Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX
Pili, ni aina gani ya mazingira ambamo ndege na wanyama na wadudu wanaishi? Licha ya kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote.
Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. Nchi kavu inajumuisha nini? Maeneo mbalimbali kama vile milima, tambarare, na vilima. Kwa hiyo, ndege na wanyama wana makazi yao yasiyobadilika na hawatazungukazunguka mahali popote tu. Makazi yao ni misitu na milima. Ikiwa, siku moja makazi yao yataharibiwa, mpangilio huu utakuwa machafuko. Mara tu mpangilio huo unapokuwa machafuko, madhara yake ni yapi? Wa kwanza kuumizwa ni akina nani? (Binadamu.) Ni binadamu! Ndani ya sheria na mipaka hii ambayo Mungu ameianzisha, je, mmewahi kuona tukio lolote la ajabu? Kwa mfano, tembo wakizungukazunguka tu jangwani kwa kawaida. Mmewahi kuona tukio hilo? Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa ni tukio la ajabu sana. Hii ni kwa sababu mazingira ambamo tembo wanaishi ni msitu, na msitu ni mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliwaandalia. Ana mazingira yake kwa ajili ya kuendelea kuishi na ana makazi yake yasiyobadilika, sasa kwa nini atangetange? Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuona simba na duma wakizungukazunguka baharini? Makazi ya simba na duma ni msituni na kwenye milima. Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kumwona nyangumi au papa kutoka baharini wakitembea jangwani? Nyangumi na papa makazi yao ni baharini na hawawezi kuishi kwenye nchi kavu. Katika mazingira ya kuishi ya binadamu, je, kuna watu ambao wanaishi pamoja na dubu wa kahawia? Je, kuna watu ambao siku zote wamezungukwa na tausi au ndege wengineo, ndani au nje ya makazi yao? Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kumwona ng'ombe au kondoo msituni? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaona tai au bata bukini wa mwituni wakicheza na tumbili? Kama mlishawahi kuona, basi haya yatakuwa ni matukio ya pekee sana. Hii ndio sababu Ninazungumza juu ya vitu hivi ambavyo ni matukio ya pekee machoni mwenu. Ni kuwafanya muelewe kwamba vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu–haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au vina pumzi na vinaweza kutembea–vyote vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyosimamia viumbe vyote. Ni kumwandalia binadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya viumbe vyote kila kimoja kina chakula kinachokimu maisha ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi; vimejifunga katika mazingira hayo. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, viumbe vyote vinaingiliana na binadamu kwa upatanifu, na binadamu na viumbe vyote vinategemeana.

Mungu aliviumba viumbe vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao na miongoni mwao akalea aina zote za viumbe hai. Huku viumbe vyote vikiwa vinalea aina zote za viumbe hai, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Ni vyanzo gani vingine vya vyakula ambavyo binadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa:
Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua kuhusu hilo. Je, wowote kati yenu wanawinda kwa ajili ya kuishi? Nyinyi nyote ni watu wa kisasa—hamjui jinsi ya kuwinda, jinsi ya kushika bunduki. Vyanzo vyenu vya chakula vinatoka ardhini. Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. "Windo" ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangefurahi endapo wangepata paa. "Vizuri, paa huyu anatosha kwa chakula kwa ajili ya familia kwa siku kadhaa." Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. "Kwa sasa kuna kitu cha kula; hatuna haja ya kuogopa kuwa na njaa." Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Ni mazingira ya aina gani ambayo mara nyingi watu wanaoishi kwa kutegemea uwindaji wanaishi? Wanaishi katika misitu ya milima. Kwa kiasi kikubwa hawalimi au kupanda mazao; wanaishi katika misitu ya milima. Je, kuna ardhi inayolimika katika misitu ya milima? Sio rahisi kupata ardhi inayolimika, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.
Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi hawalimi, sasa wanafanya nini? Wanafuga tu? Ikiwa yeyote miongoni mwenu hapa ni mtu wa Mongolia, mnaweza kuzungumza kidogo kuhusu mtindo wenu wa maisha ya kuhamahama. (Kwa sehemu kubwa, tunafuga ng'ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, hatulimi, na msimu wa baridi tunawachinja na kuwala mifugo wetu. Chakula chetu kikuu kinatokana na nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, tunakunywa chai ya maziwa, tunakula mchele uliokaushwa, na mbogamboga chache sana. Sasa aina zote za usafiri hazina usumbufu na tuna aina zote za mbogamboga na nafaka. Wamongolia hunywa chai ya maziwa, na Watibeti hunywa chai ya siagi. Ingawa wafugaji wanatingwa misimu yote minne, lakini wanakula vizuri. Hawapungukiwi na maziwa, bidhaa za maziwa, au nyama. Walikuwa wanaishi katika viduku lakini sasa wote wanajenga nyumba.) Chakula cha msingi cha watu wa Mongolia ni kula nyama ya ng’ome na nyama ya kondoo, kunywa maziwa, na kuendesha farasi kuenda kulisha wanyama wao. Huu ni mtindo wa maisha wa mfugaji. Mtindo wa maisha wa mfugaji sio mbaya–wanaendesha madume ya ng'ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao, na hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wote wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!
Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Aina hii ya watu hufanya uvuvi kwa ajili ya kuishi. Watu hawa wanaofanya uvuvi kwa ajili ya kuishi hutegemea nini kwa ajili ya chakula? Chanzo cha chakula chao ni nini? Ni aina zote za samaki na vyakula vya baharini? Wakati Hong Kong ilikuwa ni kijiji kidogo tu cha uvuvi, watu ambao waliishi pale waliweza kuvua kwa ajili ya kuishi. Hawakulima–walikwenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kilikuwa ni aina mbalimbali za samaki, nyama, na vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kuuza kiasi cha samaki kwa kubadilishana na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Watu wanaoishi kwa kutegemea uvuvi wote wanaishi pembezoni mwa bahari, na baadhi wanaishi kwenye mashua. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi pembezoni mwa maji. Wale wanaoishi pembezoni mwa maji wanategemea uvuvi; ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.
Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wale ambao wanategemea kulima kwa ajili ya kupata riziki zao kimsingi wanapanda mazao kwa vizazi. Wanapata chakula chao kutoka ardhini. Ama wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wote wanapata mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.
Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Hii ni sawa na kusema, ikiwa wawindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, basi wasingekuwa tena na riziki yao. Hivyo ikiwa watu ambao wanategemea uwindaji wangepoteza milima ya misitu na wasiwe tena na ndege na wanyama, wasingekuwa tena na chanzo cha riziki yao. Aina ya mbari hiyo ingeelekea upande gani; aina ya watu hao wangeelekea wapi? Uwezo wa kuendelea kuishi au la ni kiwango kisichojulikana na wangeweza tu kutoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao–wanategemea uwanda wa mbuga. Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo wao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi–uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng'ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama wangekuwa na riziki gani? Wasingekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Mara tu tatizo linapotokea na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi–zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, matokeo yake yangekuwa nini? Wasingeweza kupanda vitu, wasingeweza kupata vyakula vyao kutoka katika mimea. Matokeo yake yangekuwa ni nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali ya kiikolojia. Ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira–ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.
Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingewea kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote–ni muhimu sana! Mungu alichora mawanda ya kila aina ya kiumbe hai na aliweka mbinu ya kuendelea kuishi kwa kila aina ya binadamu. Pia aligawanya aina mbalimbali za watu na jamii mbalimbali duniani na akaweka mawanda yao. Hiki ndicho tunachotaka kujadili wakati ujao.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni