Jumatano, 7 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Thelathini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,watu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Thelathini na Moja

Sijawahi kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya watu. Ninapowatafuta watu kweli, wao hufunga na kubana macho yao na kupuuza matendo Yangu, kana kwamba yote Nifanyayo ni jaribio la kuwafurahisha, kutokana na hilo wao daima huchukizwa na matendo Yangu. Ni kana kwamba Nakosa kujitambua kokote: Mimi kila mara hujiringa mbele ya mwanadamu, kusababisha kughadhibishwa ndani ya mwanadamu, ambaye ni "mwadilifu na mwenye haki." Lakini chini ya hali mbaya kama hizo, Mimi huvumilia, na kuendeleza kazi Yangu. Hivyo, Nasema kwamba Nimeonja ladha tamu, chachu, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, kwamba katikati ya upepo na mvua, Nimepitia mateso ya familia, Nimepitia milima na mabonde ya maisha, na Nimepitia uchungu wa kuondoka kwa mwili. Hata hivyo, Nilipokuja duniani, badala ya kunikaribisha Mimi kwa sababu ya taabu Nilizokuwa Nimepitia kwa ajili yao, watu "kwa upole" walikataa makusudi Yangu mazuri. Ningekosaje kuumizwa na hili? Ningekosaje kusikitishwa. Yaweza kuwa kwamba Nilipata mwili ili yote yamalizike hivi? Kwa nini mwanadamu hanipendi Mimi? Kwa nini upendo Wangu umelipwa na chuki ya mwanadamu? Yaweza kuwa kwamba Natakiwa kuteseka kwa njia hii? Watu wametoa machozi ya huruma kwa sababu ya taabu Yangu duniani, na wameshutumu udhalimu wa msiba Wangu. Lakini ni nani amewahi kuujua kweli moyo Wangu? Ni nani anaweza daima kufahamu hisia Zangu? Mwanadamu wakati fulani alikuwa na upendo mkubwa Kwangu, na wakati fulani mara nyingi alinitamani sana katika ndoto zake—lakini ni vipi ambavyo watu wa duniani wangeweza kufahamu mapenzi Yangu mbinguni? Ingawa watu wakati fulani walifahamu hisia Zangu za huzuni, ni nani amewahi kuwa na huruma kwa ajili ya mateso Yangu kama mtesekaji mwenzi? Yaweza kuwa kwamba dhamiri ya watu duniani inaweza kusisimua na kubadilisha moyo Wangu wenye huzuni? Je, watu duniani hawawezi kuniambia Mimi kuhusu taabu isiyosemeka ndani ya mioyo yao? Roho za watu na roho Mtakatifu wakati mmoja zilitegemeana, lakini kwa sababu ya vizuizi vya mwili, akili za watu "zilishindwa kuzuia hasira." Wakati fulani Niliwakumbusha watu waje mbele Yangu—lakini miito Yangu haikuwasababisha watu kutimiza Nilichowaambia; wao walitazama tu angani, macho yakijaa machozi, kana kwamba walibeba taabu isiyosemeka, kana kwamba kulikuwa na kitu kilichowazuia. Hivyo, walishikana mikono yao na kuinama chini ya mbingu kwa maombi ya unyenyekevu Kwangu. Kwa kuwa Mimi ni mwenye huruma, Natoa baraka Zangu miongoni mwa binadamu, na kufumba na kufumbua, wakati wa majilio Yangu binafsi miongoni mwa binadamu hufika—lakini mwanadamu amesahau kitambo kiapo chake kwa Mbingu. Je, huu sio uasi kwelikweli wa mwanadamu? Kwa nini mwanadamu kila mara husumbuliwa na "usahaulifu"? Je, Nimemchoma kisu? Je, Nimeubwaga mwili wake? Namwambia mwanadamu kuhusu hisia zilizo ndani ya moyo Wangu, na kwa nini kila mara yeye huniepa? Katika kumbukumbu za watu, ni kana kwamba wamepoteza kitu fulani na hakiwezi kupatikana popote, lakini pia kana kwamba kumbukumbu zao si sahihi. Hivyo, watu daima husumbuliwa na usahaulifu katika maisha yao, na siku za maisha ya wanadamu wote ziko katika mchafukoge. Lakini hakuna anayesimamia hili, watu hawafanyi chochote ila kukandamizana, na kuuana, ambayo yamesababisha hali ya ushinde mkali leo, na kusababisha wote chini ya ulimwengu kuanguka ndani ya maji machafu na matope, bila nafasi yoyote ya wokovu.
Nilipokuja miongoni mwa watu wote ndio wakati hasa ambapo watu waligeuka kuwa waaminifu Kwangu. Wakati huu, joka kubwa jekundu lilianza pia kuweka mikono yake katili juu ya watu. "Nilikubali "mwaliko," na kuleta "barua ya mwaliko" kutoka kwa mwanadamu Nilipokuja "kuketi katika meza ya karamu" kati ya binadamu. Waliponiona Mimi, watu hawakunitilia maanani, kwani Sikujipamba na mavazi ya utajiri na Nilikuwa Nimeleta tu "kitambulisho" Changu kuketi mezani na mwanadamu. Hakukuwa na vipodozi vya bei ghali usoni Mwangu, hakukuwa na taji juu ya kichwa Changu, na miguuni Pangu Nilivaa tu jozi ya viatu vya kawaida vilivyotengenezwa nyumbani. Kilichowasikitisha watu sana kilikuwa ukosefu wa rangi ya midomo mdomoni Mwangu. Zaidi ya hayo, Sikuzungumza maneno ya heshima, na ulimi Wangu haukuwa kalamu ya mwandishi stadi; badala yake, kila mojawapo ya maneno Yangu lilipenya sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu, ambalo liliwapa watu fikira "yenye kufaa" zaidi ya mdomo Wangu. Kuachilia huko kulitosha kwa watu kunipa Mimi "utendewaji maalum," na hivyo walinitendea Mimi kama mwanakijiji mwenzao kutoka mashambani ambaye hakuwa na ujuzi au hekima. Lakini watu walipotoa "zawadi za pesa," watu bado hawakunichukulia kama mheshimiwa, lakini walikuja tu mbele Yangu bila heshima yoyote, wakitembea polepole wakiwa na hamaki. Mkono Wangu uliponyoshwa, walistaajabishwa mara moja, wakapiga magoti, na wakatoa sauti kubwa. Walichukua "zawadi Zangu zote za fedha". Kwa sababu kiwango kilikuwa kikubwa, walifikiria mara moja kwamba Mimi ni milionea na wakavua upesi mavazi yaliyoraruka kutoka kwa mwili Wangu bila idhini Yangu, wakayabadili na mavazi mapya—lakini hili halikunifurahisha. Kwa sababu Sikuzoea maisha rahisi kama hayo, na Nilidharau utendewaji huu wa "daraja la kwanza," kwa sababu Nilikuwa mzaliwa wa nyumba takatifu, na, inaweza kusemwa, kwa sababu Nilizaliwa katika 'umaskini," Sikuzoea maisha ya anasa ambayo Nilitumikiwa kwa kila hali. Natamani tu kwamba watu waweze kufahamu hisia zilizo moyoni Mwangu, kwamba waweze kustahimili taabu kidogo ili kukubali ukweli usiostarehesha kutoka kwa mdomo Wangu. Kwa sababu Sijawahi kamwe kuzungumza kuhusu nadharia, au kuweza kutumia siri za watu za kujuana ili kushirikiana nao, na kwa sababu Siwezi kurekebisha maneno Yangu kulingana na sura za watu au saikolojia yao, watu kila mara wamenichukia sana, wameamini Sistahili mwingiliano, na wamesema kwamba Nina ulimi wa upanga na kila mara huwaumiza watu. Lakini sina uwezo wa kuchagua: Wakati fulani Nilijifunza saikolojia ya mwanadamu, wakati fulani Niliiga falsafa ya maisha ya mwanadamu, na wakati fulani Nilienda katika "chuo cha lugha" kujifunza lugha ya mwanadamu, ili Niweze kupata ujuzi wa njia ambazo kwazo watu huzungumza, na kunena kama inavyofaa sura zao—lakini ingawa Nilitumia juhudi nyingi, na kuwatembelea "wataalam" wengi, yote yalikuwa bure. Hakujawahi kuwa na chochote cha ubinadamu ndani Yangu. Kwa miaka hii yote, juhudi Zangu hazijawahi kutoa matokeo hata kidogo, Sijawahi kuwa na welekevu hata kidogo katika lugha ya mwanadamu. Hivyo, maneno ya mwanadamu kwamba "kazi ngumu hufidia" "yanaakisiwa" na Mimi, na kutokana na hilo, maneno haya hufikia mwisho duniani. Bila watu kutambua, methali hii haijakubalika na Mungu atokaye mbinguni, kuthibitisha ya kutosha kwamba maneno kama haya ni yasiyothibitika. Hivyo Naomba msamaha kwa mwanadamu, lakini hakuna cha kufanywa—nani alinifanya Mimi kuwa "mjinga" hivi? Sina uwezo wa kujifunza lugha ya mwanadamu, wa kuwa bingwa katika falsafa ya maisha, wa kujuana na watu. Mimi huwashauri tu watu wawe wavumilivu, wafiche hasira iliyo ndani ya mioyo yao, wasijiumize kwa sababu Yangu. Nani alitufanya tuingiliane wenyewe kwa wenyewe? Nani alitufanya tukutane wakati huu? Nani alitufanya tuwe na maadili ya ushirikiano?
Tabia Yangu inajumuisha maneno Yangu yote, lakini watu hawawezi kuifahamu katika maneno Yangu. Wao hubishana tu juu ya tofauti ndogondogo kuhusu kile Nisemacho—na hiyo ina maana gani? Je, dhana zao kunihusu Mimi zinaweza kuwafanya wakamilifu? Je, vitu duniani vingeweza kutimiza mapenzi Yangu? Niliendelea kujaribu kuwafunza watu jinsi ya kuzungumza maneno Yangu, lakini ilikuwa kana kwamba mwanadamu alikuwa bubu, na hangeweza kamwe kujifunza namna ya kuzungumza maneno Yangu jinsi Ningetaka. Nilimfunza kinywa kwa kinywa, lakini hajawahi kamwe kuweza kujifunza. Ni baada ya hili tu ndipo Nilifanya ugunduzi mpya. Watu wa dunia wangewezaje kuzungumza maneno ya mbinguni? Je, hili halikiuki utaratibu wa jambo la asili? Lakini, kwa sababu ya ari na uchunguzi wa watu Kwangu, Nilianzisha sehemu nyingine ya kazi kwa mwanadamu. Sijawahi mwaibisha mwanadamu kwa sababu ya kasoro zake, lakini badala yake humpa mwanadamu kwa mujibu wa kile anachokosa. Ni kwa sababu ya hili tu ndiyo watu wana fikira zenye kufaa kidogo Kwangu, na Natumia nafasi hii kuwakusanya watu pamoja mara nyingine, ili waweze kufurahia sehemu nyingine ya utajiri Wangu. Wakati huu, watu kwa mara nyingine wamezamishwa katika furaha, uchangamfu na kicheko wakifuata upepo kandokando ya mawingu ya rangi nyeupe angani. Naufungua moyo wa mwanadamu, na mwanadamu mara moja ana uchangamfu mpya, na hayuko radhi kujificha kutoka Kwangu tena, kwa kuwa ameonja ladha tamu ya asali, na kwa hiyo analeta takataka yake yote kubadilishwa—kana kwamba Nimegeuka kuwa mahali pa kukusanyia takataka, au kituo cha kusimamia takataka. Hivyo, baada ya kuona "matangazo" yaliyobandikwa, watu huja mbele Yangu na kushiriki kwa hamu, kwa kuwa wao huonekana kufikiria wanaweza kupata "hedaya" chache, hivyo kila mmoja wao huja kuamini ili aweze kushiriki katika matukio Niliyoanzisha. Wakati huu hawaogopi hasara, kwa sababu "mtaji" wa shughuli hizi si mkuu, na hivyo wanathubutu kubahatisha kushiriki. Kama hakungekuwa na hedaya za kupatikana kwa kushiriki, watu wangeondoka uwanjani na kuuliza warudishiwe pesa zao, na wangehesabu pia "riba" wanayonidai. Ni kwa sababu viwango vya leo vya maisha vimeongezeka, kufikia "kiwango cha wastani cha ufanisi" na kutimiza "usasa," na "watu wa kada ya juu" binafsi "wakienda mashambani" kupanga kazi, kwamba imani ya watu mara moja imezidisha mara nyingi—na kwa sababu "katiba" yao inageuka kuwa bora zaidi na zaidi, wao hunitazama Mimi kwa uvutiwaji, na wako radhi kufungamana na Mimi ili wapate imani Yangu.
Aprili 11, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni