Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha
Ndugu wawili wa kawaida, Beijing
Agosti 15, 2012
Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.
Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja. Muda mfupi baada ya saa 10 jioni, nilitoka nje mtaani ili kuangalia na nikaona kuwa maji yalikuwa kila mahali. Gari la familia yetu lilikuwa tayari limeelea, na sababu ya pekee gari hilo kutosombwa na mkondo wa maji ilikuwa kwamba lilizuiwa na kitu mbele yake kilicholizuia kusonga. Maono hayo yalinifanya kuwa na wasiwasi sana, hivyo kwa haraka nilimpigia mume wangu simu, ambaye pia ni muumini, lakini sikuweza kumpata kwa simu bila kujali ni mara ngapi nilijaribu. Kisha, badala ya kutafuta mapenzi ya Mungu, niliharakisha kurudi nyumbani kumwita mume wangu kwa haraka.
Baadaye, mimi na mume wangu tulikwenda kuangalia gari hilo, miavuli mikononi. Tulipofika kando ya gari, alikuwa tu karibu kuingia ndani ili kuliendesha wakati lilipoanza kusonga lenyewe, kabla hata hajapata wakati wa kuligusa. Aliharakisha kulifuata kwa hatua kadhaa, lakini gari hilo likapelekwa na mkondo wa maji, na alivutwa pamoja nalo. Katika haraka yangu nilitaka kukimbia na kumshika, lakini kabla sijasonga, nilifyonzwa ndani ya mkondo wa maji, pia. Kufumba na kufumbua, tulisukumwa mbele na mbubujiko wa nguvu wa maji ulionguruma kwa zaidi ya mita sitini. Wakati huo huo, teksi kubwa kwa ghafla ikaelea ubavu juu mbele yetu. Mume wangu alitaka kusimama kwa kujitegemeza kwa teksi, lakini kabla hajafanya hivyo, ilibiringia mbele na tukazolewa pamoja kwa mita kadhaa pia. Mahali fulani ambapo mkondo uligeuka, mume wangu hatimaye aliweza kujilazimisha kuinuka wima. Akasema, "Haraka! Ingia katika kibanda kilichoinuka!" Kwa kushikana mkono kwa mkono, sote wawili tulipanda kwa shida na kuingia katika kibanda kilichoinuka. Hapo hapo mafuriko yakatuna sana. Tulishikilia kwa nguzo kikiki, tukiwa na hofu ya kuzolewa tena. Ni hapo tu, katika hali hii ya hatari ya kufa na kupona, ndipo nilipokumbuka kumtegemea Mungu. Katika moyo wangu, niliendelea kumwomba Yeye na kusihi, "Mungu! Kama nikiishi au kufa leo viko mikononi Mwako; hata kifo changu kitakuwa haki Yako!" Niliendelea kumwomba Mungu tena na tena, bila kuthubutu kumwacha Yeye hata kidogo. Ghafla, muujiza ukafanyika: Vijiti vingi vilizuia mkondo wa maji kutiririka kutuelekea, na tukaacha kuhisi maumivu yoyote wakati mafuriko yalipoendelea kuipiga miili yetu. Maji yalivyoendelea kuinuka, sote wawili tukaendelea kuomba na kuimba nyimbo katika kumsifu Mungu. Baadaye, mkondo wa maji ulipozidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, nilikuwa nimeishiwa na nguvu kabisa na ikaanza kuonekana kama singeweza kushikilia mhimili kwa muda mrefu. Kwa haraka, nikapiga ukelele kwa mume wangu, "Siwezi kushikilia kwa muda mrefu. Niko kwa shida kubwa!" Ghafla, mafuriko yakanichukua. Mume wangu kwa haraka alininyakua, na kwa wakati huo, tulikuwa katikati ya maisha na kifo. Wakati huo tu gari lilielea mbele yetu na lilikwama kati ya nguzo. Mbubujiko wa nguvu wa maji ulikurupua pande zote mbili za gari, na tulikuwa salama salimini! Mungu ni wa ajabu sana! Mungu ni mwenyezi sana! Kama Mungu hangeniokoa siku hiyo, ningesombwa na mafuriko, na kufia kusikojulikana. Alikuwa ni Mwenyezi Mungu ambaye Alinipa fursa ya pili katika maisha. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema, "Mungu Hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo
hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa madaraka na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuufahamu au kuuelewa kwa urahisi, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha" ("Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili).
hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa madaraka na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuufahamu au kuuelewa kwa urahisi, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha" ("Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili).
Na hivyo ilikuwa kwamba tulikuwa kwa mvua kwa masaa matano mfululizo. Kwa kweli, kufikia wakati huo waokozi wachache walikuwa tayari wametuona, lakini kwa kuona jinsi mkondo wa maji ulivyokuwa na nguvu, walihofia kusombwa na maji, hivyo badala yake wakaangalia tu kutoka mbali bila kuja kutuokoa. Yamkini, wanapokabiliwa na maafa, kila mtu ni mwenye ubinafsi na wasiojiweza; watu hawawezi kabisa kuokoana wao kwa wao. Ni Mwenyezi Mungu pekee Aliye chanzo chetu cha uzima; zaidi ya hayo, Yeye ndiye pekee Ambaye anaweza kutuokoa mapema. Kumwacha Mwenyezi Mungu ni kufa. Sasa mimi mwenyewe nimeonja upendo wa Mungu, napenda kula kiapo mbele Yake: Kuanzia siku hii kwendelea, nataka kumfuata Mwenyezi Mungu kwa uamuzi; napenda kutumia uzoefu wangu wa kibinafsi kueneza injili, kuwaleta watu zaidi mbele ya Mungu, ili nipate kulipa deni la wema ninalomwia Yeye kwa wokovu Wake!
kutoka kwa Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni