"Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari" (4) - Kwa Nini Binadamu Humwasi Mungu?
Miaka elfu mbili iliyopita, Mungu alipopata mwili kama Bwana Yesu na kuja miongoni mwa wanadamu kuwakomboa binadamu Alikataliwa katika enzi ya giza, hatimaye kusulubiwa msalabani na binadamu waovu wenye upotovu. Bwana Yesu alitabiri kwamba Angekuja tena katika siku za mwisho, Akisema: "Kwa kuwa kama vile umeme, umulikavyo toka upande mmoja chini ya mbingu, na kumulika upande mwingine chini ya mbingu; ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. Lakini kwanza, ni lazima apate mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.” (Luka 17:24-25). Kwa nini Bwana Yesu atakapokuja tena katika siku za mwisho “Atakataliwa na kizazi hiki”? Mungu alipoonekana mara mbili katika mwili kufanya kazi Yake kwa nini alikumbwa na uasi na shutuma kali na binadamu wapotovu? Je, unajua sababu katika hili? Video hii fupi itakufichulia jibu.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni