Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Sita
Miongoni mwa maneno haya yote, hakuna yasiyoweza kusahaulika zaidi kama yale ya leo. Awali maneno ya Mungu yalifichua hali za mwanadamu au siri za mbinguni, lakini tamko hili halifanani na yale ya wakati uliopita. Halidhihaki wala kufanya mzaha, lakini ni kitu kisichotarajiwa kabisa: Mungu aliketi chini na Akazungumza na watu kwa utulivu. Kusudi Lake ni gani? Unaona nini Mungu anaposema, “Leo, Nimeanza kazi mpya juu ya ulimwengu. Nimewapa watu walio duniani mwanzo mpya, na Nimewaambia wote watoke nyumbani Mwangu. Na kwa kuwa kila mara watu hupenda kujideka, Nawashauri wajijue, na wasiisumbue kazi Yangu kila mara”? Ni huu "mwanzo mpya" ambao Mungu anazungumzia ni upi?