Jumapili, 5 Novemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema: Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno.

Jumamosi, 4 Novemba 2017

Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu



Mwenyezi Mungu anasema, "Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.

Ijumaa, 3 Novemba 2017

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha.

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo.

Alhamisi, 2 Novemba 2017

Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani.

Jumanne, 31 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema, Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja.

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu.

Jumatatu, 30 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Waovu Lazima Waadhibiwe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Zaidi ya unavyokubali neno la Mungu wakati huu, ndivyo unavyoweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo unavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake.

Jumapili, 29 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sitisha Huduma ya Kidini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,


Mwenyezi Mungu alisema: Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni.

Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema, Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa.

Jumamosi, 28 Oktoba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maonyo Matatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki


Mwenyezi Mungu anasema, "Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu.