Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kumwabudu-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kumwabudu-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 15 Juni 2019

Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne



Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne


Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. 

Alhamisi, 13 Desemba 2018

Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote

Sura ya 1 Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Kila kitu

1. Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote

Maneno Husika ya Mungu:
Yote yaliyo duniani humu yanabadilika haraka sawasawa na mawazo ya Mwenye uweza, na chini ya macho Yake. Mambo ambayo wanadamu hawajawahi kuyasikia yanaweza kuja kwa ghafla, ilhali vitu ambavyo wanadamu wamemiliki kwa muda mrefu vinaweza kutoweka bila wao kujua. Hakuna anayeweza kutambua mahali alipo Mwenye uweza sembuse yeyote kuweza kuhisi kuzidi uwezo wa mwanadamu na ukuu wa nguvu za uzima za Mwenye uweza. Anazidi uwezo wa mwanadamu kwa vile Anavyoweza kufahamu yale ambayo wanadamu hawawezi. 

Jumamosi, 12 Mei 2018

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mkristo

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Li Li     Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilitiwa moyo na Mungu na kupandiswa cheo kuwa mfanyakazi wa eneo. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje?

Jumatano, 9 Mei 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Watu! Furahini!

Mwenyezi Mungu alisema,  Katika nuru Yangu, watu wanaona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata vitu vya raha. Nimekuja kutoka Mashariki nami Natoka huko. Wakati ambapo utukufu Wangu unang'aa, mataifa yote yanaangaziwa, vitu vyote vinaletwa katika nuru, hakuna kitu kinachobaki katika giza. Katika ufalme, maisha ya watu wa Mungu pamoja na Mungu ni ya furaha isiyolinganishwa.

Jumatatu, 30 Aprili 2018

Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu


Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu

Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu.

Alhamisi, 22 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Ufafanuzi wa Matamko ya Arubaini na Nne na Arubaini na Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada


TanguMungu alipomwambia mwanadamu kuhusu "upendo wa Mungu”—somo la maana zaidi kati ya yote—Alilenga kuzungumza juu ya mada hii katika "matamko ya Roho mara saba," kusababisha watu wote kujaribu kujua utupu wa maisha ya mwanadamu, na hivyo kuchimbua upendo wa kweli ulio ndani yao. Na wale wanaoishi katika hatua ya sasa wanampenda Mungu kiasi gani? Je, mwajua? Hakuna mipaka kwa somo la "kumpenda Mungu." Na je, kuhusu ufahamu wa maisha ya mwanadamu ndani ya watu wote? Mtazamo wao kwa kumpenda Mungu ni upi? 

Jumamosi, 17 Februari 2018

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho "Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote"

Utambulisho

    Mwenyezi Mungu alisema, "Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga."

Jumatatu, 12 Februari 2018

Swahili Christian Video | Nyendo za Mateso ya Kidini "Kuficha Uhalifu"


Utambulisho

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inayoonyesha kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Mkristo Mchina aliyeitwa Song Xiaolan–kifo ambacho kwacho polisi wa CCP walitoa maelezo yasiyopatana na yaliyogongana.

Jumanne, 23 Januari 2018

Sura ya 54. Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja

Sura ya 54. Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja

Mwenyezi Mungu alisema, Kama utajielewa, ni lazima uielewe hali yako ya kweli; jambo muhimu zaidi katika kuielewa hali yako mwenyewe ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zako na mawazo yako. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa; ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo.

Jumatatu, 1 Januari 2018

Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,imani


Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro


Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawawezi kuainisha ni watu gani wana ukweli, watu gani hawana ukweli na watu gani husema mambo yaliyo na ukweli. Unapoulizwa kueleza ni nini maana ya "ukweli," huwezi kueleza kwa wazi. Lakini mara tu mtu anaposema kitu, unasema: “Mtazamo wake ni wa kweli. Maneno ayasemayo yanaonyesha ufahamu wa utendaji uliopatikana kupitia kwa uzoefu.”