia gani unayopaswa uwe nayo wakati wote? Ni hii: Mungu huwa hatoki kandoni mwangu kamwe, Yeye yu pamoja nami kandoni mwangu wakati wote, Yeye hajawahi kuniacha, na ninaweza kuhisi hili. Bila kujali ni mahali gani nipo, bila kujali ninafanya nini, kama ninapumzika au kulala, kula chakula, au kwa mkutano, au kama sisemi chochote mchana kutwa ninapotekeleza wajibu wangu, najua moyoni mwangu kwamba Mungu ananiongoza kwa mkono, na kwamba Yeye hajawahi kuniacha. Wakati mwingine, wewe hufikiria jinsi umefaulu kwa miaka hii michache iliyopita, mwezi baada ya mwezi, na unahisi moyoni mwako kwamba kimo chako kimekomaa na kwamba ni Mungu anayekuongoza, na kwamba ni upendo wa Mungu ambao unakulinda daima. Unapofikiri hivi, unaomba moyoni mwako: "Nakushukuru Wewe, Mungu!" Na wewe unatoa shukrani zako, na kusema: "Mimi ni dhaifu sana, mwenye woga sana, na mpotovu kwa kina sana. Kama Hukuniongoza kwa njia hii, mimi mwenyewe singeweza kufanikiwa hadi leo. Asante Mungu!" Je, si huu ni ushirika wa kiroho? Kama ungekuwa jinsi hii, basi si ungekuwa na mengi ya kumwambia Mungu? Hungeishi siku baada ya siku bila kuwa na kitu cha kumwambia Mungu. Ikiwa huna chochote cha kumwambia Mungu, basi inamaanisha kwamba Mungu hayuko ndani ya moyo wako. Kama una Mungu ndani ya moyo wako, basi unaweza kumwambia Mungu mambo unayoweza kusema kwa wandani wako—Mungu ni msiri wako wa karibu zaidi. Unapomruhusu Mungu kuwa msiri wako wa karibu zaidi, rafiki yako wa karibu zaidi, familia unayoweza kuitegemea zaidi, kuiegemea zaidi, na Aliye mwaminifu zaidi, Aliye mwandani sana na wa karibu, basi itakuwa vigumu kutokuwa na mambo ya kusema Kwake. Wakati daima una mambo ya kumwambia Mungu, si basi utaweza kuishi daima mbele ya Mungu? Unapoweza kuishi mbele ya Mungu daima, basi wakati wote utaweza kutambua jinsi Mungu anavyokuongoza, jinsi Mungu anavyokulinda, jinsi Anavyokutunza, jinsi Anavyokuwa amani yako na furaha, Anavyokupa baraka na nuru, jinsi Mungu anavyokushutumu, kukufundisha nidhamu, kukuadhibu, kukuhukumu na kukuadibu. Wakati unapoishi mbele ya Mungu daima, moyo wako utajua kwa dhahiri sana kile Mungu anachofanya ndani yako. Hutakuwa na siku ambapo utakuwa mpumbavu kabisa na kutojua chochote, ukisema tu maneno "Ninamwamini Mungu, mimi hutekeleza wajibu wangu, mimi huhudhuria mikutano, mimi husoma kila siku na huomba kila siku." Huwezi tu kupitia mifanyiko tendani hii yote au kuwa tu na aina hii ya tabia ya nje.
Mnapaswa kujua sasa, kwa hiyo ni nini kitu muhimu zaidi katika kumwamini Mungu? Unapomwamini Mungu, kama Mungu hayuko ndani ya moyo wako na Yeye hakuhusu, na kama humwoni Mungu kama mwandani wako sana, wako wa karibu sana, familia na msiri mwaminifu sana na wa kutegemewa sana, basi Mungu si Mungu wako. Sawa, kwa hiyo sasa nendeni na mtende kwa muda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema, na muone kama hali yenu ya ndani itabadilika au la. Tenda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema na hakika utaishi mbele ya Mungu, utaishi katika tabia ya kawaida na kuwa katika hali ya kawaida. Wakati hali ya mtu ni ya kawaida, ni hapo tu ambapo mambo anayoyaonyesha na kuyafichua kwa kila hatua, au miongoni mwa watu tofauti, masuala, na mambo, au katika mazingira tofauti, yatakuwa ya kawaida. Ni kwa njia hii tu ambapo maisha yake yanaweza kukomaa na anaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli kidogo kidogo. Unaelewa? (Ndiyo.)
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni