Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 27 Novemba 2019

Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana” (Yohana 5:22).
Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu” (Yohana 5:27).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

Jumatano, 6 Novemba 2019

Wimbo Mpya wa Kuabudu 2019 | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” (Swahili Gospel Song)



Wimbo Mpya wa Kuabudu 2019 | “Kristo wa Siku za Mwisho Ameleta Enzi ya Ufalme” (Swahili Gospel Song)



Yesu alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu,
Akatamatisha Enzi ya Sheria,
Alileta Enzi ya Neema.
Mungu mara nyingine akakuwa mwili katika siku za mwisho.
Akitamatisha Enzi ya Neema,
Alileta Enzi ya Ufalme.
Wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili
wataongozwa katika Enzi ya Ufalme na kupokea uongozi Wake.
Baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake,
Mungu alirudi mwilini kumwongoza.
Atamwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya.
Ameanza kazi ya hukumu
ili kumleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi.
Wote wanaotii utawala Wake
watavuna ukweli wa juu na baraka kuu.
Ee wataishi katika mwangaza!
Na kupata njia, ukweli, na uzima!

Jumamosi, 13 Aprili 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 59

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

        Mwenyezi Mungu anasema, “Tafuta mapenzi Yangu zaidi katika mazingira unayoyakabili na kwa hakika utapata kibali Changu. Ilmradi uwe tayari kwenda katika utafutaji na kuhifadhi moyo ambao unanicha, Mimi Nitakupea yote unayokosa. Kanisa sasa linaingia utendaji rasmi na mambo yote yanaingia kwenye alama sahihi. Mambo hayako yalivyokuwa wakati mlipokuwa na limbuko la mambo yajayo. 

Jumatatu, 18 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 120


Mwenyezi Mungu anasema, “Sayuni! Salamu! Sayuni! Ita kwa sauti! Nimerudi kwa ushindi, Nimerudi nikiwa mshindi! Watu wote! Harakisheni mpange foleni kwa utaratibu! Vitu vyote! Mtakuja kusimama kabisa, kwa sababu nafsi Yangu inaukabili ulimwengu mzima na nafsi Yangu inaonekana katika Mashariki ya dunia! Nani anayethubutu kutopiga magoti katika ibada? Nani anayethubutu kutosema kumhusu Mungu wa kweli? 

Ijumaa, 15 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 30


Mwenyezi Mungu anasema, "Watu wengine wanaweza kuwa na utambuzi kidogo katika maneno ya Mungu, lakini hakuna yeyote kati yao ambaye huamini hisia zake; wao huogopa sana kuingia katika ukanaji. Hivyo, wao kila mara wamegeuka kati ya furaha na huzuni. Ni haki kusema kwamba maisha ya watu wote yamejaa huzuni; kusongeza hili katika hatua nyingine zaidi, kuna usafishaji katika maisha ya kila siku ya watu wote, lakini Naweza kusema kwamba hakuna anayepata ufunguliwaji wowote katika roho yake kila siku, na ni kana kwamba milima mitatu mikuu inakilemea kichwa chake.

Jumatatu, 11 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 26



Mwenyezi Mungu anasema, "Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani. 

Jumamosi, 9 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 41

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 41


Wakati mmoja Nilianza shughuli kubwa miongoni mwa wanadamu, lakini hawakutambua, kwa hivyo ilinibidi Nitumie neno Langu ili kuwafichulia. Na hata hivyo, mwanadamu bado hangeweza kuyaelewa maneno Yangu, na akasalia kutojua malengo ya mpango Wangu. Na hivyo kwa sababu ya kasoro na dosari za mwanadamu, alifanya mambo ili kukatiza mpango Wangu wa usimamizi, na pepo wachafu wakachukua nafasi ya kujidhihirisha, wakawafanya wanadamu kafara wao, mpaka wakateswa na pepo hao wachafu na wakachafuliwa kila mahali. 

Alhamisi, 31 Januari 2019

"Wimbo waUshindi" (7) - Hukumu ya Mungu katika Siku za mwisho Huwafanya Washindi Kamili.



"Wimbo waUshindi" (7) - Hukumu ya Mungu katika Siku za mwisho Huwafanya Washindi Kamili.


Ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu huvumilia shida kali na mateso kutoka kwa Chama Cha Kikomunisti cha China na ulimwengu wa dini. Kwa nini wanaendelea kukataa kujisalimisha, kuendelea kuhubiri injili na kumshuhudia Mungu? Je, Mwenyezi Mungu anawaongozaje kupitia hukumu na taabu ya Mungu ili kufikia utakaso na kuwa washindi? Tazama video hii!

Tazama Video: Filamu za Injili

Jumatatu, 28 Januari 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 17

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Sura ya 17


Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao.  

Jumapili, 27 Januari 2019

"Wimbo wa Ushindi" (6) - Njia Inayoongoza kwenye Utakaso na Wokovu




"Wimbo wa Ushindi" (6) - Njia Inayoongoza kwenye Utakaso na Wokovu


Je, kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho humtakasa na kumwokoa vipi mwanadamu? Je, kwa kweli tunapitiaje hukumu na kuadibiwa na Mungu ili tuweze kupata ukweli, uzima, na kustahili wokovu na kuingia katika ufalme wa mbinguni? Video hii itakuambia majibu, na kukuelekeza kwa njia ya kuingia ufalme wa mbinguni.

Tazama Video: Filamu za Injili

Alhamisi, 24 Januari 2019

"Wimbo wa Ushindi" (5) - Kwa nini Bwana Anarudi Kufanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho


"Wimbo wa Ushindi" (5) - Kwa nini Bwana Anarudi Kufanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho


Watu wengi wanaamini kwamba tayari dhambi zetu zimesamehewa na kupata wokovu kwa sababu tulitangaza imani yetu kwa Bwana, basi kwa nini Bwana anakuja kutuchukua moja kwa moja hadi kwenye ufalme wa mbinguni? Kwa nini bado Anahitaji kuwahukumu na kuwatakasa? Je, hukumu ya Mungu kwa wanadamu katika siku za mwisho ni utakaso na wokovu, au ni shutuma na uharibifu wa wanadamu? Kipande hiki kitakufunulia siri hizo.

    Yaliyopendekezwa: Filamu za Injili, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumanne, 22 Januari 2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 11

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya kristo | Sura ya 11

Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima.