Alhamisi, 7 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 107

Matamshi ya Mungu | Sura ya 107
Wakati maneno Yangu ni makali kwa kiwango fulani, watu wengi huondoka kwa sababu ya maneno Yangu. Ni wakati huu hasa ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanafichuliwa. Nimesema kuwa Sitafanya lolote, lakini Nitatumia tu maneno Yangu kutimiza mambo yote. Ninatumia maneno Yangu kuwaangamiza wote ambao Ninawachukia, na pia Ninatumia maneno Yangu kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. (Maneno Yangu yatakaponenwa, ngurumo saba zitatoa sauti, na wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja na Mimi tutabadili sura na kuingia katika ulimwengu wa kiroho.)  Niliposema Roho Wangu hufanya kazi binafsi, Nilichomaanisha ni kuwa maneno Yangu hutimiza yote, na kupitia kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi. Kwa hiyo, mtu anaweza kuona kwa uwazi mkubwa hata zaidi lengo na kusudi la kila moja ya sentensi Zangu. Nimesema awali, kila kitu Ninachosema ndani ya ubinadamu Wangu ni kipengele cha dhihirisho Langu. Kwa hiyo, wale watu ambao hawawezi kuwa na uhakika na ambao hawaamini kweli kile Ninachosema ndani ya ubinadamu Wangu wa kawaida lazima waondolewe! Nimesisitiza tena na tena kwamba ubinadamu Wangu wa kawaida ni kipengele muhimu cha uungu Wangu kamili, ilhali watu wengi sana bado wanalenga uungu Wangu kamili huku wakipuuza ubinadamu Wangu. Wewe ni kipofu! Unasema kwamba Silingani na dhana zako, kwamba mwanadamu Niliye halingani na wazo lako kuhusu Mungu[a]. Je, watu hawa wanaweza kusalia katika ufalme Wangu? Nitakukanyaga chini ya miguu Yangu! Hebu thubutu tu kuniasi! Hebu thubutu tu kuwa mkaidi sana! Tabasamu Yangu hairidhishi dhana unazoshikilia, usemi Wangu haukufurahishi, na matendo Yangu si yenye manufaa kwako, sivyo? Mambo haya yote yanapaswa kuwa kama uyapendavyo—je, hivyo ndivyo Mungu alivyo? Na watu hawa wanataka kusalia nyumbani Kwangu, na kupokea baraka katika ufalme Wangu? Je, si unaona njozi? Kungewezaje kuwa na jambo la ajabu kama hilo! Unataka kuniasi, ilhali bado upokee baraka kutoka Kwangu. Nakwambia: Haiwezekani! Wale ambao huingia katika ufalme Wangu na kupokea baraka lazima wawe watu ambao Ninawapenda, kama Nilivyosema mara nyingi. Kwa nini Ninasisitiza maneno haya? Najua na kuelewa kile ambacho kila mtu anafikiri moyoni mwake, Sihitaji kuonyesha mawazo yao yote. Sura zao za kweli zitafichuliwa kupitia kwa maneno Yangu ya hukumu na wote watalia kwa huzuni mbele ya kiti Changu cha hukumu. Huu ni ukweli dhahiri ambao hakuna anayeweza kubadilisha! Mwishowe, Nitawaamuru kuingia katika shimo lisilo na mwisho mmoja baada ya mwingine. Hii ni athari ya mwisho ya hukumu Yangu ya ibilisi Shetani. Lazima Nitumie hukumu na amri za utawala kumtendea kila mtu, na hii ndiyo mbinu Yangu ya kuadibu. Je! mna utambuzi wa kweli kuhusu jambo hili? Sihitaji kumpa Shetani sababu, Mimi hutumia tu fimbo Yangu ya chuma kumpiga mpaka afikie kiwango cha kukaribia kufa na kuomba msamaha. Kwa hiyo watu wanapasoma maneno Yangu ya hukumu, hawawezi kuyaelewa hata kidogo, lakini kutoka kwa mtazamo Wangu, kila neno, kila sentensi ni utekelezaji wa amri Zangu za utawala. Huu ni ukweli dhahiri.
Tangu leo ​​Ninatoa hukumu, hii inahusisha kiti cha hukumu. Awali mmesema mara nyingi kuwa mtapokea hukumu mbele ya kiti cha Kristo. Mna ufahamu kuhusu hukumu, lakini hamwezi kuwazia kiti cha hukumu. Labda watu wengine wanafikiri kwamba kiti cha hukumu ni kitu cha kimwili, wanaweza kukifikiria kuwa meza kubwa, au labda kukifikiria kuwa kiti cha hukumu kama katika dunia ya kilimwengu. Bila shaka, katika ufafanuzi Wangu wakati huu, Sitakataa yale ambayo mmesema, lakini Kwangu, mambo yaliyomo katika mawazo ya watu bado yana maana yenye ishara. Hivyo ghuba kati ya mawazo ya watu na maana Yangu ya asili bado ni pana kama umbali kati ya mbinguni na dunia. Katika dhana za watu, kunao watu wengi waliolala chini mbele ya kiti cha hukumu, wakilia kwa huzuni na kuomba msamaha. Huu tayari ni upeo wa mawazo ya binadamu na hakuna mtu anayeweza kufikiria chochote zaidi ya hayo. Kiti cha hukumu ni nini basi? Kabla Nifichue siri, lazima mkanushe yote ambayo mmefikiri awali na ni wakati huo tu ndipo lengo Langu linaweza kufikiwa. Hii ndiyo njia ya pekee ambayo dhana na mawazo yenu katika eneo hili yanaweza kuondolewa. Lazima msikilize kwa makini nyakati zote Ninaponena. Sharti msiwe wazembe. Kiti Changu cha hukumu kimekuwa thabiti tangu uumbaji wa ulimwengu. Katika enzi na vizazi vilivyopita, watu wengi wamekufa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na watu wengi wamefufuka mbele ya kiti hicho, wakiurudia uzima. Pia inaweza kusemwa kuwa tangu mwanzo hadi mwisho hukumu Yangu haikomi kamwe, na hivyo kiti Changu cha hukumu kipo daima. Kiti cha hukumu kinapotajwa, wanadamu wote wanakuwa na dalili ya hofu ndani yao. Bila shaka, kutokana na kile Nilichosema awali, hamjui kabisa kiti cha hukumu ni nini. Kiti cha hukumu na hukumu vinaishi pamoja kwa amani, lakini ni vifaa viwili tofauti. (Kifaa si kitu cha kimwili, lakini kinahusu maneno. Watu hawawezi kukiona kabisa.) Hukumu inahusu maneno Yangu. (Bila kujali kama ni makali au ya upole, yote yanajumuishwa katika hukumu Yangu. Hivyo, chochote Ninenacho kutoka kinywani Mwangu ni hukumu.) Awali, watu waliyagawanya maneno Yangu katika aina nyingi, ikiwa ni pamoja na maneno ya hukumu, maneno mapole, na maneno ambayo hutoa uhai. Leo, Nitawafafanulia kuwa hukumu na maneno Yangu yameunganishwa moja kwa nyingine. Kwa maneno mengine, hukumu ni maneno Yangu, na maneno Yangu ni hukumu. Hampaswi kuvizungumzia vikiwa vimetengana. Katika mawazo ya watu, wanafikiri kwamba maneno makali ni hukumu, lakini watu wana ufahamu kiasi tu. Kila kitu Ninachosema ni hukumu. Mwanzo wa hukumu uliosemwa zamani unahusu Roho Wangu akianza kufanya kazi rasmi kila mahali na kutekeleza amri Zangu za utawala. Katika sentensi hii, "hukumu" inahusu ukweli halisi. Sasa Nitaeleza kiti cha hukumu: Kwa nini Ninasema kuwa kiti cha hukumu kipo milele hata milele na huenda na hukumu Yangu? Je! mnalielewa kutoka kwa ufafanuzi Wangu wa hukumu? Kiti cha hukumu kinanihusu Mimi mwenyewe. Milele hata milele, daima Mimi hueleza na kunena. Naishi milele, hivyo kiti Changu cha hukumu na hukumu Yangu vitaishi pamoja kwa amani milele. Lazima jambo hili liwe dhahiri sasa! Watu hunichukulia kama kitu katika mawazo yao, lakini kuhusu suala hili Siwalaumu na mimi Siwahukumu. Natamani tu kuwa mtakuwa na mioyo mitiifu na kukubali ufunuo Wangu, na kujua kutoka kwa ufunuo huo kwamba Mimi ndimi Mungu wa mambo yote Mwenyewe.
Maneno Yangu hayaeleweki na watu kabisa, haiwezekani kwao kupata nyayo Zangu, na haiwezekani kwao kuelewa mapenzi Yangu. Kwa hiyo, hali mliomo leo (kuweza kupokea ufunuo Wangu, kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani yake, na kufuata nyayo Zangu kupitia kwa ufunuo huo) ni matokeo ya vitendo Vyangu vya ajabu kabisa, neema Yangu na rehema Zangu. Siku moja, hata Nitawaruhusu muione hekima Yangu, muone yale Niliyoyatenda kwa mikono Yangu, na kuona ajabu ya kazi Yangu. Basi, mipangilio ya mpango Wangu wote wa usimamizi itafichuliwa kabisa machoni penu. Kotekote katika ulimwenguni wa dunia na kila siku, kuna dhihirisho la vitendo Vyangu vya ajabu, na wote wanatoa huduma ili mpango Wangu wa usimamizi uweze kutimizwa. Hii itakapofichuliwa kabisa, mtaona ni aina gani ya watu Niliowapanga kutoa huduma, ni aina gani ya watu Nimewapanga kutimiza mapenzi Yangu, kile ambacho Nimetimiza kwa kumnyonya Shetani, kile ambacho Nimetimiza Mimi mwenyewe, ni aina gani ya watu wanaolia, ni aina gani ya watu wanaosaga meno yao, ni aina gani ya watu watakaoangamia, na ni aina gani ya watu watakaoteseka milele. Kwa kutaja maangamizi, Ninanena kuhusu wale ambao Nitatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, watakaochomwa kabisa, na kwa kutaja kuteseka milele Ninanena kuhusu wale ambao Nitatupwa katika shimo lisilo na mwisho kwa ajili ya kudhoofika milele. Kwa hiyo msifikirie visivyo kuwa maangamizi na kuteseka milele ni kitu kimoja. Badala yake, mambo haya mawili ni tofauti kabisa. Watendaji huduma wanaoliacha jina Langu leo ​​watateseka milele, na wale ambao si wa jina Langu wataenda kwa uangamizi. Hii ndiyo maana Ninasema wale wanaoteseka milele watanipa sifa za milele baada ya hukumu Yangu, lakini watu hao hawataepuka kuadibu Kwangu kamwe, watakubali utawala Wangu daima. Ndiyo maana Ninasema kwamba shimo lisilo na ni mkono ambao Ninatumia kuwaadibu watu. Pia Ninasema kwamba yote yako mikononi Mwangu. Ingawa shimo lisilo na mwisho linahusu ushawishi wa Shetani, pia liko katika mikono Yangu ambayo Natumia kuwaadibu watu. Kwa hiyo, Ninaposema kuwa yote yako mikononi Mwangu, hakuna kweli kinzani. Maneno Yangu si ya kutoaminika. Hayo ni sahihi na yenye kueleweka. Si yaliyobuniwa au ya upuuzi, na kila mtu anapaswa kuamini maneno Yangu. Hapo baadaye, mtateseka kwa sababu ya hili. Kwa sababu ya maneno Yangu, watu wengi hukosa mhemuko, au hukata tamaa, au kusikitika, au hulia, au hutoa machozi. Kutakuwa na aina zote za kiitikio. Siku moja, wakati watu wote Ninaowachukia wataondoka, kazi Yangu itatimizwa. Hapo baadaye, watu wengi wataanguka kwa sababu ya wazaliwa wa kwanza, na mwishowe wataondoka hatua kwa hatua. Kwa maneno mengine, nyumba Yangu itakuwa takatifu hatua kwa hatua, na kila aina ya pepo wabaya watakimbia polepole kutoka upande Wangu, kimya, kwa unyenyekevu, na bila malalamiko yoyote. Baada ya hapo, wazaliwa Wangu wa kwanza watafichuliwa, nami Nitaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu. Ni wakati huo tu ndipo wazaliwa wa kwanza watakuwa wafalme pamoja nami na kuutawala ulimwengu mzima. Hizi ndizo hatua za kazi Yangu, na zinafanyiza sehemu muhimu ya mpango Wangu wa usimamizi. Usikose kutilia maanani jambo hili, vinginevyo utakuwa umekosea.
Wakati ambapo maneno Yangu yatafichuliwa kwenu ni wakati ambapo Nitaanza kazi Yangu. Hakuna hata neno moja kati ya maneno Yangu ambayo halitatimizwa. Kwangu, siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Je, mnalifikiriaje? Dhana yenu ya muda ni tofauti sana na Yangu, kwa sababu mimi huudhibiti ulimwengu wa dunia, na Mimi hutimiza mambo yote. Kazi Yangu inafanyika kila siku, hatua kwa hatua, na kipindi kwa kipindi, na zaidi ya hayo kasi ya kazi Yangu haikomi hata kidogo, inaendelea kila wakati. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, maneno Yangu hayajakatizwa. Nimeendelea kunena na kueleza, hata leo, na haitabadilika katika siku za baadaye. Hata hivyo, muda Wangu unapangwa na kuratibiwa kwa uangalifu, na makini kabisa. Nitafanya Ninachohitaji kufanya wakati Ninahitaji kukifanya (na Mimi, wote wataachiliwa huru, wote watakuwa huru), na hakuna kitu kinachovuruga hatua za kazi Yangu. Ninaweza kumpanga kila mtu nyumbani Kwangu, Ninaweza kumpanga kila mtu duniani, lakini Sina shughuli nyingi hata kidogo, kwa sababu Roho Wangu anafanya kazi, Roho Wangu hujaza kila mahali, kwa sababu Mimi ni Mungu wa pekee Mwenyewe na ulimwengu wa dunia wote uko mikononi Mwangu. Hivyo, mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi, Mimi ni mwenye hekima na utukufu Wangu hujaza kila pembe ya ulimwengu.
Tanbihi:
a. Nakala ya kwanza inaacha "wazo la."
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni