Ijumaa, 26 Januari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 62. Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 62. Ili Kuwa Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa

Mwenyezi Mungu alisema, Tazama, kwa kila kifungu cha maneno yaliyosemwa na Mungu, au kila tukio ambalo Mungu anatoa mahitaji kwa watu, Mungu ataonyesha njia ya kutenda na kanuni za kutendea. Kwa mfano, tulipozungumza kuhusu kuwa waaminifu hivi karibuni, Mungu aliwaonyesha watu njia, Aliwaambia jinsi ya kuwa waaminifu, na jinsi ya kutenda wanapokuwa waaminifu ili kuchukua njia sahihi kwa kuwa waaminifu, Akisema: “Kama huko tayari kabisa kuwaambia wengine kuhusu siri zako—matatizo yako—na kutafuta njia ya mwanga, basi Ninasema kuwa wewe ni mtu ambaye ni mgumu kuokoa, mtu ambaye hawezi kuibuka kutoka kwa giza kwa urahisi.” Matokeo ya maneno haya ni kuwa tunahitajika kuweka wazi mambo tunayoamini kuwa siri au binafsi, na lazima tuweze kuyachambua. Hili halikutokea kwenu; hamkuelewa au kujua kwamba haya maneno ya Mungu yalikuwa ili kuwafanya mtende kwa hii njia. Wakati mwingine, jinsi unavyotenda ni aina ya udanganyifu, na hivyo inapaswa kubadilika, na motisha zako pia zinapaswa kubadilika, Inawezekana kwamba hakuna anayetambua kwamba maneno yako ni danganyifu, lakini kuna motisha katika njia unavyotenda, na motisha hizi ni danganyifu, na kwa hivyo zinapaswa kubadilika—na kama zinafaa kubadilika, lazima uzichambue: Je, Mungu anachukia motisha hizi? Je, njia unavyotenda na motisha zako zinamchukiza Mungu? Je, huwezi kuziweka wazi? Ni vigumu kuongea kuzihusu? Zinapingana na ukweli? Kama, unapozichambua na kuzichunguza, unasema, “Eh, inaonekana kuwa hizi zinapingana na ukweli, inaonakena kuwa ninapotenda kwa njia hii, si rahisi kuweka mambo wazi, na kutenda hivi kunachukiwa na Mungu,” basi unafaa kubadilisha jinsi unatenda—hakuna haja ya kutenda kusivyohitajika sana. Mnahisi huzuni Ninawasilisha hili kwenu, mkifikiri: “Iwapo nafaa kumwamini Mungu kwa njia hii, basi inaonekana lazima nianze kutoka mwanzo. Imekuwa vigumu vya kutosha kufika mahali niko leo, kwa nini lazima nianze kutoka mwanzo tena”? Kwa kweli, wakati huu ndio mwanzo, na unapoanza, lazima uanze vizuri. Tangu mwanzo kabisa lazima ufahamu umuhimu wa kuingia katika uhalilisi—lazima uweke msingi mzuri; kama, kule mwanzoni kabisa, uliweka msingi wa barua na mafundisho, basi utakuwa katika shida. Ni kama wakati watu hujenga nyumba ufuoni nyumba hiyo itakuwa hatarini bila kujali umeijenga kwa urefu gani, na haitadumu sana. Bado, leo, mna faida—mna uwezo wa kukubali kile tunachowasiliana nanyi, na mko tayari kusikiza. Ni vyema! Unapaswa kufahamu kilicho muhimu, kilicho cha umuhimu wa kufuatia, and jinsi unavyopaswa kuingia. Na kuhusu makosa, dhambi, na dosari unazo ambazo zinayopaswa kurekebishwa, lazima uharakishe na uzirekebishe. Usisubiri; muda haumgoji yeyote! Ukipoteza miaka hii, na kuitumia bure, basi hivi karibuni utagutuka na kusema: Jamani! Sina kimo. Mambo yakinifanyikia, bado sina uwezo wa kushughulika nayo, na kwa kila kitu nimechanganyikiwa na sionyeshi hisia; kwa kila kitu nategemea tabia yangu potovu na falsafa yangu ya maisha kuishi, au mawazo yangu mwenyewe, au maarifa na mafundisho. Ya kusikitisha mno! Siku ikifika utakapoulizwa kufanya baadhi ya kazi kwa kanisa, au kutimiza wajibu fulani, utajipata mkono mtupu, na kuwa na wasiwasi. Zaidi ya hayo, kazi ya Roho Mtakatifu haisubiri watu. Katika miaka michache ya kwanza Alikupa baadhi ya neema, huruma, usaidizi, na utoaji. Lakini kama, baada ya Yeye kukusubiri kwa muda mrefu, bado hujabadilika au kuingia katika uhalilisi, na unaelewa tu barua na mafundisho, basi umekwisha—umeshakosa nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mwanzoni unapoweka msingi, unapaswa kukaza miguu yako katika njia ya uhalilisi, na si kwa njia ya barua na mafundisho. Unapaswa kuchagua kuingia katika uhalisi, na kwa kila kitu unapaswa kuingia katika uhalisi, na kuukubali uhalisi uathiri wazo lako, na kujiuliza: “Napaswa kutenda vipi katika suala hili? Napaswa kutenda vipi katika suala hilo? Na kanuni ya kutenda katika suala hili ni ipi? Kanuni ya kutenda katika suala hilo ni ipi? Ni nini kinapaswa kufanywa ili kumridhisha Mungu? Napaswa kufanya nini ili kutimiza mahitaji ya Mungu na viwango Vyake? Haya ndiyo unayopaswa kuuliza. Lakini kimo cha watu ni kidogo sana, na kila wakati wanauliza kuhusu mambo yasiyohusika na kuweka ukweli katika vitendo, au yasiyokuwa na uhusiano na kujijua na kuwa waaminifu. Unasemaje, hiyo si ovyo? Kimo chao si kidogo? Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wafuasi tangu Mungu alipoanza hatua hii ya kazi; hata kuna wale walioanza na kuanza kufuata wakati Roho Mtakatifu alikuwa anafanya kazi katika mkondo huu—lakini kuwa wamefuata hadi leo, bado hawaelewi maana ya “uhalisi”, na kuwa wamefuata hadi leo, hawajawahi kuingia katika uhalisi wowote. Watu wengine husema: “Si sahihi kusema kwamba, kwa kuwa wamefuata hadi leo, hawajaingia katika uhalisi. Angalau wamejitumia na kujitolea; watu wengine hata wameacha matarajio yao, kazi, na familia, na hata kuna wale walioacha ndoa. Huku si kutenda? Kwa nje unaweza kuwa umeonyesha baadhi ya moyo wa ibada na kujitolea, na kutenda kwa njia fulani, lakini kufanya mambo haya hakumanishi kuwa wewe ni mwaminifu, wala kumaanisha kuwa umepata ukweli kutokana na imani yako kwa Mungu. Matendo haya hudokeza tu ushirikiano wa watu ili kuokolewa kupitia kwa imani kwa Mungu; matendo yao si onyesho la kuingia katika uhalisi wa ukweli. Na hivyo, watu wengi ambao wamemfuata Mungu kwa miaka ishirini bado wanaweza kumwacha Yeye, na kuwa wamemfuata kwa miaka ishirini bado wanaweza kufukuzwa kutoka kwa nyumba ya Mungu. Kuna hata wale ambao, ingawa wamefuata hadi leo, hawajawahi kuwa waaminifu, hawajawahi weka kuwa mwaminifu katika vitendo, kwa vile hawaoni kuwa waaminifu au kuweka ukweli katika vitendo na kuingia katika uhalisi kuwa muhimu. Na wanaona imani kwa Mungu kama nini? Wanafikiri: “Mradi nikimbie hapa na pale, nijitolee mwenyewe, lipa gharama, na kuacha kazi yangu, basi Mungu anapaswa kufanya ukumbusho wa tabia yangu,” au, “Nastahili kuwa mmoja wa wale waliookolewa.” Hii ni ruya, na ndoto za mchana. Ikiwa tunafaa kuokolewa, na kwa kweli kuja mbele ya Mungu, basi lazima tuulize kwanza: “Eh Mungu! Napaswa kuweka nini katika vitendo? Viwango Vyako ni vipi? Viwango Vyako vya kuokoa watu ni vipi? Unaokoa watu wa aina gani?” Haya yanaashiria urazini wa kweli, hii ndiyo tunapaswa kuulizwa juu ya yote, na ile tunapaswa kutafuta na kujua juu ya yote. Ukiweka mizizi yako katika uhalisi na ukweli, ukifanya kazi kwa bidii katika vipengele vyote vya ukweli na uhalisi, basi wewe ni mtu aliye na mizizi, na kumiliki uhai. Ukiweka mizizi yako katika barua na mafundisho, na hivyo usiwahi kuweka ukweli wowote katika vitendo au kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya ukweli wowote, basi utakuwa mtu ambaye kamwe hawi na uhai. Ona, kuwa mwaminifu kunapendwa na Mungu. Tunapoweka kuwa waaminifu katika vitendo, tunakuwa pia na maisha ya kuwa waaminifu, na uhalisi na dutu ya kuwa waaminifu—na hivyo tunao utendaji wa kuwa waaminifu, na onyesho la kuwa waaminifu. Angalau, upande wetu ulio mwaminifu unapendwa na Mungu na kukubaliwa na Mungu. Lakini bado tunazo sehemu nyingi ambazo hatuko waaminifu, na tunahitaji kuendelea kubadilika na kufuata—Mungu anatungoja, na kutupa nafasi. Kama kamwe hatupangi kuwa waaminifu, na kamwe hatutafuti jinsi ya kuwa waaminifu, au kutafuta matendo na maneno yapi ni onyesho la kuwa waaminifu, basi hatutawahi kuwa na dutu ya kuwa waaminifu, na hakungekuwa na uwezekano wa sisi kuwa na maisha ya kuwa waaminifu. Aina yoyote ya uhalisi ulio nao ni kimo unacho, na kipengele cha ukweli ambao umejiandaa nao. Kama huna uhalisi wa aina hii, basi huna maisha hayo ama kimo kama hicho. Na basi, wakati unakutana na majaribu au mitihani, au agizo, kama huna uhalisi, wakati mambo haya yatakufanyikia itakuwa rahisi kwako kuanguka, kufanya makosa, kufanya dhambi dhidi ya Mungu, na kuasi dhidi ya Mungu—yote ambayo yatakuwa nje ya udhibiti wako. Hatimaye, watu wengine wataondolewa, Roho Mtakatifu atawaacha na kukoma kufanya kazi ndani yao, na hata kutakuwa na wale ambao, kwa kusababisha uharibifu kwa nyumba ya Mungu, wataishia kufukuzwa. Hili ni tokeo lisiloweza kuepukwa. Lakini kama, leo, utaweka ukweli katika vitendo na kuwa mwaminifu, nani anaweza kuchukua sehemu yako ambayo ni aminifu? Hakuna anayeweza, hakuna anayeweza kukuvua kipengele hiki cha uhalisi na maisha haya. Na kama, wakati fulani katika siku zijazo, unasema: “Nimekuwa mwaminifu kwa muda mrefu sana, naweza kurudi kuwa mtu ambaye ni mdanganyifu?” kuna uwezekano haitafanyika kwa urahisi, kwa vile tayari unaishi katika mwanga wa Mungu, na kuishi katika njia ya mwanga. Si rahisi kubadilika kutoka kuwa mtu ambaye ni mdanganyifu hadi mtu ambaye ni mwaminifu. Kubadilika tena kutoka kuwa mtu mwaminifu kwa kweli anayependwa na Mungu—huko hakuwezekani wala si rahisi. Watu wengine husema, “Nimekuwa nikiweka kuwa mwaminifu katika vitendo kwa muda fulani. Mara nyingi ninaweza kuongea maneno ya kweli, na mimi ni mwaminifu kiasi, lakini wakati mwingine nafichua tabia yangu ya danganyifu, naonyesha dutu yangu ya danganyifu.” Hii inafaa kutatuliwa baadaye hatua kwa hatua. Mradi ufuate, na kufanya kazi kwa bidii na kufikia kuingia kuhusu suala hili, basi hufai kuwa na wasiwasi kuhusu jinsi utakuwa katika siku zijazo. Unapopanda miche ardhini, kama unainyunyizia maji na kuipa mwangaza kila siku, hufai kuwa na wasiwasi kama itazaa matunda; majira ya kupukutika kwa majani yanapokuja, lazima kutakuwa na kitu cha kuvuna. Leo, kinachotuhusisha zaidi kinapaswa kuwa kama tayari tunaweka kuwa waaminifu katika vitendo, na kama tunashiriki katika uhalisi huu. Ukisema, “Najua kuwa mimi ni mdanganyifu, lakini sitawahi kuweka kuwa mwaminifu katika vitendo,” basi huna uhalisi wowote wa kuwa mwaminifu, na lazima bado ufanye kazi kwa bidii: Kila utondoti wa maisha yako, kila njia unavyotenda katika maisha yako, njia ambayo daima umetenda, namna yako ya mara kwa mara ya kutenda, na jinsi unavyowatendea watu—lazima yote yachambuliwe. Usipoyachambua, bado utakuwa mwenye majivuno, na bado utaridhika na jinsi unavyofanya vitu—lakini unapoyachambua, utashtuka: Jamani, inaonekana kwamba mimi katika mawazo yangu ni wa chini sana, mbaya sana, mwenye kudhuru kwa siri sana! Utashangaa; utagundua nafsi yako ya kweli, na utajua kwa kweli shida zako mwenyewe na makosa, na udanganyifu wako mwenyewe. Na kama huchambui? Daima utajiamini kuwa mwaminifu, na mtu asiye na udanganyifu. Mdomo wako utasema wewe ni mdanganyifu, lakini ndani ya moyo wako bado utajiamini kuwa mwaminifu. Hapo basi, hutawahi kubadilika. Usipojichambua, ungewezaje kujijua? Usipojichambua, unawezaje kujiweka wazi? Unawezaje kuchimbua mambo na motisha katika kina cha moyo wako? Na usipoyachimbua, unawezaje kubadilika? Usipoyachimbua, utakuwa mjinga kuhusu mwelekeo wa kutendea, na cha kulenga katika matendo yako. Hii hasa ndiyo maana ya kweli ya maneno “Usipoingia katika uhalisi, utakuwa bila uhalisi wa ukweli milele.”
Maneno yote ya Mungu yana maana ya kweli, na ni ya watu kuyatumia kama kigezo. Si ya kukupa kitu cha kusoma, au kuridhisha mahitaji yako kadhaa ya kiroho, au ya wewe kunung’unikia kutoka mdomo wako, ukikitimiza hitaji lako la maneno na mafunzo. Maneno yote ya Mungu yana dutu yao yenyewe, na hali yao halisi, na kama usipojaribu na kuweka kipengele hiki cha uhalisi katika vitendo au kujaribu kukiingia, basi milele utakuwa mtu aliyeachana na uhalisi. Ukiweka kuwa mwaminifu katika vitendo, basi utakuwa na uhusiano na uhalisi wa kuwa mwaminifu na utaingia hali ya kweli ya kuwa mwaminifu. Pia utaelewa watu wa aina gani ni waaminifu, aina gani sio, na kwa nini Mungu anachukia wale ambao ni wadanganyifu; kwa kweli utaelewa maana ya mambo haya, na kufahamu nia za Mungu katika kuomba watu wawe waaminifu, na kwa nini Anatoa mahitaji haya. Baada ya kugundua jinsi ulivyo mdanganyifu, utataka sana kubadilika, utachukizwa na udanganyifu wako mwenyewe na uhalifu, utatiwa kinyaa na tegemeo lako lisilo la aibu la udanganyifu na uhalifu ili kuishi, na hivyo utahisi zaidi jinsi ilivyo muhimu kuwa mwaminifu, na jinsi mahitaji ya Mungu kuwa watu wawe waaminifu ni ya wakati wa kufaa, na nzuri, na jinsi maneno Yake ni sahihi. Unasemaje, si muhimu kuwa Mungu atoe mahitaji haya? Ndiyo. Na hivyo, kuanzia leo, tunapaswa kuchambua sehemu yetu ambayo ni danganyifu na halifu. Baada ya kuichambua, utagundua kuwa nyuma ya kila kipande cha udanganyifu kuna motisha, malengo fulani, aibu yako, na kuwa pia vinaonyesha ujinga wako, na hali yako ya chini. Baada ya kugundua hili, utautazama uso wako wa kweli, na baada ya kugundua uso wako wa kweli utajichukia. Unapojichukia na kujua wewe kwa kweli ni kitu cha aina gani, bado utaringa wakati huo? Bado utajigamba katika kila kitu? Bado utajaribu na kupata kibali cha watu wengine kwa kila kitu? Na bado utasema kuwa Mungu anauliza mengi sana? Kwamba hakuna haja ya mahitaji ya Mungu? Utaacha kutenda kwa njia hii na kusema mambo haya, utasema amina kwa, na kukubaliana na maneno yaliyotamkwa na Mungu, na kuaminishwa kwa kweli na kabisa nayo. Hii ndiyo fanisi zaidi kuhusu kuweka kila moja ya maneno ya Mungu katika vitendo, na kuingia katika uhalisi, na ukizidi kuweka maneno ya Mungu katika vitendo, utazidi kuhisi jinsi yalivyo sahihi na muhimu. Tuseme hutendi, na daima unasema, “Eh, mimi si mwaminifu, mimi ni mdanganyifu!” Unapokuwa mdanganyifu, unafikiri mwenyewe, “Nitatenda tu namna hii; si danganyifu sana, bado inahesabika kama kuwa mwaminifu. Mimi niko wazi kabisa, usaliti huu kidogo hauwezi kuchukuliwa kama udanganyifu,” na ni hayo tu. Jambo sawa linapokufanyikia tena, wewe ni mtawala na mhalifu mara nyingine tena; punde unapofungua mdomo wako, maneno yanayotoka ni madanganyifu, baada ya hapo unafikiri kwa muda, na kusema: “Nilikuwa mhalifu leo?” Unakuwa na wazo, na kujisemea kuwa haionekani kama umekuwa, na hakuna zaidi; unasema, “Hakuna shida, sikuwa mhalifu.” Wakati unaofuata, unadanganya tena, na baada ya kudanganya unafikiri kwa muda, na kujisemea: “Eh, nilikuwa mhalifu na mdanganyifu tena? Nilidanganya tena? Haionekani kama nilidanganya.” Ukiuomba mbele ya Mungu, unasema: “E Mungu! Ona jinsi mimi daima ni mtawala , jinsi daima mimi ni mhalifu na mdanganyifu. Nakuomba unisamehe, na kunikomesha kuwa mhalifu na mdanganyifu wakati ujao—na kama mimi ni hayo, tafadhali nifundishe nidhamu, Mungu.” Unafuta kwa kawaida mambo kama haya. Huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mtu asiyependa ukweli, na asiye tayari kuweka ukweli katika vitendo. Unaweza kuwa umelipa gharama ndogo na kutumia wakati mdogo kwa ajili ya kutekeleza jukumu lako, kumhudumu Mungu, na kusikiza ujumbe, na unaweza kuwa umetumia muda ambao ungetumia vinginevyo kufanya kazi na kupata pesa kidogo, lakini kwa kweli, hujaweka ukweli katika vitendo hata. Ikujapo kuweka ukweli katika vitendo, wewe kweli ni mtu juu juu, na aliyekosa uwajibikaji, na asiyejali; hivyo, pia, wewe ni mzembe kuhusu kuweka ukweli katika vitendo. Hii inathibitisha kuwa mtazamo wako kwa ukweli ni wa chuki, kuwa wewe ni mtu asiye tayari kuweka ukweli katika vitendo, aliyepotea kutoka kwa ukweli, asiyemwacha Mungu kwa sababu tu unatamani kupata baraka na kuogopa adhabu. Kwa ajili ya kuwa sawa na mtindo, unaiga kile ndugu zako wote wanasema, unajifunza maneno fulani ya kitaaluma ya kiroho, baadhi ya nyimbo zinazojulikana, na baadhi ya maneno ambayo kila mtu husema mara nyingi, na unafikiri unafuata mwenendo, na kwamba unakuwa mroho. Hatimaye, matukio haya ya juujuu yatakuchezea hadi kifo chako, utakapomalizwa, mwisho wako utatangazwa, na utaenda jahanamu. Katika hili, kuna haja ya kumwamini Mungu? Hakuna uhalisi katika “imani” yako, hujaingia katika uhalisi wowote, na hivyo, vivyo hivyo, mwisho wako utakuwa jahanamu, na hutazaa tunda. Mungu husema nini? Mungu anataka tunda, si maua; bila kujali hadi kiasi gani utachanua, jinsi ulivyo mrembo, Mungu hakutaki. Ambayo ni kusema, bila kujali jinsi mambo unayosema ni mazuri, bila kujali jinsi kujitolea na kutoa kwako sadaka kwa nje ni kukubwa, au mambo mangapi wewe huacha, hakuna kati ya haya yanayopendwa na Mungu. Mungu anaangalia kiasi gani umebadilika kwa kweli, kiasi gani umeingia katika uhalisi, kiasi gani umeingia katika ukweli, na mambo mangapi umefanya yanayoridhisha moyo wa Mungu, na yaliyolingana na mahitaji Yake. Hii ndiyo Mungu huangalia. Wakati watu hawamfahamu Mungu, wakati hawauelewi moyo Wake, wao daima wanauelewa vibaya moyo Wake, na daima wanaleta baadhi ya mambo ya juujuu mbele Yake kutoa maelezo, wakisema: “E Mungu! Ona kwa muda gani nimejitolea Kwako, ona kwa muda gani nimekuamini, ona jinsi nimezunguka zunguka kwa ajili Yako, ona watu wangapi nimekushindia, ona ni vifungu na sentensi ngapi za maneno Yako ambayo nimekariri, ona idadi ya nyimbo hizi za kidini ninaweza kuimba—je mimi sijalipa gharama kubwa? Kila siku narauka saa kumi asubuhi kuomba, kusema maombi yangu ya asubuhi. Hata jambo kubwa linapotendeka, au niko katika ugumu, au nimefanya makosa, nafunga na kuomba. Na natumia muda mwingi kusoma maneno ya Mungu kila siku....”Lakini bado matokeo ni kwamba Mungu anasema: “Wewe ni mwaminifu sasa? Kumekuwa na mabadiliko katika ujanja wako? Umewahi kulipa gharama yoyote kwa kuwa mwaminifu? Umewahi kuleta mambo ya hila ambayo umefanya na ufunuo wa ujanja wako mbele Yangu kuuweka wazi? Udanganyifu wako Kwangu umepunguka kwa kiasi gani? Wewe mwenyewe unajua udanganyifu wako Kwangu, na uongo ambao umeniambia? Umeweka mambo haya kando? Hebu wewe fikiria kuhusu mambo haya—inaonekana hujafikiria, hata kidogo. Umeshtuka, na kushangaa kuhisi kuwa huna namna ya kutoa maelezo mbele ya Mungu. Nia Yangu katika kusema haya yote ni kwamba mnapaswa kuwa makini katika kuweka ukweli katika vitendo. Kila neno, mawasiliano, na ukweli haupaswi kupitishwa tu kwa wengine, lakini pia kuwekwa katika vitendo. Kwa nini Mungu husema kuwa ukweli ni maisha yako, kuwa unaweza kutenda kama maisha yako? Kwa sababu ukweli unaweza kukubadilisha, na katika hili, unakuwa maisha yako. Kama ukweli haujakubadilisha, hiyo si kwa sababu haujatenda kazi yake, lakini kwa sababu hujauweka katika vitendo, au kuuingia; hujaukubali ukweli ulio ndani yako ili kutoa na kubadilisha mambo yale yako yaliyo potovu, kubadilisha mambo yale ndani yako yanayoasi na kupingana na mapenzi ya Mungu. Hatimaye, kama ukweli haujatekeleza kazi yoyote ndani yako, kama haujabadilisha tabia yako yoyote potovu, basi siku moja, wakati maisha yako ya imani kwa Mungu yako karibu kuisha, majaliwa yako yataamuliwa pia. Tunapowasiliana kuhusu hili leo, hamhisi umuhimu wa kuweka ukweli katika vitendo? Usikuwe kama watu wa zamani, kusubiri miaka mitatu au mitano, mitano au sita kabla ya kuanza kuweka ukweli katika vitendo. Hakuna wakati umewekwa wa kuweka ukweli katika vitendo: Ukiweka ukweli katika vitendo mapema, utabadilika mapema. Ukiuweka katika vitendo baadaye, utabadilika baadaye—lakini kama umekawia sana na ukose nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kukosa mkondo wa kazi ya Roho Mtakatifu, basi wewe umekwisha kabisa. Ukingoja hadi mpango wa usimamizi wa Mungu umefika kikomo na mkondo wa wokovu wa Mungu umepita, basi utakuwa umekosa nafasi yako kabisa, na wakati umekosa nafasi yako utasema: “Eh! Siku hizo za nyuma sikuweka bidii yoyote. Nitaanza kuweka ukweli katika vitendo leo.” Wakati huo utakuwa umekawia sana, na si rahisi kufanya, kwani Roho Mtakatifu anapoacha kufanya kazi, maarifa yako ya jambo lolote au ukweli yatakuwa ya juujuu, na kukosa mazingira, na bila nguvu—na wakati huo, kutakuwa na haja gani ya kujipiga kifua chako na kuomboleza kwa huzuni?
Unasemaje, kuishi na watu walio wadanganyifu kunakufanya uhisi mchovu? Ndio. Na wao huchoka? Wanachoka, pia, kwa sababu kuwa mdanganyifu si nzuri kama vile kuwa mwaminifu. Kuwa mwaminifu ni rahisi, mawazo na akili yako si ngumu—lakini ukiwa mdanganyifu, lazima uwe wa kukwepa daima. Gani huchukua muda mrefu zaidi: njia ya mzunguko, au ile ya moja kwa moja? Ile ya mzunguko, kwa hakika. Na mabomba ya maji, ikiwa bomba ni laini maji hutatoka moja kwa moja, ni rahisi, si vigumu kupata maji. Lakini ukipitisha maji kupitia katika bomba lililo na kona kadhaa ndani lake, je si maji hutoka polepole zaidi? Kuenda polepole huchukua nguvu zaidi. Nguvu zaidi hufanya watu wahisi kama ni ya ziada, na uziada hufanya watu wahisi karaha. Na hivyo watu wadanganyifu wenyewe pia huhisi uchovu; kuwa mdanganyifu daima kunachosha. Unajua umbali gani watu wengine hata huenda wanapokuwa wadanganyifu? Wanazozana na kila mtu. Na kwa kiasi kipi? Inakuwa hadi hawawezi kulala usiku, na ni kwa sababu kugombana siku nzima kunachosha, na kunawachosha kiakili. Unasemaje, wakati mambo yamefika kiwango hicho, mtu huyu ni mdanganyifu kiasi kipi? Iwapo angekuwa mwaminifu, hakuna vile angekuwa amechoshwa kiakili na kukosa uwezo wa kulala usiku. Kuishi maisha kama mtu mwaminifu hakuchoshi: Anasema chochote kilicho kwa akili yake, anafichua anachofikiria, na anatenda chochote anachofikiri katika akili yake, akitafuta mapenzi ya Mungu katika kila kitu anachofanya na kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu. Kunaweza kuwa na mambo kumhusu yaliyo majinga, kwa hivyo katika siku zijazo lazima awe mwenye busara zaidi, na lazima daima akue. Lakini watu wadanganyifu hutegemea falsafa yao wenyewe, mambo, na dutu kuishi. Wao si kama wale walio waaminifu; lazima wawe na tahadhari katika kila kitu wanachofanya isiwe wengine wawe na kitu dhidi yao, lazima watumie njia zao, utawala wao wenyewe wa udanganyifu na uhalifu ili kulinda na kuficha nyuso zao za kweli katika kila kitu wanachofanya. Karibuni au baadaye wataonyesha tabia zao za kweli, na wakifanya hivi watajaribu kugeuza mambo. Wanapojaribu kusema kitu ili kugeuza mambo, kuna nyakati ambazo si rahisi sana, na wasipoweza, wanaanza kuwa na wasiwasi. Wanaogopa kuwa wengine wataweza kuona ndani yao; hiyo inapofanyika, wanahisi wamejiaibisha wenyewe, na wanapoaibika lazima wafikirie njia za kusema kitu cha kuokoa hali. Si kuenda mbele na nyuma hivi kunachosha? Lazima wafikiri yote tena katika akili zao: kama hawangefanya hivi, maneno haya yangetoka wapi? Kama wewe ni mwaminifu, na uko bila motisha au nia, basi utatenda kwa njia wazi na kukosa kitu kisichoweza kuletwa kwa mwanga. Lakini watu walio wadanganyifu daima huficha nia katika maneno wanayoyasema na mambo wanayoyafanya, na mara tu wanapowekwa wazi, wanafikiri njia za kubadili mambo, watakapokupa fikra nyingine ya uongo, na kukufanya kutoelewa suala hilo tena, itakayowafanya wachovu. Kuishi nao unahisi jinsi ni ujinga kwao kutenda kwa njia hii, na ni bure kusema hivyo. Kwa kweli hakuna haja wao kujieleza kwako, hudhani ni muhimu, lakini wanendelea kueleza na kueleza, wakijaribu kuokoa hali. Unachoka kuwasikiza, kwa hivyo ili kuvumilia nao, kwa hivyo ili kuwavumilia, ili kuwaheshimu kidogo na kuwasamehe, unalazimika kuwa mvumilivu na mstahamilivu kwao, na wanafikiri kwa wenyewe: Ona jinsi daima lazima niseme mambo ambayo ni ya kweli; kama singelazimika kueleza mambo haya kwako haingekuwa ya kuchosha sana. Katika akili zao, daima lazima wafikiri kuhusu jinsi ya kukuzuia kutowaelewa, jinsi ya kukufanya usikize kile wanachosema na kutazama wanachofanya kwa njia inayofikia malengo na motisha zao. Na hivyo wanaipitia tena na tena katika akili yao: Wanapokosa uwezo wa kulala usiku wanafikiri kuihusu; wakati wa mchana, kama hawana uwezo wa kula wanafikiri kuihusu; wakati wa majadiliano na wengine wanaifikiri sana. Daima wanavalia sura ya kujifanya, ili usifikiri wako hivyo, ili usifikiri wano ni wazuri, au kuwa hivyo sivyo walivyomaanisha. Wakati wewe, mtu mdanganyifu, uko na mtu mwaminifu, anaweza kukuona jinsi ulivyo. Hawakukosoi, lakini: Wanakuvumilia, na ni hayo tu. Lakini ikiwa wote wawili ni wadanganyifu, basi kutoelewana kati yao kutakuwa wa kina zaidi na hawatakuwa na uwezo wa kuelewana. Lakini kama wewe ni mwaminifu, na wao ni wadanganyifu, basi bila shaka utachukizwa na jinsi wanavyotenda. Wanapoendelea kutenda kwa njia hii utawaona kuwa hasa wa kuchukiza. Wanapofanya hivyo mara kwa mara, utasema: “Watu wote wana tabia potovu, hakuna kitu cha kufanywa,” lakini wakiendelea kuifanya, utawaona kuwa hasa wa kuchukiza, utachukia jinsi wanavyotenda, utachukia nyuso zao, utachukia nia zao—na kuwachukia kwa kiasi hicho, bado ungetaka kuwa na mawasiliano nao bado? Bado ungetaka kuadhiriana nao? Ila wakibadilika, sivyo?
Je, haichoshi sana kuwa mdanganyifu? Kwa vile inachosha sana, kwa nini watu bado wako tayari kuwa wadanganyifu badala ya waaminifu? Mmewahi kufikiri kuhusu hiyo? Hili ndilo tokeo la jinsi asili ya kishetani inacheza na watu, ikiwaacha bila uwezo wa kutoroka maisha haya na tabia hii. Pia wako tayari kukubali kuchezewa kwa njia hii; wako tayari kuishi ndani ya hii, na hawako tayari kuweka njia ya mwanga katika vitendo. Unahisi kuwa kwao kuishi hivi kunachosha, kuwa hakuna sababu ya kutenda kwa njia hii—lakini wanahisi kuwa inahitajika sana, wanafikiri kuwa wana mengi ya kupoteza wasipotenda kwa njia hio, kuwa maslahi yao wenyewe yatadhuruiwa, kuwa watapata aibu nyingi na sifa yao itaharibika. Wanahisi watapoteza mengi sana, na wanayathamini mambo haya; wanathamini heshima yao na motisha zao. Hii ndiyo sura ya kweli ya chuki ya watu ya ukweli. Hata hivyo, watu hawaweki ukweli katika vitendo na hawako tayari kuwa waaminifu kwa sababa hawapendi ukweli. Na mbona hiyo? Daima unathamini mambo hayo. Umeamini katika Mungu kwa siku moja au mbili tu, wewe si mtu ambaye ameanza tu kuamini katika Mungu, mtu asiyeelewa ukweli na hana ufahamu wa aina gani ya watu wanapendwa na Mungu, na nani hivyo anategemea mambo yale ya wasioamini ili kuishi, anayetegemea mambo ya Shetani ili kuishi. Leo, kuna watu ambao wanajua ukweli. Tayari wameskia mengi, na wamefichua mengi, la sivyo wamesikiza kwa muda na wanafahamu kuamini katika Mungu kunahusu—lakini kwa nini bado hakujakuwa na mabadiliko ndani yao? Kwa sababu hawapendi ukweli. Na wale wasiopenda ukweli wanafaa kufanya nini? Hakuna njia ya mkato katika hili! Wao wenyewe lazima walipe gharama, wateseke, na kuomba na kujiweka wazi mbele ya Mungu, na baadaye wanahitaji kujiweka wazi hatua kwa hatua na kujichambua mbele ya watu wengine. Hii inahitaji ujasiri, inahitaji uasi dhidi yako mwenyewe, na inahitaji kujinyima. Usipojinyima na kuasi dhidi yako mwenyewe, kama unatamani kuweka ukweli katika vitendo bila kuvumilia mateso yoyote au kulipa gharama yoyote, basi hakutakuwa na matokeo. Watu wengine huuliza maswali kama, “Nifanye nini kama sipendi ukweli?” Kama hupendi ukweli, basi fanya mambo yale yanayoenda dhidi ya ukweli, na uone kama Mungu atafundisha nidhamu! Watu wengine husema: “Nifanye nini kama sitaki kishiriki katika mikutano?” Basi nenda na uishi na wale wasioamini, nenda na uchezecheze nao, uone ni nini hatimaye kitafanyika! Watu wengine husema: “Nataka kuwa mdanganyifu, sitaki kuwa mwaminifu. Kuwa mwaminifu, nitapoteza mengi sana, siwezi kufanya hivi. Kuwa mwaminifu, maslahi yangu mwenyewe yatateseka sana, na siri zangu nyingi sana zitajulikana na wengine. Sitaki kuwaruhusu watu wengine kujua mambo yangu ya binafsi, sitaki kuwaacha wanijue au kunielewa, napaswa kuwa na udhabiti wa majaliwa yangu.” Hivyo jaribu—uone nini kitakachofanyika kwako mwishowe, uone ni nani ataenda jahanamu na kuteseka adhabu!
Mko tayari kuwa waaminifu? Mnapanga kufanya nini baada ya kusikiza mawasiliano haya? Mtaanza na nini kwanza? (Kwanza nitamakinikia kutodanganya.) Sahihi. Kutodanganya si rahisi. Je, uwongo huwa na motisha? Hivyo kwanza, usiseme uongo wenye motisha. Hiyo ni rahisi kufikia? Kwa mfano, unahisi maneno haya yana motisha, kwamba yana madoa, kwamba ni uwongo—na unajua unapodanganya, sivyo? Hivyo kwanza usiseme uwongo huu. Upeleke mbele ya Mungu kuweka katika maombi yako na kuweka wazi; kwanza weka hii katika vitendo. Baada ya kufanya hivyo kwa muda, unapaswa kuomba kwa Mungu na kuuliza kwamba Akufundishe nidhamu na kukushutumu kama utawahi kudanganya tena, baada ya hapo unapaswa kuleta uwongo wako hatua kwa hatua mbele ya ndugu zako ili uchambuliwe.... Kwa njia hii, hatua kwa hatua, uwongo wako utakuwa daima chache, daima pungufu. Leo utasema uwongo kumi, kesho unaweza kusema tisa, siku baada ya hiyo utasema nane, baada ya hapo utasema mbili au tatu pekee. Utasema ukweli zaidi na zaidi. Kuwa mwaminifu, utakuja karibu na mapenzi ya Mungu, mahitaji Yake, na viwango Vyake daima zaidi—na hiyo itakuwa vyema iliyoje! Lazima uwe na lengo, lazima ukuwe na njia. Kwanza usiseme uongo huo, kisha chambua motisha zilizo ndani wake: Kwa nini umemiliki motisha kama hizi? Na dutu yao ni nini? Hii pia lazima uichambue hatua kwa hatua, na kama ukiendelea kuweka hii katika vitendo, basi kwa hakika kutakuwa na tokeo. Siku moja utasema: “Haya, ni rahisi kuwa mwaminifu. Kuwa mdanganyifu kunachosha sana! Sitaki kuwa mdanganyifu tena daima, kunachosha! Kuna mengi sana yanayofanyika ndani ya moyo wangu, kila kitu kimechanganyika ndani ya ubongo wangu, akili yangu daima lazima ifikiri mambo na kujadili: ‘Nitasemaje hili? Maneno yanaweza kutumiwa vipi kudanganya watu na kuwalaghai? Daima lazima nifikiri sana na kupima mambo hivi; maneno yangu hayawezi kuwa machangamfu sana, lakini pia hayawezi kuwa mazito zana—na ndani ya moyo wangu sina uwezo wa kubeba shinikizo hili, sitaki kuishi namna hii tena, kuishi namna hii kunachosha sana!” Wakati huu, utakuwa na matumaini ya kuwa kweli mwaminifu, na inathibitisha kuwa umeanza kuchukua hatua kuelekea kuwa mwaminifu. Haya ni mafanikio mapya. Bila shaka, kunaweza kuwa na baadhi yenu ambao, mwanzoni, baada ya kuongea maneno maaminifu, watahisi: Nilipojiweka wazi leo ilikuwa inadhalilisha, uso wangu ulikuwa mwekundu, ilikuwa aibu sana!” Unapokutana na wengine, utajisemea: “Kila mtu anajua ni nini nilimfanyia, ni nini nilisema nyuma yake, na uwongo mdanganyifu niliosema! Mimi nimeisha. Kila mtu anajua jinsi nisivyo na thamani. Walikuwa wanafikiri nilikuwa sawa, watu wengine walikuwa na wazo nzuri kunihusu; leo, kwa kuwa nimejiweka wazi, hakuna anayefikiri mimi ni wa maana. Nifanye nini?” Lazima uombe kuhusu hii mbele ya Mungu, ukisema: “Mungu, nataka kuwa mwaminifu. Leo naweka kuwa mwaminifu katika vitendo. Nakuomba uniruhusu kuingia kwa kina zaidi, nakuomba uniruhusu kuweka kando kiburi changu, na kuniruhusu kutoongozwa na kuzuiwa na maneno haya madanganyifu na motisha danganyifu. Nataka kuisha katika mwanga, sitaki kuishi katika miliki ya Shetani na kuzuiwa na Shetani, sitaki kutawaliwa, kudhibitiwa, kuzuiwa na tabia potovu ya kishetani, au hata kuumizwa nayo.” Unapoomba kwa njia hii, kutakuwa na mwangaza zaidi ndani ya moyo wako, na utajisemea: “Ni vyema kuweka hili katika vitendo. Leo nimeweka ukweli katika vitendo—vyema! Nahisi kwamba wakati huu tu ndio naishi kama mtu halisi.” Na unapoomba hivi, je Mungu hajakupa nuru? Mungu ameanza kufanya kazi ndani ya moyo wako, Amekugusa, na kukuruhusu kuthamini jinsi inavyohisi kuwa mtu halisi. Hivi ndivyo ukweli unapaswa kuwekwa katika vitendo. Kutoka kutojua njia mwanzoni, hadi kujua njia; baada ya hapo, utalipa gharama na kuteseka, kisha upitie ugumu wa kiakili hadi utakapopata raha ya kiroho, ukihisi kuwa kumridhisha Mungu kuna umuhimu sana, kuwa faraja ya kiroho na hisia ya kutimiza unayopata baada ya kumridhisha Mungu ni muhimu sana. Wakati huo, utaelewa inamaanisha nini kuweka ukweli katika vitendo kwa kweli, utaelewa inamaanisha nini kumridhisha Mungu, na inamaanisha nini kuwa mtu halisi—na katika hii, utakuwa umechukua njia sahihi katika imani kwa Mungu.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni