Jumanne, 24 Oktoba 2017

4. Kueneza kwa Injili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu Nchini China

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


Mwaka wa 1995, kazi ya kushuhudia kwa injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu ilianza rasmi China Bara. Kwa njia ya shukrani kwa Mungu na kwa upendo ambao ulikuwa wa kweli, tulishuhudia kwa kuoenekana na kazi ya Mwenyezi Mungu kwa ndugu wa kiume na kike katika madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini. Hatukutarajia hata kidogo kukumbwa na upinzani na kukashifiwa kulikokithiri kutoka kwa viongozi wao. Tungeweza tu kuja mbele ya Mwenyezi Mungu kusali kwa ari, tukimsihi Mungu kufanya kazi binafsi. Kutoka 1997 na kuendelea, tulimwona Roho Mtakatifu akifanya kazi kwa kiwango kikubwa.

Jumatatu, 23 Oktoba 2017

Sifa Kamili | Dansi ya Kilatini ''Tukuzeni Ufanikishaji wa Kazi ya Mungu"



Tukuzeni Ufanikishaji wa Kazi ya Mungu
Kazi kubwa ya Mungu hubadilika haraka sana, vigumu kuipima, kuridhisha kwa mtu.
Angalia kandokando yako, si kama awali, kila kitu ni kizuri na kipya.
Kila kitu kimehuishwa, vyote vimetengenezwa upya, vyote vimetakaswa.
Tunamsifu Mungu, tukijawa furaha, nyimbo za sifa zinapepea mbinguni Kwake.
Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Watu wote msifuni Mungu kwa vigelegele.
Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Watu wote msifuni Mungu kwa vigelegele.
Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu, isifuni hekima Yake, isiyoshindwa.
Isifuni tabia Yake yenye haki, msifuni kwa kuwa ni Mungu mwaminifu.

Jumapili, 22 Oktoba 2017

3. Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu aliwaahidi wafuasi wake, “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.” (Yohana 14:3) Kadhalika Alitabiri, “Kwa maana kama umeme utokavyo mashariki, na kumulika hata magharibi; hivyo ndivyo ujio wake Mwana wa Adamu utakavyokuwa.” (Mathayo 24:27) Katika siku za mwisho, kama ilivyoahidiwa na kutabiriwa na Yeye, Mungu tena Amekuwa mwili na kushukia Mashariki ya dunia—China—kufanya kazi ya kuhukumu, kuadibu, ushindi, na wokovu Akitumia neno, kwa msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu.

Jumamosi, 21 Oktoba 2017

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya. Matokeo yake, hakuna mahali pagumu zaidi ya hapa kueneza injili ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu. Wakati Chama cha Kikomunisti Cha China kiliposhika madaraka mwaka wa 1949, imani za kidini katika China bara zilizimwa kabisa na kupigwa marufuku. Mamilioni ya Wakristo walipitia mateso na fedheha hadharani, na kifungo. Makanisa yote yalifungwa kabisa na kufutiliwa mbali. Hata mikutano ya nyumbani ilipigwa marufuku.

Ijumaa, 20 Oktoba 2017

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. 

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa

    Mwenyezi Mungu alisema: Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika.

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

Mungu Amekuja Mungu Ametawala | " Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"


Kwaya za Injili :
1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
2. Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi
1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji.

Jumanne, 17 Oktoba 2017

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)


Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa
I
Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.
Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.
Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.
Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,
yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.
Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu.
Nainua mikono yangu kwa sifa, ninafurahia kwamba Ulikuja katika dunia hii.

Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi MunguWengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa


Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu. Wanadamu wote wakitofautishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

Jumamosi, 14 Oktoba 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli


Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Ijumaa, 13 Oktoba 2017

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)


Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu
Mpaka siku moja,
utahisi kuwa Muumba
sio fumbo tena,
kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako,
kwamba Muumba
hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako,
kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo,
kwamba Muumba siye Yule unayemtamania katika mawazo yako

Alhamisi, 12 Oktoba 2017

Mwenyezi Mungu|Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu



Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote.