Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. Ndani Yangu kila kitu ni cha wazi; chochote Ninachosema kukamilisha kinakamilika na chochote Ninachosema kuanzisha kinaanzishwa, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuiga mambo haya kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa pekee.
Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong’aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu.