Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu?
Tamko la Themanini na Nne
Kwa sababu ya ukosefu wao wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizo na idadi, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele.