Mwenyezi Mungu anasema, "Leo, wote wako tayari kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua tabia ya Mungu, lakini hakuna anayejua kwa nini hawezi kufuata matamanio yake, hajui kwa nini moyo wake daima humsaliti, na kwa nini hawezi kutimiza kile anachotaka. Kwa hiyo, yeye anakabiliwa tena na hali mbaya ya kukata tamaa, lakini pia anaogopa. Asiweze kuonyesha hisia hizi zinazopingana, anaweza tu kuonyesha huzuni na kuendelea kujiuliza: Je, inaweza kuwa Mungu hajanipa nuru?
Inaweza kuwa Mungu ameniacha kwa siri? Pengine wengine wote wako sawa, na Mungu amewapa wote nuru isipokuwa mimi. Kwa nini daima mimi husikia kusumbuliwa wakati ninasoma maneno ya Mungu, kwa nini siwezi kuelewa chochote? Ingawa akili za watu hufikiri mambo haya, hakuna mtu anayethubutu kuyaonyesha; wao huendelea tu kupambana kwa ndani. Kwa kweli, hakuna mtu ila Mungu anayeweza kuelewa maneno Yake au kufahamu mapenzi Yake ya kweli. Hata hivyo daima Mungu huwataka watu waweze kufahamu mapenzi Yake—je, huku si kama kujaribu kumpeleka bata kwenye kitulio cha ndege? Je, Mungu hajui kasoro za mwanadamu? Haya ndiyo makutano ya kazi ya Mungu, ni kile ambacho watu hawaelewi, na hivyo Mungu anasema, "Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani." Kulingana na maneno ya Mungu na kile Anachotaka kutoka kwa mwanadamu, hakuna mtu atakayeokoka, kwa maana hakuna chochote katika mwili wa mwanadamu kinachoyakubali maneno ya Mungu, kwa hiyo kama watu wanaweza kutii maneno ya Mungu, kutunza kwa upendo na kutamani sana maneno ya Mungu, na kutumia maneno hayo katika matamshi ya Mungu yanayoonyesha hali za binadamu kwa hali zao wenyewe, na hivyo kujijua, basi hiki ndicho kiwango cha juu zaidi. Wakati ufalme utafanikishwa hatimaye, wale wanaoishi katika mwili bado watakuwa hawawezi kufahamu mapenzi ya Mungu, na bado watahitaji uongozi wa Mungu Mwenyewe. Ni kwamba tu watu hawataingiliwa na Shetani, na watakuwa na maisha ya kawaida ya mwanadamu, ambalo ni lengo la Mungu katika kumshinda Shetani, na hasa ni kwa ajili ya kupata tena kiini cha asili cha mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu. Katika mawazo ya Mungu, "mwili" unahusu mambo yafuatayo: kutoweza kujua asili ya Mungu, kutoweza kuona mambo ya ufalme wa kiroho, na, zaidi ya hayo, uwezo wa kupotoshwa na Shetani lakini pia kuelekezwa na Roho wa Mungu. Hiki ni kiini cha mwili ulioumbwa na Mungu. Kwa kawaida, pia ni ili kuepuka machafuko yanayosababishwa na ukosefu wa utaratibu katika maisha ya wanadamu. Mungu anavyozidi kunena, na maneno Yake yanavyozidi kuwa makali, ndivyo watu huyaelewa maneno Yake zaidi. Watu hubadilika bila kujua, na wanaishi katika nuru bila kujua, na hivyo "Kwa sababu ya nuru, watu wote wanakua, na wameliacha giza." Haya ndiyo mandhari mazuri ya ufalme, nayo ni kama kile kilichozungumziwa mara nyingi hapo zamani: "kuishi katika nuru, kuondoka kwa kifo." Wakati Sinim inapofanikishwa duniani—wakati ufalme unapofanikishwa—hakutakuwa na vita tena duniani, hakutakuwa tena na njaa, tauni, na zilizala, watu wataacha kutengeneza silaha, wote wataishi kwa amani na utulivu, na watu pamoja na nchi wataingiliana kwa kawaida. Hata hivyo wakati uliopo haulinganishwi na hili. Yote chini ya mbingu yako katika machafuko, mapinduzi yanaanza hatua kwa hatua katika kila nchi. Mungu anapotamka sauti Yake watu wanabadilika hatua kwa hatua, na, kwa ndani, kila nchi inaharibika polepole. Misingi imara ya Babiloni inaanza kutetemeka, kama kasri linalofika mbinguni, na kama mapenzi ya Mungu yanavyobadilika, mabadiliko makubwa yanatokea ulimwenguni bila kutambuliwa, na kila aina ya ishara zinaonekana wakati wowote, zikiwaonyesha watu kuwa siku ya mwisho ya dunia imewadia! Huu ni mpango wa Mungu, hizi ni hatua ambazo kwazo Yeye anafanya kazi, na hakika kila nchi itapasuka vipande vipande, Sodoma ya kale itaangamizwa mara ya pili, na hivyo Mungu anasema "Dunia inaanguka! Babeli imelemaa!" Hakuna mtu ila Mungu Mwenyewe anayeweza kufahamu jambo hili kabisa; kuna, hata hivyo, kikomo kwa ufahamu wa watu. Kwa mfano, mawaziri wa masuala ya ndani wanaweza kujua kwamba hali za sasa si imara na kuna machafuko, lakini hawawezi kuzishughulikia. Wanaweza tu kuvumilia, wakitaraji mioyoni mwao siku ambayo wanaweza kuwa na ujasiri, wakitamani kwamba siku itakuja wakati jua litachomoza tena upande wa mashariki, likiangaza kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa nchi na kugeuza hali hii ya kusikitisha ya mambo. Hawajui hata kidogo, hata hivyo, kwamba wakati jua linapochomoza kwa mara ya pili, sio kwa ajili ya kurejesha utaratibu wa kale, ila ni kurudi tena na nguvu mpya, na kuleta mabadiliko kamili. Huo ndio mpango wa Mungu kwa ulimwengu wote. Yeye atasababisha ulimwengu mpya, lakini zaidi ya yote, Atamfanya mwanadamu upya kwanza. Leo, kuwaleta watu katika maneno ya Mungu ndilo lililo muhimu, sio tu kuwakubalia kufurahia baraka za hadhi. Zaidi ya hayo, kama Mungu anavyosema, "Katika ufalme, Mimi ni Mfalme—lakini badala ya kunichukulia kama Mfalme, mwanadamu ananichukulia kama Mwokozi aliyeshuka kutoka mbinguni. Kwa sababu hii, anasubiri kwa hamu Nimpe sadaka, na hafuatilii ufahamu Wangu." Hizo ni hali halisi za watu wote. Leo, jambo muhimu ni kuondoa kabisa ulafi wa mwanadamu, hivyo kuwapa watu fursa ya kumjua Mungu bila kuomba chochote; si ajabu, basi, kwamba Mungu anasema, "Wengi sana wamelia mbele Zangu kama waombaji; wengi pia wamenifungulia 'mifuko' yao na kunisihi Niwape chakula ili waendelee kuishi." Hizi hali mbalimbali zinaonyesha ulafi wa watu, na huonyesha kwamba watu hawampendi Mungu lakini humdai Mungu, au labda hujaribu kupata vitu wanavyotamani sana. Watu wana asili ya mbwa mwitu mwenye njaa, wote ni wajanja na walafi, na hivyo Mungu hutoa mahitaji kwao mara kwa mara, Akiwalazimisha kutoa ulafi katika nyoyo zao na kumpenda Mungu kwa uaminifu. Kwa kweli, hadi leo, bado watu hawajampa Mungu mioyo yao yote, hawajakata shauri bado, wakati mwingine wakijitegemea, wakati mwingine wakimtegemea Mungu bila kumwamini Mungu kabisa. Wakati kazi ya Mungu inapofikia hatua fulani, watu wote wataishi katikati ya upendo na imani ya kweli, na mapenzi ya Mungu yatatimizwa; hivyo, mahitaji ya Mungu sio makubwa.
Malaika daima huenda miongoni mwa wana na watu wa Mungu, wakiharakisha kati ya mbingu na dunia na kushuka kwa ulimwengu wa binadamu baada ya kurejea kwa ulimwengu wa kiroho kila siku. Huu ni wajibu wao, na hivyo kila siku wana na watu wa Mungu huchungwa, na maisha yao hubadilika hatua kwa hatua. Siku ambayo Mungu atabadilisha umbo Lake, kazi ya malaika duniani itakamilika rasmi na watarudi kwenye ulimwengu wa mbinguni. Leo, wana na watu wa Mungu wote wako katika hali sawa. Kadri sekunde zinavyopita, watu wote wanabadilika, na wana na watu wa Mungu wanakomaa zaidi hatua kwa hatua. Kwa ulinganishi, waasi wote pia wanabadilika mbele ya joka kubwa jekundu: Watu si watiifu tena kwa joka kubwa jekundu, na pepo hawafuati tena mipango yake. Badala yake "watu wote anaendesha shughuli zake, wakichukua njia inayowafaa zaidi." Hivyo wakati Mungu anasema, "Je, mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuangamia? Mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuanguka?" Mbingu zinaanguka kwa kishindo na kwa haraka.... Ni kama kwamba kuna hisia ya kuogofya inayoashiria mwisho wa wanadamu. Ishara mbalimbali za kuogofya zilizotabiriwa hapa hasa ndilo linalotendeka katika nchi ya joka kubwa jekundu, na hakuna hata mmoja kati ya walio duniani anaweza kuepuka. Hilo ndilo linalotabiriwa katika maneno ya Mungu. Katika jakamoyo za watu leo, wanahisi kuwa muda ni mfupi, na wanaonekana kuhisi kuwa msiba unakaribia kuwafika—lakini hawana njia ya kutoroka, na hivyo wote hawana matumaini. Mungu anasema, "Ninapokipamba 'chumba cha ndani' cha ufalme Wangu siku baada ya siku, hakuna yule ameingia katika 'chumba Changu cha kazi' kwa ghafla ili kuvuruga kazi Yangu." Kwa kweli, maana ya maneno ya Mungu hayajajikita tu katika kuwafanya watu wamjue Mungu katika maneno Yake. Zaidi ya yote, yanaonyesha kuwa kila siku Mungu hupanga kila aina ya maendeleo kotekote ulimwenguni ili kutumikia sehemu inayofuata ya kazi Yake. Madhumuni ya Yeye kusema "Hakuna yule ameingia katika 'chumba Changu cha kazi' kwa ghafla ili kuvuruga kazi Yangu." ni kwa sababu Mungu hufanya kazi katika uungu, na ingawa watu wanaweza kutaka, hawawezi kushiriki katika kazi Yake. Ningependa kuuliza: Je, unaweza kuyapanga maendeleo yote ya ulimwengu wote? Je, unaweza kuwafanya watu wa dunia kuwakataa mababu zao? Je, unaweza kuwashawishi watu ulimwenguni kote wayatumikie mapenzi ya Mungu? Je, unaweza kumfanya Shetani afanye fujo? Unaweza kuwafanya watu wahisi kwamba dunia ni yenye ukiwa na tupu? Watu hawawezi kufanya mambo kama haya. Zamani, wakati "ujuzi" wa Shetani ulipokuwa bado haujajitokeza kwa ukamilifu, kila mara Shetani angeingilia kila hatua ya kazi ya Mungu; katika hatua hii, Shetani ameishiwa na hila, na hivyo Mungu humruhusu Shetani kuonyesha tabia yake ya kweli ili watu wote waweze kumjua. Huu ndio ukweli wa maneno "Hakuna mtu aliyewahi kuivuruga kazi Yangu."
Kila siku, watu wa makanisa husoma maneno ya Mungu, kila siku wao huchanguliwa kwenye meza ya upasuaji. Kwa mfano, maneno ya dhihaka kama vile "kupoteza nafasi zao" "kufukuzwa," "hofu yao kutoweka na hali tulivu kurejea." "kutelekeza," kutokuwa na "hisia" na kadhalika huwaacha wakiwa wamenyamaa kwa kuaibika; ni kama kwamba hakuna sehemu ya mwili wao wote—kutoka kichwani hadi wayoni, kutoka ndani hadi nje—inakubaliwa na Mungu. Kwa nini maneno ya Mungu huvua maisha ya watu kuwa wazi hivyo? Je, Mungu anafanya mambo kuwa magumu kwa watu kwa makusudi? Ni kama kwamba nyuso za watu wote zimepakwa matope ambayo hayawezi kuoshwa. Wakiwa wameinamisha vichwa vyao, kila siku wao hutoa maelezo ya dhambi zao kama kwamba ni wasanii wa kashfa. Watu wamepotoshwa na Shetani kiasi kwamba hawana ufahamu kamili wa hali zao ya kweli. Lakini kwa Mungu, sumu ya Shetani iko katika kila sehemu ya miili yao, hata katika uboho wa mifupa yao; kwa hiyo, kadri ufunuo wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo watu wanavyozidi kuwa na hofu. Hivyo, watu wote wanaweza kumjua Shetani na kumwona Shetani ndani ya mwanadamu, kwa kuwa hawajaweza kumwona Shetani kwa macho yao. Na kwa kuwa yote yameingia katika uhalisi, Mungu anafunua asili ya mwanadamu—ambalo ni kusema, Anaifunua sura ya Shetani—na hivyo Anamruhusu mwanadamu kumwona Shetani aliye wa kweli na dhahiri, ambalo linaweza kuwasaidia kumjua Mungu wa vitendo vizuri zaidi. Mungu humruhsu mwanadamu kumjua Yeye katika mwili, na humpa umbo Shetani, hivyo Anamruhusu mwanadamu kumjua Shetani aliye wa kweli na dhahiri katika mwili wa watu wote. Hali hizi mbalimbali ni udhihirisho wa matendo ya Shetani. Na kwa hiyo, ni haki kusema kwamba wote ambao ni wa mwili ni mfano halisi wa umbo la Shetani. Kwa sababu Mungu halingani na adui Zake, kwa sababu wao wanachukiana, nao ni majeshi mawili tofauti, pepo ni pepo, Mungu ni Mungu, wao hawalingani kama moto na maji, na daima wametengana kama mbingu na dunia. Wakati Mungu alimuumba mwanadamu, aina moja ya watu walikuwa roho za malaika; aina moja haikuwa na roho, hivyo walimilikiwa na roho za pepo, na hivyo wanaitwa pepo. Hatimaye, malaika ni malaika, pepo ni pepo—na Mungu ni Mungu. Hii ndiyo maana ya kila mmoja kuainishwa kulingana na aina, na kwa hiyo wakati malaika wanatawala duniani na kufurahia baraka, Mungu anarudi kwenye makao Yake, na wengine—maadui wa Mungu—wanageuzwa kuwa majivu. Kwa kweli, nje, watu wote wanampenda Mungu—lakini asili yake iko katika kiini chao; ni vipi ambavyo wale walio na asili ya malaika wanaweza kuepuka mkono wa Mungu na kuanguka kuzimu? Na ni vipi ambavyo wale walio na asili ya pepo wanaweza kumpenda Mungu kweli? Kwa kweli, watu hawa hawampendi Mungu kweli, kwa hiyo wangewezaje kuwa na nafasi ya kuingia katika ufalme? Yote yalipangwa na Mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kama vile Mungu anavyosema, "Mimi naendelea kati ya upepo na mvua, na nimeishi mwaka baada ya mwingine miongoni mwa wanadamu, na hiyo inafuatwa na wakati wa sasa. Je, hizi sio hatua za mpango Wangu wa usimamizi? Ni nani amewahi kuongeza chochote katika mpango Wangu? Ni nani anaweza kuepuka hatua katika mpango Wangu?" Baada ya kuwa mwili, lazima Mungu apitie maisha ya mwanadamu, na je, huu sio upande wa kweli wa Mungu wa vitendo? Mungu hafichi chochote kutoka kwa mwanadamu kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu; badala yake, Yeye huuweka wazi ukweli kwa mwanadamu, kama vile Mungu anavyosema, "Nimekaa mwaka baada ya mwaka kati ya wanadamu." Ni kwa sababu Mungu ni Mungu aliyepata mwili ndio Amepitia mwaka baada ya mwaka duniani; kwa hiyo, baada ya kupitia tu michakato ya aina zote ndio Anaweza kuchukuliwa kuwa Amepata mwili, baada ya hapo tu ndio Anaweza kufanya kazi katika uungu ndani ya mwili. Na kisha, baada ya kufichua siri zote tu ndio Atabadilisha umbo Lake. Haya ni maelezo ya mpokezano ya "kutokuwa wa miujiza," na yanafunzwa moja kwa moja na Mungu.
Lazima watu wapite mtihani wa kila neno la maneno ya Mungu, bila uzembe—hili ni agizo la Mungu!"
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni