Ijumaa, 19 Aprili 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 63


Mwenyezi Mungu anasema, “Zielewe hali zako mwenyewe, na zaidi ya hayo, kuwa wazi kuhusu njia unayohitaji kutembea; usubiri tena Mimi niyainue masikio yako na kukuonyesha mambo. Mimi ni Mungu ninayekagua moyo wa ndani kabisa wa mwanadamu nami najua kila fikra na wazo lako, hata zaidi Naelewa matendo na tabia yako. Lakini matendo yako na tabia yana ahadi Yangu? Je, yana mapenzi Yangu? Umetafuta haya kwa kweli? Je, kweli umetumia wakati wowote kuhusu suala hili? 

Alhamisi, 18 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | 84. Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu

Wimbo wa Kuabudu | 84. Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu

I
Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu,
na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake.
Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho.

Jumatano, 17 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 62


Mwenyezi Mungu anasema, “Kuyaelewa mapenzi Yangu hakufanywi ili tu kwamba uweze kujua, ila pia kwamba uweze kutenda kulingana na nia Yangu. Watu hawauelewi moyo Wangu. Ninaposema huku ni mashariki, wanalazimika kuenda na kutafakari, wakijiuliza, “Kweli ni mashariki? Pengine sio. Siwezi kuamini kwa urahisi hivyo. Nahitaji kujionea mwenyewe.” Ninyi watu ni wagumu sana kushughulikia, na hamjui utii wa kweli ni nini.

Jumanne, 16 Aprili 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 61


Mwenyezi Mungu anasema, “Ukiwa na ufahamu wa hali yako mwenyewe basi utafanikisha mapenzi Yangu. Kwa kweli, mapenzi Yangu si magumu kushika, ni kwamba tu katika siku zilizopita hukuweza kutafuta kulingana na lengo Langu. Ninachotaka si dhana wala fikira za binadamu, sembuse pesa zako wala mali yako. Ninachotaka ni moyo wako, unaelewa? Haya ni mapenzi Yangu, na hata zaidi ni kitu ambacho Nataka kupata. 

Jumapili, 14 Aprili 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”


Mwenyezi Mungu anasema, “‘Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu’ na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri.

Jumamosi, 13 Aprili 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 59

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

        Mwenyezi Mungu anasema, “Tafuta mapenzi Yangu zaidi katika mazingira unayoyakabili na kwa hakika utapata kibali Changu. Ilmradi uwe tayari kwenda katika utafutaji na kuhifadhi moyo ambao unanicha, Mimi Nitakupea yote unayokosa. Kanisa sasa linaingia utendaji rasmi na mambo yote yanaingia kwenye alama sahihi. Mambo hayako yalivyokuwa wakati mlipokuwa na limbuko la mambo yajayo. 

Ijumaa, 12 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 56


Mwenyezi Mungu anasema, “Nimeanza kuchukua hatua kuadhibu wale ambao hufanya uovu, wale ambao hushika madaraka, na wale ambao hutesa wana wa Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, yeyote anayenipinga katika moyo wake, mkono wa amri Zangu za utawala utakuwa daima juu yake. Fahamu hili! 

Alhamisi, 11 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 55

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu anasema, “Ubinadamu wa kawaida ambao huzungumziwa si wa mwujiza sana kama watu wanavyofikiria, lakini unaweza kuvuka mipaka ya mafungo ya watu wote, matukio, na vitu, kupita mipaka ya nguvu za mazingira, na unaweza kunikaribia Mimi na kuwasiliana kwa karibu na Mimi mahali popote na katika mazingira yoyote. Ninyi daima hutafsiri vibaya nia Zangu. Ninaposema mnapaswa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, mnajizuia na kudhibiti miili yenu. 

Jumatano, 10 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 54

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 54

Ninalielewa kila kanisa kama kiganja cha mkono Wangu. Usifikiri kwamba Siko wazi au sielewi. Ninawaelewa na kuwajua watu wote mbalimbali wa kila kanisa hata zaidi. Ninahisi hisia ya umuhimu kwamba ni lazima Nikufundishe. Nataka nikufanye ukue hadi utu uzima haraka zaidi ili kwamba siku ambayo unaweza kuwa wa msaada Kwangu itakuja haraka zaidi. Nataka vitendo vyenu viwe vimejaa hekima Yangu ili muweze kumdhihirisha Mungu kila pahali. 

Jumanne, 9 Aprili 2019

Swahili Gospel Movie | “Fichua Siri Kuhusu Biblia” Movie Clip: Tunaweza Kupata Uzima kwa Kuamini Katika Biblia?



Swahili Gospel Movie | “Fichua Siri Kuhusu Biblia” Movie Clip: Tunaweza Kupata Uzima kwa Kuamini Katika Biblia?


Mara kwa mara wachungaji na wazee huwafundisha watu kuwa hawawezi kuitwa waumini wakiondoka kwenye Biblia, na kwamba kwa kushikilia Biblia pekee ndiyo wanaweza kupata uzima na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, je, kweli hatuwezi kupata uzima tukiondoka kwenye Biblia?

Jumatatu, 8 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 52


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 52

Ninatokea kama Jua la haki, na nyinyi pamoja na Mimi tunashiriki utukufu na baraka, milele na milele! Huu ni ukweli thabiti, na tayari umeanza kutimizwa kwenu. Kwa yote ambayo Nimewaahidi, Nitawatimizia; yote Nisemayo ni ya kweli, na hayatarudi tupu. Baraka hizi za ajabu ziko juu yenu, hakuna yeyote mwingine anayeweza kuzidai; ni matunda ya utumishi wenu kwa kukubaliana na Mimi kwa maafikiano. Zitupilie mbali dhana zenu za kidini; yaamini maneno Yangu kuwa ya kweli na msiwe mwenye shaka! 

Jumapili, 7 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 51


Ee! Mwenyezi Mungu! Amina! Ndani Yako yote yanaachiliwa, yote ni huru, yote ni wazi, yote hufichuliwa, yote hung’aa, bila sitara au maficho yoyote. Wewe ni Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Umetawala kama Mfalme. Umefichuliwa wazi, wewe tena si fumbo lakini Umefichuliwa kabisa milele na milele! Kwa kweli Nimefichuliwa kabisa, Nimefika hadharani, na Nimejitokeza kama Jua la haki kwa kuwa leo si enzi ya kuonekana kwa nyota ya asubuhi tena, si awamu ya sitara tena. Kazi Yangu ni kama mwanga wa umeme, inakamilishwa na wepesi wa ajabu.