Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X |
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X
2. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani
Tumemaliza kujadili mzunguko wa uhai na mauti wa kundi la kwanza, wasioamini. Hebu sasa tujadili ule wa kundi la pili, watu mbalimbali wenye imani. “Mzunguko wa uhai na mauti wa watu mbalimbali wenye imani” vilevile ni mada muhimu sana, na inafaa kwamba muwe na kiasi fulani cha uelewa wake. Kwanza, hebu tuseme ni imani gani “imani” katika “watu wenye imani” inarejelea nini: Inamaanisha Uyahudi, Ukristo, Ukatoliki, Uisilamu, na Ubudha, dini hizi kuu tano. Pamoja na wasioamini, watu ambao ni waumini katika hizi dini tano wanajumuisha idadi kubwa ya watu duniani.
Miongoni mwa dini hizi tano, wale ambao wametengeneza ajira kutokana na imani yao ni wachache, lakini hizi dini zina waumini wengi. Waumini wake huenda sehemu tofauti wanapokufa. “Tofauti” na nani? Na wasioamini, watu wasiokuwa na imani, ambao tumemaliza kuzungumzia. Baada ya kufa, waumini wa hizi dini tano huenda mahali pengine, mahali tofauti na wasioamini. Lakini ni mchakato sawa. Ulimwengu wa kiroho pia utafanya uamuzi juu yao kutegemea yale yote waliyoyafanya kabla wafe, baadaye watatayarishwa ipasavyo. Lakini mbona hawa watu wanawekwa sehemu tofauti kutayarishwa? Kuna sababu muhimu ya hili. Na hii sababu ni gani? Nitawaambia kutumia mfano. Lakini kabla nifanye hivyo, mnaweza kuwa mkijiwazia: “Labda ni kwa sababu wana imani ndogo katika Mungu! Wao si wasioamini kabisa.” Hii ndiyo sababu mbona. Kuna sababu muhimu sana kwa wao kuwekwa mahali pengine.
Chukua Ubudha: Hebu Niwaambie ukweli. Mfuasi wa Budha, kwanza kabisa, ni mtu aliyebadili dini kwenda Ubudha, na ni mtu ajuaye imani yake ni nini. Mfuasi wa Budha akinyoa nywele zake na kuwa mtawa wa kiume au mtawa wa kike, hii inamaanisha kuwa wamejitenga na mambo ya kidunia na kuacha nyuma ghasia ya dunia ya mwanadamu. Kila siku wanakariri maandiko ya Kibudha na kula chakula bila nyama, wanaishi maisha ya kujinyima anasa za kimwili, na kupitisha siku zao ndani ya mwangaza baridi, na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi. Wanaishi maisha yao yote kwa njia hii. Maisha yao ya kimwili yaishapo, wanatengeneza muhtasari wa maisha yao, ila mioyoni mwao hawajui watakapoenda baada ya kufa, watakutana na nani, na watakuwa na hatima ya aina gani—mioyoni mwao hawana uhakika na haya mambo. Hawajafanya chochote zaidi ya kuishi bila mwelekeo maisha yao yote wakiambatana na imani, baadaye wanaondoka duniani wakiambatana na matamanio na maadili wasiyoyafahamu. Hiyo ndiyo tamati ya maisha yao ya kimwili wanapoiaga dunia ya walio hai, na wakati maisha yao ya kimwili yanapoisha, wanarudi katika sehemu yao asilia katika ulimwengu wa kiroho. Kama hawa watu watapata mwili na kurudi duniani kuendelea na kujikuza kwao inategemea mienendo na kujikuza kwao kabla ya kifo chao. Ikiwa hawakufanya kitu kibaya wakati wa uhai wao, watapata mwili haraka na kurudishwa duniani, ambapo watakuwa watawa wa kiume au watawa wa kike tena. Kulingana na utaratibu wa mara ya kwanza, mwili wao unajikuza wenyewe, baada ya hapo wanakufa na kurudi katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanatathminiwa, baada ya hapo—ikiwa hakuna shida—wanaweza kurudi tena katika ulimwengu wa wanadamu, na kuweza kubadili dini hadi Ubudha tena na kuendelea kujikuza. Baada ya kupata mwili mara tatu hadi mara saba, watarudi tena katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanakwenda kila mara ambapo maisha yao ya kimwili yanamalizika. Ikiwa viwango na mienendeo yao mbalimbali katika ulimwengu wa wanadamu inaambata na sheria za mbinguni za ulimwengu wa kiroho, basi watabaki huko kutoka wakati huu kuendelea; hawatapata mwili tena kama wanadamu; wala hakutakuwa na tishio la wao kuadhibiwa kwa kutenda maovu duniani. Hawatawahi kupitia tena mchakato huu. Badala yake, kulingana na hali zao, watachukua nyadhifa katika milki ya kiroho. Hili ndilo wafuasi wa Budha wanaliita kupata uzima wa milele. Kupata uzima wa milele kunamaanisha hasa kuwa afisa wa ulimwengu wa kiroho, na kutokuwepo na nafasi zaidi ya kupata mwili au adhabu. Zaidi ya hayo, ina maana kwamba hakuna kupata taabu tena ya kuwa mwanadamu baada ya kupata mwili. Hivyo basi, bado kuna uwezekano wao kupata mwili tena kama wanyama? (La.) Hili linamaanisha kwamba wanabaki kushika nafasi katika ulimwengu wa kiroho, na kamwe hawatapata mwili. Huu ni mfano mmoja wa kupata uzima wa milele katika Ubudha. Na kuhusu wale ambao hawapati uzima wa milele baada ya wao kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanatathminiwa na kuthibitishwa na msimamizi anayehusika, na kuonekana hawakujikuza kwa makini au kuwa makini katika kukariri maandiko ya Kibudha kama inavyotakiwa na Ubudha; badala yake, walitenda maovu mengi, na kutenda mengi yaliyo mabaya. Katika ulimwengu wa kiroho hukumu inatolewa basi juu ya uovu wao, na baada ya hapo wana hakika ya kuadhibiwa. Hakuna vighairi katika hili. Basi, mtu wa aina hii atapata lini uzima wa milele? Katika maisha ambamo hawatatenda maovu—wakati, baada ya kurudi katika ulimwengu wa kiroho, inaonekana hawakufanya chochote kibaya kabla hawajafa. Wanaendelea kupata mwili, wanaendelea kukariri maandiko ya Kibudha, wanapitisha siku zao ndani ya mwangaza baridi na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi, bila kuua chochote chenye uhai, bila kula nyama, na hawaufurahii ulimwengu wa mwanadamu, kuachana na vurugu zake kabisa, na kuepuka migogoro na wengine. Katika mchakato huu, hawafanyi maovu, kufuatia hayo wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na baada ya matendo na mienendo yao yote kutathminiwa, wanatumwa tena katika ulimwengu wa wanadamu, kwa mzunguko unaojirudia mara tatu au saba. Ikiwa hakuna kikwazo wakati huu, basi kupata kwao uzima wa milele hakutaathiriwa, na hakutacheleweshwa. Hii ni sifa ya mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani: wanaweza kupokea uzima wa milele na kushikilia wadhifa katika ulimwengu wa kiroho. Hili ndilo linawafanya kuwa tofauti na wasioamini. Kwanza kabisa, wanapokuwa hai duniani, matendo ya wale wanaoweza kushika wadhifa katika ulimwengu wa kiroho ni yapi? Ni sharti wasifanye kabisa ovu lolote: ni lazima wasifanye mauaji, uchomaji, ubakaji, au wizi; wakifanya hila, udanganyifu, au ujambazi, basi hawawezi kupata uzima wa milele. Ina maana kwamba, wakiwa na uhusiano au ushirikishaji wowote na uovu, hawataweza kuepukana na adhabu ya ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho unafanya mipango inayofaa kwa wafuasi wa Budha wapatao uzima wa milele: wanaweza kuteuliwa kusimamia wale ambao wanaonekana kuamini katika Ubudha, na yule Mzee aliye Angani, na wafuasi wa Budha watapewa mamlaka, wanaweza tu kuteuliwa kuwasimamia wasioamini, vinginevyo wanaweza kuwa wasimamizi wadogo sana. Ugavi huo unalingana na asili ya hizi roho. Huu ni mfano wa Ubudha.
Miongoni mwa dini tano tulizozungumzia, Ukristo ni maalum kiasi fulani. Ni nini maalum kuhusu Ukristo? Hawa ni watu wanaomwamini Mungu wa kweli. Je, inawezekanaje wale wanaomwamini Mungu wa kweli waorodheshwe hapa? Kwa sababu Ukristo ni aina ya imani, basi, bila shaka, unahusiana tu na imani—ni aina ya sherehe, aina ya dhehebu, aina ya dini, na kitu tofauti na imani ya wale wanaomfuata Mungu kweli. Kilichonifanya kuuorodhesha miongoni mwa hizi dini tano ni kwa sababu Ukristo umeshushwa hadi kiwango sawa na Uyahudi, Ubudha, Uislamu. Wakristo wengi hawaamini kuna Mungu, au kwamba Anatawala juu ya vitu vyote, seuze kuamini katika uwepo Wake. Badala yake, wanatumia tu Maandiko Matakatifu kuzungumza kuhusu elimu ya dini, wakitumia elimu ya dini kuwafundisha watu kuwa wema, kuvumilia mateso, na kufanya vitu vizuri. Ukristo ni wa aina hiyo ya dini: Unazingatia tu nadharia za mafundisho ya kidini, hauna kabisa uhusiano wowote na kazi ya Mungu ya kusimamia na kuokoa wanadamu, ni dini ya wale wanaomfuata Mungu ambayo haitambuliwi na Mungu. Lakini pia Mungu ana kanuni kuhusu mtazamo Wake kwao. Hawatendei na kuwashughulikia wapendavyo bila mpango, njia sawa na wasioamini. Mtazamo Wake kwao ni sawa na Alio nao kwa wafuasi wa Budha: Ikiwa, angali hai, Mkristo anajiheshimu, anaweza kuzifuata kabisa Amri Kumi za Mungu na kuzingatia sheria na amri katika mahitaji yao kwa tabia zao wenyewe—na ikiwa wanaweza kufanya hivi katika maisha yao yote—basi pia watalazimika kuchukua muda sawa kupitia mzunguko wa uhai na mauti kabla hawajaweza kweli kupata huko kuitwako kuchukuliwa kuenda mbinguni. Baada ya kupata huku kunyakuliwa wanabaki katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanashika wadhifa na kuwa miongoni mwa wasimamizi. Vivyo hivyo, wakifanya maovu duniani, ikiwa ni watenda dhambi na kufanya dhambi nyingi, basi haiepukiki kwamba wataadhibiwa kwa ukali unaotofautiana. Katika Ubudha, kupata uzima wa milele kunamaanisha kuingia Sukhavati, lakini hii inaitwaje katika Ukristo? Inaitwa “kuingia mbinguni” na “kunyakuliwa.” Wale ambao kwa kweli “wananyakuliwa” pia wanapitia mzunguko wa uhai na mauti mara tatu hadi saba, halafu, wakiwa wamekufa, wanaingia katika ulimwengu wa kiroho, kana kwamba walikuwa usingizini. Ikiwa walikuwa wanafaa wanaweza kusalia kushika wadhifa, na tofauti na watu walio duniani, hawatapata mwili kwa njia rahisi, au kulingana na mazoea.
Miongoni mwa dini hizi zote, mwisho wanaouzungumzia na kuupigania ni sawa na kupata uzima wa milele katika Ubudha—tofauti ni kuwa unapatikana kwa njia tofauti. Wote ni wa aina moja. Kwa hili kundi la watu wa dini hizi ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini katika tabia zao, Mungu huwapa hatima nzuri, sehemu nzuri ya kwenda, na kuwatendea inavyofaa. Haya yote ni sawa, ila si jinsi ambavyo watu wanadhani, siyo? Sasa, baada ya kusikia yanayowatokea Wakristo, mnajihisi vipi? Je, mnawasikitikia? Mnawahurumia? (Kidogo.) Hakuna linaloweza kufanywa—watajilaumu wenyewe. Kwa nini Ninasema hivi? Kazi ya Mungu ni ya kweli, Mungu yu hai na kweli, na kazi Yake inawalenga wanadamu wote na kila mtu—basi mbona Wakristo wasikubali hili? Ni kwa nini wanampinga kwa nguvu na kumtesa Mungu? Wana bahati hata kuwa na mwisho kama huu, basi mbona mnawaonea huruma? Kwa wao kutendewa namna hii kunaonyesha uvumilivu mkubwa. Kulingana na kiasi ambacho wanampinga Mungu, wanapaswa kuangamizwa—bali Mungu hafanyi hili, anaushughulikia Ukristo sawa tu na dini ya kawaida. Sasa kuna haja ya kutoa maelezo ya kina kuhusu dini nyinginezo? Maadili ya dini zote hizi ni kuwa watu wapitie shida zaidi, wasifanye maovu, waseme mambo mazuri, watende mambo mema, wasiwaapize watu wengine, wasifanye mahitimisho ya ghafla juu ya wengine, wajitenge na ugomvi, wafanye vitu vizuri, kuwa watu wazuri—mafundisho ya kidini mengi ni ya aina hii. Na kwa hiyo, kama hawa watu wa imani—hawa watu wa dini na madhehebu mbalimbali—wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, basi hawatafanya makosa au dhambi nyingi wakati wangali duniani, na baada ya kupata mwili mara tatu hadi saba, basi kwa jumla watu hawa, watu ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, watabaki kushikilia wajibu katika ulimwengu wa kiroho. Na je, kuna watu wengi wa aina hii? (La, hakuna wengi.) Jibu lako linategemea nini? Si rahisi kutenda mazuri, au kufuata amri na sheria. Ubudha haumruhusu mtu kula nyama—unaweza kufanya hilo? Ungepaswa kuvaa kanzu za kijivu na kukariri maandiko ya Kibudha katika hekalu la wafuasi wa Budha siku nzima, ungeweza kufanya hivyo? Haingekuwa rahisi. Ukristo una Amri Kumi za Mungu, amri na sheria, je, ni rahisi kufuata? Si rahisi! Chukua mfano wa kutowaapia wengine: Watu hawawezi kufuata hii amri. Kwa kushindwa kujizuia wenyewe, wanaapa—na baada ya kuapa hawawezi kurudisha kiapo, basi wanafanya nini? Usiku wanakiri dhambi zao. Wakati mwingine baada ya kuwaapia wengine, bado kuna chuki mioyoni mwao, na hata wanazidi zaidi na kupanga ni lini watawadhuru. Kwa jumla, kwa wale wanaoishi katika hii imani iliyokufa, si rahisi kukosa kufanya dhambi au kutenda maovu. Na kwa hiyo, katika kila dini, ni watu wachache tu ndio wanaweza kupata uzima wa milele. Unadhani kwamba kwa sababu watu wengi sana wanafuata hizi dini, wengi wataweza kubaki kuchukua nafasi katika milki ya kiroho. Lakini si wengi hivyo, ni wachache tu ndio wanaweza kulifikia hili. Kwa jumla ni hayo tu kwa mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani. Kinachowapambanua ni kwamba wanaweza kupata uzima wa milele, ambayo ni tofauti yao na wasioamini.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni