Jumapili, 29 Julai 2018

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri.

Jumapili, 15 Julai 2018

Tamko la Pili

Kufuata kuanza kazi kwa mtazamo mpya, kutakuwa na hatua mpya katika kazi Yangu. Kama ilivyo katika ufalme, Nitafanya mambo moja kwa moja kupitia kwa uungu, Nikiongoza kila hatua ya njia, sahihi hadi kwa maelezo madogo, na bila kutiwa najisi na nia za binadamu hata kidogo. Yafuatayo yanaeleza kwa muhtasari namna ya utekelezaji halisi: Kwa vile ni kupitia katika ugumu na usafishaji ndiyo wamepata jina la “watu”, na kama walivyo watu wa ufalme Wangu, lazima Niwafanye watii kwa mahitaji kali, ambayo ni ya juu kushinda mbinu za kazi Yangu kwa vizazi vilivyopita.

Jumamosi, 14 Julai 2018

Tamko la Kwanza

Tamko la Kwanza

Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli.

Jumanne, 10 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dibaji

Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu.

Jumatatu, 9 Julai 2018

Swahili Worship Song "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Seeing the Love of God

Swahili Worship Song "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Seeing the Love of God
Wakati hamumwelewi Mungu na hamjui asili Yake,

mioyo yenu haiwezi kamwe kufunguka, kufunguka kwa Mungu.

Mara utakapomwelewa Mungu wako,

utaelewa kile kilicho moyoni Mwake,

na kufurahia kile kilicho ndani Yake

kwa imani na usikivu wako wote.

Jumamosi, 7 Julai 2018

Tamko la Kwanza

Tamko la Kwanza

Sifa zimekuja Uyahudi na makazi ya Mungu yameonekana. Jina tukufu takatifu linasifiwa na watu wote, na linaenea. Ah, Mwenyezi Mungu! Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa, na Ameinuka juu ya Mlima Sayuni ulio na uadhimu na mzuri kabisa katika ulimwengu mzima ...

Ijumaa, 6 Julai 2018

Tamko la Hamsini

Tamko la Hamsini

Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni: Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe.

Jumapili, 1 Julai 2018

Utangulizi

Utangulizi

"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni matamshi yanayoonyeshwa na Kristo, ambayo kwayo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Katika fungu hili la matamshi, Mungu anaonyesha maneno Yake kutoka kwa mtazamo wa Roho. Namna ambayo Anazungumza haiwezi kufikiwa na wanadamu walioumbwa.