Jumapili, 12 Mei 2019

Maneno ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”



Maneno ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”


 Mwenyezi Mungu anasema, “Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa.

Jumamosi, 11 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 69


Mwenyezi Mungu anasema, “Mapenzi Yangu yatokapo, yeyote anayethubutu kupinga na yeyote anayethubutu kuhukumu au kuwa na shaka, mara moja Nitamfukuza. Leo, yeyote ambaye hatendi kulingana na mapenzi Yangu, au yeyote anayeyafikiria mapenzi Yangu visivyo, ni lazima atupwe nje na kuondolewa kutoka kwa ufalme Wangu. Katika ufalme Wangu hakuna mtu mwingine—wote ni wana Wangu wa kiume, wale ambao Nawapenda na hunifikiria Mimi. 

Ijumaa, 10 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 68


Mwenyezi Mungu anasema, “Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa.

Alhamisi, 9 Mei 2019

Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"



Maonyesho ya Mungu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu"


Mwenyezi Mungu anasema, "Chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe vyote, haijalishi tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai cha aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu aelewe kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani katika maisha na kupoteza madhumuni ya kusudi katika maisha."

Jumatano, 8 Mei 2019

Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"



Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"


Mwenyezi Mungu anasema, "Kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. 

Jumanne, 7 Mei 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza


      Mwenyezi Mungu anasema, "Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.

Jumatatu, 6 Mei 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”


      Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli

Jumapili, 5 Mei 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”


      Mwenyezi Mungu anasema, “Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. 

Jumamosi, 4 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini
2. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

Ijumaa, 3 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 67


Mwenyezi Mungu anasema, “Wana Wangu wanaonekana wazi, na wanaonekana mbele ya watu wote. Nitawaadhibu vikali wale wanaothubutu kuwakataa wao kwa wazi; hiyo ni hakika. Leo, wale wote wanaoweza kusimama na kuchunga kanisa wote sasa wamepata cheo cha wana wazaliwa wa kwanza na sasa wako pamoja katika utukufu Na Mimi—yale yote yaliyo Yangu ni yenu pia. Ninawakabidhi wale wanaonitii Mimi kwa dhati neema tele, ili uweze kuwa wenye nguvu, zaidi ya nguvu ya wanadamu wengine. 

Alhamisi, 2 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 66


Kazi Yangu imeendelea hadi hatua ya sasa na yote imefuata mipango ya busara ya mkono Wangu, na pia kuwa fanikio Langu kuu. Nani kati ya wanadamu anaweza kufanya kitu kama hiki? Na je, si wanaona ni afadhali waingilie kati usimamizi Wangu? Lakini lazima ujue kuwa hakuna namna yeyote anaweza kufanya kazi Yangu badala Yangu, sembuse kuizuia, kwani hakuna yeyote anayeweza kusema au kufanya vitu Nifanyavyo na kusema. Ingawa hii ndio hali, watu bado hawanijui Mimi—Mwenyezi Mungu mwenye busara! 

Jumatano, 1 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne




Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Uzao: Awamu ya Tano
1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake
2. Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Hufaidi Ufahamu Mpya wa Hatima Yao
3. Kusadiki Katika Hatima si Kibadala cha Maarifa ya Ukuu wa Muumba
4. Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli

Tazama Zaidi: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Tano. App ya Kanisa la Mwenyezi Mungu