Jumanne, 6 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Thelathini na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Thelathini na Nne

Wakati mmoja Nilimwalika mwanadamu kama mgeni nyumbani Kwangu, lakini alikimbia huku na huko kwa sababu ya miito Yangu–kama kwamba, badala ya kumwalika kama mgeni, Nilikuwa nimemleta kwenye eneo la kuuawa. Kwa hiyo, nyumba yangu inaachwa tupu, kwa maana mwanadamu ameepukana Nami daima, na daima amejilinda dhidi Yangu.Hili limeniacha bila njia yoyote ya kutekeleza sehemu ya kazi Yangu, ambalo ni kusema, ni kama kwamba Nimeirudisha karamu Niliyomtayarishia, kwa maana mwanadamu hayuko radhi kuifurahia karamu hii, na kwa hiyo Sitamlazimisha kufanya hivyo. Lakini mwanadamu ghafula hujikuta akizongwa na njaa, kwa hiyo anakuja kubisha mlangoni Mwangu akiomba msaada Wangu—na Nikimwona amepata mashaka kama hayo, Ningewezaje kukosa kumsaidia? Hivyo, kwa mara nyingine Namwandalia mwanadamu karamu, ili aweze kuifurahia, na wakati huo tu ndio anahisi jinsi Ninavyopendeka, na hivyo anakuja kunitegemea. Na kwa sababu ya mtazamo wangu kwake, anakuja kunipenda polepole "bila kusita," na hashuku tena kwamba Nitamtuma katika "nchi ya uchomaji maiti," kwani haya si mapenzi Yangu. Na kwa hiyo, ni baada ya kuona moyo Wangu tu ndio mwanadamu hunitegemea kweli, ambalo linaonyesha tu jinsi alivyo na "tahadhari". Lakini Siwi macho kwa mwanadamu kwa sababu ya udanganyifu wake, lakini Husisimua mioyo ya watu kwa kumbatio Langu changamfu. Je, hili silo Nifanyalo sasa? Je, hili silo linalodhihirika ndani ya watu katika hatua ya sasa? Kwa nini wana uwezo wa kufanya mambo kama haya? Kwa nini wana hisia ya moyoni kama hiyo? Je, ni kwa sababu wananijua kwa kweli? Kwa sababu wana upendo usio na mipaka Kwangu kwa kweli? Simlazimishi mtu yeyote kunipenda, lakini Nampa tu uhuru wa kujifanyia uchaguzi wake mwenyewe; katika hili, Siingilii, wala kumsaidia kufanya uchaguzi kuhusu majaliwa yake. Watu waliweka uamuzi wao mbele Yangu, waliuleta mbele Yangu ili Niuchunguze, na wakati Nilipofungua mfuko ulio na "azimio la mwanadamu," Niliona mambo yaliyovurugika ndani. Lakini mambo yaliyokuwa ndani yalikuwa "mengi," na watu walinitazama kwa macho yaliyokodoa, wakiwa na hofu kubwa kwamba Ningeondoa azimio lao. Lakini kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu, Sikutoa hukumu mwanzoni kabisa, na badala yake Niliufunga mfuko na kuendelea kufanya kazi Niliyopaswa kufanya. Mwanadamu, hata hivyo, haingii katika mwongozo Wangu katika mwamko wa kazi Yangu, lakini anaendelea kujishughulisha na kama azimio lake limesifiwa na Mimi. Nimefanya kazi nyingi sana, Nimenena maneno mengi sana, lakini hadi sasa, mwanadamu bado hawezi kuyaelewa mapenzi Yangu, na hivyo kila kitendo chake cha kushangaza kinaacha "kichwa Changu kikizunguka." Kwa nini hawezi kuelewa mapenzi Yangu daima, na hufanya mambo kwa haraka kama apendavyo? Je, ubongo wake umepatwa na mshtuko? Inawezekana kuwa hafahamu maneno Nisemayo? Kwa nini yeye daima hutenda na macho yake yakiangalia mbele kabisa, lakini hawezi kuunda njia na kuonyesha mfano kwa watu wa baadaye? Je, kulikuwa na mtu yeyote wa kuonyesha mfano kabla ya Petro? Je, si chini ya mwongozo Wangu ndipo Petro akanusurika? Kwa nini watu wa leo hawawezi kufanya hili? Kwa nini, baada ya kuwa na mfano wa kufuata, bado hawawezi kuridhisha mapenzi Yangu? Hili linaonyesha kwamba bado mwanadamu hana imani Kwangu, ambalo ndilo limesababisha hali za leo zenye taabu.
Mimi hufurahia kuwatazama ndege wadogo wakipaa angani. Ingawa hawajaweka azimio lao mbele Yangu, na hawana maneno ya "kunipa" Mimi, wanapata raha katika ulimwengu ambao Nimewapa. Mwanadamu, hata hivyo, haliwezi hili, na uso wake umejaa huzuni—yawezekana kwamba Nina deni lake lisiloweza kulipwa? Kwa nini uso wake daima una michirizi ya machozi? Mimi hustaajabia mayungiyungi yanayochanuka vilimani. Maua na nyasi zinanyooka toka upande mmoja hadi upande mwingine wa miteremko, lakini mayungiyungi yanaongeza mng’aro kwa utukufu Wangu duniani kabla ya kufika kwa majira ya kuchipua—-je, mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki? Je, angeweza kunishuhudia duniani kabla ya kurudi Kwangu? Je, angeweza kujitolea kwa ajili ya jina Langu katika nchi ya joka kubwa jekundu? Ni kama kwamba matamko Yangu yamejaa matakwa kwa mwanadamu—ananichukia sana kwa sababu ya matakwa haya; kwa sababu mwili wake ni dhaifu sana, na hawezi kimsingi kufikia kile Ninachotaka, anaogopa maneno Yangu. Ninapofungua kinywa Changu, Nawaona watu duniani wakikimbia kila upande, kama kwamba wanajaribu kuitoroka njaa. Ninapofunika uso Wangu, wakati Ninapogeuza mwili Wangu, watu ghafla huwa wanaingiwa na hofu, hawajui cha kufanya, kwani wanaogopa kuondoka Kwangu; katika dhana zao, siku Nitakayotoka ndiyo siku ambayo msiba utashuka kutoka mbinguni, siku Nitakayoondoka ndiyo siku ambayo adhabu yao itaanza. Lakini Ninachofanya ni kinyume kabisa na dhana za mwanadamu, Sijawahi kutenda kulingana na dhana za mwanadamu, Sijaruhusu kamwe dhana zake kuwa zenye kuchukuana na Mimi. Wakati Ninapotenda ni wakati ambapo kwa usahihi mwanadamu anawekwa wazi. Kwa maneno mengine, vitendo Vyangu haviwezi kupimwa na dhana za binadamu. Tangu wakati wa uumbaji mpaka leo, hakuna mtu aliyewahi kugundua "bara mpya" katika mambo ambayo Ninafanya, hakuna mtu aliyewahi kuelewa sheria ambazo kwazo Ninatenda, hakuna mtu aliyewahi kufungua njia mpya. Hivyo, leo, watu bado hawawezi kuingia katika njia sahihi—ambayo ndiyo hasa wanayokosa, na wanayopaswa kuingia ndani yake. Tangu wakati wa uumbaji mpaka leo, Sijawahi kamwe kuanza shughuli kama hiyo hapo awali, Nimeongeza tu vipande vipya kwa kazi Yangu katika siku za mwisho. Lakini hata chini ya hali kama hizo dhahiri, watu bado hawawezi kuelewa mapenzi Yangu—hiki sio kile ambacho wanakosa kabisa?
Baada ya kuingia katika kazi mpya, Nina matakwa mapya kwa mwanadamu. Kwa mwanadamu, ni kama kwamba matakwa ya zamani hayajakuwa na matokeo, ambayo ndiyo sababu anayasahau. Ni njia gani mpya ambayo kwayo Nafanya kazi? Ninataka nini kwa mwanadamu? Watu wenyewe wanaweza kupima kama yale waliyofanya katika siku za nyuma yalifuatana na mapenzi Yangu, ikiwa matendo yao yalikuwa ndani ya mipaka ya kile Nilichotaka. Hakuna haja ya Mimi kukagua kila kitu kimoja kimoja; wanaelewa kimo chao wenyewe, na kwa hiyo katika mawazo yao, wanaelewa wanaweza kutenda hadi kiasi gani, na hakuna haja ya Mimi kuwaambia waziwazi. Ninapozungumza, pengine, watu wengine watajikwaa; hivyo, Nimeepuka kusema sehemu hii ya maneno Yangu ili kuzuia watu kugeuka kuwa wadhaifu kutokana na hilo. Je, hili sio la manufaa makubwa zaidi kwa ufuatiliaji wa mwanadamu? Je, sio la manufaa makubwa zaidi kwa maendeleo ya mwanadamu? Nani hataki kusahau mambo yake ya zamani, na kujitahidi kuendelea mbele? Kwa sababu ya "kutofikiri" Kwangu, Sijui kama watu wanaelewa kuwa njia ambazo kwazo Nanena tayari zimeingia katika eneo jipya. Kwa kuongeza, kwa sababu kazi Yangu ni ya "shughuli nyingi," sana, Sijakuwa na wakati wa kuuliza kama watu wanaelewa sauti ambayo kwayo Nanena. Hivyo, Nataka tu kwamba watu wanihurumie zaidi. Kwa sababu kazi yangu ni ya "shughuli nyingi," sana, Siwezi binafsi kutembelea vituo vya kazi Yangu ili kuwaongoza watu, na kwa hiyo Nina "ufahamu mdogo" kuwahusu. Kwa jumla, chochote kingine, Nimeanza sasa kuongoza mwanadamu kuingia rasmi katika mwanzo mpya, na katika mbinu mpya. Katika matamko Yangu yote, watu wameona kwamba kuna kuchekesha, ucheshi, na sauti ya nguvu ya dhihaka hasa katika kile Ninachosema. Hivyo, maelewano kati ya mwanadamu na Mimi huvurugwa bila kujua, na kusababisha kifuniko kizito cha mawingu juu ya nyuso za watu. Mimi, hata hivyo, Sizuiliwi na hili, lakini Naendelea na kazi Yangu, kwani yote ambayo Nasema na kufanya ni sehemu ya lazima ya mpango Wangu, yote yanayonenwa kutoka kinywa Changu humsaidia mwanadamu, na hakuna chochote Nifanyacho ni cha upuuzi, lakini cha kuadilisha watu wote. Ni kwa sababu mwanadamu anapungukiwa ndio Naachilia huru na kuendelea kunena. Watu wengine, labda, wananisubiri bila tumaini Nitoe matakwa mapya kwao. Ikiwa ndivyo, basi Naridhisha mahitaji yao. Lakini kuna jambo moja ni lazima Niwakumbushe: Ninapozungumza, Natumai kuwa watu wanapata ufahamu zaidi, Natumai kuwa wanatambua zaidi, ili waweze kupata zaidi kutoka kwa maneno Yangu na hivyo kutimiza matakwa Yangu. Hapo awali, katika makanisa, lengo la watu lilikuwa ni kushughulikiwa na kuvunjwa. Kula na kunywa Maneno yangu kulikuwa juu ya msingi wa kuelewa malengo yao na chanzo—lakini leo si kama siku za nyuma, watu hawawezi kabisa kuelewa chanzo cha matamko Yangu, na hivyo hawana nafasi ya kushughulikiwa na kuvunjwa na Mimi, kwa sababu wao hutia juhudi zao zote katika kula na kunywa maneno Yangu. Lakini hata katika hali hizi, bado hawawezi kuridhisha matakwa yangu, na hivyo Nafanya madai mapya kwao: Nawataka waingie katika majaribio pamoja nami, kwamba waingie katika kuadibu. Lakini hebu Niwakumbushe jambo moja: Huku si kumwua mwanadamu, lakini kinachohitajika na kazi Yangu, kwa kuwa, katika hatua ya sasa, maneno Yangu hayaeleweki kabisa na mwanadamu, na mwanadamu hawezi kushirikiana na Mimi—hakuna cha kufanya! Naweza tu kumfanya mwanadamu aingie katika utaratibu mpya pamoja nami. Kuna nini kingine cha kufanya? Kwa sababu ya kasoro za mwanadamu, Mimi pia lazima Niingie katika mkondo ambao mwanadamu huingia—je, si Mimi ambaye atawafanya watu wawe kamili? Je, si Mimi Niliyeonyesha mpango huu? Ingawa matakwa yale mengine si magumu, si ya pili kwa ya kwanza. Kazi Yangu kati ya kundi la watu wa siku za mwisho ni shughuli iliyo ya pekee, na hivyo, ili utukufu Wangu uweze kujaza ulimwengu, watu wote wanapitia taabu ya mwisho kwa ajili Yangu Mimi. Je unaelewa mapenzi Yangu? Haya ndiyo matakwa ya mwisho ambayo Nataka kutoka kwa mwanadamu, ambalo ni kusema, Natumai kwamba watu wote wanaweza kutoa ushuhuda wenye nguvu, unaovuma Kwangu mbele ya joka kubwa jekundu, kwamba waweze kujitolea wenyewe Kwangu kwa mara ya mwisho, na kutimiza matakwa Yangu kwa mara nyingine ya mwisho. Je, nyinyi mnaweza kufanya hili kweli? Nyinyi hamkuweza kuuridhisha moyo Wangu katika siku zilizopita—je, mnaweza kuvunja mpangilio huu katika mara ya mwisho? Nawapata watu fursa ya kutafakari, Nawaacha watafakari kwa makini kabla ya kunipa jibu hatimaye—je, ni kosa kufanya hili? Nasubiri jibu la mwanadamu, Nangoja "barua yake ya kujibu"—je, nyinyi mna imani ya kutimiza matakwa Yangu?
Aprili 20, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni