Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neno Laonekana-katika-Mwil. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neno Laonekana-katika-Mwil. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 5 Septemba 2018

Tamko la Mia moja na Kumi na Nne

Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, furaha

Tamko la Mia moja na Kumi na Nne

Niliumba ulimwengu dunia; Nilitengeneza milima, mito, na vitu vyote; Niliunda miisho ya mifumo ya sayari; Niliwaongoza wana Wangu na watu Wangu; Niliamuru vitu na mambo yote. Sasa, Nitawaongoza wazaliwa Wangu wa kwanza warudi kwenye Mlima Wangu Sayuni, kurudi mahali ambapo Naishi, ambayo itakuwa hatua ya mwisho katika kazi Yangu. Yote ambayo Nimeyatenda (kila kitu kilichofanyika kutoka uumbaji mpaka sasa) yalikuwa kwa sababu ya hatua ya leo ya kazi Yangu, na zaidi ni kwa sababu ya utawala wa kesho, ufalme wa kesho, na kwa ajili ya Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza kuwa na furaha ya milele. 

Jumatatu, 27 Agosti 2018

Tamko la Kumi na Mbili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, ukweli, Kanisa
Tamko la Kumi na Mbili
Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya.

Ijumaa, 24 Agosti 2018

Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Sita

Mwenyezi Mungu, ushuhuda , majaribio

Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Sita

Miongoni mwa maneno haya yote, hakuna yasiyoweza kusahaulika zaidi kama yale ya leo. Awali maneno ya Mungu yalifichua hali za mwanadamu au siri za mbinguni, lakini tamko hili halifanani na yale ya wakati uliopita. Halidhihaki wala kufanya mzaha, lakini ni kitu kisichotarajiwa kabisa: Mungu aliketi chini na Akazungumza na watu kwa utulivu. Kusudi Lake ni gani? Unaona nini Mungu anaposema, “Leo, Nimeanza kazi mpya juu ya ulimwengu. Nimewapa watu walio duniani mwanzo mpya, na Nimewaambia wote watoke nyumbani Mwangu. Na kwa kuwa kila mara watu hupenda kujideka, Nawashauri wajijue, na wasiisumbue kazi Yangu kila mara”? Ni huu "mwanzo mpya" ambao Mungu anazungumzia ni upi?

Jumatano, 22 Agosti 2018

Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini

Mwenyezi Mungu, siku za mwisho, hukumu
Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini
Mungu aliwaumba wanadamu wote, na amewaongoza wanadamu wote mpaka leo. Hivyo, Mungu anajua yote yafanyikayo miongoni mwa wanadamu: Anajua uchungu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, Anaelewa utamu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, na kwa hiyo kila siku Yeye hufafanua hali za maisha za wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, hushughulikia udhaifu na upotovu wa wanadamu wote.

Jumatatu, 13 Agosti 2018

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Umeme wa Mashariki, Roho Mtakatifu, ukweli

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Je, ushawishi wa giza ni nini?
Ushawishi wa giza ni utumwa wa Shetani, ni ushawishi wa Shetani, na ni ushawishi ambao una hali ya kifo.
Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako kwa Mungu kikamilifu, katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa ya Mungu, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya uangalizi na ulinzi wa Mungu. Kama watu hawawezi kutenda maneno ya Mungu, daima wakimpumbaza Mungu na kutenda katika namna ya uzembe na Mungu, bila kuamini katika uwepo wa Mungu, watu kama hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza.