Jumanne, 31 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema, Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja.

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu.

Jumatatu, 30 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Waovu Lazima Waadhibiwe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Zaidi ya unavyokubali neno la Mungu wakati huu, ndivyo unavyoweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo unavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake.

Jumapili, 29 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sitisha Huduma ya Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,


Mwenyezi Mungu alisema: Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni.

Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema, Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa.

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maonyo Matatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki


Mwenyezi Mungu anasema, "Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. 

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Mwenyezi Mungu alisema: Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo.

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo.

Alhamisi, 26 Oktoba 2017

Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili Ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, injili


Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi.

Jumatano, 25 Oktoba 2017

5. Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

Kutanafusi kwa Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huwezi kuijua hapo kwa sabubu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua likiangaza angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu alikupatia. Umeingia katika bahari ya uchungu isiyokuwa na mwisho, pasipo uwezo wa kukuokoa, hukuna tumaini la kuishi, umeachwa ukipambana na kuzunguka zunguka. …

Jumanne, 24 Oktoba 2017

4. Kueneza kwa Injili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu Nchini China

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


Mwaka wa 1995, kazi ya kushuhudia kwa injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu ilianza rasmi China Bara. Kwa njia ya shukrani kwa Mungu na kwa upendo ambao ulikuwa wa kweli, tulishuhudia kwa kuoenekana na kazi ya Mwenyezi Mungu kwa ndugu wa kiume na kike katika madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini. Hatukutarajia hata kidogo kukumbwa na upinzani na kukashifiwa kulikokithiri kutoka kwa viongozi wao. Tungeweza tu kuja mbele ya Mwenyezi Mungu kusali kwa ari, tukimsihi Mungu kufanya kazi binafsi. Kutoka 1997 na kuendelea, tulimwona Roho Mtakatifu akifanya kazi kwa kiwango kikubwa.

Jumatatu, 23 Oktoba 2017

Sifa Kamili | Dansi ya Kilatini ''Tukuzeni Ufanikishaji wa Kazi ya Mungu"



Tukuzeni Ufanikishaji wa Kazi ya Mungu
Kazi kubwa ya Mungu hubadilika haraka sana, vigumu kuipima, kuridhisha kwa mtu.
Angalia kandokando yako, si kama awali, kila kitu ni kizuri na kipya.
Kila kitu kimehuishwa, vyote vimetengenezwa upya, vyote vimetakaswa.
Tunamsifu Mungu, tukijawa furaha, nyimbo za sifa zinapepea mbinguni Kwake.
Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Watu wote msifuni Mungu kwa vigelegele.
Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Watu wote msifuni Mungu kwa vigelegele.
Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu, isifuni hekima Yake, isiyoshindwa.
Isifuni tabia Yake yenye haki, msifuni kwa kuwa ni Mungu mwaminifu.

Jumapili, 22 Oktoba 2017

3. Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu aliwaahidi wafuasi wake, “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.” (Yohana 14:3) Kadhalika Alitabiri, “Kwa maana kama umeme utokavyo mashariki, na kumulika hata magharibi; hivyo ndivyo ujio wake Mwana wa Adamu utakavyokuwa.” (Mathayo 24:27) Katika siku za mwisho, kama ilivyoahidiwa na kutabiriwa na Yeye, Mungu tena Amekuwa mwili na kushukia Mashariki ya dunia—China—kufanya kazi ya kuhukumu, kuadibu, ushindi, na wokovu Akitumia neno, kwa msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu.

Jumamosi, 21 Oktoba 2017

2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili


China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya. Matokeo yake, hakuna mahali pagumu zaidi ya hapa kueneza injili ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu. Wakati Chama cha Kikomunisti Cha China kiliposhika madaraka mwaka wa 1949, imani za kidini katika China bara zilizimwa kabisa na kupigwa marufuku. Mamilioni ya Wakristo walipitia mateso na fedheha hadharani, na kifungo. Makanisa yote yalifungwa kabisa na kufutiliwa mbali. Hata mikutano ya nyumbani ilipigwa marufuku.

Ijumaa, 20 Oktoba 2017

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. 

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa

    Mwenyezi Mungu alisema: Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika.

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

Mungu Amekuja Mungu Ametawala | " Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"


Kwaya za Injili :
1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
2. Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi
1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji.

Jumanne, 17 Oktoba 2017

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)


Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa
I
Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.
Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.
Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.
Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,
yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.
Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu.
Nainua mikono yangu kwa sifa, ninafurahia kwamba Ulikuja katika dunia hii.

Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi MunguWengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa


Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu. Wanadamu wote wakitofautishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

Jumamosi, 14 Oktoba 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli


Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Ijumaa, 13 Oktoba 2017

Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)


Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu
Mpaka siku moja,
utahisi kuwa Muumba
sio fumbo tena,
kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako,
kwamba Muumba
hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako,
kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo,
kwamba Muumba siye Yule unayemtamania katika mawazo yako

Alhamisi, 12 Oktoba 2017

Mwenyezi Mungu|Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu



Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote.