Jumamosi, 31 Machi 2018

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Mwenyezi  Mungu anasema: "Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Ijumaa, 30 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Fumbo la Kupata Mwili (4)


Mwenyezi Mungu alisema, Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? 

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake.

Alhamisi, 29 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi Katika Enzi ya Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kumcha mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi Katika Enzi ya Sheria

Mwenyezi Mungu anasema, "Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake.

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza kwa urasimu kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinayotakiwa na Mungu.

Jumatano, 28 Machi 2018

Ni Wale Tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Ni Wale Tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika.

Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote.

Jumanne, 27 Machi 2018

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Mwenyezi Mungu alisema, Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka.

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. 

Jumatatu, 26 Machi 2018

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Mwenyezi Mungu alisema,  Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. 

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni.

Jumapili, 25 Machi 2018

Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Mwenyezi Mungu alisema, Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu.

Jumamosi, 24 Machi 2018

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu alisema, Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi.

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Mwenyezi Mungu alisema, Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu.

Ijumaa, 23 Machi 2018

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kumjua Mungu

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika.

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Mwenyezi Mungu alisema, Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri.

Alhamisi, 22 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka.

Ngurumo Saba Zatoa Sauti— Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Ngurumo Saba Zatoa Sauti— Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mwenyezi Mungu alisema, Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine.

Jumatano, 21 Machi 2018

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu  

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu.Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe. Huzuni iliyoje! Kuokolewa kwa mwanadamu hakuwezi kutenganishwa na usimamizi wa Mungu, aidha hakuwezi kutenganishwa na mipango ya Mungu. Na bado mwanadamu hafikirii chochote kuhusu usimamizi wa Mungu, na hivyo anaendelea kujitenga mbali na Mungu. Kutokana na hayo, idadi ya watu wanaomfuata Mungu inaendelea kuongezeka bila kujua mambo yanayohusiana na kuokolewa kwa mwanadamu kama vile uumbaji ni nini, kuamini kwa Mungu ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kadhalika. Kufikia sasa, basi, lazima tuzungumze kuhusu usimamizi wa Mungu, ndiposa kila mfuasi ajue wazi umuhimu wa kumfuata Mungu na kumwamini. Watakuwa na uwezo wa kuchagua njia watakayoifuata ipasavyo, badala ya kumfuata Mungu tu ili kupata baraka, au kuepukana na majanga, au kuwa na mafanikio.
Japo usimamizi wa Mungu waweza kuonekana mkubwa kwa mwanadamu, si jambo la kutofahamika kwa mwanadamu, kwa kuwa kazi yote ya Mungu imefungamanishwa na usimamizi wake, inahusiana na Kazi ya kuokoa mwanadamu, na inajishughulisha na maisha, kuishi, na hatima ya wanadamu. Kazi ambayo Mungu Anaifanya kati ya na kwa mwanadamu, yaweza kusemwa kuwa, ni ya utendaji na yenye maana kubwa. Inaweza kuonekana na mwanadamu, kuhusishwa na mwanadamu, na iko mbali na dhahania. Kama mwanadamu hana uwezo wa kukubali kazi zote Anazozifanya Mungu, basi ni upi umuhimu wa kazi hii? Na ni vipi usimamizi huu unaweza kusababisha kuokolewa kwa mwanadamu? Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, wacha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia zao, hata hivyo, ni muhimu sana kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.
Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiri yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye na kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haitawaliwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.
Ni viumbe wangapi wanaoishi na kuzaana katika ulimwengu mpana, wakifuata sheria ya maisha tena na tena, wakifuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao?… Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi unaoweza kuonekana kwa macho na ambao akili zaweza kuufahamu kutuliza moyo wake. Na bado ujuzi wa kisayansi kama huu hauwezi kuwazuia wanadamu kutafiti yasiyofahamika. Wanadamu hawajui ni nani Mkuu wa kila kitu katika ulimwengu huu, aidha hajui mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelefu ya miaka.
Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.
Baada ya hapo, Mungu Alimkabidhi mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu aliishi chini ya miliki ya Shetani, na hili taratibu lilisababisha kazi ya Mungu ya enzi ya kwanza: hadithi ya Enzi ya Sheria…. Kipindi cha miaka elfu kadhaa za Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wazoefu wa maelekezo ya Enzi ya Sheria, na wakaanza kupuuza, na taratibu wakaacha ulinzi wa Mungu. Na hivyo, pamoja na kushikilia sheria, walimwabudu Mungu na kutenda matendo maovu. Walikuwa bila ulinzi wa Yehova, na waliishi tu mbele ya madhabahu ndani ya hekalu. Kwa kweli, Kazi ya Mungu ilikuwa imejitenga nao kitambo sana, na hata kama Waisraeli walijikita katika sheria, na kulitaja jina la Yehova, na kwa majivuno kuamini kuwa wao pekee ndio walikuwa watu wa Yehova na walikuwa wamechaguliwa na Yehova, utukufu wa Mungu uliwaacha kimyakimya…
Mungu Anapofanya kazi Yake, huacha sehemu moja na taratibu hutekeleza kazi Yake katika sehemu nyingine mpya. Hii huonekana ya kiajabu sana kwa watu ambao wamepooza. Watu wameishi kukithamini cha zamani na kukirejelea kipya, vitu visivyofahamika kwa uhasama, au hata kuonekana kama bughudha. Aidha, kazi yoyote mpya Aifanyayo Mungu, kutoka mwanzo hadi mwisho, mwanadamu ndiye huwa wa mwisho kufahamu kuihusu miongoni mwa kila kitu.
Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili, kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini, na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. Kwa taabu, palitokea mmoja aliyeitwa Paulo, aliyejitolea kuwa adui wa kuua watu wa Mungu. Hata kama aliangushwa chini na kuwa mtume, hali yake ya zamani haikubadilika, na akaandika barua nyingi. Kwa bahati mbaya, baadaye vizazi vilichukua barua zake kama neno la Mungu la kufurahiwa, kiasi kwamba ziliwekwa ndani ya Agano Jipya na kutatizana na maneno yaliyosemwa na Mungu. Hii kwa kweli ni aibu kubwa tangu majilio ya Maandiko Matakatifu. Je, hili kosa halikutendwa na mwanadamu kutokana na upumbavu wake? Hawakujua kuwa, katika rekodi za kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema, barua na maandiko matakatifu ya mwanadamu hayafai kuwa hapo kuiga kazi na maneno ya Mungu. Lakini hii ni kando na hoja, wacha turejelee mada ya awali. Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.
Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. Katika kazi ya usimamizi wa Mungu wa wakati huu, wanadamu ndio chombo cha maovu ya Shetani, na kwa wakati uo huo ni chombo cha ukombozi wa Mungu, aidha ni sababu ya vita dhidi ya Mungu na Shetani. Wakati sawia na wakati wa kutekeleza kazi Yake, Mungu taratibu Humtoa mwanadamu kutoka mikononi mwa Shetani, na hivyo mwanadamu anakuja karibu zaidi na Mungu…
Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale bado hayajaonekana na yeyote. Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa "kuufurahia." Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua?… Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza "utukufuna "mapenzi" ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa ukweli wa kuwa mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza…ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!
Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu anayemilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.


Yalisimuliwa mnamo Septemba 23, 2005


kutoka kwa Maneno Bora zaidi ya Mungu Kuhusu Injili ya Ufalme (Chaguzi)


Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki  

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

 
Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
 

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote


Mwenyezi Mungu alisema, Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu.

Jumanne, 20 Machi 2018

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya



Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaisha, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? 

Jumatatu, 19 Machi 2018

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, na kwa kiwango cha chini zaidi hawaijui kazi ya Mungu.

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu"

Yongxin, Jiji la Yibin, Mkoa wa Sichuan
Hatukuwahi kumwamini Mungu kabla. Mnamo mwaka wa 2005, tukitiwa moyo na Mungu, mume wangu, baba mkwe wangu, mjomba wangu, na mimi wote tuliikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Baada ya muda mfupi, kanisa lilinipangia kufanya wajibu wa kuhifadhi vitabu.

Jumapili, 18 Machi 2018

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa"

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa"
Wenzhong , Beijing
Agosti 11, mwaka wa 2012
Usiku wa Julai 21, mwaka wa 2012, tulikuwa na mafuriko makubwa hapa, ambayo hutokea kwa nadra. Ningependa kumwambia kila mtu aliye na kiu ya Mungu kile nilichokipitia kwa kweli na kukiona wakati huo.
Siku hiyo mume wangu nami tuliutunza uga wa chakula kikavu cha mifugo wa dada yangu. Wakati wa usiku mvua nzito iliendelea kunyesha, na tulienda kulala mapema sana.

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,watu wa Mungu

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu"
Zhang Min, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mvua ilianza kunyesha sana asubuhi. Kufikia wakati wa adhuhuri wakati nilipaswa kwenda kwa mkutano, niliona mvua ilikuwa nzito sana kiasi kwamba sikutaka kwenda. Lakini ulikuwa mara moja tu kwa wiki, kama singeenda singekuwa na njia yoyote ya kufanya kazi yangu ya kanisa.

Jumamosi, 17 Machi 2018

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa"

Wang Lan, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mafuriko makubwa zaidi tangu miaka sitini yalipitia kijijini mwetu kwa nguvu mno. Maafa yalianguka kutoka mbinguni, maji ya mafuriko yalichanganya matope na mawe na kuharibu kijiji chote. Nyumba nyingi ziliharibiwa na maji na maporomoko ya matope. Baada ya saa kumi na moja alasiri hiyo, mvua ilikuwa ikinyesha kwa nguvu sana.

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli" Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu"

Li Jing, Beijing
7 Agosti, mwaka wa 2012
Siku hiyo, ilianza kunyesha asubuhi. Nilikwenda kwa mkutano nyumbani mwa ndugu mmoja, wakati mvua ilipoendelea kuongezeka zaidi na zaidi kwa uzito. Kufikia alasiri ilikuwa ikinyesha kana kwamba ilitoka mbinguni moja kwa moja. Wakati tulipomaliza mkutano wetu, mvua ilikuwa imeingia katika ua wa ndugu yangu, lakini kwa sababu nilikuwa na wasiwasi juu ya familia yangu, nilijitahidi kwenda nyumbani.

Ijumaa, 16 Machi 2018

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli"Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli"Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo"

Fang Xin, Beijing
Agosti 15, mwaka wa 2012
Tangu mwaka wa 2007, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ingawa nimeonekana juu juu kuwa na kazi nyingi sana kutekeleza majukumu yangu, sijaupa moyo wangu kwa Mungu, na mara nyingi nimehisi kufungwa kiasi cha msongo wa pumzi na masuala madogo ya familia. Kila wakati ninapowaza kuhusu ukweli kwamba binti yangu tayari ana umri wa miaka thelathini, na angali bado hajapata mwenzi wa kufaa, mimi hulalamika kwa Mungu; 

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli“ Moto Ulioshtua Taifa katika Wilaya ya Ji, Mji wa Tianjin”

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli“ Moto Ulioshtua Taifa katika Wilaya ya Ji, Mji wa Tianjin”

Chen Yao, Tianjin
Jengo la Laide lilikuwa mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya ununuzi katika wilaya ya Ji. Juni 30, mwaka wa 2012 ilikuwa ni Jumamosi, na Laide lilikuwa na ukuzaji wa bidhaa, hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya wateja. Wakati fulani baada ya saa tisa alasiri hiyo, jengo likashika moto ghafla. Mkuu wa jengo, akiogopa kuwa wateja katika machafuko haya wangechukua vitu au kutolipa, alifunga na kuweka vizuizi kwa lango kuu kwenye ghorofa ya kwanza, na kuwafukuza wateja hadi ghorofa ya pili na ya tatu. Kitu ambacho hakikutarajiwa ni kwamba moto ulikuwa mkali zaidi na zaidi, hatimaye ukifika kiwango cha kutodhibitika kabisa.

Alhamisi, 15 Machi 2018

Ushuhuda wa Washindi"Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe"

Ushuhuda wa Washindi"Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe"

Dong Mei, Mkoa wa Henan
Mimi ni mtu wa kawaida. Niliishi maisha ya kawaida. Kama wengi wanaotamani sana mwanga, nilijaribu njia nyingi kutafuta maana ya kweli ya uwepo wa wanadamu, nikijaribu kuyapa maisha yangu umuhimu zaidi. Mwishowe, juhudi zangu zote zilikuwa bure. Lakini baada ya kuwa na bahati ya kutosha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, mabadiliko ya muujiza yalitokea katika maisha yangu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako

Mwenyezi Mungu alisema, Katika miaka yote ya kuipitia kazi na kusikiliza mahubiri, kuna watu wengine ambao wanajifahamu, na watu wengine ambao hawana ufahamu wowote kujihusu; watu wengine wanaweza kuzungumza kuhusu vitu fulani halisi, na kuwasiliana hali halisi zao wenyewe, kuingia kwao wenyewe, maendeleo yao wenyewe, dosari zao, na jinsi wanapanga kuingia ndani.

Jumatano, 14 Machi 2018

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo"Kuvunja Pingu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada


Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo"Kuvunja Pingu"

Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena
Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu mipangilio ya kanisa. Ningetii ikiwa ilinifaa, lakini iwapo haingenifaa ningechagua iwapo ningetii au la. Hili lilisababisha kukiuka sana mipangilio ya kazi wakati wa kutimiza wajibu wangu. Nilifanya jambo langu mwenyewe na kuichukiza tabia ya Mungu, na hivyo baada ya hapo nilitumwa nyumbani. Baada ya miaka kadhaa ya kujitafakari, nilikuwa kwa kiwango fulani na maarifa ya asili yangu mwenyewe, lakini kuhusu kipengele cha ukweli ambacho ni kiini cha Mungu bado sikuwa na maarifa mengi. Baadaye, kanisa lilinipa nafasi nyingine, lakini nilipokuwa nikisimamia kazi ya injili, nilianza kuwa na shaka kumhusu Mungu: Mimi ni mpotovu sana na pia nilikuwa nimeichukiza tabia ya Mungu. Ni kwa nini Mungu angenitumia mimi? Je, Ananidanganya? Je, nitaondolewa baada ya kudanganywa? Aa! Kwa kuwa kanisa lilinipa nafasi nitaitunza, hata kama ni lazima niwe mtenda huduma. Kuanzia wakati huo kuendelea, nilitimiza wajibu wangu nikiwa na akili kama hiyo, lakini bila kutafuta lengo la juu—kufanywa mkamilifu na Mungu.
Wakati fulani, nilipokuwa nikitenda ibada ya roho, niliona maneno haya ya Mungu: “Leo hii, huwezi tu kuridhika na jinsi wewe umeshindwa, lakini lazima pia uzingatie njia ambayo utatembelea siku zijazo. Lazima uwe na matarajio na ujasiri wa kufanywa mkamilifu, na hupaswi daima kufikiria kwamba huwezi. Je, ukweli una maonevu? Je, ukweli huwapinga watu kwa makusudi? Kama wewe utaufuata ukweli, je unaweza kukushinda? Kama wewe utasimama imara kwa ajili ya haki, je utakuangusha chini? Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli haukutambui, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha…. Kama huwezi kufuata, basi inaweza kusemwa kwamba wewe ni taka usiye na maana, na huna ujasiri katika maisha Yako, na huna roho ya kupinga nguvu za giza. Wewe ni mdhaifu mno! Huwezi kutoroka nguvu za Shetani ambazo zimekuzingira, na kuwa uko tayari tu kuishi haya maisha ya usalama na kufa katika ujinga. Kile unachopaswa kufanya ni kutekeleza azma Yako ya kuwa mshinde; huu ni wajibu wako uliokushikilia. Kama wewe umeridhika na kushindwa, basi unafukuza kuwepo kwa mwanga” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kula na kunywa kifungu hiki cha neno la Mungu, niliguswa sana ndani. Niliona kwamba nia ya Mungu ni kuwaruhusu watu wote kutafuta kufanywa wakamilifu na wanaofaa kutumiwa na Mungu. Kisha nilifanya uamuzi: Nitaweka mbali wasiwasi wangu mwenyewe na nisiwe tena hasi na baridi. Nitaamini katika maneno ya Mungu na nifanye bidii ili kukamilishwa na Mungu. Lakini pole pole, kwa sababu bado sikujua kiini cha uaminifu wa Mungu, nilianza kuacha kuamini katika maneno ya Mungu tena, kila mara nikiamini kuwa maneno haya yalilengwa kwa mtu mwingine, na kwa mtu kama mimi yangetoa tu faraja na kutia moyo kwa kiasi kidogo. Nilizidi kukumbuka jinsi wakati mmoja nilivyoikosea tabia ya Mungu, kwamba asili yangu ni potovu sana, kwamba wakati mwingine hata nilifichua tabia yangu potovu huku nikitimiza wajibu wangu, kwamba singeweza kukamilishwa haijalishi jinsi nilivyofuatilia, na kufikiri kwamba ninapaswa kuridhika tu na kuwa mtenda huduma. Kwa namna hiyo tu, bila kujua nilianza kuishi katika ubaridi tena. Yule wa juu kisha aliwasiliana mara nyingi juu ya kipengele cha ukweli kuhusu kujua kiini cha Mungu, lakini bado sikuwa nimepata nuru sana. Mpaka siku moja nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno yafuatayo ya Mungu: “Kiini cha Mungu ni uaminifu—Yeye hufanya Anachosema na chochote Afanyacho hutimizwa. Yeye ni mwaminifu …” (“Kipengele cha Pili cha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Wakati huu, ilionekana kana kwamba wazo lilieleweka ndani mwangu kwa ghafla, kana kwamba ukungu uliokuwa umetanda juu ya moyo wangu ulitawanyika mara moja. Miaka mingi ya kutoelewa na wasiwasi kwa ghafla iliisha. Kisha tena nikakumbuka kile kifungu cha neno la Mungu ambalo nilikuwa nikila na kunywa: “Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli haukutambui, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha …” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huu, nilihisi upitishaji wa haki ya ajabu na upendo usio na mipaka kutoka katikati ya mistari ya maneno ya Mungu, yakimfanya Aonekane mwema na mkuu, huku wakati uo huo yakinifanya nione upweke wangu mwenyewe, ufinyu, na uoza. Mungu ni mwaminifu. Hili ni bila shaka na lisiloweza kushukiwa. Mungu ana kiini cha uaminifu, Yeye ni wa kuaminika, na Anajaribu kumwokoa binadamu kwa kiasi kikuu iwezekanavyo. Mradi tu binadamu anafuatilia ukweli na mabadiliko katika tabia kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu atamfanya mwanadamu kamili, kwa sababu kile asemacho Mungu atafanya, Atakifanya na kile Afanyacho kitafanyika! Badala yake, nilishuku kuwa Mungu alikuwa kama binadamu na Angenitupilia mbali mara tu ningekoma kuwa mwenye maana. Sikulichukulia neno la Mungu kama ukweli hata kidogo, na zaidi ya hayo sikuamini katika Mungu kwa kweli na kwa uzuri. Badala yake, niliishi katika fikira na shaka katika mawazo yangu, nikikosa ujasiri mbele ya ukweli na kwa woga kukubali ushawishi wa giza, nisiweze kutetea haki. Ilikuwa ni hapo ndipo nilifahamu kwa kweli kuwa kufuatilia maarifa ya kiini cha Mungu ni muhimu sana. Kama ningekuwa tayari nimekuwa makini kufuatilia ufahamu wa tabia ya Mungu na kiini Chake kabla, nisingeliishi miaka mingi vile katika wasiwasi, nikichelewesha kuendelea kwa maisha yangu mwenyewe.
Asante, Mwenyezi Mungu! Ni Wewe uliyenitunza na kunipa nuru na kuniongoza kujitoa katika pingu ambazo zilikuwa zimenidhibiti kwa miaka mingi sana, kuniruhusu kutoka katika ukungu. Zamani, sikukujua Wewe na mara nyingi niliishi katika kutoelewa, nisiweze kuamini neno Lako na kulichukulia kama tu la kuliwaza na kuwatia watu moyo. Sikulichukulia neno Lako kama ukweli na uzima, na zaidi sikukuchukulia wewe kama Mungu. Lakini hukunitendea kulingana na dhambi zangu. Ulinivumilia, Ulikuwa mwenye subira kwangu, na kunipa fursa ya kutubu. Ulinipa nuru na kuangaza mwanga Wako kwangu, ili kwamba niwe na ufahamu kidogo wa kiini Chako cha haki na uaminifu. Hii hasa ni mfano kamili wa upendo Wako kwa mwanadamu. Ee Mungu! Kuanzia sasa kuendelea nitaweka juhudi kubwa katika ukweli kuhusu kukujua Wewe, kufuata kile unachotarajia kutoka kwangu, nifuatilie ufahamu wa kiini Chako, na kutafuta mabadiliko katika tabia hivi karibuni ili niweze kukamilishwa na Wewe!
Baada ya kujua mambo haya, aina ya nguvu nzuri mno ilivimba ndani ya moyo wangu. Mimi siko baridi tena nikikabiliwa na ugumu, na miaka yangu mingi ya kutoelewa, shaka, na wasiwasi yote imepotea. Sasa ninaishi kabisa katika hali ya kujishughulisha, nikitafuta kukamilishwa na Mungu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.