Ijumaa, 22 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 18


Maneno yote ya Mungu yana sehemu ya tabia Yake; tabia Yake haiwezi kuonyeshwa kwa ukamilifu kwa maneno, kwa hiyo hii inaonyesha kiasi gani cha utajiri kiko ndani Yake. Kile ambacho watu wanaweza kukiona na kukigusa ni, hata hivyo, finyu, kama ulivyo uwezo wa watu. Ingawa maneno ya Mungu ni dhahiri, watu hawawezi kuyaelewa kwa ukamilifu. Kama maneno haya tu: "Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi.  Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope!" Maneno yote ya Mungu yana nafsi Yake, na ingawa watu wote wanajua maneno haya, hawajawahi kuelewa maana yake. Machoni pa Mungu, wote wanaompinga ni adui Zake, yaani, wale ambao ni wa pepo wabaya ni wanyama. Kutokana na hili hali halisi ya kanisa inaweza kuchunguzwa. Bila kupitia hotuba ya watu au kuadibu, bila kupitia kufukuzwa kwa watu moja kwa moja au sehemu ya mbinu za kibinadamu au kutajwa na watu, wanadamu wote wanajichunguza chini ya mwangaza wa maneno ya Mungu, na kuona kwa dhahiri kwa mtazamo wa "hadubini" kiasi gani cha maradhi kiko ndani yao kweli. Katika maneno ya Mungu, kila aina ya roho imeainishwa na umbo la asili la kila roho linafichuliwa. Roho za malaika huangazwa zaidi na kupata nuru zaidi, kwa hiyo kile Mungu alisema, kwamba "wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja" inategemea matokeo ya mwisho yaliyotimizwa na Mungu. Bila shaka sasa bado hayawezi kutimizwa kwa ukamilifu—hili ni limbuko tu. Mapenzi ya Mungu yanaonekana kupitia kwa hili na inaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu wataanguka katika maneno ya Mungu na watashindwa katika mchakato wa watu wote kuwa watakatifu hatua kwa hatua. "Kuyeyuka na kuwa tope" kulikotajwa hapa hakupingani na Mungu kuuangamiza ulimwengu kwa moto, na "umeme" unahusu ghadhabu ya Mungu. Wakati Mungu atatoa ghadhabu Yake kubwa, ulimwengu wote utapata maafa ya kila aina kama matokeo, kama kufoka kwa volkano. Ninaposimama juu ya anga, inaweza kuonekana kuwa juu ya dunia kila aina ya maafa yanawakaribia wanadamu wote, siku baada ya siku. Nikiangalia chini kutoka juu, dunia inafanana na mandhari mbalimbali kabla ya tetemeko la ardhi. Maji ya moto yanatiririka kila mahali, lava inatiririka kila mahali, milima inahama, na mwanga wa baridi unametameta kila mahali. Dunia nzima imezama katika moto. Hii ndiyo mandhari ya Mungu akitoa ghadhabu Yake, nao ni wakati wa hukumu Yake. Wale wote ambao ni wa mwili hawataweza kutoroka. Kwa hiyo vita kati ya nchi na migogoro kati ya watu havitahitajika kuharibu ulimwengu mzima, lakini "itafurahia kwa kufahamu" chanzo cha kuadibu kwa Mungu. Hakuna mtu atakayeweza kuiepuka na wataipitia mmoja mmoja. Baada ya hapo ulimwengu wote utaanza tena kuangaza kwa miale takatifu na wanadamu wote wataanza tena maisha mapya. Na Mungu atakuwa Amepumzika juu ya ulimwengu na Atawabariki wanadamu wote kila siku. Mbingu haitakuwa na ukiwa usiovumilika, lakini itarudia nguvu ambayo haijawahi kuwa nayo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na "siku ya sita" itakuwa wakati Mungu ataanza maisha mapya. Mungu na mwanadamu wote wataingia katika pumziko na ulimwengu hautakuwa tena mchafu au wenye najisi, lakini utapata upya tena. Ndio maana Mungu alisema: "Dunia si kimya na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena." Katika ufalme wa mbinguni hakujakuwa na udhalimu au hisia za kibinadamu, au tabia zozote za wanadamu za upotovu kwa sababu usumbufu wa Shetani haupo. Watu wote wanaweza kuelewa maneno ya Mungu, na maisha mbinguni ni maisha yaliyojaa furaha. Wote walio mbinguni wana hekima na heshima ya Mungu. Kwa sababu ya tofauti iliyoko kati ya mbingu na dunia, raia wa mbinguni hawaitwi "watu," lakini huitwa "roho" na Mungu. Maneno haya mawili yana tofauti muhimu, na sasa wale wanaoitwa "watu" wote wamepotoshwa na Shetani, wakati "roho" hazijapotoshwa. Mwishowe, Mungu atawabadilisha watu wote duniani kuwa na sifa za roho mbinguni na hawatapitia tena vurugu ya Shetani. Hii ndiyo maana halisi ya maneno "utakatifu Wangu umeenea kila mahali katika ulimwengu." "Nchi katika hali yake ya asili ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wake, kwa ajili yake kufanywa upya, mbingu haijafichwa tena kutoka kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu." Hili linasemwa kuhusu watu walio na roho za malaika, na wakati huo malaika watakuwa tena na uwezo wa kuishi pamoja kwa amani na kupata tena hali yao ya awali, na hawatagawanywa tena kati ya maeneo mawili ya mbingu na dunia kwa sababu ya mwili. Malaika walio duniani wataweza kuwasiliana na malaika walio mbinguni, watu walio duniani watajua siri za mbinguni, na malaika walio mbinguni watajua siri za ulimwengu wa binadamu. Mbingu na dunia zitaunganishwa na hakutakuwa n umbali kati yao. Huu ni uzuri wa utambuzi wa ufalme. Ni kile ambacho Mungu anataka kukamilisha, na pia ni kitu ambacho wanadamu wote na roho hutamani sana. Lakini wale walio katika ulimwengu wa kidini hawajui chochote kuhusu hili. Wao wanamngojea tu Yesu Mwokozi juu ya wingu jeupe ili Aichukue mioyo yao, na kuacha "takataka" kila mahali duniani (takataka inahusu maiti). Je, hili silo wazo la wanadamu wote? Hii ndiyo maana Mungu alisema: "Dunia ya dini—ingekosaje kuangamizwa na mamlaka Yangu duniani?" Kwa sababu ya kukamilika kwa watu wa Mungu ulimwenguni ulimwengu wa kidini utapinduliwa. Hii ndiyo maana ya kweli ya "mamlaka" ambayo Mungu alizungumzia. Mungu alisema: "Kunao wale ambao, katika siku Yangu, hulifedhehesha jina Langu? Binadamu wote huelekeza macho yao ya heshima Kwangu, na wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao." Hili ndilo Alilosema juu ya matokeo ya uharibifu wa ulimwengu wa dini, ambao wote watanyenyekea mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kwa sababu ya maneno Yake na hawatasubiri tena wingu jeupe kuteremka chini au kutazama anga, lakini watashindwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kwa hiyo, "wao hunililia kwa siri katika nyoyo zao"—haya ndiyo matokeo ya ulimwengu wa dini, ambao wote utashindwa na Mungu, na huu tu ndio unaoitwa uweza wa Mungu—ukiwaangusha watu wa dini, waasi wakuu kati ya wanadamu, ili wasiyashike tena mawazo yao wenyewe, lakini watamjua Mungu.
Ingawa maneno ya Mungu yametabiri uzuri wa ufalme mara kwa mara, yamesema juu ya hali zake mbalimbali na kuzielezea kwa mitazamo tofauti, bado hayawezi kueleza kikamilifu kila hali ya Enzi ya Ufalme kwa sababu uwezo wa watu wa kupokea umepungukiwa sana. Maneno yote ya matamko Yake yamenenwa, lakini watu hawajayaangalia kwa undani, ambalo limesababisha watu kutokuwa na hakika na kutofahamu, na hata kuvurugika na kuchanganyikiwa. Hii ni kasoro kubwa zaidi ya mwili. Ingawa ndani ya mioyo yao, watu wanataka kumpenda Mungu, wanampinga kwa sababu ya usumbufu wa Shetani, kwa hiyo mara kwa mara Mungu amegusa mioyo ya watu yenye ganzi na isiyoelewa ili waweze kufufuliwa. Yote ambayo Mungu hufunua ni ubaya wa Shetani, kwa hivyo kadri maneno Yake yalivyo makali zaidi, ndivyo Shetani huaibika zaidi, na ndivyo mioyo ya watu inavyozidi kutofungika, na ndivyo upendo wa watu unavyozidi kuamshwa. Hivi ndivyo Mungu anavyofanya kazi. Kwa sababu Shetani amefunuliwa na kwa sababu ametambuliwa, hathubutu tena kumiliki mioyo ya watu, na hivyo malaika hawasumbuliwi tena. Ni kwa njia hii ndio wanampenda Mungu kwa moyo na akili zao zote. Ni wakati huo tu ndipo wanaonyesha kwamba tabia zao za kweli ni za Mungu na kumpenda Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio wanaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. "Ndani ya nyoyo zao, wametengeneza mahali kwa ajili Yangu. Sitakumbana tena na chuki na kukataliwa miongoni mwa wanadamu, kwani kazi Yangu kubwa imekwisha tekelezwa, na haizuiliwi tena." Hiki ni kidokezo cha yale yaliyoelezwa hapo juu. Kwa sababu ya usumbufu wa Shetani, watu hawawezi kupata wakati wa kumpenda Mungu, daima wao hutatizwa na mambo ya ulimwengu, na wanadanganywa na Shetani kiasi kwamba wanatenda wakiwa wamechanganyikiwa. Hii ndiyo maana Mungu amesema kuwa wanadamu "wameyapitia matatizo mengi sana ya maisha, dhuluma nyingi sana kutoka kwa ulimwengu, mema na mabaya mengi ya ulimwengu, lakini sasa huishi katika nuru Yangu. Je, ni nani ambaye halii kwa ajili ya dhuluma za jana?" Baada ya watu kusikia maneno haya wanahisi kama kwamba Mungu ni mwenzao katika taabu, Anasikitika nao, na wakati huo Anamwelezea wazi mwanadamu matatizo Yake. Wanahisi ghafla maumivu ya ulimwengu wa binadamu na kufikiri: "Je, hiyo si kweli—Sijawahi kufurahia chochote duniani. Tangu nitoke tumboni mwa mama yangu hadi sasa nimepitia maisha ya binadamu na sijawahi kupata kitu chochote, lakini nimeteseka sana. Ni tupu kwa kweli! Na sasa nimepotoshwa sana na Shetani! Oh! Ikiwa si kwa ajili ya wokovu wa Mungu, wakati wa kifo changu unapokuja sitakuwa nimeishi maisha yangu yote bure? Je, Kuna maana yoyote kwa maisha ya binadamu? Si ajabu Mungu alisema kuwa kila kitu chini ya jua ni tupu. Kama Mungu hangenipa nuru leo ningekuwa bado niko gizani.Inasikitisha sana!" Wanapofikiri juu ya jambo hili wanazingatia kiasi katika moyo wao: "Ikiwa siwezi kupata ahadi ya Mungu nitawezaje kuendelea kuwa na uzoefu wa maisha?" Kila mtu anayesoma maneno haya atakuwa na kilio kizuri katika sala. Hii ni saikolojia ya binadamu. Ikiwa unasema kuwa mtu angeweza kusoma hili na asiwe na jibu lolote, hilo haliwezekani kabisa isipokuwa awe na ugonjwa wa akili. Mungu hufunua hali za kila aina ya watu kila siku. Wakati mwingine Yeye hutoa malalamiko kwa niaba yao. Wakati mwingine Huwasaidia watu kushinda na kupitia mazingira fulani. Wakati mwingine Anawaelezea watu migeuzo yao. La sivyo, watu hawangejua jinsi maisha yao yalivyo makubwa. Wakati mwingine Mungu huonyesha uzoefu wa watu kwa uhalisi, na wakati mwingine Huonyesha upungufu na makosa yao. Wakati mwingine Hutoa matakwa mapya kutoka kwao, na wakati mwingine Huonyesha kiwango cha kumwelewa Yeye. Hata hivyo, Mungu amesema pia: "Nimesikia maneno yaliyozungumzwa kutoka kwa moyo na watu wengi, visa vilivyosimuliwa na watu wengi sana juu ya matukio machungu ya mateso; Nimeona wengi sana, katika dhiki kubwa sana, wakinipa utiifu wao bila kukosa, na kuona wengi sana, walipopitia kwenye shida, wakipambana kutafuta suluhisho " Haya ni maelezo ya wahusika wa kujenga. Katika kila tukio la "tamthilia ya historia" kumekuwa na wahusika wa kujenga na vilevile wahusika hasi, kwa hiyo baada ya hili, Mungu amefichua pia ubaya wa wahusika hasi. Kwa njia hii, ni kupitia tu kutofautisha kwa "wasaliti" ndio uaminifu usiokubali kushindwa na ujasiri usio na hofu wa "wanadamu wenye haki" unafichuliwa. Katika maisha ya watu wote kuna vipengele hasi na, bila ubaguzi, vipengele vya kujenga. Mungu hufichua ukweli juu ya watu wote kutoka katika mambo haya mawili ili wasaliti wainamishe vichwa vyao na kukubali dhambi zao, na ili watu wenye haki wataendelea kuwa waaminifu chini ya himizo. Maana inayodokezwa ya maneno ya Mungu ni ya kina kirefu sana. Wakati mwingine, watu huangua kicheko baada ya kuyasoma na wakati mwingine, huinamisha vichwa vyao na kunyamaza. Wakati mwingine wanakumbuka, wakati mwingine wanalia kwa uchungu na kukiri dhambi zao, wakati mwingine wao hututusa, na wakati mwingine wanatafuta. Kwa jumla, kuna mabadiliko katika mijibizo ya watu kwa sababu ya usuli tofauti kwa maneno ya Mungu. Wakati mtu anasoma maneno ya Mungu, wakati mwingine watazamaji wanaweza hata kuamini kwa makosa kwamba mtu huyo ni mgonjwa wa akili. Unaweza kuangalia: "Na kwa hivyo, migogoro yenye ubishi haipo tena, na, kufuatia maneno yanayotoka Kwangu, baadhi ya 'silaha' za enzi ya kisasa zimeondolewa pia." Neno "silaha" ni utani wa kutosha kwako kwa siku nzima, na bila kutambua, wakati watu wanafikiria kuhusu "silaha" watacheka kwa siri. Sivyo? Yawezekana kuwa hungecheka kwa sababu ya hili?
Unapocheka, usisahau kuelewa matakwa ya Mungu kwa wanadamu, na usisahau kuona hali halisi za kanisa: "Binadamu wote wamerudia hali yao ya kawaida na kuanza maisha mapya. Wakiishi katika mazingira mapya, idadi kubwa ya watu huangalia kandokando yao, wakihisi kana kwamba wameingia katika ulimwengu mpya kabisa, na kwa sababu ya hili wanashindwa kubadilika mara moja katika mazingira yao ya sasa ama kushika njia nyofu." Hizi ni hali halisi za sasa za kanisa. Usiwe na hamu sana kuwafanya watu wote waingie mara moja kwenye njia sahihi. Kazi ya Mungu itakapokuwa imeendelea hadi hatua fulani, watu wote wataingia ndani yake bila kutambua. Unapofahamu kiini cha maneno ya Mungu, utajua Roho Wake amefanya kazi hadi hatua gani. Mapenzi ya Mungu ni: "Mimi husimamia tu, kulingana na matendo yake dhalimu, kipimo mwafaka cha 'elimu,' bora zaidi ili kumwezesha kila mtu kushika njia nyofu." Hii ndio mbinu ya Mungu ya kuzungumza na kufanya kazi, na pia ni njia maalum ya mazoezi kwa binadamu. Baada ya hili, Aliwaashiria watu hali nyingine za wanadamu: "Kama wanadamu hawataki kufurahia upeo wa furaha iliyo ndani Yangu, Ninaweza tu kukubaliana na uchu wao na kuwatupa kuzimu." Mungu alinena kwa ukamilifu na kuwaacha watu bila fursa hata kidogo ya kulalamika. Hii hasa ni tofauti iliyopo kati ya Mungu na mwanadamu. Daima Mungu huzungumza kwa mwanadamu waziwazi na kwa uhuru. Uaminifu Wake unaweza kuonekana katika kila mojawapo ya maneno Yake, kuwafanya watu wajiweke katika hali ambayo Yumo na pia kuwafanya wawe na uwezo wa "kuonyesha hisia zao wazi" ili Mungu aone ni rangi gani ya upinde wa mvua. Mungu hajawahi kusifu imani mtu au upendo wa mtu yeyote, lakini daima Ametoa matakwa kwa watu na kufunua ubaya wao. Hii inaonyesha "kimo" kidogo walicho nacho watu na jinsi "katiba" yao ilivyo na upungufu. Wanahitaji kupata "mazoezi" zaidi ili kufidia mapungufu hayo, ndiyo maana daima Mungu huwakasirikia watu. Siku moja ambapo Mungu atafunua ukweli wote kuhusu wanadamu, watu watakamilishwa, na Mungu atastarehe. Watu hawatamdanganya Mungu tena na Yeye "Hatawaelimisha" tena. Kuanzia hapo na kuendelea, watu wataweza "kuishi peke yao," lakini huu si wakati. Bado kuna mengi ambayo ni "bandia" ndani ya watu hivyo wanahitaji uchunguzi mara kadhaa na "vituo vya ukaguzi" zaidi kuanzishwa ili "ushuru" wa wanadamu uweze kulipwa katika kila kituo cha ukaguzi. Ikiwa bado kuna bidhaa bandia, basi zitatwaliwa na haziwezi kuuzwa, na kisha bechi hilo la bidhaa za magendo litaharibiwa. Je, hilo si jambo jema kufanya?
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni