Jumanne, 16 Oktoba 2018

209. Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu


209. Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu


I
Matendo maovu ya wanadamu yanapomchukiza Mungu,
Ataiteremsha hasira Yake juu yao,
ila wanapotubu kwa kweli mbele Yake.
Watu wanapoendelea kumpinga Mungu,
Ghadhabu Yake haitakoma, hata watakapoangamizwa.
Hii ni tabia ya Mungu.
Kwa maneno mengine, rehema au ghadhabu ya Mungu
inategemea matendo ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu. Ah ...
II
Mungu akiendelea kumtia mtu mmoja kwa ghadhabu Yake,
moyo wa mtu huyu humpinga Mungu bila shaka,
kwa sababu hajapata kutubu kwa kweli,
kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu, au kuwa na imani ya kweli kwa Mungu.
Hajawahi kupata rehema ya Mungu na uvumilivu.
III
Ikiwa mtu mara nyingi atapokea utunzaji wa Mungu na kupata rehema na uvumilivu Wake,
basi mtu huyu bila shaka ana imani ya kweli kwa Mungu ndani ya moyo wake.
Na moyo wake haumpingi Mungu. Mara kwa mara anatubu kwa Mungu.
Hata kama nidhamu ya Mungu itashuka juu ya mtu huyu, ghadhabu Yake haiwezi.
Kwa maneno mengine, rehema au ghadhabu ya Mungu
inategemea matendo ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu. Ah ...
kutoka kwa "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni