Umeme wa Mashariki | Utendaji (8)
Kuna mengi kupita kiasi juu ya watu ambayo yamekengeuka na yasiyo sahihi, hawawezi kamwe kujishughulikia wenyewe, na hivyo bado ni muhimu kuwaongoza katika kuingia kwenye njia sahihi; kwa maneno mengine, wana uwezo wa kudhibiti maisha yao ya kibinadamu na maisha ya kiroho, kuweka mambo yote mawili katika vitendo, na hakuna haja ya wao mara nyingi kusaidiwa na kuongozwa. Wakati huo tu ndipo watakuwa na kimo cha kweli.
Hii itamaanisha kuwa, katika siku za baadaye, wakati ambapo hakuna mtu wa kukuongoza, utakuwa na uwezo wa kuwa na uzoefu mwenyewe. Leo, ikiwa umepata kuvumulia kilicho muhimu na kisicho, baadaye, utakuwa na uwezo wa kuingia katika hali halisi. Leo, mnaongozwa kwenye njia sahihi, kukuruhusu kuelewa ukweli mwingi, na baadaye mtakuwa na uwezo wa kwenda kwa kina zaidi. Inaweza kusemwa kuwa kile ambacho watu wanafanywa kuelewa sasa ni njia safi zaidi. Leo, unachukuliwa kwenye njia sahihi—na wakati, siku moja, hakuna mtu wa kukuongoza, utaweka katika vitendo na kuendelea zaidi kwa njia ya njia zilizo safi kuliko zote. Sasa, watu wamefanywa kuelewa yaliyo sahihi, na ambayo ni mkengeuko, na baada ya kuyaelewa mambo haya, baadaye uzoefu wao utaendelea kuwa wa kina zaidi. Leo, vitu ambavyo hamvielewi vinageuzwa, na njia nzuri ya kuingia inafunuliwa kwenu, na ni baada ya hapo ndipo hatua hii ya kaziitakapoisha, na mtaanza kutembea katika njia ambayo ninyi wanadamu mnapaswa kutembelea. Wakati huo, kazi Yangu itamalizika, na kutoka hapo kuendelea hamtakutana Nami tena. Leo, vimo vyenu bado ni vidogo sana. Kuna matatizo mengi ambayo ni mambo ya dutu na asili ya mwanadamu, na hivyo, pia, kuna vitu vilivyokita mizizi ambavyo bado havijachimbuliwa. Huyaelewi maelezo mazuri ya dutu na asili za watu, na bado wanahitaji Mimi kuwaelezea; ikiwa siyo, hamngejua. Wakati ambapo hii imefikia hatua fulani na mambo yaliyo ndani ya mifupa na damu yenu yanafunuliwa, hii ndiyo inayojulikana kama kama kuadibiwa na hukumu. Ni wakati tu ambapo kazi Yangu imetekelezwa kikamilifu na kutekelezwa kabisa ndipo Nitaitamatisha. Kadiri mnavyozidi kufunuliwa wazi kwa undani sana, ndivyo mtakavyozidi kuwa na maarifa zaidi, na hii itakuwa na umuhimu mkubwa kwa ushuhuda wenu na ukamilifu wa baadaye. Ni wakati tu ambapo kazi ya kuadibu na hukumu imefanywa kikamilifu ndipo hii itakuwa ukamilifu wa kazi Yangu, kuwawezesha ninyi nyote kunijua kutoka kwa kuadibu Kwangu na hukumu. Hamtakuja tu kujua tabia Yangu na haki, bali, muhimu zaidi, mtajua kuadibu Kwangu na hukumu. Wengi kati yenu wana dhana kuu juu ya upya na utondoti unaohusika katika Kazi Yangu. Bila kujali, mnapaswa kuona kwamba kazi Yangu ni mpya na ya kina, na kwamba Ninawafundisha kutenda uso kwa uso, mkono kwa mkono. Hii tu ndiyo ya manufaa kwa utendaji wenu na kwa kusimama kwenu imara katika siku zijazo; vinginevyo, mngekuwa kama majani ya majira ya kupukutika kwa majani, yaliyonyauka, yaliyo manjano na makavu, bila hata chembe ya thamani. Mnapaswa kujua kwamba Ninajua kila kitu cha mioyo na roho zenu; na hivyo, pia, kazi Niliyofanya na maneno Ninayosema ya ustadi mkubwa. Kulingana na tabia zenu na ubora wa tabia, mnapaswa kushughulikiwa hivyo. Ni kwa njia hii tu ndiyo marifa yenu juu ya kuadibiwa Nami na hukumu Yangu vitakuwa wazi, na hata kama hamjui leo, kesho mnaweza kujua. Kiumbe yeyote aliyeumbwa atakaanguka katikati ya maneno Yangu ya kuadibu na kuhukumu, kwa maana Sivumilii upinzani wa mtu yeyote.
Lazima nyote muwe na udhibiti wa maisha yenu wenyewe. Kila siku unaweza kuandaa unavyotaka, una uhuru wa kufanya chochote unachopenda, unaweza kusoma, kusikiliza, na kuandika, na ikiwa kunakuvutia, unaweza kuandika nyimbo za kidini. Je, si haya yote yanajumuisha maisha yanayofaa? Hivi vyote ni vitu vinavyopaswa kuwepo ndani ya maisha ya kibinadamu. Watu wanapaswa kufanya kile kinakuchoja kwa kawaida; ni wakati ambapo wamevuna matunda katika ubinadamu wao na maisha ya kiroho tu ndipo wanaweza kufikiriwa kuwa wameingia katika maisha ya kawaida. Leo, hujakosa kuwa na utambuzi na kuondolewa busara inapofikia ubinadamu tu. Kuna maono mengi ambayo yanapaswa kujulikana ambayo watu wanapaswa kujizatiti nayo, na somo lolote unalokutana nalo, hilo ndilo somo unalopaswa kujifunza; lazima uweze kuangalia mazingira, na kuyakubali. Kuboresha kiwango chako cha elimu na ujuzi wa kusoma lazima kufanyike kwa muda mrefu. Ni wakati huo tu ndipo utapata mavuno. Kuhusu kuishi katika ubinadamu wa kawaida, bado kuna vitu ambavyo lazima ujizaititi navyo, na lazima pia ufikie na kuingia kwa maisha yako mwenyewe. Baada ya kufika leo, kuna vitu vingi vilivyozungumzwa hapo awali ambavyo hukuvielewa—lakini baada ya kuvisoma tena leo unavielewa, na kwa moyo wako unakuwa imara zaidi. Huku pia ni kuvuna mavuno. Siku ambayo unakula na kunywa maneno ya Mungu na kuna maarifa kidogo ndani yako, unaweza kushirikiana kwa uhuru na ndugu na dada zako. Je, haya siyo maisha unayopaswa kuwa nayo? Wakati mwingine, wewe huuliza maswali au kutafakari juu ya mada na inakufanya kuwa bora katika kutofautisha, na inakupa umaizi zaidi na hekima, kukuwezesha kuelewa ukweli fulani—na je, hii sio iliyomo ndani ya maisha ya kiroho ambayo inazungumziwa leo? Haikubaliki kuweka tu sehemu moja ya maisha ya kiroho katika vitendo; kula na kunywa maneno ya Mungu, kuomba, na kuimba nyimbo za kidini, yote hufanya maisha ya kiroho, na unapokuwa na uzima wa kiroho, lazima uwe na maisha ya ubinadamu wa kawaida. Leo, mengi ya yale yanayosemwa ni ili kuwapa watu urazini na umaizi, ili kuwawezesha kuwa na maisha ya ubinadamu wa kawaida. Maana ya kuwa na umaizi, maana ya kuwa na mahusiano ya kawaida ya kibinafsi, jinsi unapaswa kuingiliana na watu—unapaswa kujiandaa kwa mambo haya kupitia kula na kunywa maneno ya Mungu, na kile kinachohitajika kwako kinaweza kufikiwa na ubinadamu wa kawaida. Unapaswa kujitayarisha kwa mambo ambayo yanakupasa, lakini usiende mbali sana; watu wengine hutumia maneno na msamiati wa kila aina, na kwa hili wanajionyesha. Pia kuna wengine wanaosoma kila aina ya vitabu, ambavyo vinaruhusu utawala huru wa mwili. Wao hata hujifunza na kuiga wasifu na semi za watu mashuhuri wa dunia, na kusoma vitabu vya ponografia— hii ni ya kuchekesha hata zaidi! Watu kama hawa hawajui tu njia ya kuingia katika maisha, lakini, zaidi ya hayo, pia hawajui kazi ya Mungu leo, na hawajui jinsi ya kutumia kila siku. Maisha yao ni matupu sana! Wao hawajui kabisa yale ambayo wao wenyewe wanapaswa kuingia katika. Yote wafanyayo ni kuzungumza na kuwasiliana na wengine, kana kwamba kuzungumza kunachukua mahali pa kuingia kwao wenyewe. Je, hawajui aibu? Hawa ni watu ambao hawajui jinsi ya kuishi, na ambao hawaelewi maisha ya binadamu; wanatumia siku nzima kushindilia nyuso zao, na kufanya vitu visivyo na maana—na nini maana ya kuishi kwa njia hii? Nimeona kuwa kwa watu wengi, isipokuwa kufanya kazi zao, kula, na kuvaa, siku nzima wakati wao wa thamani unajaa vitu visivyo na maana, iwe ni kufanya mzaha na kuchezacheza, kukutana na marafiki na kula udaku, au kulala unono. Je, maisha kama hayo ni maisha ya watakatifu? Je, haya ni maisha ya watu wa kawaida? Je, unaweza kufanywa mkamilifu wakati ambapo maisha yako ni ya chini, yenye maendeleo kidogo, na ya kutojali? Je, uko tayari kujitwaa kwa Shetani bila gharama? Wakati ambapo maisha ya watu ni rahisi, na hakuna mateso katika mazingira yao, hawawezi kupata uzoefu. Katika mazingira mazuri, ni rahisi kwa watu kukengeushwa—lakini mazingira mabaya hukufanya wewe kuomba kwa haraka zaidi, na kukufanya kutothubutu kumwacha Mungu. Kadiri maisha yao yanavyozidi kuwa rahisi na ya ugoigoi, ndivyo watu wanavyozidi kuhisi kuwa hakuna maana ya kuishi, na kwamba ni bora zaidi wafe. Hivi ndivyo mwili wa watu ulivyopotoka; wanaweza tu kupata faida wakiyapitia majaribio.
Hatua ya kazi ya Yesu ilifanyika katika Yudea na Galilaya, na Mataifa hawakujua kuihusu. Kazi Aliyoifanya ilikuwa ya siri sana, na hakuna mataifa mbali na Israeli walioijua. Ni wakati Yesu alipomaliza kazi Yake tu na kusababisha vurumai ndipo watu walijua, na wakati huo Alikuwa ameondoka. Yesu alikuja kufanya hatua moja ya kazi, alipata kundi la watu, na kukamilisha hatua ya kazi. Katika hatua yoyote ya kazi ambayo Mungu anafanya, kuna wengi ambao huhudumu kama utumbuizo. Ikiwa ingetekelezwa na Mungu Mwenyewe tu, ingekuwa bila maana; lazima kuwe na watu wa kumfuata Mungu na kutekeleza hatua hii ya kazi mpaka mwisho. Ni wakati tu ambapo kazi ya Mungu Mwenyewe imekamilika ndipo watu huanza kutekeleza kazi waliyoagizwa na Mungu, na wakati huo tu ndipo kazi ya Mungu huanza kuenea. Mungu hufanya tu kazi ya kukaribisha enzi mpya, na kazi ya kuiendeleza hufanywa na watu. Hivyo, kazi ya leo haitadumu kwa muda mrefu; Maisha Yangu na mwanadamu hayataendelea kwa muda mrefu sana. Mimi hukamilisha tu kazi Yangu, na kuwafanya kufanya kazi ambayo mnahitajika kufanya, ili kwamba kazi hii na injili hii iweze kuenea haraka iwezekanavyo kati ya Mataifa na mataifa mengine—wakati huo tu ndipo wajibu wenu enyi wanadamu utakamilika. Wakati wa leo ni wa thamani zaidi kuliko wote. Ukiupuuza, wewe ni mmoja wa wale wapumbavu; ikiwa, katika mazingira haya, unakula na kunywa maneno haya na kuipitia kazi hii, na bado huna nia ya kufuatilia, na huna hisia hata kidogo ya mzigo, una matumaini gani ya kuzungumzia? Je, si watu kama hao wataondolewa?
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni