Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo"Tafakuri kuhusu Kubadilishwa“
Yi Ran Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa. Inawezekana kwamba yeye alizungumza juu ya maonyesho yake mwenyewe ya upotovu sana, na hivyo kiongozi wake kwa makosa alimchukua kuwa mtu asiyefuatilia ukweli, na kumbadilisha? Kama hili ndilo lililotokea kweli, basi si fursa ya mafunzo kwa mtu ambaye alikuwa anafuta ukweli imeangamizwa?
Nilipokuwa tu nikihisi kukanganywa sana kuhusu hili, nilisoma kifungu hiki katika mpango wa kazi uliotolewa na kanisa: "Familia ya Mungu huamua kufundisha na kutumia watu kulingana na asili yao. Kama kiini cha mtu ni kile ambacho hutafuta ukweli, basi familia ya Mungu kabisa haitamtelekeza, kama mtu yu tayari kutafuta ukweli, basi bila shaka atapitia mabadiliko. Kama kiini cha mtu ni kile ambacho hakitafuti ukweli, ni mzembe kwa majukumu yake na ni ambaye haipitii barabara sahihi, basi si mzuri wa kufundisha na wala Mungu hawezi kukamilisha aina hii ya mtu. Kwa mtu ambaye Mungu hataki kumkamilisha, familia ya Mungu pia haiwezi kumfundisha. ... Hivyo ushughulikiwaji wa watu ni lazima ujongelewe kwa mujibu wa mahitaji ya kazi ya Mungu na kiini cha watu. Hii tu ndiyo njia ya kufaa ya kufanya kazi pamoja na Mungu na kwa hakika kumtumikia Mungu. Kama njia hii ifaayo ya kufanya kazi pamoja na Mungu haitumiwi, basi kazi ya Mungu inavurugwa na mapenzi ya Mungu inakiukwa kabisa" ("Kushirikiana Maswali Kadhaa" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I). Kujaribu mara kwa mara kuelewa maneno haya, nilielewa kwamba kulikuwa na kanuni zilizokuwa zikifanya kazi kama kanisa lilikuwa likimpandisha mtu cheo au kumbadilisha. Nilielewa kwamba ulikuwa ukijongelewa kwa mujibu wa mahitaji ya kazi ya Mungu na kiini cha watu, na sio kutumia watu kwa upofu au kuwabadilisha watu upendavyo. Aidha, kanisa huwa haliwabadilishi watu kwa msingi wa kuwa walionyesha upotovu, lakini badala yake huamua mambo kwa msingi wa asili yao. Kama kiini cha mtu ni kile ambacho hutafuta ukweli, basi bila shaka kanisa halingemwacha, bila shaka halingemtelekeza au kumwangamiza mtu yeyote akitafuta ukweli. Kwa hiyo nilikwenda mbele ya Mungu kuomba na kutafuta mwongozo: "Ee Mungu! Najua kwamba nimepotoshwa sana na Shetani, na sina ufahamu wa kazi Yako, nikiwa na dhana nyingi ndani yangu na maoni mengi ambayo hayawezi kupatana na Wewe. Leo, chini ya mwongozo Wako, sasa ninajua kuwa kama ni katika kuchagua, kufundisha au kubadilisha watu, kanisa huyajongelea yote kwa mujibu wa mahitaji ya kazi Yako na kiini cha watu. Lakini bado sielewi vizuri kiini cha dada aliyebadilishwa, na matokeo yake ni kuwa nina maoni juu ya utaratibu wa kanisa. Ninakuomba Unielekeze na kuniongoza, niruhusu nipate kuona kwa dhahiri ili, katika kazi yangu tangu sasa na kwendelea, nisiweze kuvuruga kazi Yako kwa sababu ya kupotoka kwangu na makosa yangu."
Nilipokuwa nimekwisha kuomba, nilichukua utaratibu wa kazi na, chini ya uongozi wa Mungu, nilisoma maneno haya: "Kwa kusoma maneno ya Mungu, wale wanaotafuta ukweli wanaweza kupima hali yao potovu dhidi ya maneno ya Mungu. Ushirika wao juu ya maneno ya Mungu haufanyiki tu ili kuzungumza juu ya kuelewa maneno ya Mungu, bali pia kuzungumza juu ya kujielewa wenyewe. Bila kujali ni upotovu upi unaonyeshwa, wanaweza kuufichua wazi ili ndugu wa kiume na wa kike waweze kufanikisha kitu halisi, wakati huo huo wakitatua upotovu wao wenyewe. Huu pia ndio utaratibu bora ya kabisa wa kuwaongoza watu kwenye maneno ya Mungu. ... Wale wote ambao huzungumza tu kuhusu maana halisi na ambao hawana uhalisi, hawastahili kuwa viongozi katika familia ya Mungu. Aina hii ya viongozi na wafanyakazi wanapaswa kubadilishwa" ("Kumtumikia Mungu ni Lazima Mtu Ajifunze Jinsi ya Kuwa na Tambuzi na Watu" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I). Maneno haya yalinifanya nielewe kwamba kwa kusoma maneno ya Mungu, wale ambao kwa kweli hutafuta ukweli wanaweza kupima hali yao wenyewe potovu dhidi ya maneno ya Mungu, kuwa na ufahamu wa kweli wa kiini cha maneno ya Mungu, na wanaweza kuelewa kwa hakika asili na nafsi ya upotovu wao wenyewe. Ushirika wao unaweza kufichua njia halisi ya watu na unaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Zaidi ya hayo, wakati huo huo wa kutatua matatizo ya wengine, wanaweza pia kutatua matatizo yao wenyewe, na kulenga kuingia kwao katika maisha na mabadiliko yao katika tabia.
Wakati huu, nilianza kukumbuka kinaganaga mwenendo mngʼangʼanivu na utendaji wa dada aliyebadilishwa. Ingawa wakati wa kutatua matatizo ya watu wengine alizungumza kwa umbuji na kwa urefu, akitumia maneno yaliyofikiriwa na yaliyoelezwa kwa ufasaha, hakuwa ametatua ugumu wa kuingia kwake katika maisha na daima aliishi katika hali ya kujidai, akijihisi kujivuna mno, akiamini kwamba alifanya kila kazi vizuri. Kwa kweli, kazi yake ilifanywa vibaya. Kama kile alichopata na kushirikiana kwa kweli kilikuwa ufahamu wa kiini cha kweli, kwa nini hakuweza kutumia ufahamu wake ili kujisaidia? Kiongozi alipoonyesha hali yake ya makosa, kuchukua kwa uzito kabisa na kuchangua matatizo makubwa yaliyokuwemo katika kazi yake, na kushirikiana naye kuhusu hilo, ingawa kwa nje alikubali kwa kichwa chake mara kwa mara, akionyesha kukubali kwake na nia yake ya kufanya hivyo kwa kanuni, yeye hata hivyo kwa siri aliendelea katika njia zake za zamani kwa ukiukaji wa kanuni hiyo, akifanya mambo jinsi alivyotaka akidhuru kazi tena. Wakati alipokuwa akishughulikiwa, ingawa sura yake ya nje ilionyesha kuwa alikuwa na huruma sana, baadaye hakufanya mabadiliko yoyote kabisa. Ingawa alizungumzia ufahamu wake wa nafsi yake mwenyewe na kutoa upotovu wake mwenyewe waziwazi, matokeo yake yalikuwa kwamba alifanya wengine kumtegemea, kumpa heshima sana, akiwaleta watu mbele yake. Njia yake ya kutoa vitu nje waziwazi haikuweza kumletea mtu yeyote faida yoyote kabisa. Ingeweza tu kuwadhuru watu na kuwadanganya. ... Niliweza kuona kutoka kwa utendaji wake mngʼangʼanivu kwamba, ingawa alikuwa amefanya kazi kwa miaka mingi na kujiandaa na ufahamu mwingi halisi, tabia yake katika maisha haikuwa imepitia mabadiliko yoyote kabisa. Kwa kinyume chake, alikuwa ashakuwa mwenye kiburi na majivuno zaidi na zaidi. Ni sasa tu ninapotambua kwamba hakuwa mtu ambaye alitafuta ukweli, wala hakuwa mtu ambaye alipokea ukweli halisi au aliyefanya ushirika kwa werevu. Bila shaka hakuwa mzuri wa kufundisha na, kama angekuwa amewekwa katika cheo yake, angechelewesha tu kazi ya kanisa na kuwaharibu ndugu zake wa kiume na wa kike. Kubadilishwa kwake kwa kweli kulikuwa ni haki ya Mungu na ilikuwa njia nzuri zaidi ya Mungu kumwokoa. Vinginevyo, bado angeweza kudanganywa na sura yake ya nje na hangeweza kuona makosa ya njia zake, mwishowe akianguka katika adhabu ya Mungu.
Ni kwa njia ya jambo hili tu nilipoona jinsi nilivyoelewa kiasi kidogo cha ukweli, nikilenga tu maana halisi ya mipango ya kazi na ukweli, kuwa tu na maarifa ya kinadharia. Hakika sikuwa nikilenga juu ya kuelewa mapenzi ya Mungu katika mipango ya kazi, wala sikuwa na ufahamu muhimu wa ukweli. Kwa hivyo sio tu kwamba niliishia kutoweza kuelewa kabisa viini vya watu, lakini kwa kinyume chake nilihofia kwa kiburi kwamba mtu ambaye alitafuta ukweli alikuwa amebadilishwa kwa makosa.
Ee Mungu! Ninatoa shukurani kwa ajili ya ufunuo Wako na kupata nuru ambavyo vilinifanya nione ufukara wangu mwenyewe, upofu na jinsi nilivyokuwa wa kusikitisha, vilivyonifanya kutambua kwamba bila ukweli, mtu hawezi kuelewa kabisa kiini cha suala hili, badala yake akidanganywa tu na sura ya nje. Ni kwa kuelewa ukweli tu, mtu anapoweza kufanya kazi muhimu vyema. Ee Mungu! Kuanzia leo kwendelea, napenda kufanya jitihada nyingi katika ufuatiliaji wangu wa ukweli, kutafuta mapenzi Yako katika vitu vyote, kufanya vitu kama Unavyohitaji na hivi karibuni kuwa wa manufaa Kwako.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni