Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo makusudi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo makusudi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 24 Julai 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote. 

Jumatano, 10 Julai 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 94


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, “Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni. Hili linamaanisha kwamba tutarudi kutoka kwa nyama hadi kwa mwili wa awali. Hii ndiyo maana ya kweli ya “kurudi Sayuni.” 

Jumatano, 3 Julai 2019

14. Mungu Anatafuta Wale Walio na Kiu ya Kuonekana Kwake

14. Mungu Anatafuta Wale Walio na Kiu ya Kuonekana Kwake

Mungu huwatafuta wale wanaomtamani, wanaotamani Aonekane.
Mungu huwatafuta wale wasiopinga, watiifu kama watoto mbele Yake.
Mungu hutafuta wale ambao wanaweza, wanaweza kusikia maneno Yake,
wanaokubali yale ambayo Amewaaminia na kutoa moyo wao na mwili Kwake.
Kama hakuna kinachoweza kutikisa, kinachoweza kutikisa kujitoa kwako kwa Mungu,
Atakuangalia, Atakuangalia na fadhila, oo …
Mungu ataweka baraka Zake juu yako, juu yako, oo …
Mungu ataweka baraka Zake juu yako, juu yako!

Ijumaa, 28 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”




Matamshi ya Mungu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Saba”


Mwenyezi Mungu anasema, “Katika furaha na huzuni ya kutengana na kisha kuunganika Kwangu na mwanadamu, hatuwezi kubadilishana mawazo. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejawa na wasiwasi mwingi.

Jumamosi, 11 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 69


Mwenyezi Mungu anasema, “Mapenzi Yangu yatokapo, yeyote anayethubutu kupinga na yeyote anayethubutu kuhukumu au kuwa na shaka, mara moja Nitamfukuza. Leo, yeyote ambaye hatendi kulingana na mapenzi Yangu, au yeyote anayeyafikiria mapenzi Yangu visivyo, ni lazima atupwe nje na kuondolewa kutoka kwa ufalme Wangu. Katika ufalme Wangu hakuna mtu mwingine—wote ni wana Wangu wa kiume, wale ambao Nawapenda na hunifikiria Mimi. 

Ijumaa, 10 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 68


Mwenyezi Mungu anasema, “Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 63


Mwenyezi Mungu anasema, “Zielewe hali zako mwenyewe, na zaidi ya hayo, kuwa wazi kuhusu njia unayohitaji kutembea; usubiri tena Mimi niyainue masikio yako na kukuonyesha mambo. Mimi ni Mungu ninayekagua moyo wa ndani kabisa wa mwanadamu nami najua kila fikra na wazo lako, hata zaidi Naelewa matendo na tabia yako. Lakini matendo yako na tabia yana ahadi Yangu? Je, yana mapenzi Yangu? Umetafuta haya kwa kweli? Je, kweli umetumia wakati wowote kuhusu suala hili? 

Jumatano, 17 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 62


Mwenyezi Mungu anasema, “Kuyaelewa mapenzi Yangu hakufanywi ili tu kwamba uweze kujua, ila pia kwamba uweze kutenda kulingana na nia Yangu. Watu hawauelewi moyo Wangu. Ninaposema huku ni mashariki, wanalazimika kuenda na kutafakari, wakijiuliza, “Kweli ni mashariki? Pengine sio. Siwezi kuamini kwa urahisi hivyo. Nahitaji kujionea mwenyewe.” Ninyi watu ni wagumu sana kushughulikia, na hamjui utii wa kweli ni nini.

Jumatano, 10 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 54

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 54

Ninalielewa kila kanisa kama kiganja cha mkono Wangu. Usifikiri kwamba Siko wazi au sielewi. Ninawaelewa na kuwajua watu wote mbalimbali wa kila kanisa hata zaidi. Ninahisi hisia ya umuhimu kwamba ni lazima Nikufundishe. Nataka nikufanye ukue hadi utu uzima haraka zaidi ili kwamba siku ambayo unaweza kuwa wa msaada Kwangu itakuja haraka zaidi. Nataka vitendo vyenu viwe vimejaa hekima Yangu ili muweze kumdhihirisha Mungu kila pahali. 

Jumapili, 7 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 51


Ee! Mwenyezi Mungu! Amina! Ndani Yako yote yanaachiliwa, yote ni huru, yote ni wazi, yote hufichuliwa, yote hung’aa, bila sitara au maficho yoyote. Wewe ni Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Umetawala kama Mfalme. Umefichuliwa wazi, wewe tena si fumbo lakini Umefichuliwa kabisa milele na milele! Kwa kweli Nimefichuliwa kabisa, Nimefika hadharani, na Nimejitokeza kama Jua la haki kwa kuwa leo si enzi ya kuonekana kwa nyota ya asubuhi tena, si awamu ya sitara tena. Kazi Yangu ni kama mwanga wa umeme, inakamilishwa na wepesi wa ajabu. 

Jumamosi, 6 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 49


Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kutumikia kwa uratibu, mtu lazima ajiunge kwa usahihi, na pia awe mchangamfu na dhahiri. Zaidi ya hayo, mtu lazima awe na uchangamfu, nguvu, na kujawa na imani, ili kwamba wengine waruzukiwe na watakuwa wakamilifu. Kunitumikia Mimi lazima utumikie Ninayonuia, sio tu kuupendeza moyo Wangu, lakini zaidi ya hayo kuridhisha nia Zangu, ili Niridhishwe na kile Ninachotimiza ndani yako. 

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 48


Mwenyezi Mungu anasema, “Mimi nina wasiwasi, lakini wangapi kati yenu wanaweza kuwa na nia moja na mawazo sawa na Mimi? Ninyi hamyasikilizi tu maneno Yangu, mkipuuza kabisa na kushindwa kuyatilia maanani, badala yake mkizingatia tu mambo yenu wenyewe ya juu juu. Mnachukulia kujali Kwangu kwa bidii na juhudi kama jitihada za bure; je, dhamiri yenu haiwahukumu? Ninyi ni wajinga na hamna mantiki; ninyi ni wapumbavu, na hamwezi kuniridhisha kabisa. 

Jumamosi, 30 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 46

Mwenyezi Mungu anasema, “Yeyote anayejitumia na kujitolea kwa uaminifu kwa ajili Yangu, hakika Nitakukinga mpaka mwisho kabisa; mkono Wangu hakika utakushikilia ili kwamba daima una amani na mwenye furaha daima na kila siku una mwanga Wangu na ufunuo. Hakika Nitakupa baraka Zangu mara dufu, ili uwe na kile Nilicho nacho na umiliki kile Nilicho. Kile unachopewa ndani yako ni maisha yako, na hakuna mtu anayeweza kukichukua kutoka kwako. 

Jumatatu, 25 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 43


Matamshi ya Mungu | Sura ya 43

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, Sijawakumbusha? Msiwe wenye hofu; ninyi hamjanisikiliza tu, watu wasio na fikira ninyi! Je, mtaweza kuuelewa moyo Wangu lini? Kila siku kuna nuru mpya, kila siku kuna mwanga mpya. Ni mara ngapi mmeuelewa kwa ajili yenu wenyewe? Je, Sijawaambia Mwenyewe? Bado ninyi ni wa kukaa tu kama wadudu ambao watasonga tu wanaposukumwa, lakini hamwezi kuchukua hatua ya kushirikiana na Mimi, kuufikiria mzigo Wangu. 

Jumamosi, 23 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa | Sura ya 40

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa | Sura ya 40

Kwa nini ninyi ni wa mwendo wa polepole? Kwa nini hamsikii? Makumbusho kadhaa hayajawazindua; hili linanihuzunisha. Kwa kweli Sipendi kuwaona wanangu namna hii. Moyo Wangu unawezaje kustahimili hili? Ah! Lazima Niwafundishe kwa mkono Wangu mwenyewe. Mwendo Wangu unaendelea kuwa wa kasi. Wanangu! Inukeni haraka na mshirikiane na Mimi. Nani wanajitumia kwa dhati kwa ajili Yangu sasa? Ni nani anayeweza kujitolea kikamilifu bila malalamiko hata kidogo? 

Alhamisi, 21 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 39

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 39

Fungua macho yako na uangalie na unaweza kuona nguvu Zangu kuu kila mahali! Unaweza kuwa na uhakika na Mimi kila mahali. Ulimwengu na anga unaeneza nguvu Zangu kuu. Maneno ambayo Nimenena yametimia katika ongezeko la joto la hali ya hewa, mabadiliko ya hali ya hewa, vioja vya watu, ulemavu wa elimumwendo ya kijamii, na udanganyifu wa mioyo ya watu. Jua linakuwa jeupe na mwezi unakuwa mwekundu; Yote yako katika machafuko. Je, bado huoni haya?

Ijumaa, 8 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 109

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 109
Ninatoa matamko kila siku, kuzungumza kila siku, na kufichua ishara Zangu kuu na shani kila siku. Haya yote ni kazi ya Roho Wangu. Machoni pa watu Mimi ni mwanadamu tu, lakini hasa ni katika mwanadamu huyu ndipo Ninafichua vyote Vyangu na nguvu Yangu kuu.
Kwa kuwa watu humpuuza mwanadamu Niliye na huyapuuza matendo Yangu, wanafikiri kuwa hivi ni vitu ambavyo hufanywa na wanadamu. 

Jumamosi, 2 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 93

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mungu | Sura ya 93

Ukweli unatimizwa mbele ya macho ya mtu na mambo yote yametimizwa. Kazi Yangu inapata hatua, ikipanda juu kama roketi iliyofyatuliwa, ambayo hakuna mtu aliwahi kutarajia. Ni baada ya vitu kufanyika ndipo mtaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu. Watoto wa joka kubwa jekundu si wa pekee na lazima wafanywe kushuhudia matendo Yangu ya ajabu kwa macho yao wenyewe. Usidhani kwamba Sitakutelekeza, sasa kwa kuwa una uhakika kunihusu baada ya kuona matendo Yangu—si rahisi hivyo! 

Jumanne, 26 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 18

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 18

Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! 

Jumamosi, 23 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 22 na 23

Mwenyezi Mungu anasema, "Leo, wote wako tayari kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua tabia ya Mungu, lakini hakuna anayejua kwa nini hawezi kufuata matamanio yake, hajui kwa nini moyo wake daima humsaliti, na kwa nini hawezi kutimiza kile anachotaka. Kwa hiyo, yeye anakabiliwa tena na hali mbaya ya kukata tamaa, lakini pia anaogopa. Asiweze kuonyesha hisia hizi zinazopingana, anaweza tu kuonyesha huzuni na kuendelea kujiuliza: Je, inaweza kuwa Mungu hajanipa nuru?