Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 48. Ni kwa Kuzielewa Hali Zako tu Ndipo Utakapoweza Kutembea Katika Njia Sawa
Ndani ya mwanadamu mara nyingi zipo baadhi ya hali mbaya. Miongoni mwao ni baadhi ya hali ambazo zinaweza kuwaathiri watu au kuwadhibiti. Kunazo baadhi ya hali ambazo zinaweza hata kumfanya mtu kuiacha njia ya kweli na kuelekea katika njia mbovu.
Kile mwanadamu anachokitafuta, kile wanachozingatia na njia wanayochagua kuifuata—haya yote yanahusiana na hali zao za ndani. Hata zaidi ni udhaifu wa mwanadamu au nguvu inayohuhusiana moja kwa moja na hali zao za ndani. Kwa mfano, watu wengi sasa hutilia mkazo hasa kwa siku ya Mungu; wote wana hamu nayo, wakiionea shauku siku ya Mungu ifike haraka ili waweze kujinasua kutoka kwenye mateso haya, magonjwa haya, mateso haya na zaidi. Watu wanadhani kwamba wakati siku ya Mungu itakapofika basi wataachiliwa kutoka kwenye mateso haya, hawatapata mateso tena kamwe, nao watakuwa huru.
Kama mtu anahitaji kutafuta kumwelewa Mungu au kuutafuta ukweli katika hali ya aina hii, basi kutafuta kwao kutakuwa finyu. Wakati kikwazo chochote au kitu chochote kibaya kinawapata, basi udhaifu wote, uhasi na ukaidi ndani mwao unajitokeza. Hivyo kama hali ya mtu si ya kawaida au sio sahihi, basi lengo la kutafuta kwao pia halitakuwa sahihi na bila shaka litakuwa lisilo safi. Baadhi ya watu wanatafuta kuingia kutokana na hali zisizo sahihi, lakini wanafikiri wanafanya vizuri katika kutafuta kwao, kwamba wanafanya mambo kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu nao wanatenda kwa mujibu wa ukweli. Hawaamini kwamba wameenda kinyume na kusudi la Mungu au wamendoka kwa mapenzi Yake. Unaweza kuhisi hivyo, lakini wakati tukio fulani baya au mazingira magumu yanakusababishia mateso, basi linagusa maeneo yako dhaifu nalo linagusa mambo unayoyaonea shauku kwa kina katika nafsi yako. Matumaini yako yanatoweka na ndoto zako hazifaulu hivyo kwa kawaida unakuwa mdhaifu. Hivyo hali yako kwa wakati huo itaamua ikiwa wewe ni mwenye nguvu au mdhaifu. Sasa kunao wengi ambao wanahisi kuwa wao wana nguvu sana nao wanacho kimo kiasi, au kwamba wanayo imani zaidi kuliko awali, kwamba wako kwenye njia sawa nao hawamhitaji tena mtu yeyote kuwavuta au kuwachochea. Hivyo ni kwa nini wao wanaweza kuwa wadhaifu wakati wanapokabiliwa na mazingira magumu? Kwa nini mazingira haya huwasababisha kupoteza imani yao? Hadi pale ambapo hata wanaurudia ulimwengu? Aidha, kunao wale ambao hukiri kwamba kuna Mungu lakini hawana hiari ya kumwamini. Hii inaonyesha kwamba kila mtu anazo hali zisizo za kawaida. Hata kama unawamini Mungu na kuutafuta ukweli, bado huwezi kuyaacha mambo fulani ndani mwako kabisa. Baadhi ya mambo machafu ndani ya mwanadamu hayaachwi kwa urahisi, basi mwanadamu anaweza tu kubadilisha hatua kwa hatua mara tu anapokuwa na uelewa wao kupitia ufunuo wa Mungu. Baadhi ya watu wanadhani bado hawaoni mabadiliko baada ya kuzungumza kuhusu hali zao. Hiki si kitu kimoja! Baada ya kulizungumzia wao hutambua kwamba hali si sawa nao watakuwa na uwezo wa kulitambua kama si kawaida wakati linaporejea katika siku za usoni. Pia watatambua kwamba, kwa moyo kama huu, kutafuta kwao kuingia na kutekeleza wajibu wao hakuwezi kufikia kiwango ambacho Mungu anahitaji, hata kwa kiasi kidogo hakuwezi kumridhisha Mungu. Watu wengi huanza kuamini kwa kutafuta kwao katika kigezo cha uongo, matokeo yake ni kwamba mara nyingi zaidi wanakuwa hasi na wadhaifu, nao hawawezi kubaki wamesimama. Kuchukua mfano mfano: Baadhi ya watu huhisi katika mawazo yao kwamba Mungu huwapa ahadi kwamba hawatapatikana, au kwamba sasa wameitelekeza familia yao, Mungu atahakikisha kuwaangalia kwa muda wote wa maisha yao. Wanahisi kwamba lazima Mungu awe hivi, hadi siku moja jambo linatokea ambalo linatofautiana na hamu zao; inaweza kuwa ugonjwa, na kuishi na familia zinazowakaribisha hakuna raha kama kuishi na familia zao wenyewe kulivyokuwa, wakati walikuwa na uwezo wa kula kile walichotaka na kulala wakati waliotaka, nao wanahisi hawawezi kuvumilia ikiwa utunzaji wa wengine kwao kidogo unakosa, hivyo wanakuwa wadhaifu katika hali hizi. Jambo kama hili linaweza kuwasababisha kuvunjika moyo na kuwa wadhaifu, nao watalalamika kwa muda mrefu, hata kufikia kiwango ambacho wanakoma kuutafuta ukweli na kukana umuhimu wa imani katika Mungu. Hivyo kama watu hawaelewi baadhi ya hali ndani mwao au kama hawahisi kwamba wamekosea, basi haijalishi wanavyoutafuta ukweli kwa bidii au jinsi walivyo na shauku, wanaweza kuanguka siku moja. Watu wachache sana wanaweza kuupata ukweli, hata hivyo. Kuuelewa ukweli si jambo rahisi. Inachukua muda mrefu kuelewa hata kiasi kidogo, muda mrefu kuwa na uelewa kidogo kwa njia ya uzoefu, kutambua uelewa safi kwa kiasi kidogo au kupata mwanga kidogo. Kama hutatatua uchafu wote ndani mwako, basi huo mwanga kidogo unaweza kuzama wakati wowote au mahali popote. Ugumu mkubwa na mwanadamu sasa ni kwamba kila mtu anao ubunifu fulani ndani mwake, dhana, hamu na maadili tupu ambao wao wenyewe hawawezi kugundua. Mambo haya mara kwa mara huambatana na watu, yakiwachanganya kwa ndani. Hii kwa hakika ni hatari sana nao labda watakosea wakati wowote, wakiongea upuuzi au kuanza kunung'unika. Kunao uchafu mwingi sana ndani ya mwanadamu. Ingawa wanaweza kuwa na hamu nzuri, kama vile “Lazima niutafute ukweli, lazima niwe muumini mzuri katika Mungu,” bado hawawezi kuyatimiza malengo yao. Aina hii ya kitu kinatokea mara nyingi katika uzoefu wa kila mtu. Watu wengine wanaweza kufikiri kwamba masuala haya madogo yanaweza kuachwa kwa urahisi, lakini mbona huwezi kuyaacha? Kwa nini wale ambao kwa kawaida wana uzoefu kiasi, ambao wanaonekana wenye nguvu zaidi kulingana na wengine, na wenye kuelewa haraka, huanguka wanapokumbana na jambo dogo, na kuanguka haraka sana? Ni kweli kwamba mwanadamu yuko chini kubadilika badilika kwa bahati; wanawezaje kulitabiri? Ndani ya kila mtu kunayo baadhi ya mambo ambayo wana hiari ya kuyafuatilia na kuyapata, na kila mtu anayo mambo yake anayoyapenda. Mara nyingi, watu hawawezi kutambua hili wenyewe, au wanaamini mambo haya ni mazuri, kwamba hakuna jambo lolote baya nao. Kisha siku moja jambo kama hili linatokea nao wanajikwaa, wanakuwa hasi, wadhaifu, nao hawawezi kurudi juu. Pengine hawajui wenyewe tatizo ni nini, wao huhisi tu kwamba wana haki na kwamba ni Mungu ambaye amewadhulumu. Kama hujielewi basi kamwe hutaweza kujua mahali matatizo yako yapo, wala hautajua jinsi utakavyokutana na hatima yako. Ni ya kusikitisha. Inaonekana kama uchafu ndani ya mwanadamu unaweza kuwaletea uharibifu wakati mwingine.
Watu wengi wamesema hivi mbeleni: “Naelewa ukweli wote, ni vile tu siwezi kuutia katika vitendo.” Sentensi hii inafichua tatizo la msingi , ambayo pia ni tatizo katika asili ya watu. Kama asili ya mtu imechoshwa na ukweli basi kamwe kuwatautia ukweli katika vitendo. Wale ambao wamechoka na ukweli bila shaka watakuwa na hamu badhirifu na imani yao katika Mungu; haijalishi kile wanachokifanya, nia zao daima huwepo. Kwa mfano, baadhi ambao wamepitia mateso nao hawawezi kurudi nyumbani wanatamani na kusema: "Ah, mimi bado hawezi kwenda nyumbani baada ya muda huu wote. Lakini najua kwamba siku moja Mungu atanipa makazi bora. Ataniondoa matesoni naye atanipa chakula nile haijalishi ninapoishi. Mungu hatanielekeza katika mwisho usio na mafanikio. Kama Angefanya basi Atakuwa amefanya vibaya, Atakuwa Amefanya makosa. Halitakuwa kosa langu.” Je, si watu huwa na mawazo haya ndani mwao? Au kunao baadhi yao wanafikiria, “Nagharimika pakubwa kwa ajili ya Mungu, hivyo Hafai kuniweka katika mikono ya mamlaka tawala.” Au wanafikiri, “Nimetelekeza mengi nami nautafuta ukweli kwa dhati, hivyo ni haki tu kwa Mungu kunilipiza kwa kufanya hiki-na-kile” au “Tunaitazamia sana siku ya Mungu kuwasili, hivyo siku ya Mungu inapaswa kuwasili haraka na Mungu ayatimize matakwa yetu”. Zaidi ya hayo, watu hufanya madai badhirifu kwa Mungu, kama vile: “Tumefanya hili, hivyo ni haki tu kwa Mungu kufanya kitu hiki-na-kile. Tumetimiza mambo fulani kwa hivyo lazima Mungu aturidhie zawadi fulani na kutupa baraka fulani.” Watu wengi wanayo mawazo haya ndani mwao. Wanapowaona wengine wakiyaacha makazi yao, wakiwaacha waume zao na familia zao, kisha kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu katika njia ya burudani, wanasononeka na kufikiri: “Wengine wameacha makazi yao kwa muda mrefu sana, wanawezaje kushinda? Siri yao ni nini? Kwa nini mimi siwezi kushinda kamwe? Kwa nini daima mimi hukumbuka nyumbani? Kwa nini siwezi kamwe kuiachilia familia yangu, mume wangu na watoto wangu?” Hatimaye, wanafikiri:" Kwa nini Mungu ni mwenye huruma kwake lakini sio kwangu? Kwa nini daima nakumbuka nyumbani? Kwa nini Roho Mtakatifu hanikirimii neema? Kwa nini Mungu hayuko nami?” Hii ni hali gani? Watu hawana busara. Hawautii ukweli katika vitendo lakini badala yake wanalalamika kuhusu Mungu. Hawana juhudi zao wenyewe wala kitu chochote wanachostahili kufikia wenyewe cha dhahania. Wamekata tamaa kuhusu maamuzi ambayo wanapaswa kuyafanya wenyewe na njia wanayopaswa kutembea. Mara zote wanamhitaji Mungu kufanya hili au lile, nao wanamtaka Mungu awe na huruma kwao bila kusaza, kuwaneemesha bila kusaza, kuwaongoza, kuwapa raha. Wanafikiri: Nimeyaacha makazi yangu, nimetelekeza mengi sana, ninatenda wajibu wangu nami nimeteseka sana. Kwa hiyo Mungu anastahili kunineemesha, anifanye nisikumbuke nyumbani, anipe azimio la kuyatelekeza mambo, na kunifanya mwenye nguvu zaidi. Kwa nini mimi ni mdhaifu sana? Kwa nini watu wengine wana nguvu sana? Mungu anastahili kunifanya niwe mwenye nguvu.” Ukimwona mtu akisema maneno haya, ni wazi kwamba wao hawana busara kabisa, hata zaidi hawana ukweli wowote. Je, malalamiko ya watu yanatokeaje?” Ah, mbona watu wengine wana familia inayowakaribisha wakati wao hawawezi kurudi nyumbani? Mbona sina mahali popote pa kukaribishwa? Kwa nini siwezi kupata hayo? Watu wengine wote wanaweza kwenda nyumbani, lakini kwa nini kuna hali mbaya nyumbani kwangu? "Haya ni mawazo ambayo yanatokea kutoka ndani ya watu nayo kabisa yanawakilisha asili zao. Mambo haya ndani mwao, haijalishi ni mazingira gani wanayokumbana nayo, yanaweza kuwasababisha kuitelekeza njia ya kweli na kumsaliti Mungu wakati wowote. Haijalishi kimo chao ni kikubwa kiasi gani, haijalishi wanauelewa ukweli kwa kiasi gani, kama hawawezi kuyatupilia mbali mambo haya ndani mwao, kamwe hawatakuwa na uhakika wowote kubaki wamesimama. Itawezekana kwao kumsaliti Mungu, kwao kumkufuru Yeye na wao kuitelekeza njia ya kweli wakati wowote na mahali popote. Hili ni jambo ambalo linaweza kutokea kwa urahisi sana. Je, mnaelewa kwa uwazi sasa? Watu wanapaswa kuelewa na kuwa weledi jinsi asili zao zinaweza kufichuka wakati wowote; lazima walikabili tatizo hili kwa busara. Wale walio na uelewa mzuri zaidi wa ukweli wakati wingine watakuwa na ufahamu kiasi. Basi wanaweza kuligundua tatizo na kujichunguza kwa kina. Wakati mwingine, hata hivyo, hawatakuwa na ufahamu wa tatizo na hivyo hakutakuwa na lolote wanaloweza kufanya. Wanaweza tu kumsubiri Mungu awafichulie au awafunulie ukweli huo kwao. Watu wasio na fikra mara kwa mara watafahamu, lakini watakuwa tu wacheshi, wakisema: “Oo’, watu wote wako hivi kwa hivyo haina maana yoyote. Mungu atanisamehe na wala hatalikumbuka. Hii ni kawaida tu.” Kile wanapaswa kuchagua na kile wanapaswa kufanya hawakifanyi na wala hawakifikii. Wote ni wapumbavu, wametepetea kabisa, nao wana utegemezi sana, hata wakitarajia yasiyowezekana: “Kama Mungu atatubadilisha kabisa siku moja, hatutakuwa watepetevu tena. Kisha tunaweza kuendelea kutembea bila msaada. Basi Mungu hatakuwa na haja kujisumbua nasi sana.” Kwa hivyo, lazima uone wazi sasa. Kutembea njia hii inamaanisha kwamba unapaswa kuwa na maamuzi yako mwenyewe, na jinsi kila mtu anaamua ni muhimu. Unao ufahamu huu, hivyo una nguvu kiasi gani inapohusu kujinyima? Je, unayo nguvu kiasi gani inapohusu kujitelekeza. Hiki ni kigezo cha kuutenda ukweli nayo ni sehemu muhimu. Wakati unakumbana na chochote au unapofanya lolote katika hali ambayo unafahamu jinsi ya kulifanya kulingana na ukweli, unafanya uamuzi gani? Je, unapaswa kutia nini katika vitendo? Baada tu ya kulibainisha jambo kwako mwenyewe ndipo utakapojua jinsi ya kuendelea. Kama unaweza kufahamu ukweli na ubaya wa hali zako mwenyewe lakini huwezi kuwa wazi kabisa nawe unaendelea tu katika njia yako ya kipumbavu, basi hutapata maendeleo yoyote au kuwa na uzoefu wa mafanikio yoyote. Kama hauko makini kuhusu kuingia katika maisha, basi unajirudisha nyuma tu, na hii inaweza tu kuthibitisha kwamba huupendi ukweli. Hapo awali, baadhi ya watu waliwaza: “Tunatamani joka kubwa jekundu lianguke haraka nasi tunayo hamu ya siku ya Mungu iwasili haraka. Je, si madai haya ni sahihi? Si kuwa na shauku ya siku ya Mungu kufika kwa haraka ni sawa na shauku ya kutukuka kwa Mungu kwa haraka?” Watu huweka katika matendo tafsiri zao zilizofichika lakini zilizo nzuri wakati, kwa kweli, watu wanafanya haya tu kwa ajili yao wenyewe. Ni nini wanachokuwa na shauku nacho ambacho sio kwa ajili yao wenyewe? Hakuna. Wao hufanya hivi tu ili wao wenyewe waweze kuwekwa huru kutokana na mazingira yao magumu, ili wawekwe huru kutoka katika dunia hii chungu kwa haraka. Kuna baadhi ya watu hasa ambao wanaona ahadi iliyotolewa mwanzo kwa wazaliwa wa kwanza wa Mungu nao wanapata kiu ya ajabu kwalo. Wakati wowote wanayaposoma maneno hayo, ni kama kujifariji na matumaini ya uongo. Tamaa na hamu za kibinafsi ndani ya mwanadamu bado hazijaachwa kabisa, hivyo haijalishi ni jinsi gani wanavyoutafuta ukweli, utakuwa tu wa kusitasita milele. Wakati baadhi ya waumini wanaionea shauku siku ya Mungu lakini hairejei, jinsi gani wanavyopiga makelele na kulia kwa maumivu! Wakiwa na huzuni kana kwamba wao ndio waliounguzwa na kuchomwa kwa moto, wao karibu hupiga kelele kwa sauti kubwa: “Oo! Siwezi kuvumilia hili tena! Ni lini siku ya Mungu itarejea? Hatuwezi kuvumilia tena! Oo, mbona siku ya Mungu haiji upesi? Hebu tuombe pamoja.” Wanahisi kana kwamba miaka hii miwili imekuwa haivumiliki. Jinsi gani wale wakongwe wa kanisa ambao daima wamemfuata Mungu bado wanamfuata Mungu sasa? Je si haya maneno yanawaendeleza? Je, ni sawa kwako kuwa uchafu mwingi ndani mwako lakini usikubali usafishaji? Unawezaje kubadilika bila kuvumilia mateso? Ni kwa kusafishwa tu kwa kiwango fulani ndipo utakapoweza kuzingatia mipango ya Mungu kwa hiari na kutokuwa na malalamiko yoyote kamwe. Wakati huo utakapofika, utakuwa umebadilika kabisa.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni