Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Arubaini na Mbili
Punde tu kazi mpya inapoanza, watu wote wanakuwa na kuingia kupya, na wanasonga mbele nami bega kwa bega, tunatembea pamoja kwenye barabara kubwa ya ufalme, na kuna urafiki mkubwa kati ya mwanadamu na Mimi. Ili kuonyesha hisia Zangu, ili kudhihirisha mtazamo Wangu kwa mwanadamu, Nimemzungumzia mwanadamu kila mara.
Sehemu ya maneno haya, hata hivyo, yanaweza kuwaumiza watu, huku mengine yanaweza kuwa ya msaada mkubwa kwao, na kwa hiyo Nawashauri watu kusikiliza kwa makini sana kile kinachotoka kinywani Mwangu. Matamko Yangu huenda yasiwe sanifu na yenye ustarabu, lakini yote ni maneno kutoka kina cha moyo Wangu. Kwa kuwa mwanadamu alikuwa rafiki Yangu mwanzoni, Nimeendelea kutekeleza kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, na mwanadamu, pia, anafanya kila awezalo kushirikiana nami, akiogopa sana kuikatiza kazi Yangu. Wakati huu, moyo Wangu umejaa furaha kuu, kwani Nimeipata sehemu ya watu, na kwa hiyo "biashara" Yangu haiko tena katika hali ya kuporomoka, si maneno matupu tena, na "soko Langu la haki maalum" halifanyi kwa uvivu tena. Watu wana akili hata hivyo, wote wako radhi "kujitolea" kwa ajili ya jina Langu na utukufu Wangu, na kwa njia hii "idara Yangu ya haki maalum" inapata "bidhaa" zingine mpya, na kwa hiyo katika ulimwengu wa kiroho "wateja" wengi wanakuja kununua "bidhaa" Zangu. Ni wakati huu tu ndipo Napata utukufu, wakati huo tu ndipo maneno yaliyonenwa kutoka kinywani Mwangu si maneno matupu tena. Nimekuwa mshindi, na Nimerudi kwa ushindi, na watu wote wananisherehekea. Ili kuonyesha upendo wake Kwangu, ili kuonyesha kwamba linakubali kushindwa chini ya magoti Yangu, wakati huu joka kubwa jekundu linakuja pia "kusherehekea," nami Natukuzwa kwa hili. Tangu wakati wa uumbaji mpaka leo, Nimepigana vita vingi vya ushindi, nami Nimefanya mambo mengi ya ajabu. Wakati mmoja watu wengi walinisherehekea, na kunisifu, na kunichezea dansi. Ingawa haya yalikuwa maonyesho ya kusisimua, na yasiyosahaulika, Sikuonyesha tabasamu Yangu kamwe, kwani Nilikuwa bado Sijamshinda mwanadamu, na Nilikuwa Nafanya tu sehemu ya kazi inayofanana na uumbaji. Leo si kama na wakati uliopita. Natoa tabasamu katika kiti cha enzi, Nimemshinda mwanadamu, na watu wote wanainama kwa ibada mbele Yangu. Watu wa leo si wale wa wakati uliopita. Ni wakati gani ambapo kazi Yangu haijakuwa kwa ajili ya wakati huu? Ni wakati gani ambapo haijakuwa kwa ajili ya utukufu Wangu? Kwa ajili ya kesho yenye matumaini, Nitaeleza waziwazi kazi Yangu yote ndani ya mwanadamu mara nyingi, ili utukufu Wangu wote "utulie" ndani ya mwanadamu, aliyeumbwa. Nitaichukua hii kuwa kanuni ya kazi Yangu. Wale ambao wako radhi kushirikiana nami, huinuka na kufanya bidii ili utukufu Wangu mwingi uweze kuijaza anga. Huu ndio wakati wa mtu kutumia vizuri sana vipaji vyake. Wale wote ambao wako chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo Wangu wana nafasi ya kutumia uwezo wao hapa, mahali Pangu, na Nitavishawishi vitu vyote "kugeuka" kwa ajili ya kazi Yangu. Ndege wanaopuruka angani ni utukufu Wangu angani, bahari zilizo juu ya dunia ni mambo Yangu juu ya dunia, utawala wa vitu vyote ni onyesho Langu miongoni mwa vitu vyote, nami Natumia kila kilichoko juu ya dunia kama rasilimali ya usimamizi Wangu, na kuvifanya vitu vyote kuzidisha, kusitawi, na kujawa na uhai.
Wakati wa uumbaji, Nilikuwa tayari Nimeamua kwamba kazi Yangu duniani itakamilika katika enzi ya mwisho. Wakati ambapo kazi Yangu itaisha ndio hasa wakati ambapo mambo Yangu yote yatadhihirishwa katika anga. Nitawafanya watu walio duniani wakubali mambo Yangu, na mbele ya "kiti cha hukumu," matendo Yangu yatathibitishwa, ili yakubalike miongoni mwa watu walio kote duniani, ambao watasalimu amri. Hivyo, baadaye, Nitaanzisha shughuli ambayo haijawahi kamwe kutekelezwa katika enzi zilizopita. Tangu leo na kuendelea, Nitatoa waziwazi matendo Yangu hatua kwa hatua, ili hekima Yangu, ajabu Yangu, na kutoeleweka Kwangu vitakubaliwa na kuthibitishwa katika kila eneo la jamii. Hasa, mbele ya washiriki wote wanaotawala duniani kutakuwa hata kukubali zaidi kwa matendo Yangu, kiasi kwamba mambo Yangu yatahukumiwa na "mahakimu," na "kutetewa" na "mawakili," na hivyo mambo Yangu yatakubaliwa, na kusababisha watu wote kuinamisha vichwa vyao na kusalimu amri. Tangu wakati huu na kuendelea, matendo Yangu yatatambuliwa na kila eneo la jamii, na huu utakuwa wakati ambapo Nitapata utukufu wote duniani. Katika wakati huo, Nitamwonekania mwanadamu na Sitajificha tena. Wakati huu, matendo Yangu bado hayajafika kilele. Kazi Yangu inaendelea mbele, na wakati ambapo itafika kilele chake ndio wakati ambapo itamalizika. Nitawashinda kabisa watu wa mataifa yote, Nitasababisha wanyama wakali wageuke kuwa wa kuweza kufugwa kama wanakondoo mbele Yangu, na Nitasababisha joka kubwa jekundu kutii mbele Yangu kama watu walio duniani. Nitawashinda adui zangu wote mbinguni, na Nitasababisha washindani Wangu wote duniani kushindwa. Huu ni mpango Wangu, na ajabu ya matendo Yangu. Mwanadamu anaweza tu kuishi chini ya ushawishi wa asili chini ya uongozi Wangu—hawezi kufanya uamuzi wake mwenyewe! Ni nani anaweza kuuponyoka mkono Wangu? Nimeainisha asili yote, na kuisababisha kuwapo katikati ya sheria, na ni kwa sababu ya hili tu ndipo duniani kuna sheria kama vile uvuguvugu wa majira ya kuchipua na ubaridi wa majira ya kupukutika kwa majani. Madhumuni ya maua yaliyo duniani kunyauka wakati wa majira ya baridi na kuchanua wakati wa majira ya joto ni kwa sababu ya ajabu ya mkono wa Wangu, madhumuni ya bata bukini kupuruka kwenda kusini wakati wa majira ya baridi ni kwa sababu Narekebisha halijoto, na madhumuni ya bahari kunguruma ni kwa sababu Nataka kuvizamisha majini vitu vilivyo juu ya ardhi. Ni kipi kisichopangwa na Mimi? Tangu wakati huu na kuendelea, "uchumi wa asili" wa mwanadamu unashindwa kabisa kwa maneno Yangu, na watu hawakomeshi tena kuwapo Kwangu kwa sababu ya kuweko kwa "sheria asilia." Ni nani atawahi tena kana kuweko kwa Mtawala wa vitu vyote? Mbinguni, Mimi ni Mkuu; miongoni mwa vitu vyote, Mimi ni Bwana; na miongoni mwa watu wote, Mimi ni wa kwanza. Ni nani anayethubutu kulifunika hili kwa "rangi"? Je, uwongo ungeweza kuvuruga kuweko kwa ukweli? Katika nafasi hii ya thamani, Naanza kwa mara nyingine kazi iliyo mikononi Mwangu, Sikubali tena kuingilia kwa mwanadamu, Nikidumisha kuzunguka kwa mitambo.
Nimeongeza "viungo" mbalimbali katikati ya maneno Yangu, na hivyo ni kana kwamba Mimi ni mpishi mkuu wa mwanadamu. Ingawa watu hawajui ni viungo gani vimeongezwa, wanaifurahia ladha; wakiwa wameshika "sahani," wote wanafurahia "vyakula" ambavyo Nimetayarisha. Sijui ni kwa nini, watu kila mara hutaka kula zaidi vyakula ambavyo Mimi Hutayarisha binafsi. Ni kana kwamba wao hunistahi sana, kana kwamba wao huniona Mimi kuwa kiungo cha hali ya juu sana kati ya vyote, na hawajali kabisa kuhusu wengine. Kwa sababu Najiheshimu sana, Sitaki kuvunja "bakuli la chuma la wali" la wengine kwa madhumuni Yangu mwenyewe. Hivyo, Nachukua nafasi ya kuondoka jikoni na Nawapa wengine nafasi ya kujibainisha. Ni kwa namna hii tu ndipo moyo Wangu uko thabiti; Sitaki kuwafanya watu wanitegemee na kuwadharau wengine, hiyo si sawa. Ni nini thamani ya kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya watu? Je, kweli Mimi ni wa kifidhuli na Asiye na mantiki hivyo? Je, kweli Niko radhi kukaa katika nafasi? Kama ni hivyo, basi kwa nini Naanzisha shughuli kubwa kama hiyo? Sitaki kung'ang'ania umaarufu na bahati dhidi ya wengine, Nadharau umaarufu na bahati ya kidunia, hilo silo Ninalofuatilia. Simchukulii mwanadamu kama mfano mwema wa kuigwa, Sipigani wala kupokonya, lakini Napata riziki kwa kutegemea "ustadi" Wangu, nami Sifanyi matendo ya kupita kiasi. Hivyo, wakati ambapo Natembea kila mahali duniani, Natenda kwanza na kudai "malipo ya kazi ya mikono" baadaye—hii pekee ndiyo haki na maana inayozungumziwa na mwanadamu, hakuna kutia chumvi katika hili, halijapunguzwa hata kidogo, Nazungumza kulingana na maana ya asili ya ukweli. Natembea kwenda mbele na nyuma miongoni mwa wanadamu, Nikitafuta wale ambao ni wenye haki na wa maana, lakini hakujakuwa na matokeo. Na kwa kuwa watu wanapenda kupiga bei, ama bei ni ya juu sana au ya chini sana, na kwa hiyo bado Nafanya wajibu ulio mikononi Mwangu. Leo, bado Sijui ni kwa nini mwanadamu hazingatii wajibu wake, kwa nini hajui jinsi kimo chake kilivyo kikubwa. Watu hata hawajui kama ni gramu kadhaa au liang[a] kadhaa. Na hivyo, bado wao wananidanganya. Ni kana kwamba kazi Yangu yote imekuwa bure, kana kwamba maneno Yangu ni mwangwi ndani ya milima mikubwa, na hakuna ambaye amewahi kutambua asili ya maneno na matamko Yangu. Na kwa hiyo Natumia hili kama msingi wa kufanya muhtasari wa methali ya tatu: Watu hawanijui, kwa kuwa hawanioni. Ni kana kwamba, wakiwa wamekula maneno Yangu, watu wanakunywa dawa fulani ili kusaidia mmeng'enyo wa chakula, na kwa sababu athari za dawa hiyo ni kubwa sana, wanapoteza kumbukumbu, na kwa hiyo maneno Yangu yanakuwa kile kinachosahaulika, mahali Nilipo panakuwa pembe wanayoisahau, na kwa ajili ya hili Ninatanafusi. Kwa nini Nimefanya kazi nyingi sana, lakini hakuna thibitisho lake ndani ya watu? Je, kwani Sijatia bidii ya kutosha? Au ni kwa sababu Sijaelewa kile ambacho mwanadamu anahitaji? Nimepungukiwa na mawazo katika hili, chaguo Langu pekee ni kutumia amri Zangu za utawala ili kuwashinda watu wote. Sitakuwa tena mama mwenye upendo, bali Nitawasimamia wanadamu wote kama baba mkali!
Mei 15, 1992
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni