Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kukamilishwa na Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kukamilishwa na Mungu. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 16 Novemba 2018

Matamshi ya Mungu | Tamko la Sitini


Matamshi ya Mungu | Tamko la Sitini


Mwenyezi Mungu anasema, " Si jambo rahisi kwa maisha kukua; yanahitaji mchakato, na aidha, kwamba muweze kulipa gharama na kwamba mshirikiane na Mimi kwa uwiano, na hivyo mtapata sifa Yangu. Mbingu na dunia na vitu vyote vinaanzishwa na kufanywa kamili kupitia maneno ya kinywa Changu na chochote kinaweza kutimizwa nami.

Jumanne, 13 Novemba 2018

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu


Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu


Mwenyezi Mungu anasema, "Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika.

Jumatatu, 12 Novemba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Sitini na Mbili


Umeme wa Mashariki | Tamko la Sitini na Mbili

Kuyaelewa mapenzi Yangu hakufanywi ili tu kwamba uweze kujua, ila pia kwamba uweze kutenda kulingana na nia Yangu. Watu hawauelewi moyo Wangu. Ninaposema huku ni mashariki, wanalazimika kuenda na kutafakari, wakijiuliza, “Kweli ni mashariki? Pengine sio. Siwezi kuamini kwa urahisi hivyo. Nahitaji kujionea mwenyewe.” Ninyi watu ni wagumu sana kushughulikia, na hamjui utii wa kweli ni nini.

Ijumaa, 9 Novemba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Nane


Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu. 

Jumatatu, 5 Novemba 2018

Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni?


     
Kuhusiana na ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu alisema, "ila yule atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21). Kwa hivyo ni mtu aina gani hasa anayefanya mapenzi ya Baba wa mbinguni? Watu wengi husadiki kwamba wale wanaofuata mfano wa Paulo na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni.

Ijumaa, 26 Oktoba 2018

Tamko la Sitini na Nane


Tamko la Sitini na Nane



Mwenyezi Mungu anasema, "Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa. Acha wale wanaonipinga na wale wasioanza kushirikiana na Mimi wateseke uchungu wa maafa mbalimbali. 

Jumamosi, 20 Oktoba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Tatu

Umeme wa Mashariki | Tamko la Tatu

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi.