Jumanne, 4 Juni 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 79


Mwenyezi Mungu anasema, “Vipofu! Wajinga! Rundo la takataka lisilo na maana! Nyinyi hutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu Wangu! Je, hamfikiri kuwa hii ni dhambi dhidi Yangu? Na zaidi ni kuwa ni kitu ambacho ni vigumu kusamehe! Mungu wa vitendo anakuja miongoni mwenu leo lakini mwajua tu upande Wangu mmoja ambao ni ubinaamu Wangu wa kawaida, na hamjaona kabisa upande Wangu ambao ni wa kiungu kabisa. Je, unafikiri kuwa Sijui anayejaribu kunidanganya kisirisiri? Sikukosoi sasa, ila tu kutazama ni kiwango gani ambacho unaweza kufikia na hatima yako itakavyokuwa. Maneno Yangu yamesemwa kwa maelfu na ninyi mmetenda mambo mengi mabaya. Kwa nini ninyi hujaribu kunidanganya tena na tena? Tahadhari kuhusu kupoteza maisha yako! Iwapo utachochea hasira Yangu kwa kiwango fulani basi Sitakuonyesha huruma na Nitakufukuza. Sitatazama jinsi ulivyokuwa hapo awali, iwapo ulikuwa mwaminifu au mwenye shauku, ni kiasi gani umejishugulisha, ni kiasi gani umetoa rasilmali kwa ajili Yangu—Sitatazama mambo haya hata kidogo. Unahitaji tu kunichokoza hivi sasa na Nitakutupa katika kuzimu. Nani bado anathubutu kujaribu kunidanganya? Kumbuka hili! Kuanzia sasa Ninapokasirika, bila kujali ni nani, Nitakutokomeza mara moja ili kwamba kusiweko na taabu ya siku za baadaye na ili Nisiweze kukuona tena. Ukiniasi Nitakuadibu mara moja—Je, mtakumbuka hili? Wale ambao ni werevu watatubu mara moja.
Leo, yaani sasa, Mimi ni mwenye ghadhabu. Ninyi nyote lazima muwe waaminifu Kwangu, na kutoa nafsi yako yote kwangu. Hakuwezi kuwa na kukawia tena. Usipoyasikiza maneno Yangu Nitaunyosha mkono Wangu na kukupiga. Kutokana na hili Nitamfanya kila mtu anijue, na leo Mimi ni mwenye ghadhabu na uadhama kwa vyote (hii ni kali zaidi kuliko hukumu Yangu). Nimesema maneno mengi sana lakini ninyi hamjaonyesha hisia kabisa; je, ninyi ni wapumbavu sana? Sidhani ninyi ni wapumbavu, au siyo? Ni ibilisi wa zamani ndani yenu anayetekeleza utundu—je, mnaona hili kwa uwazi? Fanyeni hima ili kuleta mabadiliko ya kimsingi. Leo, kazi ya Roho Mtakatifu imesonga kufikia hatua hii—Je, ninyi hamjaliona hilo? Jina Langu litaenea nyumba hadi nyumba katika mataifa yote na katika pande zote na litatangazwa kutoka kwenye vinywa vya watu wazima na watoto vilevile katika ulimwengu wa dunia; huu ni ukweli mtupu. Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, hata zaidi Mimi ni nafsi moja na ya pekee ya Mungu, na Mimi, ukamilifu wa mwili, ni hata zaidi dhihirisho kamili la Mungu. Yeyote anayethubutu kutonicha, yeyote anayethubutu kunionyesha uasi katika macho yake, yeyote anayethubutu kuyasema maneno ya uasi dhidi Yangu hakika atakufa kutokana na laana Yangu na ghadhabu (kutakuwa na kulaani kwa sababu ya ghadhabu Yangu). Na yeyote anayedhubutu kutokuwa mwaminifu au na upendo Kwangu, yeyote anayethubutu kujaribu kunifanyia hila hakika atakufa katika chuki Yangu. Haki Yangu, uadhama na hukumu vitadumu milele na milele. Mwanzoni, Nilikuwa mwenye upendo na rehema, lakini hii si tabia ya uungu Wangu kamili; haki, uadhama na hukumu ni tabia Yangu tu—Mungu Mwenyewe mkamilifu. Wakati wa Enzi ya Neema Nilikuwa mwenye upendo na rehema. Kwa sababu ya kazi Niliyopaswa kumaliza Nilikuwa na fadhila na rehema, lakini baadaye hakukuwa na haja ya fadhila yoyote au rehema (hakujakuwepo na yoyote tangu wakati huo). Yote ni haki, uadhama na hukumu na hii ni tabia kamili ya ubinadamu Wangu wa kawaida pamoja na uungu Wangu kamili.
Wale ambao hawanijui wataangamia katika kuzimu na wale ambao wana uhakika kunihusu wataishi milele, ili watunzwe na kulindwa ndani ya upendo Wangu. Mimi husema neno moja na ulimwengu hutetemeka kutoka mwisho mmoja hadi mwIngine—ni nani anayeweza kusikia maneno Yangu na asitetemeke kwa hofu? Nani hawezi kukuza moyo ambao unanicha? Nani hawezi kujua haki Yangu na uadhama kutokana na matendo Yangu? Na nani hawezi kuona uweza Wangu na hekima ndani ya matendo Yangu? Yeyote atakayekosa kujichunga kwa hakika atakufa. Hii ni kwa sababu wale ambao hawajali ni wale ambao wananiasi, ambao hawanijui, na wao ni malaika wakuu, washenzi zaidi. Jiangalieni wenyewe—yeyote aliye mshenzi, mwenye majisifu, mwenye kiburi hakika ni mlengwa wa chuki Yangu na ataangamia!
Sasa Natamka amri za utawala wa ufalme Wangu: Vitu vyote vimo ndani ya hukumu Yangu, vitu vyote vimo ndani ya haki Yangu, vitu vyote vimo ndani ya uadhama Wangu, na haki inatendwa kwa wote. Wale ambao husema wananiamini Mimi ilhali wananipinga mioyoni mwao, au ambao mioyo yao imeniacha watafukuzwa, lakini yote ni kwa wakati Wangu mzuri. Wale ambao huzungumza kwa kejeli kunihusu, lakini kwa njia ambayo watu hawatambui, watakufa mara moja (watafariki katika roho, mwili na nafsi). Kwa wale ambao huwadhulumu ama kuwadharau wale Ninaowapenda, ghadhabu Yangu itawahukumu mara moja. Hii ni kusema kwamba wale ambao wana mioyo ya wivu kwa wale Ninaowapenda na kufikiri kuwa Mimi si mwenye haki watakabidhiwa kwa wale ambao Ninawapenda ili kuwahukumu. Wale wote wenye tabia nzuri, wanyenyekevu (pamoja na wale ambao hawana hekima) na ambao ni watiifu kwa dhati Kwangu watabaki wote katika ufalme Wangu. Wale ambao hawajapitia katika mafunzo, kumaanisha watu ambao ni waaminifu wanaokosa hekima na ufahamu, watakuwa na uwezo katika ufalme Wangu. Hata hivyo wao pia wamepitia ushughulikiwaji na kuvunjwa. Kwamba hawajapitia mafunzo si hakika, lakini badala yake kupitia mambo hayo Nitaonyesha kila mtu uweza Wangu na hekima Yangu. Nitawafukuza wale ambao bado wananishuku sasa, Sitaki hata mmoja wao (Ninawachukia sana wale ambao bado hunituhumu wakati kama huu). Kwa matendo ambayo Mimi hufanya katika ulimwengu wote, Nitawaonyesha watu waaminifu matendo Yangu ya kustaajabisha, papo kukuza busara zao, ufahamu na utambuzi, na Mimi mara moja Nitasababisha watu wadanganyifu kuharibiwa kwa ajili ya matendo Yangu ya kustaajabisha. Wazaliwa wote wa kwanza waliokuwa wa kwanza kulikubali jina Langu (kumaanisha wale watakatifu wasio na dosari, watu waaminifu) watakuwa wa kwanza kuingia katika ufalme na kutawala mataifa yote na watu wote pamoja na Mimi, kutawala kama wafalme katika ufalme na pamoja kuhukumu mataifa yote na watu wote (kumaanisha wazaliwa wote wa kwanza katika ufalme, na sio wengine). Wale walio katika mataifa yote na watu wote ambao wamekwisha kuhukumiwa na wametubu wataingia katika ufalme Wangu na kuwa watu Wangu, na wale ambao ni wakaidi na wasiotubu watatupwa katika shimo la kuzimu (ili waangamie milele). Hukumu katika ufalme itakuwa mara ya mwisho na itakuwa utakaso Wangu kwa kina duniani. Hakutakuwa tena na udhalimu wowote, huzuni yoyote, machozi yoyote na hata zaidi hakutakuwa na dunia. Kila kitu kitakuwa dhihirisho la Kristo, kila kitu kitakuwa ufalme wa Kristo. Utukufu ulioje! Utukufu ulioje!”
Chanzo: Sura ya 79
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni