Ijumaa, 22 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 18


Maneno yote ya Mungu yana sehemu ya tabia Yake; tabia Yake haiwezi kuonyeshwa kwa ukamilifu kwa maneno, kwa hiyo hii inaonyesha kiasi gani cha utajiri kiko ndani Yake. Kile ambacho watu wanaweza kukiona na kukigusa ni, hata hivyo, finyu, kama ulivyo uwezo wa watu. Ingawa maneno ya Mungu ni dhahiri, watu hawawezi kuyaelewa kwa ukamilifu. Kama maneno haya tu: "Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. 

Alhamisi, 21 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 15


Tofauti kubwa zaidi kati ya Mungu na mwanadamu ni kwamba kila mara maneno ya Mungu hugonga ndipo, na hakuna kilichofichwa. Kwa hiyo hali hii ya tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika maneno ya kwanza ya leo. Kipengele kimoja ni kuwa yanaonyesha tabia halisi ya mwanadamu, na kipengele kingine ni kuwa yanafichua wazi tabia ya Mungu. Hizi ni asili kadhaa za jinsi maneno ya Mungu yanaweza kutimiza matokeo. Hata hivyo, watu hawalielewi hili, kila mara wao huja kujijua tu katika maneno ya Mungu lakini "hawajamchangua" Mungu. 

Jumatano, 20 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 41


Mungu humfinyanga mwanadamu vipi? Je, unalifahamu hili? Linaeleweka? Nalohufanyika vipi kanisani? Unafikiriaje? Je, umewahi kuyafikiria maswali haya? Ni nini ambalo Anatarajia kufanikisha kupitia kwa kazi Yake kanisani? Je, yote yanaeleweka bado? Kama sivyo, yote ambayo unafanya hayana maana, yamebatilika! Je, maneno haya yanaugusa moyo wako? 

Jumanne, 19 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 40


Kwa Mungu, mwanadamu ni kama mtu anayechezewa katika mshiko Wake, kama nudo inyoshwayo kwa mkono katika mikono Yake—inayoweza kufanywa nyembamba au nzito kama apendavyo Mungu, kuifanyia Apendavyo. Ni haki kusema kwamba mwanadamu kwa kweli ni mtu anayechezewa mikononi mwa Mungu, kama paka wa Uajemi ambaye bibi amemnunua kutoka sokoni. Bila shaka, yeye ni mtu anayechezewa mikononi mwa Mungu—na kwa hiyo hakukuwa na chochote cha uongo kuhusu ufahamu wa Petro. 

Jumatatu, 18 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 12


Watu wote wanapotilia maanani, wakati vitu vyote vinafanywa upya na kuhuishwa, wakati kila mtu anamtii Mungu bila shaka, na yuko tayari kubeba jukumu zito la mzigo wa Mungu—hapa ndipo wakati umeme wa mashariki unatoka, ukiangaza yote kutoka Mashariki hadi Magharibi, ukiyatisha yote ya ulimwengu na ujaji wa mwanga huu; na wakati huu, Mungu tena huanza maisha Yake mapya.  

Jumapili, 17 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 32


Maneno ya Mungu huwaacha watu wakikuna vichwa vyao; ni kana kwamba, Anapozungumza, Mungu anaepukana na mwanadamu na kuzungumza na hewa, kana kwamba Hafikirii hata kidogo kuzingatia zaidi matendo ya mwanadamu, na Hatilii maanani kabisa kimo cha mwanadamu, kana kwamba maneno Anayozungumza hayaelekezwi kwa dhana za watu, lakini kuepukana na mwanadamu, kama lilivyokuwa kusudi la Mungu la asili. Kwa sababu nyingi sana, maneno ya Mungu hayaeleweki na mwanadamu hawezi kuyapenya. 

Jumamosi, 16 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 31


Tabia ya Mungu hujumuishwa katika matamko yote ya Mungu, lakini wazo kuu la maneno Yake ni kufichua uasi wa wanadamu wote na kufunua mambo kama kutotii, kuasi, utovu wa haki, udhalimu, na kutoweza kumpenda Mungu kweli. Ni kiasi kwamba, maneno ya Mungu yamefikia kiwango ambacho Yeye husema kwamba kila kinyweleo katika miili ya watu kina upingaji kwa Mungu, kwamba hata kapilari zao zina ukinzani kwa Mungu. Ikiwa watu hawatajaribu kuchunguza hili, wao daima watakuwa wasioweza kuyajua, na hawataweza kamwe kuyaweka kando. 

Ijumaa, 15 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 30


Mwenyezi Mungu anasema, "Watu wengine wanaweza kuwa na utambuzi kidogo katika maneno ya Mungu, lakini hakuna yeyote kati yao ambaye huamini hisia zake; wao huogopa sana kuingia katika ukanaji. Hivyo, wao kila mara wamegeuka kati ya furaha na huzuni. Ni haki kusema kwamba maisha ya watu wote yamejaa huzuni; kusongeza hili katika hatua nyingine zaidi, kuna usafishaji katika maisha ya kila siku ya watu wote, lakini Naweza kusema kwamba hakuna anayepata ufunguliwaji wowote katika roho yake kila siku, na ni kana kwamba milima mitatu mikuu inakilemea kichwa chake.

Alhamisi, 14 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 29


Mwenyezi Mungu anasema, "Kati ya kazi inayofanywa na watu, baadhi yake hutekelezwa kwa maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu, lakini kwa sehemu yake Mungu hatoi maagizo ya wazi, ikionyesha vya kutosha kwamba kile kinachofanywa na Mungu, leo, bado hakijafichuliwa kabisa—ambalo ni kusema, mengi bado yamefichwa na bado hayajajulikana na watu. Lakini mambo mengine yanahitaji kujulikana na watu, na kuna mwengine yanayohitaji kuwaacha watu wakiwa wamekanganywa na kuchanganyikiwa; hiki ndicho kinachohitajika na kazi ya Mungu.

Jumatano, 13 Februari 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 28


Mwenyezi Mungu anasema, "Hali ya watu ni kwamba kadri wanavyoelewa maneno ya Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyoshuku zaidi njia ya sasa ya Mungu ya kufanya kazi. Lakini hii haina athari kwa kazi ya Mungu; maneno Yake yanapofikia kiwango fulani, kwa kawaida mioyo ya watu itabadilika. Katika maisha yao, kila mtu huyakazia macho maneno ya Mungu, na pia wao huanza kutamani sana maneno Yake—na kwa sababu ya mfichuo wa Mungu wa siku zote, wanaanza kujidharau. 

Jumanne, 12 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 27


Mwenyezi Mungu anasema, "Leo, maneno ya Mungu yamefikia kilele chake, ambako ni kusema, sehemu ya pili ya enzi ya hukumu imefikia kilele chake. Lakini sio kilele cha juu kabisa. Wakati huu, sauti ya Mungu imebadilika, si ya kudhihaki wala ya ucheshi, na haigongi au kulaani; Mungu ametuliza sauti ya maneno Yake. Sasa, Mungu anaanza "kubadilishana maoni" na mwanadamu. Mungu anaendeleza kazi ya enzi ya hukumu na pia kufungua njia ya sehemu inayofuata ya kazi, ili sehemu zote za kazi Yake zipatane. 

Jumatatu, 11 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 26



Mwenyezi Mungu anasema, "Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani.