“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1).
Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mwanadamu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu. Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.
“Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto” (Mathayo 3:11).
Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. …
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.
2. Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana1:1).
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6).
“Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo” (Yohana 14:9-11).
Watu wote wanapotilia maanani, wakati vitu vyote vinafanywa upya na kuhuishwa, wakati kila mtu anamtii Mungu bila shaka, na yuko tayari kubeba jukumu zito la mzigo wa Mungu—hapa ndipo wakati umeme wa mashariki unatoka, ukiangaza yote kutoka Mashariki hadi Magharibi, ukiyatisha yote ya ulimwengu na ujaji wa mwanga huu; na wakati huu, Mungu tena huanza maisha Yake mapya.
Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya.
Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. "Wanajificha wenyewe katika unyenyekevu."
"Nimewahi Treni ya Mwisho" (5) : Matokeo Yanayofikiwa na Kazi yaMunguAliyepata Mwili
Bwana Yesu alitabiri kwamba katika zile siku za mwisho, ngano itatenganishwa na matawi, kondoo na mbuzi, na watumishi wema kutoka kwa watumishi waovu. Unajua jinsi unabii huu unatimizwa? Je, ungependa kujua njia ambayo Mungu anafanya kazi ya kutenganisha kila moja kwa aina yake katika zile siku za mwisho? Ikiwa unataka kupata ufahamu zaidi, tafadhali angalia video hii fupi!
“Nimewahi Treni ya Mwisho” – Kwa Nini Mungu Anapata Mwili Kufanya Kazi Yake katika Siku za Mwisho | Swahili Christian Movie Clip 3/6
Katika zile siku za mwisho, Bwana amerejea katika mwili kueleza ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumukuanzia na familia ya Mungu. Hata hivyo, ndugu wengi katika Bwana wanaendelea kuamini kwamba Yehova alifanya kazi kama Roho katika Agano la Kale na katika siku za mwisho Mungu ataendelea kufanya kazi katika umbo la Roho bila haja yoyote ya kupata mwili. Hivyo kwa nini Mungu anakuwa mwili ili kufanya kazi Yake katika siku za mwisho? Je, Roho wa Mungu hawezi kufanya kazi hii? Kuna tofauti gani kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya Roho?