Jumatatu, 12 Machi 2018

“Utamu katika Shida” - Ukweli wa Sera ya CCP juu ya Dini Iliyofunikwa na Katiba Yake | clip 6/6




Katiba ya serikali ya Kikomunisti ya Kichina hutamka dhahiri juu ya uhuru wa dini na ibada, lakini kwa siri kuna ukandamizaji wa jeuri na mashambulizi kwa dini na ibada. Wafuasi wa Kristo wanasingiziwa kuwa wahalifu wakubwa wa kitaifa na mbinu za mapinduzi zinachukuliwa ili kuwakandamiza, kuwazuilia, kuwatesa na hata kuwaua kwa ukatili. Serikali ya kikomunisti ya Kichina hutumia Katiba ili kupata umaarufu kwa kuudanganya umma lakini ni siri gani hata hivyo ambazo huathiri mambo na ambazo kufichiwa umma? 

Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Kilibuni Tukio la 5/28 la Zhaoyuan?



Baada ya kesi ya hadharani ya Tukio la Shandong Zhaoyuan, watu wenye utambuzi wote walitambua kuwa kesi hii ilibuniwa kabisa na Chama cha Kikomunisti cha China ili kulisingizia na kuliaibisha Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa makusudi. Ilikuwa kesi ya kuundwa na utumiaji vibaya wa haki. Sababu ya nia mbaya ya Chama cha Kikomunisti cha China kufanya hivi ni nini?

Jumapili, 11 Machi 2018

Kwa Nini Chama cha Kikomunisti cha China Kwa Hasira Kinakandamiza na Kutesa Imani ya Kidini?


Chama cha Kikomunisti cha China wakati huu wote kimewakandamiza kwa hasira, kuwashambulia na kupiga marufuku imani za kidini. Wanawachukulia Wakristo kama wahalifu wakuu wa taifa. Hawasiti kutumia njia za mapinduzi kukandamiza, kukamata, kutesa na hata kuwachinja. Sababu zao za kufanya mambo haya ni nini? Wale wanaoamini katika Mungu wanamheshimu Mungu kama mkuu. Wanamcha Mungu na wanalenga kutafuta ukweli na kutembea njia sahihi ya maisha. Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China kiwachukulie Wakristo kama maadui? Kwa nini hawalingani na watu wanaoamini katika Mungu? Video hii itachunguza sababu kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China kinatesa imani ya kidini.

Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Huwalazimisha Wakristo Kujiunga na Kanisa la Utatu Binafsi?




Nchini China, makanisa ya nyumbani yameteseka moja kwa moja matokeo ya ukandamizaji na utesaji wenye wayowayo wa serikali kanamungu ya Kikomunisti ya China. Wanawalazimisha kuingia katika Kanisa la Utatu Binafsi ambalo linadhibitiwa na Idara ya Kazi ya Muungano. Chama cha Kikomunisti cha China kinaficha siri gani kwa kufanya hili?

Jumamosi, 10 Machi 2018

Mjadala Kati ya Njia Mbili za Maisha na Kifo



Chama cha Kikomunisti cha China kinakandamiza kwa hasira na kushambulia imani ya kidini. Wanawafunga jela na kuwatesa kikatili Wakristo bila kujizuilia. Wanawaruhusu watu tu kufuata Chama cha Kikomunisti. Hawawaruhusu watu kumwamini Mungu na kumfuata Mungu wanapotembea njia sahihi ya maisha. Matokeo ya mwisho ya Chama cha Kikomunisti cha China yatakuwa nini? Chini ya ukandamizaji, ukamataji na utesaji wa hasira wa Chama cha Kikomunisti cha China, Wakristo kwa thabiti wanaendelea kumfuata Mungu, wakieneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu.

Ijumaa, 9 Machi 2018

Mbinu ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Kuwashurutisha Wakristo kwa Kutishia Familia Zao



Ili kuwashurutisha Wakristo kulighilibu kanisa, wamsaliti Mungu na kuharibu nafasi zao za kuokolewa na Mungu, Chama cha Kikomunisti cha China kwa ufidhuli kinawatishia wanafamilia wa Wakristo na kutumia hisia za familia za Wakristo kuwashurutisha kumsaliti Mungu. Je, njama za Chama cha Kikomunisti cha China zinaweza kuendelea? Katika mapambano haya kati ya mema na mabaya, Wakristo watawezaje kumtegemea Mungu ili kushinda majaribu ya Shetani na kusimama imara na kuwa na ushuhuda kwa Mungu?

Alhamisi, 8 Machi 2018

"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (2) - Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (2)




Waumini wengi wa Bwana wanahisi kwamba almradi tukiyafuata maneno ya Bwana, tukitenda unyenyekevu na uvumilivu, na kufuata mfano wa Paulo kwa kujitolea, kutumia rasilmali na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tutayaridhisha mapenzi ya Mungu. Na tutaletwa katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Hata hivyo, je, tumewahi kufikiria iwapo jitihada kama hizi kweli zitastahili sifa za Bwana na ruhusa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama sivyo, tunapaswa kufuatilia kupata sifa ya Bwana na kuletwa katika ufalme wa mbinguni vipi?

"Wakati Wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni




Watu wengine huamini, kwa kuwa Mungu aliweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote kwa neno moja, kuweza kuwafufua wafu kwa neno moja, Mungu pia Ataweza kubadili taswira zetu mara moja, kutufanya watakatifu, kutuinua hewani kukutana na Bwana wakati Atakaporudi katika siku za mwisho. Je, kweli ni ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni? Je, kazi ya kurudi kwa Mungu katika siku za mwisho rahisi hivyo jinsi tunavyofikiri? Mungu husema, "Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo zaidi. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine ya kawaida.

Jumatano, 7 Machi 2018

Ukweli Wafichuliwa Kuhusu Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 – CCP Ilikuwa Mwelekezi wa Siri wa Tendo Zima



Katika mwaka wa 2014, CCP ilibuni bila msingi maalum Tukio la Zhaoyuan lenye sifa mbaya la mnamo 5/28 katika jimbo la Shandong ili kutunga msingi wa maoni ya umma kwa ajili ya ukomeshaji kamili wa makanisa ya nyumba, na ikaeneza uwongo duniani kulaani na kuliharibia jina Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, baadhi ya washiriki wasiokusudiwa ambao hawakujua ukweli walidanganywa na propaganda za CCP. Katika programu hii, mashaka kadhaa makuu yanayoizunguka kesi hii yatafichuliwa ili kuchanganua uongo wa CCP mmojammoja na kukuelezea wazi ukweli, na kufichua kabisa ukweli kuhusu Tukio la Zhaoyuan la Shandong mbele ya ulimwengu.

"Wakati Wa Mabadiliko"(1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?



Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: "Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa" (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja. 

Jumanne, 6 Machi 2018

"Ivunje Laana" (5) - Je, Wachungaji na Wazee wa Kanisa wa Ulimwengu wa Dini Wanateuliwa na Bwana Kweli?



Mungu mwenyewe hutoa ushuhuda kwa kila mtu Anayemteua na kumtumia. Angalau, wote hupokea uthibitisho wa kazi ya Roho Mtakatifu, huonyesha matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu, na wanaweza kuwasaidia watu wa Mungu waliochaguliwa kupokea utoaji wa maisha na uchungaji wa kweli. Kwa sababu Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, kila mtu Anayemteua na kumtumia lazima alingane na mapenzi ya Mungu.

"Ivunje Laana" (6) - Je, Utiifu kwa Wachungaji na Wazee wa Kanisa ni Sawa na Kumtii Mungu?


Utambulisho
Waumini wengine huamini kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini wamechaguliwa na kuteuliwa na Bwana, na kwamba wote ni watu wanaomtumikia Bwana. Hivyo wanaamini kwamba kuwatii tu wachungaji na wazee wa kanisa ni kumtii Bwana, na kwamba kuwaasi au kuwahukumu wachungaji na wazee wa kanisa ni kumpinga Bwana.