Jumanne, 12 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 27


Mwenyezi Mungu anasema, "Leo, maneno ya Mungu yamefikia kilele chake, ambako ni kusema, sehemu ya pili ya enzi ya hukumu imefikia kilele chake. Lakini sio kilele cha juu kabisa. Wakati huu, sauti ya Mungu imebadilika, si ya kudhihaki wala ya ucheshi, na haigongi au kulaani; Mungu ametuliza sauti ya maneno Yake. Sasa, Mungu anaanza "kubadilishana maoni" na mwanadamu. Mungu anaendeleza kazi ya enzi ya hukumu na pia kufungua njia ya sehemu inayofuata ya kazi, ili sehemu zote za kazi Yake zipatane. 

Jumatatu, 11 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 26



Mwenyezi Mungu anasema, "Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani. 

Jumapili, 10 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 16


Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa watu, Mungu ni mkuu mno, mwenye utele mno, wa ajabu mno, Asiyeeleweka mno; machoni pao, maneno ya Mungu hupaa juu, na huonekana kama kazi bora sana ya ulimwengu. Lakini kwa vile watu wana kasoro nyingi sana, na akili zao ni za kawaida sana, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa uwezo wao wa kukubali ni haba mno, bila kujali vile Mungu hunena maneno Yake kwa dhahiri, wanabaki palepale bila kutikisika, kana kwamba wana ugonjwa wa akili. 

Jumamosi, 9 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 41

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 41


Wakati mmoja Nilianza shughuli kubwa miongoni mwa wanadamu, lakini hawakutambua, kwa hivyo ilinibidi Nitumie neno Langu ili kuwafichulia. Na hata hivyo, mwanadamu bado hangeweza kuyaelewa maneno Yangu, na akasalia kutojua malengo ya mpango Wangu. Na hivyo kwa sababu ya kasoro na dosari za mwanadamu, alifanya mambo ili kukatiza mpango Wangu wa usimamizi, na pepo wachafu wakachukua nafasi ya kujidhihirisha, wakawafanya wanadamu kafara wao, mpaka wakateswa na pepo hao wachafu na wakachafuliwa kila mahali. 

Ijumaa, 8 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 28

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 28


Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao. Vitu vyote vinafuata uongozi Wangu, na vyote vinaangalia upande ulioashiriwa na mkono Wangu. 

Alhamisi, 7 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 27

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 27


Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu.

Jumatano, 6 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 26


Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni. 

Jumanne, 5 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 24

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 24

Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu, na hakuna mtu ambaye amewahi kunijua na kwa hivyo mtazamo wa mwanadamu Kwangu ni wa sitasita, na hauna uwezo wa kuwa kawaida. Lakini Nimekuwa Nikimlea na kumchunga mwanadamu na ni kwa sababu ya upumbavu wake ndiyo maana hana uwezo wa kuona matendo Yangu yote na kuelewa nia Zangu.

Jumatatu, 4 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 23

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, "Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapofyatua moto, Ninaitazama kwa uangalifu dunia nzima, Ninatazama kwa uangalifu ulimwengu mzima. Wanadamu wote wananiomba Mimi, wameinua macho yao kuelekea Kwangu, wakiomba Nipunguze hasira, na kuapa kutoniasi tena. Lakini haya siyo yaliyopita; bali yaliyopo kwa sasa. Ni nani anayeweza kubadilisha mapenzi Yangu? Kwa kweli sio sala katika moyo wa mwanadamu, wala maneno yanayotoka midomoni mwao? 

Jumapili, 3 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 22

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 22


Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Nilichunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani.  

Jumamosi, 2 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 21

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. 

Ijumaa, 1 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 20

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 20


Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja.