Jumapili, 14 Januari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, yesu
Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

 Mwenyezi Mungu alisema, Imesemwa “Yeye afuataye hadi mwisho ataokolewa,” lakini hili ni rahisi kuweka katika vitendo? Sio, na watu wengine hawawezi kufuata hadi mwisho. Pengine watakapokabiliwa na wakati wa majaribu, ama uchungu, ama jaribio, basi wanaweza kuanguka, na kutoweza kusonga mbele tena. Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu. Watu wengine wanaondoka wanapofikwa na mambo mabaya, na wanashindwa kusimama baada ya kila pingamizi. Watu hawa ni wapumbavu na watu hafifu, ambao wanaishi maisha yao yote bila kuupata ukweli, kwa hivyo watawezaje kufuata hadi mwisho? Kama kitu cha namna iyo hiyo kinakufanyikia mara kumi lakini hufaidi chochote kutokana nacho, basi wewe ni mtu hafifu na bure. Watu werevu na wale ambao kwa kweli wana ubora wa ndani wa kuelewa masuala ya kiroho ni watafutaji wa ukweli, na mara nane kwa kumi pengine wanaweza kupata ufunuo kiasi, funzo, kupata nuru na maendeleo. Kitu kama hicho kinapofanyika kwa mtu hafifu mara kumi, hatapata faida yoyote ya maisha hata mara moja, hatafanya mabadiliko hata mara moja na hataelewa asili yake hata mara moja kabla haijaisha. Anaanguka kila wakati kinapofanyika, kila wakati anahitaji mtu mwingine kumkokota ama kumvuta mbele, na wengine lazima wawachangamshe. Yeyote asipomchangamsha, kumvuta, kumgonga ama kumkokota basi itakuwa mwisho wa shindano na hasimami. Kila wakati kinapofanyika, kuna hatari ya kuanguka, na kila wakati kuna hatari ya yeye kudhoofika. Je, huu sio mwisho kwake? Je, bado kuna sababu zozote kwao kuokolewa? Kumwokoa mtu ni kuokoa sehemu yake ambayo ni nia yake na azimio lake, na sehemu yake katika moyo wake ambayo ni kutaka kwake sana ukweli na haki. Kusema mtu ana azimio kunamaanisha kuwa anataka sana haki,uzuri na ukweli, na kuwa ana dhamiri. Mungu huokoa sehemu hii yako, na kupitia kwa hili Anabadilisha kipengele cha tabia yako potovu. Kama huna vitu hivi, basi huwezi kuokolewa. Usipotaka haki kwa hamu ama kufurahi katika ukweli, huna radhi ya kutupa mbali vitu viovu ama azimio la kupitia shida, na kama dhamiri yako ni yenye ganzi, welekevu wako wa kupokea ukweli pia ni wenye ganzi, hauko makini kwa ukweli ama vitu vinavyofanyika, huwezi kutofautisha chochote, na huna uwezo huru wa kushughulikia ama kutatua mambo, basi hakuna njia ya kuokolewa. Mtu wa haina hii hana chochote cha kumpendekeza, hana chochote cha thamani cha kufanya kazi nacho. Dhamiri yake ni yenye ganzi, akili yake imejaa matope, hafurahi katika ukweli ama kutaka haki ndani kabisa mwa moyo wake, na hajibu bila kujali vile Mungu Ananena kwa wazi ama kwa dhahiri kuhusu ukweli, kana kwamba amekufa tayari. Je, haijafika mwisho kwake? Yeyote aliye na pumzi anaweza kuokolewa kwa upumuaji bandia, na pumzi yake inaweza kufufuliwa. Lakini kama amekufa tayari na roho yake imeondoka, basi upumuaji bandia hautafanya lolote. Kitu kinapokufika, unanywea, na huwi na ushuhuda wotote, kwa hivyo huwezi kuokolewa kamwe na utakuwa umefika mwisho. Unapokabiliwa na mambo, unafaa kufanya uchaguzi, unafaa kuyaendea kwa usahihi, unahitaji kutulia na unahitaji kuutumia ukweli kutatua shida ile. Kuna maana gani ya wewe kuelewa ukweli fulani kwa kawaida? Hauko hapo tu ili kujaza tumbo lako na hauko hapo kunenwa tu na si chochote zaidi, wala hauko kwa ajili ya kutatua shida za wengine; badala yake uko ili kutatua ugumu wako mwenyewe, na ni baada tu ya kutatua shida zako binafsi ndipo utaweza kutatua shida za wengine. Mbona inasemwa kuwa Petro ni tunda? Kwa sababu ana kitu cha thamani, ama kitu kilicho na thamani ya kukamilisha, ana azimio la kuutafuta ukweli na ana nia imara; ana sababu, yuko tayari kupitia shida, na anafurahia katika ukweli katika moyo wake, na anapokabiliwa na kitu hatakiachilia. Hizi zote ni hoja zenye nguvu. Kama huna yoyote kati ya alama hizi nzito, basi inabashiri shida na ni kitu kibaya. Hujui jinsi ya kupitia chochote, huna uzoefu, na hutaweza kutatua ugumu wa wale walio chini yako. Hii ni kwa sababu hujui jinsi ya kuingia, unachanganyikiwa unapofikwa na mambo, unahisi kuhuzunishwa, unalia, unakuwa hasi, unatoroka, na huna uwezo wa kuuelekea kwa usahihi kwa njia yoyote. Kuwapatia watu ukweli ni kuwapatia kanuni katika ushirika, na kama una kiwango cha hisi cha kimya kimya, basi utapata utashuhudia mkutano wa akili. Lakini kama wewe ni ganzi na huukubali ukweli, basi kuonyesha vitu hakutakuwa na maana na hutaelewa kwa kutumia mifano. Kwa kufunzwa kila wakati ukiwa umeshikiliwa mkono juu ya mkono, unapoachiliwa mkono, utaisha. Iwe ni masuala makubwa ama madogo yanayokufika, kila wakati unakuwa hasi, mnyonge, na huna ushuhuda wowote. Unachofaa kufanya ama kushirikiana nacho, unakosa kukifanya, ukithibitisha kuwa huna Mungu ama ukweli ndani ya moyo wako. Mbali na jinsi kazi ya Roho Mtakatifu inavyowagusa watu, watu wanaweza bado kufikia viwango vya chini kabisa kwa kutegemea miaka mingi ya uzoefu wao, ukweli mwingi ambao wamesikia, dhamiri kiasi, na kutegemea nia yao kutenda kwa kujizuia; ilhali bado ni bora kuliko jinsi ulivyo ganzi na mnyonge sasa. Hili haliwezi kuwazika. Pengine mmekuja kwa uzembe miaka hii miwili, vinginevyo mngewezaje kuwa ganzi na walegevu mlivyo sasa? Kwa kweli umejikataa mwenyewe, ukisema “Siko sawa, mimi ni mpotovu, hivyo tu ndivyo ilivyo, na nitakuwa tu mpotovu!” Umejifungia mlango mwenyewe, na hujajitahidi, hata ukisema “Huu ni ugumu wangu. Ni heri hata unitume tu nyumbani!” Je, huzungumzi upuuzi? Unakwepa tu na kupuuza wajibu. Kama una dhamiri hata kidogo na busara unafaa kukamilisha misheni yako vizuri; kuwa mtoro ni kitu kibaya sana na ni kumsaliti Mungu. Kufuuatilia ukweli unahitaji nia thabiti, na watu walio hasi sana ama wanyonge hawatafanikisha chochote. Hawataweza kumwamini Mungu hadi mwisho, na kuupata ukweli na kutimiza mabadiliko ya tabia kutakuwa hata zaidi bila matumaini. Wale tu wanaoutafuta ukweli kwa azimio wataupata ukweli na kukamilishwa na Mungu.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kujua zaidi: Kujua Umeme wa Mashariki  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni