Mwenyezi Mungu anasema, "Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapofyatua moto, Ninaitazama kwa uangalifu dunia nzima, Ninatazama kwa uangalifu ulimwengu mzima. Wanadamu wote wananiomba Mimi, wameinua macho yao kuelekea Kwangu, wakiomba Nipunguze hasira, na kuapa kutoniasi tena. Lakini haya siyo yaliyopita; bali yaliyopo kwa sasa. Ni nani anayeweza kubadilisha mapenzi Yangu? Kwa kweli sio sala katika moyo wa mwanadamu, wala maneno yanayotoka midomoni mwao?
Mwenyezi Mungu anasema, "Kujenga kanisa si kitu rahisi cha kufanya! Niliweka moyo Wangu wote katika kulijenga na Shetani angefanya kila kitu ingeweza kuibomoa. Kama unataka kujengwa lazima uwe na maono; lazima uishi maisha kwa Mimi, kuwa shahidi wa Kristo, shikilia Kristo juu kwa juu, na kuwa mwaminifu Kwangu. Hupaswi kutoa visingizio, lakini badala yake kutii bila ya sharti; lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi.







