Jumapili, 12 Agosti 2018

Kupitia Upendo Maalum wa Mungu

Umeme wa Mashariki, mapenzi ya Mungu, Ukweli

Kupitia Upendo Maalum wa Mungu

Jiayi     Mji wa Fuyang, Mkoa wa Anhuif
Asili yangu ni ya kiburi hasa; bila kujali ninafanya nini, mimi daima hutumia werevu na ujuzi wa kubuni ili kuonyesha akili yangu na kwa hiyo mara kwa mara hukiuka mipango ya kazi ili nifanye mambo kwa njia yangu mwenyewe. Mimi ni mwenye kiburi hasa kuhusu kuchagua watu kwa cheo fulani. Ninaamini kuwa nina talanta ya kipekee na umaizi ambavyo hunisaidia daima kumchagua mtu sahihi. Kwa sababu ya hili, nilipomchagua mtu, singechunguza kwa dhati ili kuelewa hali zote za mtu niliyetaka kumchagua. Pia singewapima kwa makini watu ambao ninataka kuchagua kulingana na maadili yanayohusiana. 

Jumamosi, 11 Agosti 2018

Niliona Kimo Changu cha Kweli kwa Dhahiri

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Roho Mtakatifu, neno la Mungu

Niliona Kimo Changu cha Kweli kwa Dhahiri

Ding Xiang    Jijini Tengzhou, Mkoa wa Shandong
Katika mkutano wa viongozi wa kanisa niliowahi kuhudhuria, kiongozi wa kanisa aliyekuwa amechaguliwa hivi karibuni alisema: “Sina kimo cha kutosha. Mimi ninahisi sifai kuutimiza wajibu huu. Mimi ninahisi kushinikizwa na vitu vingi sana, kwa kiwango kwamba mimi sijaweza kupata usingizi kwa siku na usiku kadhaa mtawalia....” Wakati huo, mimi nilikuwa nimebeba mizigo katika kumfuatilia Mungu, kwa hivyo niliwasiliana naye: “Kazi zote hufanywa na Mungu; mwanadamu hushirikiana kidogo tu. Ikiwa tunahisi kulemewa, kuja mbele za Mungu mara nyingi na kumtegemea Mungu bila shaka kutatufanya tuone uweza wote na hekima ya Mungu. Kuhisi mzigo kutokana na kazi zetu ni kitu kizuri.

Ijumaa, 10 Agosti 2018

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?


Umeme wa Mashariki, mapenzi ya Mungu, hukumu,

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Qingxin    Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu. Hiyo ni haki ya Mungu. Kutokana na ufahamu huu usio sahihi, pamoja na hofu ya kupoteza kazi yangu kutokana na kufanya makosa katika kazi yangu, nilifikiria juu ya utaratibu "mjanja": Wakati wowote ninapofanya kitu vibaya, mimi hujaribu niwezavyo kutowaacha viongozi wajue kwanza, na kwa haraka kujaribu kukifidia mwenyewe na kufanya kila linalowezekana ili kukisawazisha. Je, si hilo basi litanisaidia kuhifadhi kazi yangu?

Nilifurahia karamu kubwa

Umeme wa Mashariki, neno la Mungu, Ukweli
文字

Nilifurahia karamu kubwa

Xinwei    Mkoa wa Zhejiang
Juni 25 na 26 zilikuwa siku zisizohaulika. Eneo letu la Zhejiang lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa eneo wakiwa wamekamatwa na joka kubwa jekundu. Ni wachache wetu tu tuliokimbia bila kuumia na, mioyo yetu ikiwa imejaa shukrani, tulikula kiapo cha siri kwa Mungu: kushirikiana vizuri na kazi iliyokuwa ifuate. Kufuatia hilo tulianza kazi yenye msisimko na shughuli nyingi ya kushughulika na matokeo. Na baada ya karibu mwezi mmoja, mipango ilikuwa inakaribia kukamilika. Mwezi huo ulikuwa wa joto, na wakati tulikuwa tumeteseka kimwili mioyo yetu ilikuwa imeridhika yenye furaha, kazi yetu ikiwa imeendelea vizuri mbele ya joka kubwa jekundu. Wakati kazi ilipokuwa imekamilika mimi bila kujua nilijikuta katika hali ya kujiridhisha, nifikiria jinsi nilivyokuwa mwerevu kupanga hiyo kazi vizuri sana. Jinsi nilivyokuwa mfanyakazi mwenye uwezo! Na ilikuwa ni wakati huu ambapo Mungu alipatiliza hukumu Yake kwangu na kuniadibu …

Jumatano, 8 Agosti 2018

Watu Wasio na Hila Sio Lazima Wawe Waaminifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu

Watu Wasio na Hila Sio Lazima Wawe Waaminifu

Cheng Mingjie    Jiji la Xi'an, Mkoa wa Shaanxi
  Mimi hujiona kuwa mtu wa aina ya kuwa wazi na mchangamfu. Mimi huzungumza na watu kwa njia ya waziwazi; chochote ninachotaka kusema, mimi husema—mimi sio aina ya mtu wa kuzungukazunguka. Katika kuingiliana kwangu na watu mimi huwa ni mwaminifu na wazi kiasi. Mara kwa mara, mimi hudanganywa na kudhihakiwa kwa sababu ya kuwaamini wengine kwa urahisi. Ilikuwa tu baada ya kuanza kwenda kanisani nilipopata mahali ambapo ningepaita pangu. 

Jumanne, 7 Agosti 2018

Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu!


 Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,    

 Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu!


Xiaowei    Mji wa Shanghai
Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kumliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha.

Jumatatu, 6 Agosti 2018

Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wokovu

         Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

       Tong Xin    Mkoa wa Fujian
Nilizaliwa vijijini. Nilitoka kwa nasaba ya wakulima wanyenyekevu na zaidi ya hayo familia yetu ilikuwa na watu wachache, kwa hiyo mara nyingi tulikuwa tunadhulumiwa. Nilipokuwa na umri wa miaka 13, kulikuwa na mtoto aliyepigwa na mtu fulani kutoka nje ya kijiji chetu. Wanakijiji walimlaumu kwa uongo baba yangu kwa kuchochea hilo na wakasema walitaka kupekua nyumba yetu na kuchukua ngawira mali yetu, kuchukua nguruwe wetu na hata kumpiga baba yangu. Kulikuwa na wakati pia ambapo mwanakijiji mwingine alichukua wavu wetu wa uvuvi na kuuweka kama wake mwenyewe.

Jumapili, 5 Agosti 2018

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Tisa

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Tisa

Inaonekana kwamba katika mawazo ya watu, Mungu ni wa fahari sana naye Haeleweki. Ni kana kwamba Mungu haishi miongoni mwa wanadamu, kana kwamba anawadharau watu kwa sababu Yeye ni wa fahari sana. Mungu, hata hivyo, Huziseta fikira za wanadamu na kuzifuta zote, Akizika fikira zao zote ndani ya "makaburi" ambamo zinageuka kuwa majivu. Mtazamo wa Mungu kwa fikira za wanadamu ni sawa na mtazamo Wake kwa wafu, Akiwafafanua apendavyo. Ni kana kwamba hakuna athari kutokana na fikira. Kwa hiyo tangu uumbaji wa ulimwnegu mpaka sasa, Mungu amekuwa Akifanya kazi hii na Hajaacha kamwe. Kwa sababu ya mwili, wanadamu hupotoshwa na Shetani, na kwa sababu ya matendo ya Shetani duniani, wanadamu huunda kila aina ya fikira wakati wa uzoefu wao.

Jumamosi, 4 Agosti 2018

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba

Kwa kweli, maneno yote kutoka katika kinywa cha Mungu ni mambo ambayo wanadamu hawayajui; yote ni lugha ambayo watu hawajasikia, kwa hiyo inaweza kusemwa hivi: Maneno ya Mungu yenyewe ni siri. Watu wengi kwa kutojua wanaamini kwamba ni mambo tu ambayo watu hawawezi kutimiza kimawazo, mambo ya mbinguni ambayo Mungu anawawezesha watu kuyajua sasa, au ukweli kuhusu kile Mungu anachofanya katika ulimwengu wa kiroho ni siri.

Ijumaa, 3 Agosti 2018

Tamko la Arubaini na Sita

Sijui jinsi watu wanavyoendelea katika kuyafanya maneno Yangu kuwa msingi wa kuweko kwao. Nimehisi wasiwasi kila mara kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu, lakini watu hawaonekani kuwa na fahamu yoyote kuhusu hili—na kutokana na hilo, hawajawahi kuyatilia maanani mambo Yangu, na hawajawahi kukuza kuabudu kokote kwa ajili ya mtazamo Wangu kuhusiana na mwanadamu. Ni kana kwamba walitupa hisia zamani ili kuuridhisha moyo Wangu. Nikikumbwa na hali kama hizo, Nakimya mara nyingine.

Jumapili, 29 Julai 2018

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri.

Jumapili, 15 Julai 2018

Tamko la Pili

Kufuata kuanza kazi kwa mtazamo mpya, kutakuwa na hatua mpya katika kazi Yangu. Kama ilivyo katika ufalme, Nitafanya mambo moja kwa moja kupitia kwa uungu, Nikiongoza kila hatua ya njia, sahihi hadi kwa maelezo madogo, na bila kutiwa najisi na nia za binadamu hata kidogo. Yafuatayo yanaeleza kwa muhtasari namna ya utekelezaji halisi: Kwa vile ni kupitia katika ugumu na usafishaji ndiyo wamepata jina la “watu”, na kama walivyo watu wa ufalme Wangu, lazima Niwafanye watii kwa mahitaji kali, ambayo ni ya juu kushinda mbinu za kazi Yangu kwa vizazi vilivyopita.